Hii topi ni moja kati nyingi tu ambayo inazunguka kitu kimoja, utamaduni wa mtanzania. ..utamaduni wa mtanzania ni upi..? Tukitaka kuujua utamaduni wa mtanzania halisi labda turudi nyuma kabla hata waarabu hawajaja bongo.....na wakati huo hakukuwa na kitu kinaitwa Tanzania....
Sidhani kama kuna vazi lolote unaloweza ukalinyooshea kidole ukasema lile ni vazi la kitanzania ..yote yana asili ya nje ...ukienda club ukamkuta sistadoo anakimini....poa kimetoka ulaya ..ukienda sokoni ukamkuta dada amevaa kanga...poa... kanga imetoka uarabuni ..ila imezoeleka tu kwa sababu imekuja zamani na vimini ni vigeni kwa hiyo vinaonekana mambo flani....
...kwa hiyo mimi sioni kama kuna vazi lolote lile ambalo artist wa kibongo anaweza akalivaa na akasema hili vazi ni la kibongo ....labda lubega la kimasai....kitu pekee ambacho sifagilii ni kwa artist kupanda jukwaani akiwa amevaa t-shirt oversize na limeandika kifuani NEW YORK, CHICAGO BULLS au kitu kama hicho....hiki ni itu pekee ambacho zikifagilii lakini vingine vyote mimi poa tu simind wala nini.
UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)
Started by Guest_soulrebel_*, Aug 27 2002 08:32 AM
42 replies to this topic
#41 Guest_bond007_*
Posted 22 March 2003 - 01:14 AM
#42
Posted 23 March 2003 - 06:15 PM
Bond ni sawa hayo mavazi yamekuja Bongo kutoka nje lakini ukiangalai hakuna jamii yoyote ambayo haiazimi kutoka jamii/utamaduni mwingine actually hiyo ni necessary kwa maendeleo katika jamii yeyote. Ila kwa sasa hivi ni swala la kitu gani huwa kinakuwa identified na jamii/utamaduni/tiafa fulani? Kwa mfano nguo za batik/dashiki zinawakilisha zaidi africa (hata kama nazo zilikuwa borrowed zamani kutoka sehemu nyingine) Nguo nyingi za west Africa at some point zilitokea sehemu nyingine (at least mitindo) lakini sasa hivi ukimwona mtu kapiga kente moja kwa moja unajua katokea eneo gani!Hata kama staili hiyo ilikuja zamani kutoka Arabuni lakini sasa hivi mwarabu akivaa yeye ndio anaonekana kaazima vazi hilo...ni swala la nini kiko associated na jamii husika katika muda huu. Sidhani ukivaa FUBU kuna mtu ata associate hiyo na Bongo badala ya Marekani sijui unanipata point yangu? Mimi nadhani identity ni muhimu sana hususani kwa wanamuziki wanaoimba lugha tofauti na kiingereza tena sana sana wa africa ambapo promotion ni bomu...uvaaji/utamaduni ni mojawapo ya promotion tena isiyogharimu pesa nyingi. Watu wakimsikia mkali mmoja au wachache tu kutoka bongo halafu wote wana kitu kinachowafutisha na katika case hii mavazi itawafanya na wengine nao wapate mwanga kidogo maana binadamu tunatafutaga kitu kidogo cha kutuwezesha kutambua au kukumbuka....ni kama wale wadudu wenye rangu kama za nyuki ingawa wao wenyewe hawaumi...wanajua ukiumwa na nyuki mmoja basi utawakalia wote mbali!That's my point...identity ni muhimu sana kwa siye tusio na multimillion dollar promotions!People follow trend huwezi kujua kama wanamuziki wetu waki hit vibaya unaweza kushangaa soko la nguo za kitamaduni linapanda sana!...opinion yangu tu!
#43 Guest_used to be ambax_*
Posted 04 April 2003 - 07:21 AM
am sorry j4 ...iam so in trouble with those posts in this battle page.naomba uondoe message zangu zote zenye lugha mbovu samahani sana AM STILL DIONG HIP IN A MAD WAY lakini hizo lyrics zime nikharibia mabo yangu.
aafikiri tutashirikiana vizuri kwa hilo.
thanks in advnce.
ambax
aafikiri tutashirikiana vizuri kwa hilo.
thanks in advnce.
ambax
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












