UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)
#21
Posted 07 September 2002 - 08:17 AM
Mimi ningefurahi kama mngewapigia kelele hawa jamaa wanaogawana kodi yetu kwa kujinunulia mashangingi na ndege za gharama,pamoja na rada ambayo matumizi yake hayako tanzania.We Mkuki hebu angalia hao wabunifu wa mavazi watatoa wapi malighafi wakati viwanda vyote vya bongo vinauzwa kwa wageni kama sio kufungwa kabisa.Unategemea mchina aje autukuze utamaduni wako?
Juzijuzi tu hapa wasauzi "walopewa" kiwanda cha bia walikuwa manataka kutikisa kiberiti.Eti wanataka walete shayiri toka kwao kuja kutengenezea bia bongo.Tanzanite inachimbwa Bongo lakini Kenya wamezawadiwa boeing kwa kuwa wazalishaji wazuri wa Tanzanite,Kwa mtaji huu kwa nini msiwabane kwanza hawa jamaa waturekebishie maswala ya uchumi?kwasababu tukiwa fit kwenye mambo ya uchumi tunaweza kuanza kuongelea maswala hayo ambayo kwasasa ni ya kufikirika tu.Bado naheshimu sana mawazo yenu.
#22
Posted 07 September 2002 - 03:37 PM
Mimi kuna kitu kimoja huwa kinanisumbua kuhusu sisi waafrika nacho ni organization mimi nadhani hili ni tatizo letu kubwa kuliko hata hao viongozi (ingawa sifikiri viongozi wote ni wabovu) sisi kila siku tumekalia serikali hivi serikali vile...sasa hebu tujiulize kwa dk moja...je ni nini ambacho sisi tunafanya kwa nchi zetu/bara letu?Sio siye ambao tunakaa maofisini tunapiga soga siku nzima?sasa hapo nani alaumiwe serikali?Sio sisi ambao asilimia zaidi ya hamsini ya wenye uwezo wa kuzalisha hatuzalishi?(nikimaanisha productive population) Tumekaa tu kulalamika ajira ajira serikali hizo ajira itazitoa wapi kama uchumi wote kwa ujumla uko chini?Mimi huwa najiuliza hivi wasomi wanne waliomaliza digrii zao UDSM katika nyanja tofauti kwa mfano mchumi, business administration, sheria, na engineer au labda computer scientist hivi hawa hawawezi ku network wakajiajiri wenyewe?nikimaanisha hawa ni watu waliosoma lakini wao wanafikiria kuajiriwa...nchi hizo zilizoendelea ni sekta binafsi ndio inayoajiri watu wengi zaidi na sio serikali na hata marekani yenyewe ina tatizo la unemloyment. Hao jamaa wanaweza kuanzisha biashara yenye mafanikio kabisa kutokana na ujuzi wao na kwa sababu wamesoma wanaweza kuwa na proposal nzuri ya kupata mikopo au sponsors kutoka hata nje ya nchi kwa ajili ya kuanzia. Sasa fikiria tunge create ajira kwa watu wangapi kama wengi wangefanya hivyo? Vitu vingine ni sisi wenyewe tu kubadilisha jinsi tunavyofikiri maana kama umeona serikali haikusaidii unafanya nini kujisaidia mwenyewe? Tumekaa lawama tu wakati unasikia "duh jamaa alikuwa meneja lakini katoka kabwela tu wala hajaiba, kweli huyo mpumbavu" sasa kwa attitude hiyo ya nikiingia lazima niibe je kweli uchumi utakua? Kungekuwa na uwezo wa kukusanya takwimu mimi nina uhakika kabisa kuwa raia wana more to blame kwa sababu na wao washaamua kutosaidia chochote! Kama baba yako kaamua kuto provide home wewe utakaa tu ufe njaa au utaangalia njia ambayo unaweza ku generate income ili usaidie na wadogo zako? kama utakaa tu ulaumu basi utakuwa mwendawazimu na utakula lawama zako!Hakuna nchi ambayo viongozi hawaibi bwana tofauti ni kuwa kuna nchi ambazo raia wanafanya kazi (na Tanzania sio mojawapo!) na hii ndio haswa sababu ya mimi kutokaa nalaumu serikali maana najua haitabadili kitu!Wewe jiulize kwa nini vijana kibao wabongo wanaondoka nchini wanaenda kusoma nje halafu hawataki kurudi nyumbani. Kinachoniudhi ni kuwa hawa ndio wamekalia lawama tele ooh bongo hivi bongo vile! mimi nawauliza wewe na PHD yako ya political science unafanya nini huku marekani kama una uchungu si uende ukagombee uongozi basi ili ulete hayo mabadiliko unayoyataka? Hii ni typical attitude ya immigrants na inanichefua kishenzi kwa sababu ni hao hao wanafiki ambao hawana huruma kwa ndugu zao kwa sababu wao sasa hivi wanapulizwa na kiyoyozi na ameoa mzungu basi amekalia kulaumu tu wakati yeye ndio yuko kwenye position nzuri ya kuleta mabadiliko!Sasa mimi nauliza nani alaumiwe? nchi bila nguvu kazi hata ingekuwa na uongozi bora vipi bado ingekuwa masikini?labda iwe ya kidikteta ambapo watu wanafanyishwa kazi kwa mtutu wa bunduki!think about it!
Sedon unaona jinsi tunavyoenda nje ya topiki? Anyway turudi kwenye hoja au tuanzishe nyingine kwa ajili ya majadiliano haya tu maana bodi yenyewe hii ya HipHop tusije kuwaboa watu hapa!mida!
#23
Posted 08 September 2002 - 04:09 PM
#24 Guest_soulrebel_*
Posted 12 September 2002 - 09:15 AM
#25 Guest__*
Posted 12 September 2002 - 03:49 PM
Sina hata lakusema manake naona vichwa vinesha cover kila kitu kama vile soulrebel...mkuki...n.k yani menifurahisha sana kumbe bado kuna watu.
Lakini nikija kwenye hiphop mimi nadhani nguo sio zakulaumu, kwanini. Kwasababu hiphop "is the way of life, its how you live" sasa kama wewe kweli ni mvaaji kimasai kila siku ya maisha yako basi keep it real na nguo hizo lakini kama wewe unavaa ma fubu kinyumbani basi rep hivyohivyo.
Ila tatizo ni kuiga uvaaji wa nguo kama vile suruali kuzishusha chini yani mkundu wote nje hiyo haina aja kusema kweli au vipi masela. Kusema kweli mimi mwenyewe na changia topic lakini sijavaa kiasili na hiyo sipendi kuanzia sasa ni str8 roots...mtu anielekeze wapi nitapata vazi laki tamaduni lakini sio lawazi wazi mno sitaki kutembea uchi.
#26
Posted 12 September 2002 - 06:43 PM
Ebwana Guest noma namna hiyo mwanangu sign up basi na handle yako ili tujue wewe nani maana tayari ushakuwa mwenyeji au sio!?
Ebwana unachosema kuwa hiphop ni utamaduni wala hujakosea kabisa unajuwa tatizo linakuja wapi? tena mwenyewe umesema...tatizo liko kwenye kuiga...na mimi tatizo haswa sio kuiga nguo za nje bali tatizo langu ni kuwa tunalemaza "fashion industry" yetu kitu ambacho kwa umaarufu wa nyimbo za kwetu sasa hivi (mf:Bongo HipHop) kingekuwa kinasadia kuleta ajira kwa wanaobuni mitindo na kadhalika. Hiyo ni tukiacha swala la kujivunia utamaduni wetu; hapo tunaongelea tu katika upande wa kibiashara, mimi naamini Hiphop ya bongo kwa jinsi inavyoinukia kwa kasi ita create a whole new economy in itself kama vile Hiphop industry ya marekani. Kinachoifanya Hiphop industry ya Marekani iwe a multibillion dollar enterprise ni kwa sababu hela inazunguka ndani kwa ndani, yaani wao ndio wanatengeneza bidhaa hiyo na tayari wana soko zuri ndani ya nchi yao bila kusahau soko lao la nje ya nchi ambalo na siye wavaa FUBU tunasaidia kuliendeleza!Mimi nadhani kama tungeweza ku glorify utamaduni wetu hata kama ungekuwa modernized lakini kiini chake bado kiwe chetu; in time tungeweza ku create market ya bidhaa zetu humo humo nchini mwetu na bara letu kwa ujumla!Si wanasema charity begins at home? Mimi nadhani mtu unaweza kuwakilisha bila kuvaa rubega...nilitoa mfano awali kama mimi binafsi nina rock shati langu la kiafrika na jeans labda na raba, buti au sandals hapo tayari nishawakilisha. Badala ya kuvaa cheni ya bling bling yenye "ice" ambazo zinawaua waafrika wenzangu huko Angola,Sierra Leone,Liberia na kadhalika ninatinga Neclace yangu ya kitamaduni labda na shaba au mbao, au mfupa uliochongwa vizuri. Huu ni wakati ambao sisi kama watu weusi tuanze kubadili fikra zetu...hizi dhahabu na almasi kama nilivyosema awali zinasaidia kuwaua ndugu zetu Afrika, haya mavazi tunayonunua na huu uchumi wa hawa watu ambao tunausukuma kwa jasho letu na vijisenti vyetu vya ngama ndio huo huo unaotumika ku develop silaha za kisasa zaidi ambazo ndio zinatumika kutukandamiza ili tusiwe na sauti!Watu wanasema hizi siasa kumbe ndio reality yenyewe utajiri wa nchi za magharibi unachangiwa na sisi vilevile kuanzia katika kuwapatia soko hadi katika kuwapatia malighafi...haya nini ambacho wao wanaturudishia? Nada...sana sana wanachotuletea sisi ni matatizo tu na vita kila kona ya bara letu, magonjwa ya kila aina na madhila mengine kedekede...now how is this related to HipHop? Angalia HipHop iliyojaa redioni na HipHop isiyopigwa maredioni na kwenye Televisheni utaniambia kama sio siasa!HipHop ilitupa sauti sisi watu weusi ya kuweza kusema matatizo yetu hence the fact kuwa hiphop ni way of life; lakini ni nini sasa HipHop maisntream inawakilisha? Bling Bling, kukandamiza wanawake na violence...je kweli hiyo ni sauti ya watu wa chini? Nani yuko responsible? Hivi ni vijiswali tu!
Anyway mshkaji ulikuwa unauilizia wapi utapata gear zinazowakilisha ki home! mimi huwa navuta nguo pale mwenge kwenye duka la Afrikasana hawa jamaa kwa kweli wako fiti sio vi batik vya kichovu hawa nguo zao zinawakilisha kweli sanaa...sehemu nyingine ni nyumba ya sanaa ingawa hawa inabidi na wewe uwe na taste nzuri maana kuna nyingine kidogo michosho ila na wao wanajitahidi kuwakilisha!wewe saka saka pale bongo vitu kibao tu!Halafu kama uko nje ya nchi au kama unaweza kutuma vitu mtandaoni kuna site nitakuja kuziweka hapa nimezi bookmark!vitu kutoka Afrika Magharibi (hawa jamaa nguo zao bomba mbaya lazima tukubali!) afrika kaskazini na sehemu nyingine mbali mbali.
Oya mida masela...
#27
Posted 13 September 2002 - 07:09 AM
#28
Posted 13 September 2002 - 08:08 PM
#29 Guest__*
Posted 14 September 2002 - 08:23 PM
[/u]HIPHOP.....HIPHOP inausisha uvaaji pia...ni moja ya element ya HIPHOP...do the Ledge kabla mjaanza kucritcise.....na mavazi yanatakiwa kuwatambulisha wanahiphop popote pale duniani.
salaam
#30
Posted 15 September 2002 - 01:45 AM
Sasa tuende kwenye nilichotaka kuongelea; nilikuwa nataka kukukumbusha kuwa hapa tunaongelea African HipHop (rejea jina la website!) na hususana Tanzanian HipHop (bongo flava) sasa kama tushaamua kuimba kwa kiswahili ili kuwakilisha home sasa wewe huoni kuwa na mavazi yakiendana na home ndio tunawakilisha ipasavyo? Tukiangalia tena jinsi ulivyoongelea kuhusu mavazi ni kuwakilisha je ulikuwa unamaanisha basi hata ku rap iwe ni kwa kiingereza au maana ndio hiphop ilivyoanza si ndio? Sasa hapo tutakuwa tunamuwakilisha nani?
Hilo swala la HipHop as a culture tushaliongelea na hamna anayepinga labda ungesoma post zilizopita ungegundua kuwa tumekubali hilo!Lakini kumbuka kuwa na Tanzanian HipHop is a culture also na ndio maana kuvaa kiafrika kwa mtazamo wangu ingekuwa inawakilisha zaidi!
Lakini mshkaji ninakubaliana na wewe kuwa kuvaa ni element mojawapo ya hiphop ila pia inabidi tujiulize kuwa je element ya Tanzanian HipHop ni nini?Je Ni Phat farm (classic American flava kama slogan yao inavyosema!), Sean John, PelePele n.k?
Mwisho nilikuwa nataka kusema tu kuwa haya ni majadiliano tu sio criticism ya aina yoyote swala la kuvaa ni swala la uamuzi wa mtu ila nadhani watu hapa wanatoa mitazamo yao tu juu ya swala hili...amani!
#31
Posted 16 September 2002 - 01:26 PM
Huyo guest mwingine ni hivi, hiphop haina vazi umesikia hiyo? wewe na mimi ni hiphop. Twende unyamwezini kwanza, uleuvaaji wa mabandana, buggy jeans, head bands, Baseball hats n.k ni street wear siyo hiphop. Sasa muziki wa hiphop is from the streets kwahiyo unaona maemcee wanavaa hivyo kwasababu they are from the streets, sijui nimejielezea fresh au sijaeleweka?
Kimavazi bwana ni hivi, kama kuvaa kiasili poa kama ni kwaajili ya special occasions tu au ndio daily unavyopenda. Manake hata maofisini wazee wote wanapiga masuti na mashati, vimoka n.k ndivyo ilivyo miaka ina badilika. Tulianza uchi tukajua kujifunika majani sasa hivi tunashona vitambaa.
"HIP HOP" HAIANGALII NDUO ULIZO VAA KAMAA UMEPENDEZA AU LA, HIPHOP NI MTIZIZAMO WA MANENEO YANAYO ENDA KWA MSIKILIZAJI. FUNBA MACHO SIKILIZA KWA SABABU NI UJUMBE UNAO MATTER. NDIO MAANA HATA KWENYE MAJUKWA HUONI MAEMCEE WAKI ONYESHA SKILLZ ZAO KATIKA KUCHEZA BALI NI KATIKA MASHAIRI.
NA MA ALL IN ALL NA KADHALIKA, HIPHOP YA BONGO SIOMPAKAA MJIPAKE MIKAA NA KUVAA VIGAGULO ILIMTAMBULIKE, ILE LUGHA TU YA KISWAHILI TAYARI NDIO KIWAKILISHI.
TIZAMA HIPHOP YA GERMANY, JAPAN, SOUTH AFRICA N.K WOTE WANAVAA KAWAIDA TU KAMABINADAMU WA SASA LAKINI KINACHO WAKILISHA NI LUGHA.
***WEWE UNAPO SIKILIZA CD AU TAPE UNAMUONA MUIMBAJI KAVAA NINI? SI UNASIKILIZA MANENO TU? SASA HIYO NDIO HIPHOP****
OYA MIMI SINA MENGI ILA MSIKILIZENI MKUKI ANAJUA ANALO SEMA "SCHOOL THEM BROTHERS" :idea: .
AMANI, UPENDO NA UMOJA.
#32
Posted 16 September 2002 - 01:36 PM
NGUO SIO ELEMENT OF HIPHOP;
BREAKDANCING (B BOYING), GRAFFITTE, DJ'ING, EMCEEING N.K HIZO NDIO BASIC HIPHOP ELEMENTS.
HIPHOP SIO FASHION SHOW JAMANIIIII OOOOOOOOOO.... NADHANI WATU WANA HARIBIWA NA WAKINA NELY NA JA RULE YALE MA BLING BLING SIO HIPHOP NI WAO TU NA UPENDELEO WAO.
MFANO FOXY ANAVYO KAA UCHI, HIYO NI KUUZA TU SIO HIPHOP JAMANIII EEEE... NITAWARUDISHA BACK TO 92' ILIKUWA WEKA MAKINI :x
#33 Guest_mr blow_*
Posted 16 September 2002 - 05:55 PM
#34
Posted 16 September 2002 - 06:44 PM
Nitakupa mfano hivi Album ya Nelly unaweza kuisikiliza constantly kwa muda gani...ukienda kwenye record stores angalia albamu gani zimejaa kwenye used CD section kama sio za akina Ja rule and the likes na unakuta albamu yenyewe imetoka kama miezi mitatu tu iliyopita...sasa niambie albamu ya Dead Prez unaweza kuisikiliza kwa muda gani na nenda tena huko huko kwenye maduka ya muziki uone kama utaikuta kwenye used section (na kama ukibahatika ni bora uinyake hapohapo maana kesho huikuti!) kwanini? Kwa sababu miziki yao inashinda test of time (kitu ambacho kina define sanaa kikamilifu) Ni kama nyimbo za Bob Marley, mimi tangu natambaa hizo nyimbo zinatesa na mpaka leo bado ni noma na ukisikiliza kila siku ya mungu unaona ujumbe una reflect society yaani haupitwi na wakati...sasa hiyo ndio sanaa na real hiphoppers ndio wanawakilisha hiyo sanaa...wako kwenye game kwa sababu ya mapenzi na game na sio kwa sababu that's their way out of poverty!hawai exploit HipHop bali wanakuja ili kuchangia maendeleo ya hiphop, feel me!Sasa Ja rule leo anaimba ana Escalade ya 2002 sasa mwaka kesho hiyo Escalade ishapitwa na wakati kwa hiyo inabidi aimbe kanunua mpya ya 2003 wee huoni hao ni watu wa quick money tu...kuna sanaa katika muziki wao?hilo nakuachia uamue mwenyewe...The American Music Industry can make anybody a rap star ni swala la kuamua tu kuku market ndio maana unaona kila siku watu ni walewale kama ni mademu lazima wawe shepu fulani na kama ni mameni lazima wawe wako wako kiaina fulani yaani kama ma model vile maana wanajua kuwa looks ndio mauzo (plus sex, drugs, gangsterism etc!) yaani ukitaka recording deal usiimbe mambo yanayoendana na jamii yako...wee imba tu kuuza drugs, umelala na wanawake wangapi, kumpiga mtu shaba basi wee ndio bonge la staa kwao!kwa sababu hivyo ndio vitu vinavyouza albums na sio usanii haswa...ndio maana Jay-z pamoja na sales zake na kwenda multiplatinum hata siku moja hamfikii NAS kwa respect in the streets!...wakati mwingine huwa najiuliza hivi nini kilitokea kwa ile definition ya "sanaa ni kioo cha jamii"? duh kama jamii yetu wote tunaendesha ma Lexus na ma BMW na tunatinga almasi shingoni basi labda mimi naishi kwenye sayari nyingine! Kwa hiyo kabla watu hawajaanza ku define hiphop ni bora waiangalie vizuri maana ujue hao wanaowakilisha hiphop sasa hivi ni fakes tu na ndio hawa waliokuwa wanafanya madingi zetu kusema kuwa Rap ni uhuni na ni kweli kama ukiangalia wanaotuwakilisha sasa hivi duh!hata miye ningekuwa kidingi ningeona uhuni tu wee angalia rap videos tu!...mida masela!
#35
Posted 17 September 2002 - 01:37 PM
8)
#36
Posted 06 December 2002 - 05:03 PM
sosa said:
NGUO SIO ELEMENT OF HIPHOP;
BREAKDANCING (B BOYING), GRAFFITTE, DJ'ING, EMCEEING N.K HIZO NDIO BASIC HIPHOP ELEMENTS.
HIPHOP SIO FASHION SHOW JAMANIIIII OOOOOOOOOO.... NADHANI WATU WANA HARIBIWA NA WAKINA NELY NA JA RULE YALE MA BLING BLING SIO HIPHOP NI WAO TU NA UPENDELEO WAO.
MFANO FOXY ANAVYO KAA UCHI, HIYO NI KUUZA TU SIO HIPHOP JAMANIII EEEE... NITAWARUDISHA BACK TO 92' ILIKUWA WEKA MAKINI :x
Lakini hii ninachotaka kusema ni hiki...
Graffiti,Mceeing,D'jeeyain,BBoyin ni zile element kubwa..kuna vi-sub element kama Beatboxin na uvaaji.
Sasa kurudi kwenye uvaaji...kwanza uelewe kuwa Hip Hop na black culture Marekani vinaendana bega kwa bega.
Kwa mfano MKUKI amezungumzia kuhusu mamcee walivyokuwa wanavaa zamani i.e cheni na medali za Kiafrika kwa mfano Afrikan Bambaataa and the Zulu Nation hata ATCQ walikuwa wana rock batiki na hizo beads..
But peep this..hile ilikuwa ni trend katika history ya watu weusi na struggle yao spiritually na kikalcha..kwa mfano ulimuona Rakim amevaa batiki au beads???hapana..
Hichi ndicho kilichokuwa kinatokea:kipindi kile kulikuwa na mabadiliko ya kidini na kimaisha...THE NATION OF ISLAM NA AFROCENTRICITY ndio vilikuwa vinainuka kwa nguvu..wanamziki wengi kama Rakim,Poor Righteuous Teachers,ATCQ,KRS-1,AFRIKAN BAMBATAA ,ARRRESTED DEVELOPMENT na mamcee wengi pamoja na wamerekani wengi weusi walikuwa wafuasi au walijaribu ku-embody elimu hizo katika maisha yao na mashairi yao..AFRIKAN BAMBATAA mpaka leo ni mfuasi wa cult ya kidini ya ki-Afrocentricity hapa Marekani..
Sasa kuvaa kama AB [AFRIKAN BAMBATAA] dashiki,beads na africal medals,RAKIM..nation of islam 7 stars medallions,ATCQ..batiki na beads hazikuwa element za hip hop kusema ukweli bali ni mavaazi yaliyoendana na dini na imani zao...
kURUDI kaitka baggy jeans na mavazi mengine...hii iliingizwa kwenye Hip Hop kwa ajili ya maisha ya kimasikini watu weusi waliyokuwa wanaisha.
Hip Hop imeanzia kimasikini kimasikini na ilikuwa ndio njia ya vijana kutokea mitaani ..kwa hiyo mwanzo wake..Hip Hop,vijana weusi na umasikini vilienda bega kwa bega.
Kwa mfano kuvaa baggy jeans vijana walitumia mitaani walipokuwa wanauza drugs na kufanya biashara nyingine haramu ili kuishi..na mukumbuke kipindi kile..66-early 70's Black Panther Party kilianzishwa na hili kukizidi nguvu bila ya kuonekana waonezi serikali ya Marekani ili "mwaga" crack-cocaine na silaha maeneo walipokuwa wanaishi watu weusi ili wauane wenyewe kwa wenyewe..NA WALIFANIKIWA !
Vijana wengi walifumwa wanauza na kutumia na siasa waliiweka pembeni..Hata mwaanzilishi wa BP mwenyewe alikuwa crack addict.
TUKIRUDI kwenye mavazi..baggy jeans ni hivi..vijana walitumia hizo ili kuficha drugs na silaha..walikuwa wanavaa mpaka suluari 2,3 na kufica drugs ndani kabisa kwa ajili ya "comenti" za polisi mitaani..kwa kuwa vijana wengi weusi walikuwa wanavaa hivyo ikawa ndio kama style yao tena.
Hata hizi AIR FORCE ONE watu wanazozipigia kelele..zilivaliwa ili kufanisisha biashara ya madawa..viatu hivo vilikuwa 1]vyepesi2]cheap..inakuwa rahisi kukumbia polisi wakitokea..watu wanaona style sasa hivi lakini imetokea kwenye umasikini!
KWA HIYO BAGGY JEANS NI OFFICIAL KTK HIP HOP
hayo mavazi mengine na upuuzi watu wanaovaa sasa hivi ni maamuzi ya mtu mwenyewe..hizo BLING BLING,SUTI na nguo nyingine ni kuwa watu wanataka kuonyesha utajiri wao kwa hiyo nakubali kuwa sio mavazi ya Hip Hop ni uamuzi..
p.s nisipojibu kwa muda fulani ni kwa sababu maisha yananipeleka peleka..lakini anyway nitajaribu.
Salaam
#37
Posted 10 December 2002 - 04:10 PM
#38
Posted 10 December 2002 - 05:23 PM
#39 Guest__*
Posted 10 December 2002 - 11:33 PM
mkuki said:
Nakubaliana na wewe..
Salaam
#40
Posted 16 January 2003 - 04:36 PM
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users













