nakuja kwa ishara bado nimesimama kuliko mnara
nakukimbiza nione msala nakupiga nyundo ka sigara
ushakuwa jivu nakuachia maumivu ka sholi kwa wivu
fata hii levo utadata huna stimu wewe ni malta
acha kuchechetuka kwa hiz rhymes beua tapika
nimeandaa hili kaburi na kwa sasa nakuzika
nakuruka huu mzuka uone kama yesu anafufuka
ushadondoka staili hii iite ukimwi ushaathirika
hapa unayeyuka nakupa mistari isiyohesabika
teseka hutii timu kwenye hisia za chaka
niite jogoo kila alfajiri wa kwanza kuwika
nakuweka ndani kama mke lazima ukubali kupika
moto unafuka kaa mbali nsije kukufanya mateka!
dhurika la hili gharika nakuacha unateseka
hapa kubali ushahenyeka nakuvika kilemba cha ukoka
kimbia potea fastafasta hii ndio sumu kama nyoka!
bomoka ila haujadata kirhymes umeshachoka
bado nakuona abiria selebuka wakati mimi ndo suka!
andika! hakika katu huwezifika nakuona unakurupuka
kama chiki aliyeputuka mistari hii sasa elevuka
nakuchoma saka nakuvika tairi wewe ndio kibaka
hii kwako ni hekaheka mzee nafiti kuliko kiraka
mc unang'aka kama wakristo wanavyozuga wameokoka
gutuka mtoto budi kubanduka yani umetayadi inuka
huwezi bumbuluka ushaoza kama harufu inayonuka!
wewe kibaraka afu unajiita baraka au saka!!
hii hulka mzuka wa kushuka nakushika ka madaraka
hapa utapata tabu nakuficha kuliko siri za nyaraka!
zuzuka ukishapagawa nyanyuka mwenyewe banduka
masikio tayari nshakushika nakuacha huku ukishoboka