UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)
#1 Guest_soulrebel_*
Posted 27 August 2002 - 08:32 AM
(Ma mcee wote wa bongo: Endeleza moto!)
#2
Posted 27 August 2002 - 09:27 AM
Mida
#3 Guest_Pampukubwa_*
Posted 27 August 2002 - 03:44 PM
#4 Guest_chakubanga_*
Posted 27 August 2002 - 05:15 PM
Pampukubwa said:
#5
Posted 28 August 2002 - 08:04 PM
Mimi kwa mtazamo wangu mavazi ya kiafrika yanawakilisha zaidi...nimekuwa napiga kelele kila siku kuwa dawa ni ku "stand out" kama tunataka kutambulika nje ya mipaka ya afrika mashariki ambako ndio kiswahili kinaeleweka zaidi na mojawapo ya njia ni kwa kuvaa tofauti na mainstream hiphop culture...jamani mtanisamehe kwa kuchanganya lugha ila ndio hayo hayo mambo ya kasumba mpaka tunajikuta lugha yetu wenyewe hatuwezi kuongea na kuandika kwa ufanisi...ngoja nirudi kenye topic...mimi sioni ubaya wa mavazi ya kiasili cha muhimu ni design na wala sio kitambaa gani kinatumika.
Hebu tuangalie hili swala katika mtazamo wa kiuchumi!
Tunaona kabisa kuwa Bongo Flava imekuwa maarufu sana nchini na kwa kiwango fulani inaanza kulipa yaani mauzo yanapanda siku hadi siku kutokana na ubora wa kazi yenyewe!Mimi nadhani hii imechangiwa na redio kuamua kuzipa kipaumbele bongo flava pamoja na studio kuboreshwa zaidi pointi ninayotaka kutengeneza hapa ni kuwa hili swala la kiuchumi linapatikana kutokana na collective effort na collaboration kati ya nyanja mbalimbali za sanaa husika yaani Hiphop inahusisha DJs,Producers,wasanii wenyewe pamoja na fashion...hiki ndio kinachofanya Hiphop ya marekani kuwa a multibillion dollar industry. Kila kitu kimeungana na kinaenda kwa networking nitakupa mfano katika mavazi hayo hayo "hiphop wear" Kina P Diddy na label yao wana endorse "Sean John" Kina Master P na No Limit wana endorse P. Miller Gear, Kina Jay-z na Rocawear, NAS na ESCO, Jeniffer Lopez na J-Lo na nyingine nyingi tu...utakuta kama mtu anamzimia sana Jay-z most likely atataka kuvaa kama yeye kitu ambacho kitamfanya akanunue nguo za Rocawear...hakuna tofauti kati ya hizi nguo ila ni majina ya designers tu na ukiangalia hawa wanamuziki sio designers wenyewe ila majina na umaarufu wao ndio unatumika hapa katika kuuza hivi vitu. Ninachotaka kusema ni kuwa kama tunataka kuzifanya nguo za kiafrika kuwa cool kama hizo Phat farm ni swala la wale watu ambao ni perceived as cool (wasanii) kuanza kuvaa nguo hizi...hapa utaona hata soko la nguo hizo linaanza kuinuka mwisho wa siku tunakuta katika kufanya hivi tunatengeneza industry yetu wenyewe na badala ya kuwatajirisha hao wamarekani ambao hata hawatujali tutakuwa tunabikisha hela zetu zina zikiwa zina circulate kwenye jumuia yetu wenyewe...hizo ni grassroots economics tu, tunalalamika hamna hela,ajira na vinginevyo wakati soko lipo ila siye tumelala tu!Hapa kuna soko la managers, critics, promoters,designers wa fashion, advertisers na mengineo...yote yanategemea sisi kama tunaweza kutangaza sanaa yetu na kuifanya ikubalike...na hivi ni kwa sisi wenyewe kuanza kuikubali!
Wewe Pampu mambo ya matusi ya kizamani sana mshkaji; kama huna hoja unaweza ukasoma tu ukaondoka sio lazima utukane watu...ustaarabu kitu cha bure tu!
[quote]hoya kama ni kuvaa ni kuva aunafanya sana kazi hili uishi sasa nini hata pamba usipige acheni mambo ya ulimbwende hayo hakuna cha kuiga ila ni kujipendezesha bye.[/quote]
Chakubanga ni nini haswa kinazifanya hizo FUBU kuwa pamba na batik au nguo zozote za kiafrika kutokuwa pamba?Ndio hicho hicho nilichokiongelea hapo awali yote hiyo iko kichwani mwako tu hamna chochote special katika hizo nguo sana sana ni za bei mbaya tu wakati zinatengenezwa kwa fraction of what you pay![/quote]
#6 Guest_kizixst_*
Posted 29 August 2002 - 06:06 AM
kuvaa kwingine ni noma, kama kuna mtu anatetea kuvaa ki local aanze yeye kupiga pamba za kihazabe yaani nguo za magome ya miti halafu tumuone street, nina hakika kabisa wote hapo hamuwezi,
kuenzi pamba za kibongo ni muhimu ila zile zisizo kuwa suruali au za magome ya miti ni nmomaaaaaaaaaa,
kama mnamind mfuateni mr. ebbo tuwaone
#7 Guest_soulrebel_*
Posted 29 August 2002 - 09:45 AM
Huu mjadala wa mavazi katika bongo flava (bongo culture-kama ipo) unarandana sana na huo wa muziki. lakini kamwe hatuwezi kuepuka "historia" ya bara zima la Africa, ndio maana mara nyingi napenda kuhusisha historia katika uchambuaji wa jambo lolote lile.
Kwani kumezuka kamtindo ka wanafalsafa (siyo yule mcee) wanasiasa na wanuchumi kuangalia vitu juujuu tu. kwa kifupi tu tumetawaliwa kwa kipindi kirefu na effects zake zimekwenda mpaka kwenye mishipa ya damu! watawala(wakoloni, imperialists, modernizers, postmodernists, globalizers,) na wengine changanya huko wote sawa! wametufanya tusione vetu vya maana, tuko brainwashed(naomba tafssiri ya hili neno) kuona kwamba chochote vyenu ni ovyo. Na mbinu ambayo wantumia,hasa kuanza kuanguka kwa siasa zetu za kijamaa, na haina mjadala kuwa ni kali, ni kupitia mifumo ya technolojia ya mawasiliano, media(tv, videos, internet, redio-ndio maana kiingereza kinatawla wakti asilimia ya waijuayo haifiki 30) na hata rap ni effects za hii media ( lakini yenyewe imekuja kuchukua sura kama hiphop ilivyo chukua kule marekani- wale wasomaji wakasome kitabu cha "hiphop na the politics of modernism" cha Russell Porter)nia yao kubwa ni kuandaa masoko ya bidhaa zao (muendelezo wa ukoloni) kwa kutumia migongo ya masikini.
Kama utakumbuka (kwa wale wenye historia nzuri) Miaka ya 80, wale waliokua na info za nje, kwahapa kwetu walikua watu wa highclass fulani, na kwa sababu mzungu ameshatufanya tuone vyetu ovyo (kwenye mfumo wa kibepari ambao sasa tupo, kila mtu anataka vya juujuu) watu wote wakawa nasi tunatamani hivyo vya nje. Baada ya ujamaa wenye access na mamtoni ndio walikua "babkubwa".
Mtu(mpaka leo) akionekana kapiga raba mtoni,mapamba ya nguvu nini anaonekana bab kubwa (effects za kuwa brainwashed) matokeo yake tunakuwa ma snobber(tafadhali angalia maana yake kwenye kamusi, itaeleweka vizuri). Mtu ukienda kwa mfano billz, kama umevaa vya nje unaonekana more modern, American, au up to date, wengine wanasema eti anaonekana kama wa oysterbay au masaki(ile class ambayo baada ya uhuru ilienda kukaa huko-the aspired status)- kwa kifupi tu, brainwashing hiyo na inayo endelea kufanywa na hii mifumo ya utawala ni historical na inayowezwa kubadilishwa.
Niwape mfano ulio hai, Kuna wamarekani weusi wapo hapa dar, wamekuja kimasomo pale chuo kikuu, wanasema tunaonekana kituko hasa walipoenda billz na billards ("..they look funny and really stupid, why they wanna imitate us??) tafsiri fupi ni " wanaonekana kituko na kuchekesha, kwa nini watuige? (mi nikaona hawajui efects za media zao na ma-culture industry yao kwetu) kwa sababu wanakuja Africa na kutegemea kitu tofauti na kwao, na hisotria yetu na yao ni tofauti.
"Rap na hiphop ni vitu viwili tofauti, hiphop ni maisha na rap ni mziki"-KRS-1. Kwahiyo kama tunaimba hphop kivyetu (mfano,Kisw) kwanini tusiishe bongoflava kivyetu? Sasa swali ni tufanyeje hasa katika mfumo huu wa kitabaka na kinyonyaji? Ndio maana bongo flava (has kwenye nyimbo), muelekeo wake sasa hivi ni wa ku resist madhara ya globalization zaidi, lakini hapohapo globalizaion ama utandawazi, umetugubika sana kwenye akili zetu, tunachotaka ni bongo flava ambayo inawakilisha, tayari kiswahili ni kimojawapo, sasa twende basi kwenye nyanja zote za utamaduni, kama mavazi na vingineko, ukweli ni kwamba makampuni tunayoyapa faida kwa kununua mli zao hela zinakwenda kufaidisha mabepari wazungu ambao wanaongeza kasi ya kufanukisha na kutu-marginalize (tuwe maskini zaidi) na huo utandawazi, tunaimba kwenye nyimbo, " tunapigika' tunatabika nakadhalika ebo akauliza "unataka kuwa muamreikani mweusi?" kwanini tusifaidishe sisi wenyewe hapa bongo? kwanini ukimwona mwenzako kapiga pamba "mbovu" kimoyomoyo unamwona wa hali ya chini au vice versa unajiona tajiri fulani vile) hiyo ni matokeo ya utandawazi kama nilivyoueleza hapo juu.
kusema ukweli hiki ni kipengele tu cha "utamaduni" (material culture), na bado kinauchambuzi wa hali ya juu unaotakiwa. hapa nime jaribujaribu kutilia mkazo historia. vilevile, naweza nisielewke na kukubalika hapa kwani kuna mitazamo mingi (ethnocentric, nationalistic, apologetic, even africanist, intergrationists, separits) kwahiyo naomba tuwentunaangalia historia na current issues (kiuchumi,kisiasa, utamaduni, kijamii,etc) ambazo ndizo hasa zina affect mtazamo,muelekeo na upanukaji mzima wa bongo flava. mkuki utanipata fresh.
Ma mcee wa bongo endelezeni moto!
#8
Posted 30 August 2002 - 01:58 AM
Tatizo watu ukisema uliyoyasema wao wanasema unaleta siasa kwenye starehe, mimi nadhani hili ndio kosa kubwa sana kwa wengi wetu!kama tunavosema tunapigika lakini bahati mbaya hatujui nini kinachotupiga!Ukweli ni kuwa hii sio siasa bali ni hali halisi ya maisha na katika maisha kila kitu kinategemeana yaani ni kama mwili wa binaaamu ukikata kiungo chochote kile lazima mwili utaathirika kwa namna moja au nyingine hata kama utajifunza kuishi na ulemavu huo bado kutakuwa na shida fulani fulani...na tunachokifanya sasa hivi sisi watu weusi(wa marekani na wa barani Afrika) ni kukubali kuishi na huo ulemavu ndio maana hatuamki kubadili maisha tunayoishi nayo tunaishia kwenye icing lakini keki wanakula wengine!
Kama Soul utakuwa unafuatilia mjadala wa "reparations" kwa watu weusi utagundua kuwa mjadala mkubwa uko katika je malipo hayo yawe katika form gani?Kama ni fedha hawawezi kutulipa maana society zao ziko founded katika jasho la mtu mweusi na resources za bara letu kwa hiyo utakuta asilimia zaidi ya themanini inabidi waturudishie!Tatizo liko kwenye Madhara ya kisaikolojia...je hayo utayalipa vipi?
Niwape mfano...kulikuwa na poll moja miezi kadhaa nyuma katika bet.com ilikuwa inauliza je ukienda hospitali uko hoi karibu kufa ukakuta madaktari wawili, mmoja mweupe mwingine mweusi na wote wana kisomo sawa je utamchagua yupi akutibu ukizingatia wewe uko katika hali mbaya kwa hiyo unataka mtu aliye qualified enough!Asilimia zaidi ya 70 walisema kuwa watamchagua daktari mzungu, na usisahau bet.com ina mainly black audience sasa niambie ni kwa nini wameamua kumuamini mzungu zaidi ya mweusi mwenzao?Tunarudi pale pale soul alivyosema kuwa tumepumbazwa akili zetu kiasi cha kwamba hatuna sense of self worth tunapojilinganisha na hawa watu na ndio maana kila kitu chao tunaona kuwa ni bora zaidi ya chetu...si kila siku tunaona bongo akija mzungu hajasoma sana anapata kazi wakati mwafrika aliyempita kimasomo anaachwa!
Tujue kuwa tatizo hili hakuna wa kulitatua bali ni sisi wenyewe na njia ya kuanzia ni kuanza self purification na kuachana na kasumba zisizo na mpango...hapo juu kuna mshkaji kasema tunaosapoti hii ishu tungeanza kuvaa magome...unajua mshkaji kuna kitu kimoja unasahau...waafrika walikuwa wanavaa magome karne nyingi nyuma kwa hiyo hii leo huwezi kuvaa magome, jamii zina evolve tatizo ni kuwa wengi wetu kwa sababu ya kutojua historia yetu (mara nyingi ni kwa sababu historia yetu tumeandikiwa na mtu mwingine ambaye nia yake ilikuwa ni kuitumia kama chombo cha kututawala na kutuvua utambulisho wetu) Hili ni tatizo kubwa sana kwetu maana asiyejua anakotoka ni kama kipofu maana hawezi kujua anakokwenda na wala hawezi kujua makosa aliyofanya nyuma ili aweze kuyaepuka huko mbeleni!Kwa hiyo swala la magome hapa naona liko out of context ingawa kwa kweli kama liki designiwa fresh hilo vazi nalo linapendeza (usisahau haya magome huwa yanatengenezwa vizuri na yanakuwa kama kitambaa kabisa!) lakini mimi naona hilo vazi kwa sasa ni more ceremonial kuliko kuvaa kila wakati...mimi binafsi asilimia themanini ya mavazi yangu ni batik...nazuka disco,shule, na sehemu yoyote ile na wala sijali na ninajisikia vizuri sana!kwa hiyo personally I talk the talk and walk the walk ingawa mimi sio msanii!
Sio vibaya kuvaa hizo FUBU na kadhalika lakini mimi binafsi nilikuwa naona vizuri kwenye public places kama matamasha, kwenye interview za TV na Tours wangekuwa wanatinga kiafrika zaidi ingekuwa mwake yaani kama ku represent...mimi nadhani katika muda mfupi hata matozi slipway ungewaona wametwini batik...kama bongo flava ilivyoanza tu!matozi sa walikuwa wanaiona ya kishamba?mbona sasa wenyewe wanaenda kununua tape?Tatizo ni je hao wasanii wako tayari kufanya hivyo?Kama hiyo nukuu ya KRS ni kuwa Hiphop ni utamaduni rap ni kitu watu wanachofanya tu tatizo wasanii wengi na washabiki hawajajua kutofautisha hivyo vitu viwili!
#9 Guest_Kizixt_*
Posted 30 August 2002 - 10:00 AM
ni dhahiri mnaelewa upana wa neno "culture" na soulrebel umegusia kwa upana zaidi issue ya mavAzi ambayo ndiyo maada yetu kuu. pamoja kuwa umeonyesha okomavu katika historia ya afrika na ukoloni mamboleo kwa ujumla, na chanzo cha watu kuona vitu vya wenzao ni muhimu kuliko vyetu.
ITACHUKUA MUDA MREFU SANA
Baada ya kukubaliana na maelezo yenu kwa kiasi fulani sasa narudi katika msimamo wangu kwamba sifikirii ni rahisi kubadili culture ya jamii kirahisi kama mnavyofikiria. kutokana na sababu hii moja ntakayoieleza. Imperialists, modernizers na wengineo wanaofanana na hao walishafanikiwa kutufanya maskini wa kila hali sijui kama mnanielewa!!!nina maana masikini kiuchumi pamoja na kiakili hilo ndilo wanalotumia mpaka sasa kututawala kwa kila kitu.ninaamini wapo watu wengi ambao wanaenzi kabisa utamaduni wetu politically and not practically involved"' kiingereza kuonyesha msisitizo" Ninamaanisha utekelezaji hamna. pongezi kwa Mkuki kuwa mzee unatinga batiki full time, inaonyesha unaongea kitu unachopractice,hiyo ndiyo inatakiwa...
vilevile mjue kuwa economy & culture are parallel related, hivyo basi bila kuutokomeza umaskini kwanza watu wataendelea kuiga vya nje mpaka mwisho wa dunia.ndio maana issue ya mitumba ilivyolipuka kuwa tuache kuvaa mitumba watu wali kemea kama hawana akili nzuri, tatizo ni nini, UMASKINI.
mimi kwa mtazamo wangu watu kuiga kila kilicho cha nje source ni umasikini uliosababishwa na utumwa pamoja na ukoloni au siyo mtalamu wa historia????? teknologia yao ya hali ya juu na uchumi wao imara umesababisha waafrika kuenzi kila kilicho cha nje
tuondoe umaskini na teknologia ikue ndipo mambo mengine
tusiwe wanasiasa wazee....
#10
Posted 31 August 2002 - 04:04 AM
Mimi nakubali kuwa umaskini unachangia katika mambo mengi sana lakini vilevile ninadhani tatizo letu kubwa ni swala la kubadilisha mentality zetu!Mimi naamini tunaweza kutatua matatizo yetu bila msaada wa wageni tatizo ni je tunaamini hivyo?Je tunajiamini wenyewe?
Ninasema hivyo ili kutilia mkazo kuwa lazima tuanze sasa hii process hatuwezi kusubiri umasikini uondoke wakati hii yenyewe ni mojawapo ya njia za kupigana na umasikini kama mwenyewe ulivyosema kuwa uchumi na utamaduni ni vitu vinavyoshabihiana na mimi nakuunga mkono kabisa.Kwa mantiki hiyo basi ili uchumi uweze kukua basi inabidi na utamaduni wetu pia tuanze kuuenzi. Tatizo letu kubwa ni kuwa tuko so confused kiasi kuwa hatujui upi ni utamaduni wetu na upi ni wa kigeni; ndio tunarudi kulekule kwenye swala la mentality zetu!
Anyway naona tutaanza kutoka mbali na hiphop tuingie kwenye socio-economic issues hapa tusije kuwaboa watu wengine...lakini tusisahau kuwa hivi vitu vyote vinategemeana ndio maana ninasema kuwa siyo siasa bali ni ukweli wa maisha tu!
#11
Posted 03 September 2002 - 03:21 AM
kwanza kabisa solrebel ..brainwashed =kupumbazwa,kutiwa changa la jicho
nina mchango mmoja ...tunafahamu wabunifu wa mavazi bongo wapo lakini kuna kitu kinachonishangaza ni kwanini nguo zile za asili(batiki) zinashindana na designers labels...maana yangu ni kuwa unaenda kuangalia nguo ya kha....(sitaji jina) unakuta bei yake ni karibu na FUBU iliyotundikwa dukani sasa kwa hali kama hii situtakuwa tunajiwekea ugumu wenyewe.
lakini kuna kitu nilifikiria juzi baada ya kusikia habari za cool james..nikasema ni bahati mbaya jamaa kavuta lakini wasanii wa kibongo watachukulia kama changamoto kwa kuendeleza maendeleo yao wenyewe...kwa mfano wakikaa chini wajaribu kujadili fainali ya bongo flavor watajua nini kinahitajika kufika huko ng'ambo na labda wataweza kufikiria hata swala la vazi la asili.
#12
Posted 03 September 2002 - 08:41 AM
#13
Posted 03 September 2002 - 04:15 PM
hii forum naona mkuki na solrebel wamemaliza kuelimisha jamii isipokuwa wale wanaodhania vazi letu noma wanaweza kuangalia topic ya "je watanzania tuna vazi la asili" nadhani watu walijadili sana hili swala la uvaaji
Quote
Quote
hongera sana mkuki kwani wengi wamejaribu lakini wameshindwa
#14 Guest_soulrebel_*
Posted 04 September 2002 - 09:31 AM
Nakubali kabisa (mic 5 mzee) chanzo na muendelezo wa huu mfumo ni kutokana na umaskini wetu ambao historia yetu inajieleza wenyewe. Hata katika mavazi, kutokana na kwamba katika soko hili “huria” (si uamini kabisa tena naupinga kishenzi!) ambalo hayo ma-corporations ndio yanayo toa mwelekeo kupitia vibaraka wake kama IMF na World bank, wanakandamiza nchi maskini kama Tanzania.
Tatizo kama alivyotilia mkazo mkuki linaanzia kwenye ubongo (mental slavery) japo kidogo mtu akiwa huru kiakili, akawa concious ya kwamba ananyonywa, aweza angalau japo kuongea against, lakini wengi wetu ahtuko conscious ya hata kama tunatawaliwa kantika nyanja zote , kiuchumi, siasa, utamaduni, kijamii, kiakili, kimiondoko, kilakitu (mic 7 wamasai).
Tatizo linaenelezwa kirahisi wapi? lakini Kwanza naomba nizipongeze media zetu, hasa redio stesheni, televisheni, magazeti na vinginevyo. Katika karne hii ya sayansi na tek, na wengi tunasikia ya kwamba vyombo vya habari (kwa mtazamo wangu ni madhara ya utandawazi) vimechukua mkondo mkubwa wa kazi ya elimu,vinaitwa “kioo cha jamii” imefikia hatua ya kwamba watu wanbishana eti “ah! Unabisha nini wakati BBC wamesema?”, maana yangu ni kwamba vyombo vya habari ni “muhimu” kwa kutoa elimu zaidi ya shule au vyuo, na ndizo zenye access kubwa na jamii zaidi ya vituo maalum vya elimu. Lakini mtazamo hasa wa kitamaduni unaotolewa na hivi vyombo ni asilimia 80, kutoka nje! Asilimia 15 kutoka nchi nyingine za africa ambazo nazo zimeathiriwa na utandawazi. Mtu yeyote anayepiga pamba za mamtoni hakuamka gafla na kuanza kuvaa , (wengi wetu, ambao mamtoni ni ndoto) aliona mahali ama luningani, gazetini, au internetini. Tungekua na uwezo wa wa kuweka vitu vya hapa kwetu zaidi tungeenda mabali, lakini ndio hivyo tena, hata major media coorporations za hapa kwetu, wamilikaji wao ni mabepari wakubwa, kila mmoja wao ana lenga kuvuna mapesa MENGI bila kujali kile anacho kirusha hewani kinasaidiaje kukuua utamaduni, eti utamaduni umebaki ngoma za kwenda kupokea diplomats uwanja wa ndege! Hata presenters wetu nao utamwona kavaa ma blingbling alafu anasema “tuu enzi utamaduni wa mwafrika” wengine wanjaribu kuongea kwa kiingereza! Cha kimarekani!!!!!
Msistizo wangu bongonian ulikua kwenye njia za kuweza kufikia watu wengi na kubadilisha mitazamo yao kwa sasa, hakuna sehemu nyingine zaidi ya vyombo vya habari (kwa kuanzia),maana kama tutaweza walichofanya wachina miaka ya 60-70s, “cultural revolution” ingekua bora zaidi- kwa kifupi tu ni kwamba walitumia nguvu kuhakikisha kwamba utamaduni wakimagaribi unaondoka, watu kama wankujua wewe ni mbepari wanakuua hapohapo, hakuna kwenda polisi, kunavijana hao walikua wanaitwa “red army”, mapanga mkononi!
Na zaidi ni kwenye hiphop fani yenyewe, mamcee najua ni vigumu kuanza kupiga batiki na matenge ghafla, lakini japo waoneshe mtazamo/picha ambayo sio ya kimagaribi saana, kwani wao sidhani kama kuna ubishi, ndio kioo cha jamii kupitia vyombo vya habari, lakini still, kazi ni ngumu lakini inawezekana ( hata tukifa tusife kama mangombe, angalau tu jibu mashambulizi)
Ma mcee wa bongo endelezeni moto!
#15 Guest_kizixst_*
Posted 04 September 2002 - 01:02 PM
kama ulivyosema mamcee ni kioo cha jamii kwa kiasi fulani, ingekuwa vizuri zaidi wao wakaanza mapigo kama ya Mr. abel, batiki, nk nadhani kungekuwa na changes hilo nima amini lingeonyesha maendeleo mazuri
sasa tatizo Maemcee wetu hawapo mtandaoni tungekuwa tunapata maoni yao nao.
vile vile watu wameumbwa na tabia ya kumpenda mtu na kupenda kitu afanyacho, avaavyo, atembeavyo n.k. nadhani wazee Ni wapenzi wa soka au siyo, kama ulifuatilia last (korea & japan world cup) utakumbuka jinsi ronaldo alivyomyoa nyele, kuna wabongo walianza kunyoa kama Ronaldo kwa sababu tuu wanapenda soka lake, kwa hiyo basi nina imani kama wasanii wa bongo wakaanzisha baadhi ya pamba fulani kwenye maconcert na sehemu zingine ni lazima watapata wafuasi wa kuiga mapigo yao,
ila kama mbongonian alivyosema hapo juu lipi ni vazi la kitaifa bongo, naomba kama kuna anayelijua aniambie ili labda tuanze kutinga au siyo wazee???????
#16
Posted 04 September 2002 - 02:28 PM
Lazima tuelewe kuwa tanzania ukiangalia swala la makabila ni "very diverse" yaani tuna mavazi ya aina nyingi sana...sasa mimi kama ningekuwa designer wa nguo za kiafrika ningefanya research ya nguo zinazovaliwa katika makabila tofauti ya Tanzania halafu ninge combine elements tofauti za mavazi hayo na ningetoka na kitu kikali ambacho kinawakilisha hiyo diversity yetu watzanzania. Ningekuwa waziri wa Utamaduni ningeandaa shindano kubwa la nchi nzima kwa madesigner wa Tanzania kudesign (jamani samahanini hivi design kwa kiswahili ni nini maana naona ishakuwa taabu!...ndio mambo ya kasumba haya!) vazi rasmi la Taifa la wanawake na wanaume ambalo litatumika hata na viongozi kutuwakilisha (angalia wenzetu wa afrika magharibi haswa NIgeria) wale washindi watatu wa juu watakaa pamoja na ku design sasa final national attire. Huu nadhani haswa ni mzigo wa Wizara ya Utamaduni lakini kwa sababu najua kutegemea hawa mabwana wakubwa kuitufanyia kazi haitufikishi kokote ni wajibu wetu kuwakilisha kwa jinsi tunavyoona itafaa...mimi nadhani batik,mashati ya vikoi yanawakilisha kinoma tu hata kama hujatinga full suit lakini walau shati na jeans haina noma wala nini nakumbuka kama mara mbili niliona hard blasters wamepanda kwenye steji na batik enzi zile chemsha bongo imetoka tu!lakini sijui kama bado wanaendelea maana mimi niko mbali na home!
Kuhusu swala la vyombo vya habari ingawa nakubali kuwa wana reflect kitu watu wanachopenda nadhani ukiangalia sana utakuta wao ndio wanaochagua nini watu wapende...yaani wao ndio wana influence public opinion; na hii ni charactreristic ya vyombo vya habari vinavyioendeshwa kwa matangazo (commercial media) kwa sababu wao wanapangiwa na wafadhili wao...kwa mfano kama matangazo ya bia na sigara yaakuwa mengi kwenye TV ukifanya research utagundua kuwa mauzo ya vitu hivyo viwili yamepanda, na dnio maana unaona wanaendelea kutangaza maana wanatengeneza hela...nadhani tukiangalia cause and effect utakuta media inaanza ndio watu wanafuatia...since tuko kwenye hiphop tuangalie mfano huu: HipHop ya bongo ilianza vipi kukubalika kwa watanzania wali wengi yaani mainstream Tanzanians? ni baada ya nyimbo kuanza kupata more airplay katika vyombo vya habari tofauti na zamani ingawa kuna sababu nyingine kama ubora wa production lakini mimi naamini hiyo ndio ilikuwa sababu kuu. Kama ulikuwa unafuatilia historia ya hiphop bongo zamani ulikuwa muziki wa washamba (mabitozi walivyokuwa wanuona) lakini sasa hivi hata disko unapigwa na watu wanajirusha...mimi nakumbuka kuna wakati mmoja nilikuwa bills ukapigwa wimbo wa Hashim - shadows of a dark destiny kama sikosei watu wote wakaondoka kwenye sakafu ya kuchezea na hii sio mara moja tu mara kadhaa yaani hadi DJ inabidi autoe chapchap!Ukiangalia utakuta watu walianza kuusikia muziki huu redioni na sasa hivi unaona kuwa hadi mauzo ya kanda yamekuwa makubwa kishenzi na mpaka unaona na mamcee wameongezeka pia, na kali ka myth kuwa ni muziki wa kihuni kameanza kupungua pungua ingawa kuna wachache ambao bado wanawakilisha hiyo fikra kwa kukosa rhymes zilizo makini!
Kama hii leo media inge glorify utamaduni wetu na wakawa consistent na hilo yaani wao kila siku bango...polepole ungeona ma mcee na wanaanza kutinga mapigo ya kiafrika na mwishowe kutoka hapo unakuta na washabiki (ambao ndio sie tulio wengi) tunaanza kutinga hivyo hivyo..ukicheki utaona zamani bongo flava kama nilivyosema awali ilikuwa ya wachache tu...lakini utakuta siku hizi hata matozi wa uzunguni (ambao wengi ndio malimbukeni wanaodandia tu bila kujua undani wa kitu) nao wameanza kuusikiliza...yaani siku hizi "maisha ya uswazi" baada ya gangwe yamekuwa dili watu wanaona ujanja kujiita mtoto wa uswazi wakati zamani ilikuwa aibu...feel me!?
Jamani mida naona lishakuwa gazeti hili tena!lakini wazee pointi nzuri sana najifunza mengi kutoka kwenu :)
#17 Guest_soulrebel_*
Posted 06 September 2002 - 01:45 PM
Vazi la kitanzania naona hakuna, (kwa sababu tunamkanganyiko wa "ethnicities" mbalimbali, au vipi? kwa mfano wamasai, hawa ni watanzani na pia wako kenya(sasa unaona madhara ya kugawanywa bila kupenda?) mimi napendelea kupiga vazi lolotte lile la kiafrika! kwasababu vazi asili zetu wengine zilimezwa na wamissionari na wakoloni, tukajiona wachungaji, masisita, na mapadre zaidi ya wao waliotuletea, kwahiyo bongonian mimi napenda kustand kama afrika zaidi, mfano west Afica zile nguo ndefu wavaazo wanigeria zipo mpaka cameroun senegale (kama ushamuona rais wade wa Senegal anapiga hivyohivyo kama nigeria ingawa kuna kainfluence kaarabia) kakini still, ni Africa.
Kuna mwandishi mmoja matata sana wa Algeria aliyeitwa Franz Fanon, katika kitabu chake cha "Wretched of the Earth" alisema na nukuu "the freedom for Africa is to find the image of the blackman (nafikiri wale waafrika) which is not immediate reproduction of western parodaic projections" sidhani kama nimenukuu vibaya, yaani kumiss maneno, ila ujumbe wake anasema kwamba Africa yote iwe na mtazamo wake, alikua anaandikia kipindi kile baada ya ukoloni mkongwe, yaani nci huru zifanye nini,(total revolution).
YAANI KAMA NINGEKUA NA UWEZO WA KUUNGANISHA NCHI ZOTE ZA AFRIKA ZIKAWA MOJA "KAMA HAPO ZAMANI"....
Vazi likiwa na mtazamo wa kiafrika mi naona shegha sana, kwa maoni yangu jamani.
Ma mcee wa bongo endelezeni moto!
#18 Guest_soulrebel_*
Posted 06 September 2002 - 03:55 PM
mamcee wa bongo endelezeni moto, Mo' Faya!
#19
Posted 06 September 2002 - 04:23 PM
Sisemi hivi kwamba nayaponda mawazo yenu,hapana.Hapo tuelewane kwanza,ila ninachosema mimi ni kuwa nyinyi mmeelemea zaidi kwenye mawazo ya kufikirika zaidi kuliko kutekelezeka.
Kwa nchi kama Tanzania naomba msahau kabisa kitu kinachoitwa vazi la Taifa hata kama itapita miaka mingapi.We angalia tunasema tuna lugha ya Taifa tangu Mwalimu anaitawala nci hii lakini tizama mtiririko wa mawazo ya mheshimiwa Mkuki uniambie ni lugha gani kama si kiswanglish?Hapo ndipo tunaporudi palepale.Kama Kiswahili tumeanza nacho tangu miaka ya 1960' na bado sisi tunaojiita waswahili hatuongei kiswahili wapi litawezekana vazi la Kitanzania?
Nikienda moja kwa moja kwenye mada ni kuwa hili jambo linakuwa gumu kwa sababu mbalimbali ingawa mi nitawapa mbili kwa leo.Kwanza umasikini.Kila siku maburungutu ya mitumba tena kwa bei bwerere yanaingia nchini halafu umwambie mtu akavae bazee au batiki ambayo kabla hajaweka gharama za mashono anaweza akapata mitumba gunia mbili!Pamba za kibongo tukubali tukatae ni gharama kuliko mitumba tuliyoizoea.
Pili ni historia.Mshikaji wangu soulrebel mwenyewe ushalikubali hili halafu tena ukatoka nje!Wazungu walishatuwekea umimi.achilia mbali ile kusema mmasai yuko bongo na kenya na mngoni kuwako tz na bondeni.Ila kuna hili lamwalimu kutuchanganya wabongo hadi kushindwa kusema mi mmasai bwana!au mi mbondei kwani kila mtanzania anaishi sehemu yoyote ya bongo anayotaka yeye.Sasa niambie tuvae rubega za wamasai,mgolole wa wagogo au mashuka ya wambulu?
Tukubaliane tu kwamba kwa hali halisi iliyoko kuwako kwa vazi la kitazania au la kiafrika ndani ya nchi kama tanzania ni ndoto za alinacha.Ngoja niishie hapa kwa leo
#20
Posted 06 September 2002 - 10:51 PM
Kuhusu swala la mimi kuchanganya kiingereza katika kiswahili changu utaona kuwa sehemu nyingi katika post zangu za awali nimeweka kwenye mabano kuwa ndio matokeo ya kasumba yaani mimi mwenyewe nimekubali kuwa siko nje ya kundi lililopumbazwa na hawa wazungu na hata mimi nina kazi kubwa ya kufanya hilo wala sikatai lakini walau ninajaribu kusafisha kichwa changu na wala sikai nikasema "haiwezekani"
Hilo swala la gharama za nguo ninakubaliana na wewe kuwa litaleta ugumu lakini hata hivyo mimi naamini kuwa ni kwa sababu hiyo hiyo ya kufuata fasheni za ulaya, kama ingekuwa sio hivyo nadhani pia ingesaidia yaani kama batik zingekuwa chati ingeleta tofauti fulani lakini tatizo ni kuwa watu hawazithamini na mtu anaona ni bora mtumba kwa sababu unaendana na fasheni za ulaya. Halafu hilo swala la makabila tofauti kama utakuwa umesoma hoja zilizopita utakuwa kuna mahali nimesema ma designer wanaweza kuja na mtindo ambao unachanganya mitindo ya makabila tofauti ili kuna na vazi ambalo linawakilisha zaidi makabila ya nyumbani!Hata hivyo hoja zako za msingi ila mwanangu mie sio mheshimiwa hicho sio cheo changu unaweza kuniita Mkuki tu inatosha!
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












