Nani anataka kipaji kikuwe aje
#41 Guest_Knife_butcher_*
Posted 12 September 2003 - 11:08 AM
Kwenye battlin mc nakuegeza mwali
huwezi pambana na zangu protokali
Naona unakuja vile moto mkali
ukija kwa kasi nakupunguza mwendo
Ungana na pumbavu wenzio hamuwezi nihendo
kama paparazi nafuatilia zako nyendo
ukinletea za kuleta nalipua zako skendo
Siachi kukuchokonoa mpaka usalimu amri
Huwezi improve skillz uko limited na umri
unanifeel kwenye ubongo kila uvutapo pumzi
Nakuacha umeganda domo ganzi
Hiki ni chuma huwezi usiote kupiga kitanzi
Nishakwambia usinafate we kwangu katuni
mbio zako ni zile za sakafuni
punde si punde zitafika ukingoni
bado mchovu kama tishio sikuoni
staili yako mamantilie huwezi survive ulingoni
Hii ni sawa kumpambanisha matumla na tyson
Nakupiga chenga nakuacha unafukuza upepo
Nadhani hujatulia kichwani una mapepo
Tulizana kwanza wanathread tukupepee
Hapa huwezi win hakuna ushindi wa chee
Ndani ya game jibaba nipo okee
Nasubiri kukupiga bao kisha nipotee
Hii ni battle usichane kama una beef
Nipe respect K to tha bucha a.k.a hiphop chifu
namwaga sera ili ubaki mtiifu
Huwezi ona gizani mwanga wako koroboi
mizani yako haitishi kwangu bado goigoi
hapa mate utameza ukipaliwa hukohoi
Ni born town utaniweza shamba boy
unasema utotoni ulimiss kuchezea matoy
Ndio maana akili zako punguani
nilikuwa najiuliza ulimiss kitu gani
...............
#42 Guest_Knife butcher_*
Posted 12 September 2003 - 11:11 AM
Miale yangu inachomoza hekima cheki kwa mbali
Kwenye battlin mc nakugeuza mwali
huwezi pambana na zangu protokali
Naona unakuja vile moto mkali
ukija kwa kasi nakupunguza mwendo
Ungana na pumbavu wenzio hamuwezi nihendo
kama paparazi nafuatilia zako nyendo
ukinletea za kuleta nalipua zako skendo
Siachi kukuchokonoa mpaka usalimu amri
Huwezi improve skillz uko limited na umri
unanifeel kwenye ubongo kila uvutapo pumzi
Nakuacha umeganda domo ganzi
Hiki ni chuma huwezi usiote kupiga kitanzi
Nishakwambia usinafate we kwangu katuni
mbio zako ni zile za sakafuni
punde si punde zitafika ukingoni
bado mchovu kama tishio sikuoni
staili yako mamantilie huwezi survive ulingoni
Hii ni sawa kumpambanisha matumla na tyson
Nakupiga chenga nakuacha unafukuza upepo
Nadhani hujatulia kichwani una mapepo
Tulizana kwanza wanathread tukupepee
Hapa huwezi win hakuna ushindi wa chee
Ndani ya game jibaba nipo okee
Nasubiri kukupiga bao kisha nipotee
Hii ni battle usichane kama una beef
Nipe respect K to tha bucha a.k.a hiphop chifu
namwaga sera ili ubaki mtiifu
Huwezi ona gizani mwanga wako koroboi
mizani yako haitishi kwangu bado goigoi
hapa mate utameza ukipaliwa hukohoi
Ni born town utaniweza shamba boy
unasema utotoni ulimiss kuchezea matoy
Ndio maana akili zako punguani
nilikuwa najiuliza ulimiss kitu gani
#43 Guest_ILLA_*
Posted 12 September 2003 - 04:21 PM
ILLA a.k.a Macho
#44 Guest_HEKIMA_*
Posted 12 September 2003 - 04:27 PM
angalia kalenda uchague tarehe ya kifo
sibani….unaweza-tatizo umeanzia mwisho
kama chaukucha,nakuwasha sa knife_butcher
game hauliwezi huna kontrol-una busha! hayo yako ni madangi
siku-feel ka mteja akivuta bangi, kwa kubattle nami ni umekubali jitoa mwangwi,nakuacha umepauka-we kwangu unachuja rangi,mweupe ka yangi-yangi,hizo sera za ‘visu’ na ‘mabucha;’ ukampe mangi….
usitake nizoea, chonga hizo ‘comment’ zako uzisokemeze unakonyea
dogo mi naanzia pale upeo wako unapokomea,napotema we bonyea
mbinu zangu za kijeshi ni kama za wakorea
kabla haujastuka-na-attack na kupotea..nakuacha wajikojolea
kwangu we Mgambo, njoo nikufanye chambo-buti ninalokupa,wataenda kukuokota ng’ambo, nakulipua mbali,we m-vietnam mimi Rambo!
huwa sigongi hodi Bwa mdogo-nalipua milango…
naandika vina usiku ndani ya mapango,MCz nawagandisha na kuwaweka ka mapambo,na battle na vichwa,juu ya shingo wewe una tango
wanifanya ni-miss Bongo maana kwangu wewe Bambo..ha! ha!
Inua silaha,weka chini majigambo…..
kichwani nina-mabomu nasaka pakulipulia,na sio la machozi bwa mdogo usianze lia,ni nyuklia na wewe ndio pakujaribia…nitachofanya ni kukufagia
taa nyekundu kichwani inawaka napofikiria, nisipotema mashairi yaweza nilipukia,ni hatari kupindukia…anyway nisikutishe sana,dogo sikia..
hiyo stage uliyofikia,mi nilishaipita ka-miaka saba kukadiria..
hivyo kusanya ‘visu’,funga bucha anza kukimbia…!
nakuacha hai kusudi ili uweze kusimulia,yaliyokusibu na jinsi chupuchupu ulivyosalia,na sitaki battle nawe TENA usije ukanifia…..haya kimbia!
KINDA WE!
#45 Guest_knife_butcher_*
Posted 12 September 2003 - 05:12 PM
Hapo ulipo upo hoi bin chakari
Bao nilizokushindilia zinaitwa dogi staili
na bado unakuja unataka zaidi shari
aje mwingine huyu nishamchanachana tayari
Nampakaza mimavi kila akijipangusa
Koma mc mambo ya kunusa kunusa
nazidi kukushindila mpaka fani utasusa
We kibonde wangu na we tafuta kibonde wako
vina vyangu pima kote fasihi
ujumbe navyoubeba utadhani nabii
nakupa kipigo lakini unajifanya usikii
Nakuvuruga tu huwezi weka hitimisho
Nakula sambamba na wewe mpaka ugote mwisho
we dogo nakuona miyeyusho
Dongo ulizurusha zote bado michosho
Unanikenulia mimeno unadhani hii commercial
manundu ntakuumua usinletee za kishoo
Naongea leo huelewi mpaka kesho
rymes zako yaani vituko vichekesho
Ni bora nisikilize hadithi za abunuasi
sasa mazee naona kama unanigasi
sielewi kitu gani unaspit
Tundu la hiphop dogo bichwa lako halipiti
Huwezi penya kipaji chako hakipo taiti
Kubattle na wewe ni kama kucheka na maiti
Ukizidi kuja ntanyofoa zako nyeti
unaingia cafe unaandika mbovu beti
Mc ndani ya kuminanane nachana neti
kwenye mtandao ni balaa napoketi
nakurarua sababu umeingia kati
kama kusevu anza kupanga mikakati
Sikuonei huruma kichwani nishapoteza nati
Nakusulubu kiroho ngumu na pigo za kiman'gati
Ndani ya thread nashusha yako chati
Staili yangu kwa mbali haupati
nashangaa mpaka dakika hii haujanyuti........
#46 Guest_fobolous aka toto la mita_*
Posted 12 September 2003 - 08:14 PM
wananiamisha magereza kwa magereza mahabusu kwa mahabusu/
suka piga bao hawa ndama nauli yao nusu nusu/
butcher haya maji marefu kisu chako butu/
peperusha bendera nyeupe nikupe yako ya mwisho hukumu/
ntakupeleka lesilesi huwezi kunielewa unless uvute ndumu/
naona homa yako inapanda kula mwarubaini kunywa dawa chungu/
wengi warembo kama wewe nimewaumbua nime lost takwimu/
mimi jangiri shetani mweusi kama mjaluo alietoka kisumu/
si mind kukuelimisha hilo ni langu mimi jukumu/
kandanda nalipiga pekupeku huniwezi hata ukinivalia njumu/
fani umeingilia fungulia mbwa mimi ntakuepo milele ntadumu/
ntakuelekeza kibla shingoni nikupige kisu/
nakupa mapigo jumla jumla wewe unajificha kama taxi bubu/
kubatle na explosives hivi wewe ndama huoni aibu/
got someelse to say
#47 Guest_explosives_*
Posted 12 September 2003 - 08:16 PM
wananiamisha magereza kwa magereza mahabusu kwa mahabusu/
suka piga bao hawa ndama nauli yao nusu nusu/
butcher haya maji marefu kisu chako butu/
peperusha bendera nyeupe nikupe yako ya mwisho hukumu/
ntakupeleka lesilesi huwezi kunielewa unless uvute ndumu/
naona homa yako inapanda kula mwarubaini kunywa dawa chungu/
wengi warembo kama wewe nimewaumbua nime lost takwimu/
mimi jangiri shetani mweusi kama mjaluo alietoka kisumu/
si mind kukuelimisha hilo ni langu mimi jukumu/
kandanda nalipiga pekupeku huniwezi hata ukinivalia njumu/
fani umeingilia fungulia mbwa mimi ntakuepo milele ntadumu/
ntakuelekeza kibla shingoni nikupige kisu/
nakupa mapigo jumla jumla wewe unajificha kama taxi bubu/
kubatle na explosives hivi wewe ndama huoni aibu/
got someelse to say
#48 Guest_explosives_*
Posted 12 September 2003 - 08:18 PM
#49 Guest_Knife butcher_*
Posted 13 September 2003 - 02:12 PM
Nakubatiza kwa jina la baba mwana
kutoka leo nakwita kibena mjanja
We una wazimu kuntaja huogopi
hii si battle ya rusha labda upo confused
Naanza kukupigilia mingi misumari
Mc wa kweli namwaga mistari
Kama una kifafa mi ndio daktari
Kuchanwa chanwa naona upo tayari
mitego yangu huwezi tegua
Vina vyako vibovu nakuzuia kucheua
Hii thread ngangari..mchovu huwezi chafua
Wakongwe wamefloti bado wewe hujatambua
Kila mc unataka mchomekea
We bado unatambaa hujaweza kutembea
verse yako hapo juu kinabo inaboa
hapa ni skillz jibaba usijaribu kufosi
Sio unataka chana sababu unataka floss
Usipime uwezo wangu mimi mikosi
rymes hizo nyepesi kwa lugha ya kiemcee tunaziita kamasi
Kuelewa yangu mistari wahitaji kamusi
#50 Guest_ILLA_*
Posted 13 September 2003 - 06:36 PM
ukijipendekeza nina kutoa bikra nakuacha ukivuja damu,
beti yangu imesha zika wengi wageni kwenye hii game,
nachana wenye mashati wenye vest wana weza sevu,
kama siku gusi basi preasure imepanda minimum wage,
na julikana kwa jina "ILLA a.k.a MACHO" uwezi jificha,
bila mimi ni sawasawa mic bila b.i.g au 1pac 2pac wewe uhh,{hakuna}
ninavyo kuja kushika mic bila mikono mi noma,mulize mulla,
unazani unaweza kubattle mi sizani kama una weights E-nuff,
lakini vyovyote vile unavyo taka mimi ainisumbui njoo tu,
wajulishe...............................
#51 Guest_HEKIMA_*
Posted 15 September 2003 - 08:53 AM
PA1
#52 Guest_k-bucha_*
Posted 15 September 2003 - 03:36 PM
Mc ingia line kama wataka kibano
Nachana nyavu.. nakushindilia bao kavu kavu
Usilete jeuri hii inaitwa nyota an'gavu
Njoo kimachale..hapa utavunjwavunjwa mbavu
uzito wa vina unaelekea infinity usinipime ubavu
Walioanza vita nami wote wanasevu
Wanakimbia umande baada ya kuona unyevu unyevu
Mashairi ndio yanazidi kuroga..ANGA BADO NI PEVU
anza fungasha ukiwa bado shujaa
#53 Guest_HEKIMA_*
Posted 15 September 2003 - 03:43 PM
KAZI KWENU!!
#54 Guest_ILLA_*
Posted 15 September 2003 - 04:19 PM
Hekima wins this one,
k-butcher nice one tho,
ILLA.a.k.a MACHO
{betta keep ur sword`s swingin coz i`m comin fo ya`ll}
#55 Guest_Knife butcher_*
Posted 15 September 2003 - 08:37 PM
#56 Guest_k_bucha_*
Posted 15 September 2003 - 08:53 PM
ingia mkenge..bila ajizi nakumeza
battle na wewe ndani ya thread natangaza
Hekima refarii kipenga puliza
Tuff mshika kibendera speed ongeza
illa nakupa hiki cha kupalaza
haya twende one two daka kipaza
#57 Guest_MARK II B_*
Posted 15 September 2003 - 10:40 PM
#58 Guest_k-bucha_*
Posted 16 September 2003 - 09:21 AM
#59 Guest_Knoka_*
Posted 17 September 2003 - 08:17 AM
K-Bucha na Hekima kwenye "ringi"/
Illa refa, mi lainsi men bendera juu mgeni kaotea hii ndodi/
Vipaza twavirudisha kati ilimradi hiirauindi i'punch"/
Haya refa pulisa filimbi ili tuanze tujue nani mshindi.
Tuff
#60 Guest_RXPLOSIVES_*
Posted 17 September 2003 - 11:14 PM
2 user(s) are reading this topic
0 members, 2 guests, 0 anonymous users












