Jump to content


Nani anataka kipaji kikuwe aje


157 replies to this topic

#21 Guest_knife_bucha_*

  • Guests

Posted 09 September 2003 - 11:08 AM

Nilisahau kuweka jina kwenye post hiyo hapo juu

Knoka said:

Ni kweli Illa vijana ni kama wameonja "gun powder" katika fani, lakini warudi kwenye original thread kunilipa narudia mfano (butcher bado bado sana):

Makinda waje... kimila kaa mmakonde… ntachanja pande/
Butcher...mfano kipa-nyuma-ya-lango/uhakika ntafunga bao..kimande/
Mafinga.. gumba zote natinga kina hapo unyapo.....
Hii kambi una-rap kimwali/style yako "naiozesha".. kunuka mimavi/
Butcher ni wazi uu-level ghani/kwa bwana Masanja uu kimo ardhi/
Wapi “Knife” butu kunitisha makali?/yako style mandhari ya joto bar’di/
Pima wangu wewote mstari/unakuta nakutwika tani.. robo ngangari/
Robo tatu baki ni madongo “standadi”/
Mfano wa zogo katika rhymin' una gongo? miye ntashika “gani”/
Hatupimani “size” wangu miye "flow" chakali/
Badili zako zilipendwa hapo zakale.


Knoka a.k.a tuffjam

wajiita knocka a.k.a tuff to tha jamm
Narespect level yako ya ufahamu
kumbuka walimwengu wanasemaje
mzarau mwiba inakuwaje?
Nakotoa kamasi ingawa ulikuwa kinara hapo zamani
Mistari yako tani yangu haipimiki uzani
kama unajiamini ingia uwanjani
Nakula sambamba na vina muulize fanani
Mimi ndio nabii nakuja kuokoa fani
Nachambua mbabaishaji ni nani
Na nani ni Mc aliye makini
katika kuchana silaha yangu ni mic
Tukiingia ulingoni napora wako mashabiki
flow yangu jibaba haikamatiki
Naleta mapinduzi mbona haufikik
eti kisu butu labda una makengeza
We tupa mawe mi njia natengeneza

#22 Guest_HEKIMA_*

  • Guests

Posted 09 September 2003 - 03:23 PM

KAMA UNATAKA BATTLE NA MTU UNAMUAMBIA,SIO STAILI ZA KUDONOA-DONOANA.....TUSICHAFULIANE MAJINA..KAMA UNATAKA KUPASULIWA..WOTE WODI MNAIFAHAMU....WE 'KNIFE_BUTCHER' NA MWENZIO 'EXPLOSIVES',NATAKA NIWA-BATTLE WOTE NYI KWA PAMOJA!! NJOONI MANDE NIWAPASUE WOTE!! SIO MNADONYOA-DONYOA....
AKIWASHE MMOJA WENU..MSHUHUDIE SHUGHULI!!....AU LA ACHANENI NA HILI CHATA....!!

HE.KI.MA

HESHIMU KINA CHA MASHAIRI/WODI YA UPASUAJI

#23 Guest_ILLA_*

  • Guests

Posted 09 September 2003 - 06:17 PM

Nanukia ushindi zaidi yangu simtambui,
shahidi wangu mweyezi mungu,"oh god"
kama ni k-butcher nilisha mkinda siku nyingi,
hii hapa ni kama marudio nakuja na mbinu mpia,
kama ni ku-shock mc, crew yangu ni mobb deep,
move`s zangu ni kama nyoka kwenye majani,
jaribu ku-rewind lines hizi uone ulivyo chemsha,
una hisi joto kama ujawai kuona jua,
mbaka hapa walevi na waelevu wamesha nipata,
jaribu kwenda against mi nikupe taff,"huh"
wajulishe.........................

#24 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 09 September 2003 - 08:04 PM

HEKIMA said:

KAMA UNATAKA BATTLE NA MTU UNAMUAMBIA,SIO STAILI ZA KUDONOA-DONOANA.....TUSICHAFULIANE MAJINA..KAMA UNATAKA KUPASULIWA..WOTE WODI MNAIFAHAMU....WE 'KNIFE_BUTCHER' NA MWENZIO 'EXPLOSIVES',NATAKA NIWA-BATTLE WOTE NYI KWA PAMOJA!! NJOONI MANDE NIWAPASUE WOTE!! SIO MNADONYOA-DONYOA....
AKIWASHE MMOJA WENU..MSHUHUDIE SHUGHULI!!....AU LA ACHANENI NA HILI CHATA....!!

HE.KI.MA

HESHIMU KINA CHA MASHAIRI/WODI YA UPASUAJI
sijadonoasas hivi nadili na Mkongwe taff jamm kwanza we mtoto wa mama nitakurudia baadaye

#25 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 09 September 2003 - 08:42 PM

Waniita njuka wadhani gari ntazima
unaflow kama kipaji umeazima
Kina chako cha mashairi sikipi heshima
nyoo!! eti wajiita hekima
toa herufi h na e inabaki kima
Bucha usingizi nakunyima
masaa ishirini na nne uko wima
usiku na mchana unaweweseka
Mc napozi kwenye cyber nabaki nacheka
Nakutwisha ngumi nzito zaidi ya lumbesa
unabaki ulimi nje macho yananesa nesa
kona zote mawenge mawenge
usijaribu kuingia mkenge
Unakimbilia kubattle..eeh unadhani hizi mbio za mwenge
mc wajiona mjanja kichwani umenyoa denge
angalia jibaba usije ukallazwa milembe
We unapasua na nyembe
mi napasua na jembe
tena bila kudunga ganzi
Ukijibu hii nakupiga kitanzi
hatima yako kwenye fani ipo mikononi mwangu
Nakupa kubwa ukija wangu wangu
mi sidonyoi jibaba wacha kuongea kama changu
au we kaka poa walume wanakudonyoa

#26 Guest_knoka_*

  • Guests

Posted 10 September 2003 - 08:51 AM

Illa this is beautiful shit too...its word play .
tuffjam

ILLA said:

Nanukia ushindi zaidi yangu simtambui,
shahidi wangu mweyezi mungu,"oh god"
kama ni k-butcher nilisha mkinda siku nyingi,
hii hapa ni kama marudio nakuja na mbinu mpia,
kama ni ku-shock mc, crew yangu ni mobb deep,
move`s zangu ni kama nyoka kwenye majani,
jaribu ku-rewind lines hizi uone ulivyo chemsha,
una hisi joto kama ujawai kuona jua,
mbaka hapa walevi na waelevu wamesha nipata,
jaribu kwenda against mi nikupe taff,"huh"
wajulishe.........................


#27 Guest_knoka_*

  • Guests

Posted 10 September 2003 - 08:56 AM

now thats what i'm talkin' about Butcher....wordplay tactics...safi sana... chafuka tu jibaba.

tuff

#28 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 10 September 2003 - 10:06 AM

Mashairi yako yamechina
We kima nakuchanganya kiaina
Njoo kati tupambanishe vina
sikuchafulii jina wacha kuweka fitina
pumba mimi sizihudu
wacha kutema mashudu
Nani aliyekudonyoa mbona waongea madudu
Kuchonga sana kunaboa
unafanya battle inapoa
rusha mistari uwanjani
tuone kama uko fiti kwenye fani
mimi ndio zongwe usilete mizengwe
natibua akili zako we kikongwe
rapu kifalsafa hujaumbika kabla hujafa
sitaki kesi usinletee kifafa
kwangu we ni kama kimbofa
ingawa unaact kama kibofa
lakini huwezi chenji wako ulofa
mistari yako naichana vipande
naroga mashabiki kila upande
nawahendo maemcee hata wakija mande
siogopi mc gani wa kumfesi
naona soo kukunukisha kinyesi
ufikii level yangu naona kama unanigasi
natema gesi chafu..iite vepa huwezi kuepa
utabaki unanepa nepa
stimu zangu zinapanda kama stima
hapa ubavu huwezi kujipima...........

#29 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 10 September 2003 - 11:12 AM

kama unataka battle njoo shaa shaa
sio unaganda na kushangaa shangaa
nikichana kapela nakuacha unatambaa
usisogee karibu hiki kipaji balaa
Ntakuacha ndani ya cyber unabun'gaa
unakwenda chini mi nazidi kupaa
NareWind lines zako lakini bado hazijafaa
Dogo unapospit kwenye forum nasikia kinyaa
hii inaonyesha mashairi yako yana njaa
punch zinakulewesha kama umekunywa chan'gaa
kama utashinda labda ushindi wa mezani
tegemea kubebwa na wasio jua nini maana ya fani
.......................

#30 Guest_ILLA_*

  • Guests

Posted 10 September 2003 - 05:53 PM

Napo safari nafuka moshi na sio vumbi,
kwenye hili game nimesha zama siku nyingi,
k-butcher nazani una leta tani na sii skillz,
beti zako ziko off beat kama "Dikembe" jump shot,
mc`s wana over-hard mi na ku-use beti zangu,
cam-back yangu ni kama usiku umewadia,
mi ndio nightmare wako,fikra zime teka wengi,
kubebwa kwangu ni sifa nilizo nazo,
njaa nilio nayo niku-eat mc na ku-shock wakomavu,
kama kulewa nimesha lewa na ku-spit point,
na si trash ulizo tupa kwenya hii africanhiphop-board,
sizani kama j4 ana furahia kenge we.......................

#31 Guest_Tuffjam_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 12:47 AM

Ni kipindi tangu nimepotea/
Kuacha ngonjera nakuja Texas/
Lakini narudia fani kupoza kubonyea/
Vijana kulegea na kum'unga mteja/
Ni wazi vijana mpo "top leya".. ukianza na Butcher utakogea komesha/
Suuza ilimradi unachafua cypher..wako wasi na umati wacha... wenyewe watachochea/
Bila Hekima uhakika ni kama msiba na fani ikazikwa kisela/
Illa wakilisha kama mesenja kwani ni kijeba habari uliyobeba/
Jumla jumla tu hongera kwani hii saiti ni kama gym sogea/
Ukiilia nondo? utashiba msuli ukalemba/
Ukiilia horizontal? J4 ana haki ya kusema mmelega/
Hivyo mwanzo nilivyosema.. flow ni kaa kinyago.. chongea/
Hapo unapopata wazo ongea/
Au la upande wako naelekeza risasi bonyea.

Knoka

#32 Guest_HEKIMA_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 10:43 AM

Dogo !! hatushindani idadi ya vesi,ni uzani unaomata..kwa kuandika mavesi kibao yanayopea..haum-konvice,mtu yeyote kinda..istoshe unajichosha maana hii shughuli ndio kwanza ina-anza...soma hapo chini!!

oya!
Usiniltee mapozi, ni juu ya kichwa chako hii dogo-rukia Konzi!
hizo zako njozi…amka! Umedozi…uwe mgumu au bitozi
huwa sichagui-makatuni nawachuna ngozi..nachafua thread na kukuwaacha na vikoozi..
ni mkufunzi-ujuzi unaongezeka kwa pumzi,
battle nami ‘leo’ ka unataka uwe wa ‘juzi’ leta za kiluzi..maana hujatulia ka umetolewa bikra juzi –NAJERUHI KWA MILUZI!!
tungo nazotema zalipuka ka fataki! mi ningekuwa wewe ningeanza jichimbia Andaki,huwa sibakishi hata chembe ya mabaki!
Sitaniwi, sichekewi,sijaribiwi-silaha siishiwi-nang’ara bila kiwi..njoo nikuzibue ka wajifanya we kiziwi..una mapepe na upeo wako bao ‘teke’
nazungusha vina ka-mapanga njoo nikufyeke! Eti uko kina..dogo usitake ncheke..
‘mi’ ngingekuwa ‘nyinyi’ nisinge-battle na ‘mimi’ tungo hauzielewi njuka soma kwa makini..na pindi utapo mwenyewe utaingia mitini…
utakula kona, tungo zako zimeenda shule ila tatizo hazikusoma
pigo takatifu ninalokupa hutopona,ka ‘mkato’-uta’koma’
nakuacha umeachama, ni ka umepigwa tama ukafikia kuchutama
mkono kwenye shavu-ka Brown umeshika tama…shughuli ya wanaume hii niondoleeni huyu msichana…VICHWA hii lawama, sijui niseme kama
kwenda mapango ya Afghan kumsaka Osama!
maana hii hatari,nyumba ya nyasi inataka battle kibatari,nitaunguza hii thread muanze niona mi wa shari…chalii mi ni chatu na we ni fimbo ya mbali, nakunyima hewa kama shingo kwa kabari-uko katikati ya ajali na ukipona zali-kinyume ni umeachwa chali
kinda unihofie, ukiniona kwenye thread ukimbie, chimba site yeyote ikiwezekana ujifukie..nina historia chafu-hutopenda ijirudie, natunga vitanzi sio tungo-uning’inie-njuka usisikie!!!
We ni chekechea, waandika vishada-hivyo vina vinapea
acha jiongopea..njoo nikukojolee huo ubongo niutie mbolea

#33 Guest_knife_butcher_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 12:30 PM

vipi jibaba nani aliyesema tunashindana kuabanduka idadi ya vesi nyingi.Vunja jibaba sio unachonga.Tukienda namna hii unakuwa unaharibu battle.

#34 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 02:26 PM

kima ntakuumiza kinabo usinapandishie kibesi
unajiita mkufunzi lyrics zako kama kinyesi
kabla hujanifesi futa kwanza kamasi
Lamba hivi vina vichungu vyenye ukakasi
verse zangu babu kubwa jibaba huwezi pambanua
kinyeo chako nimekishakipanua
Nafanya domo lako pumba linacheua
kaa macho thread nishachafua
kabla ya kubattle na mimi unajifua
We Mchovu usinsoogelee ntakutifua
Sasa nakumaliza maana ushantibua
mashairi yangu yalienda shule hayakucheza yalibukua
kiwango kilizidi kukua na bado kinakua
Ndio maana kila battlin ushindi nanyakua
Usiwe mbishi jibaba sio kitu unajua
Unavunja kama mboga unapakua
usiniguse jibaba kiswazi ukipati..ngoja nirapu kimakua
Mchimba chumvi vipande nakurarua
kwenye hili game we ni kama shanta
nakupa pigo zito kila nukta
Mi kichwa cha treni we behewa nakuburuta
Nakuwekea limit ya oxygen unayotakiwa kuvuta
katika kucheza na maneno huwezi nipata
Nachana freestyle huku nanata
Naitwa k to tha BUCHA microphone shabshuta
Nin'ginia kama popo nikutungue
kama umo mashuani lazima utazama
unajawa na huzuni nikiflow washika tama
Natoa hukumu ukipenda ita kiama
kama kimbunga kwenye fani navuma
Zidi kurusha mawe hapa yatabuma
ukitazama mbele nakuvizia kwa nyuma
Nakuua kama nyani ..usoni siwezi kukutazama
Nipo stable huwezi nipiga mtama
Dogo mbona una kitete
mapepe kama mnyalokolo aliyetoka juzi makete
hili jabali..tafakari kabla ya kuattack
Mapanga yote yanadunda kukata hayataki
Mi narusha missiles we rusha fataki
Nalipua siachi hata kiduchu cha baki
Unguza thread bucha siungui
Wakisema nani mc wewe sikutambui
nachapa code nakuprogram huku wewe hujui
Nikenulie meno mi ndio adui
Nakudunga injection ya kimeta na ndui
unamtaja taja osama atakuoa ukijitanda baibui

#35 Guest_HEKIMA_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 05:01 PM

we ni bado dogo-subiri ukuwe kidogo,usilete zogo
kwa HEKIMA haugusi robo! inagongwa moja/mbili unapigwa tobo!
Bao kwa mikogo-battle na kisogo
wewe ni chalii..hata ka ujifanye hausikii..
angalia hii michezo labda baadae utatii..ni mazingaombwe ya vina nakutoza fee..
naandika vielelezo we kinda nafanya mfano
next time kabla ya ku-battle ufanye mkutano,mfanye mashauriano
napenyesha vichwa kwenye tundu za sindano! adhabu ninazotoa kwa waasi ni ka za Agano.....tena la kale,NAKUPASUA nakukushona kwa mshale
nakuacha na 'chale' kama vibaka wa Tandale..
njoo na 'explosives' kwa pamoja niwavishe sare
mi ni jua la Bongo,we ni mwali wa kipare..!
usijifanye unajua,maumivu hau-ignore maana idadi ni mvua
kama Soka,hii staili Katafunua!chomeka hicho kidali cha ndege nipasue kifua...nitachofanya si kikubwa ni kukukwapua-nakukupa Tik taka juu kwa juu kabla haujatua-kisha naruka na mbili nakukuchanua!!halaf nanyuti posti nikucheki kama wapumua....
napuliza ma-mc na kuwazima ka koroboi
nacheza na maneno-udogoni sikuwa na toy..sibahatishi bwa mdogo nakuacha hoi! vina navyochijia ma-mc huwa sinoi..
moto ninaokuwasha kinda hakika haupoi..piga magoti,omba msamaha
usini-annoy...

#36 Guest_Knife_butcher_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 07:57 PM

yes jibaba namna hiyo safi

#37 Guest_EXPLOSIVES_*

  • Guests

Posted 11 September 2003 - 10:00 PM

HIVI NI MARA NGAPI NIWAKUMBUSHE NYIE MAPUNGUANI/
KWENYE HIKI KIPAZA SAUTI MIMI SITAKI UTANI/
KILA BATTLE MKIANZISHA NAWAFURUMUSHA JUKWAANI/
MISTARI YENU MNAYO ANDIKA HAINA THAMANI/
NYIE WATOTO WA MAMA MIE NI TOTO LA MITAANI/
NAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI MPAKA WAPORI MSEME EEHH WAJAMENI/
CHUNGENI SANA MNACHOSEMA MSIJE MKAINGIA MTEGONI/
ILLA,HEKIMA NA BUTCHER UNGENI MAJESHI LAKINI BADO HAMNIKUTI/
VUNJA VUNJA LIMEINGIA JIHADHARINI WENYE VIJUMBA VYA MAKUTI/
UKICHEZA NA EXPLOSIVES UTAJISHTUKIA UNA LAMBA BUTI/
HII NI AJIRA YANGU NAITILIA MAANANI NAIVALIA SUTI/
MIC IMEGANDA MKONONI UJUMBE NAOTOA NI MADHUBUTI/

#38 Guest_Knife butcher_*

  • Guests

Posted 12 September 2003 - 09:54 AM

halo mshikaji unabattle na nani mbona hueleweki

#39 Guest_HEKIMA_*

  • Guests

Posted 12 September 2003 - 10:40 AM

Knife_butcher said:

yes jibaba namna hiyo safi

usijifanye wewe Refa!! endelea NIKUPASUE KINDA MANYOYA WE!!

#40 Guest_HEKIMA_*

  • Guests

Posted 12 September 2003 - 10:59 AM

EXPLOSIVES said:

HIVI NI MARA NGAPI NIWAKUMBUSHE NYIE MAPUNGUANI/
KWENYE HIKI KIPAZA SAUTI MIMI SITAKI UTANI/
KILA BATTLE MKIANZISHA NAWAFURUMUSHA JUKWAANI/
MISTARI YENU MNAYO ANDIKA HAINA THAMANI/
NYIE WATOTO WA MAMA MIE NI TOTO LA MITAANI/
NAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI MPAKA WAPORI MSEME EEHH WAJAMENI/
CHUNGENI SANA MNACHOSEMA MSIJE MKAINGIA MTEGONI/
ILLA,HEKIMA NA BUTCHER UNGENI MAJESHI LAKINI BADO HAMNIKUTI/
VUNJA VUNJA LIMEINGIA JIHADHARINI WENYE VIJUMBA VYA MAKUTI/
UKICHEZA NA EXPLOSIVES UTAJISHTUKIA UNA LAMBA BUTI/
HII NI AJIRA YANGU NAITILIA MAANANI NAIVALIA SUTI/
MIC IMEGANDA MKONONI UJUMBE NAOTOA NI MADHUBUTI/

nadhani unahitaji kusoma tena hii freestyle.....umekataa kujiunga na Butcher,basi njoo peke yako...NIKURARUE kinda WE! Kiwashe....!

Dogo,huna beti na hilo jina lako pia FEKI!
kumtaja HEKIMA kwenye vina vyako ni misteki
nitachofanya next time ni kukunyang'anya vyeti
siwezi battle nawe,unavyoandika havieleweki
hata kukujibu sio utani ninaona uzia
kama ulivyoambiwa,hilo Bomu litakulipukia
haugusi level yangu hata kama ukarukia
ukileta mapambano,poa! utafanywa mfano
vina ni masumbwi nilishasema-ni kibano!
kachukue wengine kama wewe-muwe watano....

KINDA MANYOYA WE!!





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users