Knoka said:
Makinda waje... kimila kaa mmakonde… ntachanja pande/
Butcher...mfano kipa-nyuma-ya-lango/uhakika ntafunga bao..kimande/
Mafinga.. gumba zote natinga kina hapo unyapo.....
Hii kambi una-rap kimwali/style yako "naiozesha".. kunuka mimavi/
Butcher ni wazi uu-level ghani/kwa bwana Masanja uu kimo ardhi/
Wapi “Knife” butu kunitisha makali?/yako style mandhari ya joto bar’di/
Pima wangu wewote mstari/unakuta nakutwika tani.. robo ngangari/
Robo tatu baki ni madongo “standadi”/
Mfano wa zogo katika rhymin' una gongo? miye ntashika “gani”/
Hatupimani “size” wangu miye "flow" chakali/
Badili zako zilipendwa hapo zakale.
Knoka a.k.a tuffjam
wajiita knocka a.k.a tuff to tha jamm
Narespect level yako ya ufahamu
kumbuka walimwengu wanasemaje
mzarau mwiba inakuwaje?
Nakotoa kamasi ingawa ulikuwa kinara hapo zamani
Mistari yako tani yangu haipimiki uzani
kama unajiamini ingia uwanjani
Nakula sambamba na vina muulize fanani
Mimi ndio nabii nakuja kuokoa fani
Nachambua mbabaishaji ni nani
Na nani ni Mc aliye makini
katika kuchana silaha yangu ni mic
Tukiingia ulingoni napora wako mashabiki
flow yangu jibaba haikamatiki
Naleta mapinduzi mbona haufikik
eti kisu butu labda una makengeza
We tupa mawe mi njia natengeneza












