MISTARI....MISUMALI...KAMALI...
#61
Posted 10 August 2007 - 12:16 PM
jitahidi kwa kaidi kibeto nikwepe ka TRA na walipakodi
mtambo huu tayari ushasetiwa kufuta shombo
piga tambo bado kingo za fikra yako mapambo
sio kisirisiri huu ulimbo unakunasa ka bisu kwa tumbo
niko tayari kukukabili niko kamili tafakari umekanyaga misumari
ilhali uko pekupeku nakuchinja dukuduku kama kuku
bado nakuona shake shake kama kibuku!!!
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#62
Posted 11 August 2007 - 02:37 AM
ntakuinua tu mwana kuanguka kwako ni lazima,
iwe leo au kesho mi nipo nshapima,
ntakuinua tu ila sema siwezi badili utabiri ilhali ndo mwendo wako kitasfiri,
hata mpofu anaijua chungu ya hiyo shubiri na ndo chako kituo katika hii safari
wakafiri ka mie ni shwari ka azaliwapo mtoto wa kiume kutahiri,
gari kwenda mbali faida kwa wakaa karibu na huko mbali wote watapanda au siyo mshairi
mwenye mashaka yasisiyo sitiri? hebu piga chini ndo hapa ni mwisho na si lelemama hilo ni dokezo sabiri,
na mwisho wa yako safari
#63
Posted 14 August 2007 - 12:52 PM
uzito huna jione puto huu ni moto mkubwa kwako we mtoto
nakuachia ndoto za mchecheto huu mkito ni bila instrumento
taharuki umekivaa kisiki hiki mwenyewe unaparamia mkuki???
bwamdogo nakushambulia kidogo tu usione kama kundi la nyuki
hamaki umeamsha hasira lukuki tahadhari usijetoka nduki
n'lishasheheni fataki kitambo hii michano hii mitambo huwezibaki
itfaki zangu kiitikadi endelea kutaradadi huwezi kwepa radi zisizoidadi.....
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#64
Posted 28 August 2007 - 03:36 PM
maswali hakuna mida mibaya lindoni umejimix na kunyuka, ndani na kusweka
uwe mwema raia,jambazi au kibaka, majibu yote kukipambazuka,
eti mi ndo last dyte!!ushaumia mwana cheki hapa au pale mi sipo mbona unamaka
mtoto wa momba ndo wanaume dunia haa huu ndo ulimwengu shujaa,
ka nilikupa bia si kwamba we rafiki, ni mzuka wa kijamaa muamala ukiwa umejaa,
tena tele mambo yote monde lete tule..last dyte hivi kweli bado upo,
au ni kivuli ndo kipo, kimekalia kopo, henu piga makofi ka shwari..
usinune mpwa mi wako mwanamistari.
oh ni j4 nikadhani ijumaa nikakupe japo safari...
mamaland au 2000 grocery? unako sign lako daftari
njoo na njaa starter ipo leo ni mtori ciao
#65
Posted 05 September 2007 - 02:05 PM
sifati zako hoja tungi bwabwaja zama kwenye hizi futi
ona kizungumkuti,naona kwa mbali unaonyesha ishara ya saluti
umejitusu pabaya ila nakuchana nusunusu kwa mikono situmii ndusu
kwenye hii topic nakuweka mahabusu ujio wangu usiungoje ka wa yesu
mad wakujisifu hili bifu naliona hafifu ila mi kumbuka ndio kiongozi wako mwadilifu
halafu ntakuongozaga makilakitu mzee kama viumbe dhaifu
sichezi rafu_tazama juu_chini sarafu inasimama sasa unazama....kima tena wima..
endelea kupima.
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#66
Posted 19 September 2007 - 10:55 AM
ama mnadhani mkionyesha vifua mtamshtua ndovu vitani
ka kumlaumu aliyejenga ukipiga ngumi ukutani
usione unatambaa ukadhani unaweza kupaa angani
haya ndio mazishi ya whack mczs
nimechoka kuwatazama hiphop mkiitia nuksi
mwajipendekeza ka mapogo mnadhani mtapata soko
kujipiga vifua mnadai respect wanoko
kumbukeni sio kila cha mvunguni hupatikana hata ukiinama
mwishowe mtakata viuno maana angazetu hatuwezi zama
AMEEN.
:evil:
#67
Posted 19 November 2007 - 01:53 PM
mzawa mkazi mjuzi
kiongoz mkombozi mwangamizi
mtimizi c mtenguzi
mnazi umepata mkwezi
mtatuzi kati ya kizazi
kisichofata maelekezi
wapuuzi hamna mabawa
mnataka fika juu bila ngazi
angaza twende sawa
umeona nini safi au masizi!
kazi makuzi mkufunzi chizi
mimi.... ndimi.... sivumi.....
mizani ya unyoya huwezi p ma tembo
rym zako lyn kama mafuta kimbo
mi ndo yakaribu fimbo
nyoka baki chimbo
hii crim jisurubu c unapenda urembo
sema THANXX! :twisted:
T.M.K akademy-non shobo squad
#68
Posted 22 November 2007 - 09:53 AM
ila jibu dogo humfanya kuku abusu mauti
kwakukwea mnazi haimaanishi utaitafuna nazi
cheky unavyoporomoka si heri ungetumia kitanzi
sikizia mshindo wa kimya ghafla ka mwizi
nakuibia uhuru oo0h haikukuokoa hirizi
wanaojua maana ya mziki wanafarijika na imani zangu
nao wafuasi wa dini ya chuki wanatamani wangekuwa mungu
vina vya kubahatisha yaani vina viso maana
ka kumulika kurunzi ujue yalofichwa moyoni na haitawezekana
#69
Posted 27 November 2007 - 09:26 AM
mtaani HIPHOP dini
baini wa pembeni
ili umjue wa mbali :roll:
usirukie bahari
c kila ufukwe beach
maisha kabali
kitaa ndo yangu pich
zingua upate kibari
cha kulibusu kaburi :shock:
damuni nimejaa zaburi
mmoja mstali kwako ajali :cry:
T.M.K akademy-non shobo squad
#70
Posted 27 November 2007 - 09:39 AM
mtaani HIPHOP dini
baini wa pembeni
ili umjue wa mbali :roll:
usirukie bahari
c kila ufukwe beach
maisha kabali
kitaa ndo yangu pich
zingua upate kibari
cha kulibusu kaburi :shock:
damuni nimejaa mithali
mmoja mstali kwako ajali :cry:
ni kama zito kabwe
mafisadi kiwewe!
vile nakata zako ngebe
kusanya vyako jibebe
R.I.P mizani kama dube :twisted:
T.M.K akademy-non shobo squad
#71
Posted 06 December 2007 - 11:10 AM
unapumzi nusunusu shingo nimeikaba kwapani
yaani usikimbilie ugali ka bado maziwa ndo yapitayo shingoni
mizani sizikiki ila nabadili wanaodhani watanifukia mimi
sa kaa chini ukue kimawazo misitari imee ndevu
la sivyo usinisumbue na misitari yako rojo ka dafu.pumbavu :evil:
#72
Posted 13 December 2007 - 09:04 AM
we c wa kwanza kupatwa na yangu mawe
hizi flo zinakufanya fake unengue
jiengue pungua endelea nikutengue
kiuno unacholingia!umeingia kilinge
kisicho! kenge huwezi kuwa mamba
ambaa na hii kamba kajinyonge
we kamasi nikupenge zengwe
huna hoja ka kingunge!
niite dokta chifu matunge
sindano ya sumu sogeza tako nikudunge :lol:
T.M.K akademy-non shobo squad
#73
Posted 20 December 2007 - 10:42 AM
nshasambaza kasa hii sumu nawachecki mnavyonasa
nna skills kihiphop kwa kipofu hizi levo ana acha kupapasa
angalia kabla hujaumia nakuachia magumashi
ni sawa na mvuta fegi anavyobwenga huoni moshi
usijiulize mara mbili, mara ya tatu nakugonga bila kiatu
wanaita pekupeku,tafakari huu ni mtama nawatega ka kuku
mistari ni ya kigaidi kamwe sishushi mdadi nararua ka radi
nshatoa displini usinione nimechill we ni budi kutia akilini
nasepa kuliko upepo afu napatika night nione popo....
Yeah.........
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#74
Posted 18 April 2008 - 09:55 AM
risasi ya kasi, yabisi ka uzalendo
konde la mwendo mdundo,uskonde
kibonde! kibonge kidoleni_bange!
pima uelewa zima pepewa hewa..
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#75
Posted 24 April 2008 - 12:22 PM
#76
Posted 12 May 2008 - 10:03 AM
mali ya wana kando ya bahari
kama zali wamekijua na wale wa mbali
fahari kujua kiswahili...zake moja mbili
kama vitendawili na mithali
hiki kizuri hakijiuzi
hiki mzuka kamili kwenye yangu makazi
HOI!!kiswahili .....one
T.M.K akademy-non shobo squad
#77
Posted 13 May 2008 - 02:56 PM
taradadi hali lijali misosi mabosi
wepesi tupu boksi jua ungua utosi pumua
itikadi wasiwasi midadi radi kemkem
chemchem rasilimali watukufu watukufuru
bendera uhuru juu wafu halafu msururu
lowea lewea wakfu milele ubia tanzania
tukufu mbele maana kitanzi cha wenye masuti
ganzi wananchi mauti taifa maafa vijisenti
balaa n"gatuka geuka shujaa tukuka stuka
we..bun"gaa mkwanja watambaa vibatiki shangaa
funzo komaa hayawani na kichaa: mafuta ya taa na mkaa
kiberiti cha gesi zika tetesi mashahidi halisi na kesi..........PA1
DYTISM......
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#78
Posted 14 May 2008 - 09:50 AM
viongozi na vitendo vya kihuni
kipimo cha ubwege wetu umasikini
nchini chini uswahilini elim duni
jembe la mkono vijijini....
slaa kaisoma ramani moto bungeni
mwamko wa kizawa vichwani
chamani malumbano alindwe nani
kwa nini na ana nini hadi lini tutakua na makufuli mdomoni
ugoni anakamatwa mzini na binti-madini
kunyongwa ndo suluhisho la mwisho
uamisho ama kujiuzuru ni kichekesho
kesho mwingine hatoogopa kufuja posho
wakati wa uamsho ni vitendo sio vitisho
........social concious........................... :shock:
T.M.K akademy-non shobo squad
#79
Posted 29 August 2008 - 03:05 PM
KWA MVUTA FEGI NI LAZIMA LITOKEE JIVU BAADA YA MOSHI
WALIOTNGULIA DAIMA HUACHA MAKOVU
KWA JAMII NA HII NI ASILIA HUTAKIWI KULIA
NI BORA KUWAOMBEA KWA MOLA SABABU KILA MTU LAZIMA ATAREJEA.....
PA1_
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
#80
Posted 30 August 2008 - 08:33 AM
gangstarr bado naroll ado ado naruka vigingi nawapiga bao bila kuingia kingi/
kimsingi mfuko wangu wa kulia na kushoto ushasheheni masimbi/
nna shillingi kinachofuata we pimbi kaa mbali bado nna vina vingi/
nimevaa kihuni ila bwamdogo nina busara kama madingi/
bongo fleva naipiga kama mitungi mirungi mibangi/
nacheza kwenye maji kubabake siloani usipime hiki kipaji/
narudi kuendeleza mauaji niogope babu sababu hii kwangu dibaji/.......
pa1
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












