Jump to content


NAWAITA MCZ


15 replies to this topic

#1 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 08 December 2006 - 08:12 AM

Nawaita`wote amboa wanajiona tite mcz,
wasogee mbele na mistari yao niwape tizi,
naona wengi mkimoka mnaishia kusizi,
saizi lazima mtatoka kama hamtaishia kufreez,
hata kama ulikuwepo kwenye forum toka enzi,
naweza kukumeza na kukupoteza na tenzi,
mi ni kama fimbo nachapa mcz washenzi,
waliogeuzwa chambo na kuubomoa huu ujenzi,
wa ngome ya mapinduzi,ya hiphop kwa upuuzi,
badala ya kuwa serious wanaleta makuzi,
wanajiunga na mabongofleva wakisanda hawana ujuzi,
zamu yao sasa imeisha no iliisha tangu tangu majuzi,

#2 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 09 December 2006 - 10:36 AM

Fasihi kwa mcs kwenye kipaza ndio asasi
asili ya mafua ndo vina vinatoka vyenyewe ka kamasi
wino kwenye karatasi naurusha hewani ka risasi
Mc wa bongofleva lala chini kupisha hii kasi
Mchizi wa kisiwa cha uasi n'nlinganishe na waasisi
ka makacha wa Sisi kwa Sisi hiz hazhitaj tiz Usihisi
naangusha tungo halisi kuliko uzito wa vifusi
mi ndio Mc hatari bora kukutana na chunusi
kwa verse hizi nafanya mauaji ka Wahutu na Watusi
ni zaidi mikosi kwa fake Mcees nazimisha ka vipisi
nalipua kijasusi nasambaa kimistari kuliko virusi
alwayz natengeneza vina vya maana linganisha na Kamusi

#3 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 11 December 2006 - 04:59 AM

nawapanda niwazalishe kabla hajavaa sanda,
fake mcz kama wewe na queen ngosha kubanda,
kama hakuna pa kutua mtaishia kurandaranda,
nawapiga danadana kama mpira wa kandanda,
hii ndio hukumu kama wamesikia parapanda,
sema hii ni ya kuzimu haina sauti ya vinanda,
usipime urijali wako kwa kupiga puri na amanda,
mi ndio Corleone wa hii kitu bwa mdogo kama hajasanda,
mi jenerali wa depo we kuruta kaza mkanda,
natimba hata pande zenu mi narule kila kanda,
si hapa hata english forum mistari yangu imemanda,
jaribu kunistudy kwanza we njuka we salamanda

#4 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 12 December 2006 - 05:20 AM

jaribu bwa mdogo ntakusafisha ka sabuni taratibu
mjukuu budi kutoa heshima kwa babu kabla sijapandisha gadhabu
Mc kinibu tubu sababu huwezi dandia mbele ya hili merikebu
ntakutoa kwa tko na hili kelbu lishapimwa kimahesabu
ucpime jawabu wakati unakuja kigubu kikubwa naharibu ndowang wajibu
hakuna kutegemea jibu zaidi ya kelele kutoka kwa Mc Bubu
huwezi fikia hivi vitabu vya mashairi usitafute lakukusibu
wajibu hodi kabla karibu ucpime majaribu ndo tabibu nikutibu
aibu mkwara wa dubu kwa mtu mtukutu sawa na kibaraka cheupe kwa waarabu
ucpime gadhabu nikufunze adabu unakuja kimaswali au unasaka majibu
nakuja kiajabuajabu natibu kistaarabu kila sampo ya matibabu
kaza mzeee nisije kukurudisha kwenye muziki wa taarabu

#5 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 12 December 2006 - 06:08 AM

michano, kibano, hapa ndo utachopata,
we bishoo levo hizi lazima uchezee mambata,
last dyte,last nite,ndo ulichuja kama mc lyte,
huna lines hauko tite,we ni bingwa wa kubite,
naona unafeel sana muziki wa mwambao,
we paka mapepe, kicheche, sasa nakupiga bao,
mi ni doa la grisi kawasafishe hao hao,
hapa sichomoki kirahisi kwani nishakaa mkao,
sina ugonjwa wowote labda we ndo mwathirika,
na usuker mc ni ugonjwa mbaya usiotibika,
tafuta wachovu wenzio sina msaada kwenye ubovu wa kipaji,
kuniamkia saa kumi na mbili hakutokithi yako mahitaji,
nshakuambia ntawalaza macho wazi kama makoro,
we njere usijipimie kwangu utaonekana soro.

#6 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 12 December 2006 - 08:49 AM

hamaki ka haya mabaki ya vina makapi
kushtaki kutaka haki ya mafake kwenye Mic
hakimu siwaachi nahakikisha hambaki
hii ndoano haiachi najua we ndio samaki
varangati la chambo kitambo humudu mikikimiki
we mamluki geuka nyuma mindio nyati toka nduki
hasira hiz zitakuacha mweupe ka mwizi na kabati
ukibang utaitwa hayati fariki bila harakati
kivina daily napanda ka hela ya Mwai Kibaki
endelea kusadiki kwenye Mic sishikiki ka uriorushwa mkuki
sibanduki jiingize kijingajinga kutana na kitako cha bunduki
nashambulia navina ka ushirikiano na mapambano kutoka kwa nyuki
adui haruki hiki kizingiti we ni hiphop msaliti
nakutreat ka wakinamama wenye saratani ya matiti

#7 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 12 December 2006 - 10:28 AM

Uushaanguka sasa checki nnavyokuruka,
nshakushikia chini huwezi kukukuruka,
kama ulidhani una vina sasa ni muda wa kushtuka,
usipofikiri utakesha kwani ushazoea kubwatuka,
mi ni mi sijifananishi na chochote hilo kumbuka,
ili next time ukiibuka usije ukaumbuka,
ushajua huna kitu long time ulishaanguka,
sema unajikamua hadi mavi usionekane umezinguka,
niko kwenye higher levo zaidi ya teja aliyefuka,
dhoruba yangu ni kubwa zaidi bahari iliyochafuka,

#8 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 12 December 2006 - 12:30 PM

usiogope umekutana na Mc ambaye ni Dope
muda wowote kokote naripuka mahala popote
haina kushtuka labda kitete cha muuza kete
nasafiri kibwete ona vina ka msafara wa Kikwete
usjaji kipaji na uasi wa kijiji kwa kufoji kitongoji
sa unakurupuka unaforce mzuka chezea hii sumu zaidi ya nyoka
hapa ndo nazidi kutibuka kuliko stimu za walevi wa labuka
tafuta mwamvuli hiki kimbunga kinagonga nyote wajingawajinga
we habari zilizotufikia mi ni mharamia ucpime nibora ukaangalia
tafuta njia ya kukimbia am the most wanted ka stimu za bia
nshakuacha nyuma ka mkia kimbia ghalika tafuta nyika usijeumia

#9 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 13 December 2006 - 06:15 AM

we dope sawa sasa checki ninavyokusmoke,ukipanda na mimi ni lazima utachoke,
sema kibaya we full kushabu stock yako haina vichwa,
masucka mc huwa nawatema hapa daily wanafichwa,
sina woga wala kitete nikiona mc shoga,
nshakushikia chini na utatambaa kama boga,
unapata hasira sababu ana njaa ya mashairi,
sijakuonesha jinsi nilivyo hapa nachana kibahiri,
ukweli uko wazi zaidi ya kuwa dhahiri,
mcz wenye magovi kama we nawatahiri,
endelea kupeleleza hadi unijue kama msoto,
huna mkia hapo nyuma nipo kukupelekea moto,

#10 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 16 December 2006 - 01:19 PM

Mc muongo nakuzawadia huu mti nibora kuendelea kunipa salute
Kaza buti hii kwako ni zaidi ya nusu kaputi
Endelea kunipa saluti kwani right now unachoface ni mauti
Nakuongezea a.k.a hayati huwezi hiz varangati
Mashambulizi hewani salimu ardhini ukisoma hii content
Umevamia kijingajinga hii ndio hasira kuliko nyati
Endelea kukaa mbali na hiki kizingiti bado nakuona kirhymes we ni anti
hizi beti wewe bado ni rap student jifiche au full kunyuti nakutoa baruti
Isharipuka stuka hii ndio tamati hiz rhymes ogopa ka nakulawiti
Nakudhibiti wewe ka msaliti unayepinga zangu harakati
Nshakuweka mtu kati unakuja na manati pambana na vagi la wamang’ati
Mbinu zakiasilia sihitaji kukujua nakuona unavyolia mabao kivina nakumiminia

#11 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 18 December 2006 - 05:26 AM

ukivimba kwa hasira ni lazima upasuke,
ukijifanya unanata ni lazima ubanduke,
lugha chafu haiongezi uzito wa rhyme lazima uandike,
kunibattle mimi lazima kimistari uchapike,
kuruta hupewi saluti hapa lazima uadhibiwe,
nusu kaputi kwangu stimu we mama hapa lazima uibiwe,

#12 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 18 December 2006 - 07:06 AM

endelea kusiz kistimu hiz rhymes ndo yako sumu
jilaumu mtoto wa mama hapa nakuhukumu
utaogopaje stimu wakati mwenyewe umegongea ndumu
how come bitoz kwa mwalimu unaforce kutia timu
ntakuchapa hapa hudumu nakumwaga ka kademu
humu kwenye hiphop gemu mi nakuona ka marehemu
niogope mnajimu najua mzuka wako ni wa msimu

#13 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 22 December 2006 - 11:40 AM

nilikuchunia sababu niliona uko mwezini,
sasa inama vua chupi na kaa tayari kuzini,
na rijali wa hip hop mi naonakana jini,
popobawa lililotumwa, fake mcs kama wewe niwashikie chini,
nilianza kumoka kabla hujajua ganja ni nini,
kufanya mistari hata sikumbuki nilianza lini,
na nazidi kuwa mkali kila sheikh akiadhini,
yaani mara tano kwa siku zadi yako na sijui maana ya dini,
mi ni kama pombe ambayo wengi hawaamini,
kwamba nina madhara mpaka wapoteze maini,

#14 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 04 January 2007 - 06:07 AM

mtoto naona unataka kujiunguza mwenyewe na haya maji ya moto
we angaika mi natisha kuliko zako ni zaidi ya ndoto
unajijua ka wewe wack mc ukaamua kuniita mimi ndo mc
nshakuvuta kitambo kwenye lensi kuruta huruki hii fensi
b-newz nakuona bado mgeni hapa AHH! mpaka zako tenzi
zinaelemewa na usingizi njozi kaza mtoto toa upuuzi
unasaka ujuzi mpuuzi kwenye bar mimi ndio lako buzi
mjenzi kwa nyie wote washenzi nione zaidi ya mkufunzi
kwa wote mnaolegeza bora kukaza hapa nawapoteza
mi ndo hisia za giza ukija kikei kei ntakuumiza angamiza

#15 breakingnewz

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 111 posts
  • LocationTanzania

Posted 04 January 2007 - 12:09 PM

mimba niliyokupa inakuletea baby blues,
ulibugi pakubwa kumess na breaking newz,
nachoona ni mc aliyebanwa na anasaka excuse,
choka kiryme akili yako imeshachoma fuse,
umejiunganisha kwenye mamegawatt ya hatari,
fungasha AHH inakutakia njema safari,
buriani marehemu ulitufaa sana,
tulipotaka kufunika na mc mbovu kumchana,
upungufu wa tungo za maana umekuuwa,
huna kitu we ni mweupe kama umejichubua,

#16 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 05 January 2007 - 03:10 PM

bado niko kitaa ani nastunt kiujanja
kiranja uwanja huu wang naona ganja
inakupunja upeo kutoona mwelekeo
bwamdoo go tokaa ume potoka unapotaka
ruka shimo futi sita mwamuz mwenyez
na katika hii ni mii huwez kutii bas nii kwa
goo tii! nakucheki..................................
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users