[b]TZII HIPHOP KING?[/b]
#1
Posted 27 March 2007 - 09:06 AM
king wa bongo hiphop?anastahiri?
T.M.K akademy-non shobo squad
#2
Posted 29 March 2007 - 11:46 AM
ameibuka juzi tu anaanza kuchonga.
#3
Posted 30 March 2007 - 07:20 PM
muda alio-po kwenye game na c vinginevyo
muda wa kuwepo kwenye gae co kipimo kinachojitosheleza
au sio vip kimashairi,styli,street capability,philosophy?
one..........................
T.M.K akademy-non shobo squad
#4
Posted 03 April 2007 - 12:12 PM
#5
Posted 27 April 2007 - 03:20 PM
umeyafannya mtu kama Mr2 anaweza kujivika
uking prof.jay aliipeleka game levo zingine
mpaka wezee wakaanza kupriciate
KIKOSI wameirudisha game mahali ilipo sasa
ambapo kila atokaye sa hivi anafanya HIPHOP
ata kama ni mamluki.
afu kuna ishu hii hapa ya ubongo flava na uhiphop
unaichukulieje?
T.M.K akademy-non shobo squad
#6
Posted 28 April 2007 - 03:24 PM
Kuhusu Ubongo wa flava kwa kweli mi naona umefikia ukingoni.Bongofleva imekufa na inazidi kudidimia siku hadi siku watu wanabaki na umaarufu mifukoni hakuna kitu.Walikuwa wanasema hiphop ni umaarufu lakini haiuziki na wao imewakuta sasa.
Nitakutolea mfano msanii Ali kiba inasemekana ndo yupo juu hivi sasa nyimbo yake inapigwa kila wakati kwenye radio lakini hadi sasa hajaperform tamasha lolote.Naamini pesa nyingi kwa wasanii wanapata kupitia matamasha na sio kwa kuuza tape na matamasha bongo ndo hamna siku hizi sasa sijui inakuwa vipi hapo.
I learned a lot in this world
Got a profession that keeps me stressin
Facin criticism,
And you still keep me happy and healthy
Nyuma naona mbali
bora mbele kuelekea.
#7
Posted 09 May 2007 - 05:39 PM
#8
Posted 11 May 2007 - 12:18 PM
mamluki ndani ya fani anajielewa kiundani/
kwanza analewa kiwewe sifa za kujisifu mwenyewe/
pili lazima akili sio king anatafsiri verses kwa kiswahili/
tatu kuwa na rasta sio hiphop mbona wanafuga hadi mafyatu/
nne bado ni softi kimistari kila wakati anapobasti/
tano hana michano anamaseji za taarabu ya malumbano/
sita sitosita joh ni mtoto tu wa kupitapita mbele ya majita/
namaliza sio miujiza naangamiza vipande vyakuumiza/
kaa mbali na hili giza wewe joh makini ........
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#9
Posted 12 May 2007 - 01:48 PM
hana mistali concious dyte
umegundua....analewa sifa anazojisifia ye mwenyewe
kimistali kwa FID hasogei kabisa
kanishangaza juz kat anadai katoa album afu ina nyimbo10!
uizi ambao wanafanya wasanii wengi wa bongo flava
mistali yake inaonyesha kama hajapitia lyf taf la kitaa
(ingawa historia yake siifaham)
T.M.K akademy-non shobo squad
#10
Posted 01 August 2007 - 06:37 PM
nachokiona wengi walio comment ni kuwa wanamponda sana Joh nakuona kama
yuko chini flani. ni wachache walianzia juu tukumbuke..
but kuhusu kujiita king si dhani ka ni big issue, kama kuna mtu anapinga nae
aende studio akapime kugombania crown.
so far nani king wa game kibongo bongo asimame na aseme.
he got ballz bwana mi naamini, wanaobisha wapime, wako kimya tu.
kikosi cha mizinga hawana lolote sema wamekuja na style ya kuipinga bongo fleva kwa nguvu na kuwapinga wasanii wengine wengi tuu kuwa si wa-ukweli.
Hii ni ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya yao ili wakubalike.
Mwisho wa siku ni yale yale bongo fleva.
Kuwa na sauti ya ukali na mikwaruzo haifanyi mistari kuwa bora, hats huko mbele tunaona walio simama wakoje. Mistari kitu kingine jama sio mnamega kwa kuwa mnawafeel tu.
weka mawazo wazi then andika, usiwe biased.
Majigambo nji sehemu tu ya sanaa, huenda ni mlengo mchizi kajichagulia.
makelele na vitisho ni stayle ya jamaa wa block 41 ni style tu, lakini iko wazi kala pina hayuko tite..sijui kwanini Hashim dogo hafanyi muziki, he was tite.
kalapina tozi tu, mgumu anakula ice cream ice-cream parlour? check video yake
#11
Posted 03 August 2007 - 12:51 PM
#12
Posted 04 August 2007 - 04:50 PM
Inabidi ujue hata Mkwawa wa wahee, Isike, Mirambo etc walipinga ukoloni then, na twasoma katika historia na wengine wengi tu. but Nyerere ni mmoja, wanaharakati ni wengi vinara wanaosikika na kujulikana ni wengi. Hapo ndo nawezza sema mchango wa Joseph Haule na huyo the late Nigger 1 haufanani,Jay kafanya watu wasikilize huo muziki, in fact kaupeleka level nyingine, upende usipende kila mtu anajua. after all ni watu wasio jua hip hop wanaweza mataja saleh ka mwanamapinduzi. Biter? Man umepotea hapo. Na udogo wangu sikuwahi kufall kwa rap za yule jamaa Saleh, it was so fake.
Nitajie mtu mmoja ambaye amewahi kuwa crowned king wa hip hop huko Mbele ambaye alikuwa undisputed? sikui ka yupo, but as far as hip hop goes challenges are there, and who claims to have the throne should be challenged. They should try joh Makini and sisi wazungumzaji na watazamaji wenye upeo tutajua.
Joh makini anajaribu kujichukulia hiyo throne na ma MC wako kimya tu........
#13
Posted 07 August 2007 - 06:51 AM
Lakini nadhani nawe bado unaegemea nguzo moja, mbili zilizobalia utaki kuzikubali,
kumbuka past creates the future, kam unavoeeleza huwezi kuzikubali nyimbo za saleh jabir wala The late Nigger one , lakini ukweli ndio huo, hao ndio wanamapinduzi kwenye historia hawafutiki hata kama saleh alikuwa anacopy, lakini alirevolize watu wakamkubali.
kuhusu Pro jize ni wakati tu ndio umembeba, pamoja nami namkubali katika mazingira fulani, lakini kama wewe bahati mapinduzi mnayoyasema kayafanya kutokana na albamu yao ya Chemsha Bongo, kwangu pale sijaona nyimbo hata moja nami ya kusikiliza, naposema pro Jize ni wakti umembeba na maana kuwa soko huria lilipoanza kushika kasi vyombo vingi vya habari vya watu binafsi vikaingia, nsa ndipo hapo waliokuwepo wakiwemo wakina Pro Jize wakapata Air Time, na wengi wakasikia na ndio wakawapenda, na hakika bahati Air time miaka ya 1991 ingekuwepo kama sasa wengi wangewafeel hawa wanamapinduzi wangu, enzi hizo single unaziskia mitaani na Beach Party, wangapi walikuwa wanakuja, wachache mno nazilikuwa hazitangazwi, walikuwa wengi tu ambao wanamapinduzi WWA weusi wagumu Asilia Kundi la kwanza kutoa Full Albamu ya Kiswahili, Fans With Sense( akina Jose Mtambo) na bado anakimbiza,Mapinduzi manaake ni kuutoa utawala uliokuwepo pamoja na mabo yake na kuleta Sera mpya Niambi {ro Jize amekuja na Sera na Utawala gani mpya
#14
Posted 09 August 2007 - 05:31 PM
aliiondoa ile dhana ya muziki wa hip hop kuonekana uhuhuni kwa lyrics zake.
Sikatai ka kwa kipindi kile kungekuwa na airtime za kutosha huenda watu wangesikika.
sipendi kuelemea hapo tu, kuna watu walipata air play kwa sana tu kipindi kile ka mr 2, alikuwa na track yake ni siku yangu, ilipigwa sana tu, but haikuwa na mantiki kwa watu wengi ilikuwa na majigambo mengi, mi sioni ka ilikuwa mbaya, ila kwa watu ambao utamaduni ule ni mpya, na tukubali kuwa kwa watanzania wengi culture ya hip hop ni dhana mpya ilikuwa. Mr 2 hakuweza kuwafanya waupende huo muziki na utamaduni wake. Lakini Jay alifanikiwa kuifanya jamii iukubali muziki, ni revolution ya aina yake. sipingani na wanaharakati walio sacrifice shughuli zao kama Saleh,Nigger 1 the late, WWA ni watu muhimu ofcoz regardless my feelings kwa baadhi. Huwezi kumkubali kila mtu hata awe wa ukweli vp, lazima unakua na chaguo. Nawakubali kama wanaharakati muhimu, huenda ndo walichangia hata wengine kuibuka hii leo,huenda tungebaki na hip hop za kiingereza maana then ndo zilikuwa popular au siyo?
Walifungua njia nakubali, ni kama wanaharakati wengine wowote but always kuna anae shine na ni kuwakutumia nyanja ambazo zishatengenezwa na walipita wanaharakati.
Sijui ka uko kartibu na physics, ntakupa tu mfano, Galileo ndo alie anza mambo, Newton ndo kila mtu anamjua. Ukweli ni kuwa kazi zake zote za newton ni mwendelezo wa mamabo ya Galileo.
#15
Posted 13 September 2007 - 11:21 AM
nyie mnapima nyie.
#16
Posted 20 May 2008 - 02:52 PM
waka- appreciate kwamba this z a lyrist.......kama hashim dogo
vilevile kuwa versitile katika kile unachokiandika katika upeo ule wa mbingu ya 7 vilevile\
inaonyesha UWEZO.....ukiangalia kama MOS DEF hana aibum zaidi ya mbili ( blak on bothside n new danger)
lakini watu wanamtambua..so Uhuru kusema kuna machizi wako pande hizo ni illest.....kuamini kuna kuja maranyingi kwa kusikia au kuona au sio.......watu wanasikiliza kisha wanatafsiri aih!
T.M.K akademy-non shobo squad
#17
Posted 01 June 2008 - 08:58 AM
Hebu sikiliza track kama HAO,MFALME
So kama sio yeye je nani ni MFALME?
#18
Posted 22 July 2008 - 12:13 PM
kwanza vina vyake ni copy n paste style watu wanajua hilo.
halafu kwa jinsi anavyopotray anaonekana ni fake mc tu kwamba anapretend kuwa hard head ila si hivyo.
fuck joh makini!!!!!!
#19
Posted 22 July 2008 - 12:39 PM
so najua nini mnaongelea na wapi mnakwama!!!!
jay naanza hiphop watu tunamuona na for ur info jay alikua hajui kuandika mistari ya kiswahili hata kidogo.
somebody couched him from ma own hood!!!!!na ni mtu huyo huyo ndiye alimpeleka j kwa hard blastaz coz hbc had a close relation wit our cru. i know dat terry (looney-t...fanani)also played a big role n shappin jizze (no lies) n if u got a chance to talk to dat dude he will tell u de same.i cud have mentioned his ticha ila itakuwa haijakaa vizuri so long as u know bongo mcs hawapendi kuwa wakweli but i tell u jizze ni mtoto mdogo sana na kuna watu akikutana nao lazima atoe saluti coz anajua ndo waliomfundisha swahili hiphop.
ask anyone from kim area (kimara) atakuambia kuwa j ametoka lutengano without no swahili lyrical skills!!!!
kuna mtu anaitwa tuff b kama umeshawahi kumsikia anajua vizuri wat i m sayin infact tuff b (brian) ni kichwa kuliko hata huyo j.
i gott a lot of evidences to prove dat jizze ni mtoto mdogo sana includin yeye mwenyewe.ingawa hawezi ku admitt this
mistari mingi ya j mwanzoni ilikuwa hopless na haikuwa na mantiki kabisa mpaka wajanja walipoifanyia marekebisho.
therefore i dont c nop revolutionary acts from tha part of j and if j ahs no right to call himself a hiphop revolutionary i dont see how cud joh makini call himself so.
#20
Posted 22 July 2008 - 02:59 PM
k-rym said:
kwanza vina vyake ni copy n paste style watu wanajua hilo.
halafu kwa jinsi anavyopotray anaonekana ni fake mc tu kwamba anapretend kuwa hard head ila si hivyo.
f*ck joh makini!!!!!!
Na nani ni KING wa HIP HOP tz kama sio yeye
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users













