Jump to content


Last Dyte Vs Breakingnewz:


10 replies to this topic

#1 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 28 February 2007 - 12:36 PM

oya raundi moja kama uko fiti!!!!!!
no matusi ni skills tu!
mistari 30!!!!!!!!!!

anza kudrop verse au sio........
peace.

PA1.


Posted Image

#2 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 01 March 2007 - 04:56 AM

sisubiri liive hata bichi nalitumbua,
mwisho wa maumivu utajua ulikuwa unajisumbua,
mishipa ya fikra iliziba sa check ninavyokuzimbua,
flow tight zaidi bikra check ninavyokuumbua,
kama skills tu haa! hapa ndo umetua,
niite runway ya airport haina kukwatua,
we sio wa kwanza hichi kichwa wengi walijaribu kupiga hatua,
wanapojisahau nakula vibaya halafu nabutua,
naweza kukuchengua mpaka ukaona nazingua,
daily slow nikija moto mkali utaungua,
haya twende fasta kabla line zako hazijapungua,
kabla hasira hazijapugua ubongo wako utakuwa umebungua,
mi ni scania heavy weight kila boda natusua,
kwa we mdogo nimekuwa ka mende kwa kuwa unasuasua,
si moja megi ninayofanya kichwa yatakupasua,
siishi kwa kufananisha hata we nitakusua,
si kosa lako ulikatiza anga mbaya bila kujua,
usiogope kama umepinda mi ntakukunjua,
utaniona kama ticha, baraka(means my name), the best chini ya jua,
mistari yako milaini naifanya mbaya hata kuibenjua,
niko fiti? kama ni upeo ntakupanua,
nakukausha kama nguo nakuanika nakuanua,
sisubiri uniletee kama ni beef mi nainunua,
masikio yako yamezibwa na udwanzi nakisanua,changanua,
uozo wako wa rhymez sasa naufukua,
ili usibattle watu wazima ile hali hujakua,
nafasi ya mwisho hiyo utaendelea kuichukua,
nakuona bado unajifunza sasa endelea kubukua,
ukimaliza uje halafu jambo lolote zua,
kwa sasa data na hizi hapa si tayari zinakuzuzua,

#3 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 01 March 2007 - 09:25 AM

nakuja kwa ishara bado nimesimama kuliko mnara
nakukimbiza nione msala nakupiga nyundo ka sigara
ushakuwa jivu nakuachia maumivu ka sholi kwa wivu
fata hii levo utadata huna stimu wewe ni malta
acha kuchechetuka kwa hiz rhymes beua tapika
nimeandaa hili kaburi na kwa sasa nakuzika
nakuruka huu mzuka uone kama yesu anafufuka
ushadondoka staili hii iite ukimwi ushaathirika
hapa unayeyuka nakupa mistari isiyohesabika
teseka hutii timu kwenye hisia za chaka
niite jogoo kila alfajiri wa kwanza kuwika
nakuweka ndani kama mke lazima ukubali kupika
moto unafuka kaa mbali nsije kukufanya mateka!
dhurika la hili gharika nakuacha unateseka
hapa kubali ushahenyeka nakuvika kilemba cha ukoka
kimbia potea fastafasta hii ndio sumu kama nyoka!
bomoka ila haujadata kirhymes umeshachoka
bado nakuona abiria selebuka wakati mimi ndo suka!
andika! hakika katu huwezifika nakuona unakurupuka
kama chiki aliyeputuka mistari hii sasa elevuka
nakuchoma saka nakuvika tairi wewe ndio kibaka
hii kwako ni hekaheka mzee nafiti kuliko kiraka
mc unang'aka kama wakristo wanavyozuga wameokoka
gutuka mtoto budi kubanduka yani umetayadi inuka
huwezi bumbuluka ushaoza kama harufu inayonuka!
wewe kibaraka afu unajiita baraka au saka!!
hii hulka mzuka wa kushuka nakushika ka madaraka
hapa utapata tabu nakuficha kuliko siri za nyaraka!
zuzuka ukishapagawa nyanyuka mwenyewe banduka
masikio tayari nshakushika nakuacha huku ukishoboka




Posted Image

#4 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 01 March 2007 - 11:58 AM

mzuka nimekubali

#5 msizwa

    Member

  • Members
  • PipPip
  • 16 posts

Posted 08 June 2008 - 05:44 AM

ebwana hii 7-0 lst dyt mzuka

#6 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 05 July 2008 - 07:01 PM

unakubali 7- bila we mwali uliyejaa hila,
unaongea ka huna kabila,ama mlupo tahira,
usilete zako hapa utagongwa mbata kwa hasira,
au ndogo utageuzwa kubwa na wasiotumia mipira,we taahira

#7 vnorm

    African Hip Hop Soldier

  • Members
  • 449 posts
  • LocationNairobi, Kenya.

Posted 16 August 2008 - 12:41 PM

last dyte took this one. kali bro.
gowsh. these battles are different. there should be a separate zone for kenyan battles. our swahili's a lil bit different. uppin for votes on the me vs mizani battle.

#8 msizwa

    Member

  • Members
  • PipPip
  • 16 posts

Posted 26 February 2009 - 07:37 PM

breakin newz!!!
punguza jazba kama malaya alie lewa takiila!!
umeshindwa ku last na dyte,,sa kinachofata ni kukufila!
usichokoze mizuka ya bahaaria mi ama killa
huu ushindi zaidi ya kiume 7 bila
rudi ujiunge na wenzako kina q chila
nabanza kipaza zaidi ya paul na asila
FSEEEEEEEEEK!!!!!!!nyammau!!!

#9 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 14 April 2009 - 11:57 AM

ni kweli we ni killa unasambaza ngoma baada ya masela kukufila,
umezidi tantalila ka machoko walioimba tatu bila,tilalila
ndivyo ntakuacha nikimaliza hii beti,
nakushusha taratibu kama nagonga vijeti,
kama ufake ni bus basi nshakukatia tiketi,
acha kunibattle kimistari utajiharibia bajeti,
huu ni ukuta wa block nenda ukapigane na betty,
uzito huu huuwezi naku K-O we ni lightweight

#10 msizwa

    Member

  • Members
  • PipPip
  • 16 posts

Posted 29 April 2009 - 12:28 AM

nakuacha huru ka TID sa muimbie rahisa//
kisha ki nyume ukalie uboo ulidisa/nikupe yote tisa,,
huna ujuzi na fasihi,,mistari yangu manii,,gusa ikutunge mimba,,,nipe mauno ya sindimba,,,
nishakupanua huwezi kubana kimba,,,ushajinyeaa,,,kwa kushobokeaaa mmeaa,,,

#11 fundiaminy

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 3 posts
  • Locationunder your bed

Posted 10 May 2009 - 12:00 PM

aka mzee wa mikoba.big up machiz kwa mnavyotembeza mistari.mzuks.





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users