[b]NJOO JIPIME USINIPIME[/b]
#1
Posted 07 December 2006 - 07:10 AM
mi ni mkali ukija kiboya unakalia sime,
nimesheheni skillz za kuua ten crewz,
unadhani kwa nini wananiita breaking newz,
navamia hata kama ikiwa zamu yako,
hata iwe watengwa,choka mbaya ama nako,
nawanyea kama mtoto anayeharisha,
nikibang hewani wote wataahirisha,
mapinduzi ndo haya wengine mumeyauza,
mmegeuzwa malaya waliochoka maajuza,
wote walioshallow ni muda wenu kukacha,
kwa hizo speed zenu gemu yenu future, muthafuckaz :arrow: :arrow: :arrow: :arrow: :arrow:
#2
Posted 25 January 2007 - 07:35 AM
Rhyme zangu si nyepesi kama mamba akiwa mtoni
Nakupasua kichwa huku sikuangalii usoni
Nakufanyishia peke yangu, yaani man alone
Usifikiri kwamba nasema tu, nenda kamuulize Boni
BN tulia,kamalize kazi jikoni
Nimepata breaking news, ati we umeolewa Mtoni.
Rhymes zako kama za brandy,zatufanya watu tunakuwa horny.
#3
Posted 25 January 2007 - 04:01 PM
levo ambazo nachezea wewe utatoka kapa,
umekosea nilikuwa namla dada yako kiwanja,
soon utakuwa shemeji lazima nikupake wanja,
usiogope mi kidume na sihanyi kukupanda,
nikupige danadana mpaka utapovaa sanda,
kinachokusumbua bado unahara,
ujanja huna kwako kitakachofuata ni tohara,
MAALLLAAAYA
#4
Posted 01 February 2007 - 08:50 AM
niko mbele nione ka kibla sio Juma Necha
vyangu vina vinashabihiana kama mapacha
sio ka wasanii ni kizazi ndani ya jamii
kichwa panzi muda wako sasa amri kutii
mi ndio lako jinamizi ntakuwewesesha ka chizi
endelea kusizi mchizi ushanyolewa kivuzi
wakenya wanakuita kimanzi tz bado kijakazi
mdwanzi wa juzi nakupoteza kwa hizi tenzi
piga tizi mi ndo tiba na huu ndo wako mwiba
#5
Posted 05 February 2007 - 08:15 AM
kama hip hop ni ajira we bado upo kijiwe,
stuka check nao usije kujiua,
ntakuchana line ambazo hujawahi kujua,
we si necha ila ni mgambo umekutana na brigadia,
huna lolote na ni fake zaidi ya noti bandia,
vaa kitenge kisha jiunge TNG upige makasia,
cheza ragga na ishia huko huku utachopata ni ghasia,
kimbia.....
#6
Posted 07 February 2007 - 05:07 AM
pimbi kimbia kwenye kandanda mimi nione bambi
umevamia kambi ya mjeda nakuchoma ka utambi
nakutimua ka vumbi nakuzamisha wewe ni mtumbwi
mi ndo maji nakulewesha mpaka unakuwa bwii
tumboni nakulisha vina mwanana unatokwa kitambi
mc unaepeapea mi nakuona ka kumbikumbi
kwenye hii kitu nanata kuliko hata gundi
ka nyundo na mafundi au sanasana mlevi na mitungi
hiki kipande chakuletea kwikwi kinachofata nduki
huwezi zuia kasi ya bunduki huku nshafyatua lock
hubaki kwenye hii ajali hata ukisali huchomoki hutoki.
#7
Posted 07 February 2007 - 08:09 AM
cheza unavyoweza utaishia kujirubuni,
nakufanya utage kirhyme kama mbuni,
na maana upate zero ama disco au kapuni,
ukibwatuka mimi nalipuka stuka,
na hii mistari ni kama fimbo nazidi kunyuka,
kama kaptura nakuacha umetatuka,
kama unajiona fresh nakuacha umechachuka,
ni zaidi ya nightmarez, mcz navyowatisha,
zaidi ya bunge la leo ninavyowakalisha,
nakuacha umesinzia ukitaka kuniamsha,
umekosa joto ntakupatia niweze kukuchangamsha
#8
Posted 09 February 2007 - 06:16 AM
kunywa huu mkojo huwezi marathoni una mkongojo
style yako ni hiphop jojo nakuuma ka ndorobo
niite kiroboto nakupelekea mioto hata kwenye joto
ukanda wa baridi kutana na gaidi budi kusanda
huku ukipigiwa vinanda nakuchezewa kama kandanda
nakuja kama kioja mtoto sina kionjo bora kukaa chonjo
hii kwako iite chanjo nakutoa kwenye game ka banjo
hufai vina hivi vinakukaanga kwenye karai
nakutoa ka moshi wa fegi nakumeza fasta ka pegi
#9
Posted 09 February 2007 - 10:48 AM
ukiondoka hujazima basi jua utaangusha,
check nao machizi bukta wasije kushusha,
maana kama si hivyo jua lilokuokoa busha,
mi ndo maskani ya mistari si unataka nikunyongee,
hamna khaki kitu ziggy lazima angani upotee,
kula moko kisha sepa usiuze sura usiongee,
nakuacha solemba mateja wajipendelee,
ulidhani ganja dry noo kitu mixer plumer,
line moja tuu colombo inaleta drama,
umeonja pombe kali halafu unamwita mama,
umegongea mwenyewe mistari halafu unashika tama,
#10
Posted 09 February 2007 - 10:49 AM
ukiondoka hujazima basi jua utaangusha,
check nao machizi bukta wasije kushusha,
maana kama si hivyo jua lilokuokoa busha,
mi ndo maskani ya mistari si unataka nikunyongee,
hamna khaki kitu ziggy lazima angani upotee,
kula moko kisha sepa usiuze sura usiongee,
nakuacha solemba mateja wajipendelee,
ulidhani ganja dry noo kitu mixer plumer,
line moja tuu colombo inaleta drama,
umeonja pombe kali halafu unamwita mama,
umegongea mwenyewe mistari halafu unashika tama,
ni msala utahama,
#11
Posted 12 February 2007 - 09:27 AM
uhalali mistari sio habari baraza mwanamwali
nyembamba sigara kali jabali nakuwa mkali
mripuko mhanga ka bali maiti tofauti saluti
bamba mc shuti kuruta vuta hii mic umbuka
monka kubabake toka mastaili nyoka fufuka
zika kifudifudi budi lala msala huu domo jalala
takataka uchafu vina zinifu sio bifu neno toka kwa mfu
ongea potea ka upepo mc huu ndio mzuka pandisha pepo
nagonga mlupo kolo kihoro huelewi usiku mchana mi popo
#12
Posted 12 February 2007 - 10:12 AM
watazunguka kwenye maduara kupima hiki kipenyo,
watajiita wanyonya damu wakitaka kwepa kifinyo,
watatishia hata kuibuka na hawafiki yangu mabinyo,
njaa ya mistari makinda wanang'ata nyonyo,
ukibeep nakuweka hewani ukizama sio onyo,
ufanisi ua udadisi, umahiri au oroho wa fisi,
nadhani wenge la ibilisi ndo huwavuta kunidiss,
wananiona lundenga wanavyonifuata hawa mamiss,
wanaona zimefika kipenga walidhani itakuwa rahisi,
#13
Posted 12 February 2007 - 01:17 PM
baki hukohuko huu ndio muungurumo jifiche kuliko mbilikimo
hiki ndio chuma cha reli kwasasa umefikia kikomo
zione falsafa huu msimamo unakuletea maafa
unaniona kinara kwani sioni tabu kumkumbatia miss mwenye papara
nakuchafua niite tope vilevile unanzingua ka demu mapepe
kimbia kila nnapotema hizi hasira vimba ka unga wenye hamira
nakujia kinyapara piga kelele kama navunja bikira
nakuona huna dira darubini langu lishakuvunja dhamira
mc unamwagika ka mtu anayehara piga yowe ushatolewa kafara
kimashairi nshakuchukua msukule afu bado nakuona mndendeule
#14
Posted 13 February 2007 - 07:34 AM
ajuza kubonga umbea ryme nyepesi ryme kejeli,
nakuchana ka toilet paper kisha nakuchambia,
ina maana kiss ma ass halafu kisha kimbia,
sioni lolote ulonalo zaidi ya hadithi mama na mwana,
siskii kitu chochote ila naumaliza uamana,
huu ndo wako mwisho mc, no missy fanya hitima,
ulichojaa vitisho line zisizo na hekima,
nakukachisha full speed hata ardhi ikiteleza,
nilikuonya usinibeep sasa utanieleza,
una ndoto za kuwa matawi mi ndo jua linalokulisha,
naweza fanya ustawi na naweza kukukausha,
ila kwa sasa acha tu nizidi kukujambisha,
usije maaliza mistari yote ushindwe kunijibisha.
#15
Posted 15 February 2007 - 08:27 AM
huna aidia umelala fofofo afu bado rhyme michosho
mwisho wa kifo chako hizi silabi zafanya hitimisho
hubaki angalia nakugeuza upande wa pili wewe samaki
nakana ufanisi wako umekutana na kitako cha bunduki
nakufinya nahizi rhymes kunywa lazima utakunya
piga tizi bado nakuona unakimbia kwenye utelezi
nakupa tenzi nakukonga na konzi lemaa na njozi
nakutreat ka mgonjwa wa kizazi yaani unahitaji malezi
nakusambazia gundu kivina nakufyeka niite mundu
hii ndio alert nyekundu mchana tambaa hapa utasinyaa
nshakurubuni kuliko ibilisi afu bado kabisa huwezi kunifesi
#16
Posted 15 February 2007 - 10:12 AM
we tako la bunduki hufyatuki huna risasi,
hiphop igekuwa mama wewe ni kitindamimba,
unajidekeza kwa battle laini unajiona umevimba,
utabaki kuwa the last muda wako uko past,
ninge, nta, ndo line zako ka kingasti,
ana ana do bora uimbe kidali po,
au uungane na H bubu upoteze po..,
line zangu kwako ni meli kwa jinsi zilivyo kubwa,
usishangae zinaelea mazee zimeundwa,
na kichwa kila kukicha kinakuuzia maumivu,
huzitaki mbichi hizi au umechoka kusaka mbivu,
kwangu beef ni isiyova napenda niile nyekundu,
nashangiliwa unazomewa hapo ni nani mwenye gundu,
majibu yako wazi yanajiuza kama malaya,
wa buku na jero jero ndo maana unagwaya,
levo zangu za blade nachinja mavampire,
hii ngome kuingia huwezi ni bonge la empire,
we ni the last mi ni 1st emperor,
ingekuwa nywele nikunyoa rhyme zote umebaki na kipara,
usije kwa papara,hapa utahara, tulia kama morani anayafanyiwa tohara,
#17
Posted 15 February 2007 - 11:52 AM
mi natisha nasonga mbele huwezi kukwepa hili gharika
unapaparika mi ndio mafuta ya moto bado nakubanika
nakukaanga kitenzi za chaka hapa utatokwa jasho la kwapa
nakuchapa kwa mademu ni kipapa unajiona ngalawa mie papa
nakutoa ka sadaka maafa hapa ushaanguka ka gonjwa lakifafa
levo za kifilosofa we lofa hiz falsafa usishangae unakufa
mi ndio swadakta we kuruta ona nakurusha mikwata
mashairi hapa utapata yani kivina lazima urushwe tuta
programu hii ione ka mkurubita usisizi skani majita wataruka ukuta
hichi ndo kichwa kinakutafuna kuliko mchwa
kila kukicha unaibuka na ndoto ka alinacha hapa game utakacha
nakuona huna thamani ka hela iitwayo kwacha vitani hujiamini
ntakung'arisha na vina utapendeza kuliko hata queen
angalia utapendwa kuliko hata madini masela matakuvutaga ka majani
mjomba nakugeuza sahani nakuosha nakurudisha barabarani ka ombaomba
huwezi kufikia huu mzuka latest nlizonazo unalia nakuchoa ova jua
unaungua na vipande ntabaki kuwa last ila we ka changu haya twende!
nakulewesha nione pombe na hii pigo lako kwenye chembe ni kimbembe
shairi lakata liite kiwembe aibu kwenye game unatumia nguvu za pembe!
nakulima ka jembe mii mkulima nakuuma vitani nakurudisha nyuma
nshakuteka kiakili wewe ni mtumwa nakupoteza fastafasta
nakufunika ka plasta nakuacha wazi ka muhubiri toka kwa pasta
niite masta na hili verse kwako ndio disasta!!!!
#18
Posted 15 February 2007 - 12:33 PM
nshakuambia kitambo unajipima usinipime,
hujasimama long time nshakukalisha kwenye sime,
nakung'oa kwenye stence nablow kama upepo wa same,
wapi na wapi mafuta kuchemsha jiwe,
nakuweka roho juu unabaki kusema lolote liwe,
ni kama bush hunishindi bila kujitoa mhanga,
falsafa za nepi utajinyea we mtoto mchanga,
nasikia kilio chenye njaa ya mashairi,
sina cha kuchukua kwako maana ushavikwa tairi,
umebakia majivu kumbukumbu iliyokosa umahiri,
omba mola ufufuke labda hapa nitaghairi,
sioni verse labda marudio ya tetesi,
sikujua we ni mlaini hivyo nakutafuna ka fenesi,
bora mi kuruta mbali na we korokoroni,
hii mistari ni majabali ninayo kutupia usoni,
ogopa nakuumua mpaka nione huoni,
kimistari nimekukamu na ninajua huponi,
unaishi matesoni kwenye ulimwengu wa kusadikika,
hutofika peponi mabawa huwezi kujibandika,
#19
Posted 15 February 2007 - 01:29 PM
nshakuacha ka moshi wa eksozi katika nyika
lazima uhangaike ka mimba kwa mwanamke
miezi tisa hapa staili hii bado inakupapasa
hii kinasa nakupiga msasa kwasasa na hasahasa
kukua mie kansa nakugeuza kitoweo we nsansa
we bush mie osama hunioni machoni nimepiga pama
omba kwa maulana nshakana wako ufanisi
kaza buti iliuweze kunidisi ucforce huwenifesi
kasi hii mikosi natimba mjomba ova fidifosi
punchline huniwezi hauingii akilini
yaani uko wazi mzee ka wavaa vimini
siwezikujipima kiwete huwezi panda huu mlima
utaishia njiani rudi nyumbani ukajihami
hapa utayeyuka mwenyewe ni kama koni
mie upepo mkali nakupagawisha ka mapepo
bwamdogo bado kuruta ndani ya yangu depo
we ndio mweupe pee! man nakuona mkorogo!!!!!
#20
Posted 16 February 2007 - 07:34 AM
kama unasubiri kuja nishinda utazidi kungoja,
huna chochote real we ni bonge la foja,
unajaribu kutumia nguvu na ubongo usio na hoja,
hii ni real world naona bado uko kwenye njozi,
utachezea kichapo cha rhyme kama mtoto kikojozi,
nakufanya uabort rhymes kama rift valley fever,
kimistari nina noti we umebaki na visilver,
siwezi kukufesi kwa sababu sikuoni,
nishakufanya uwe mdogo huonekani kwa mboni,
unajijambisha na hujui haupo chooni,
unarudia nilichosema nishakukalia kooni,
siwezi kusadiki hata dini mi siijui,
nakuharibia pande zote sita au ndo tuseme hugundui,
usijifananishe hivyo we bado ni kichuguu,
huwezi kukimbizana nami ushakatika miguu,
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












