Jump to content


MISTARI....MISUMALI...KAMALI...


92 replies to this topic

#61 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 10 August 2007 - 12:16 PM

spidi yako kipofu naku "rule" na hofu ikibidi
jitahidi kwa kaidi kibeto nikwepe ka TRA na walipakodi
mtambo huu tayari ushasetiwa kufuta shombo
piga tambo bado kingo za fikra yako mapambo
sio kisirisiri huu ulimbo unakunasa ka bisu kwa tumbo
niko tayari kukukabili niko kamili tafakari umekanyaga misumari
ilhali uko pekupeku nakuchinja dukuduku kama kuku
bado nakuona shake shake kama kibuku!!!
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#62 bahati

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 9 posts

Posted 11 August 2007 - 02:37 AM

ntakuinua tu mwana shaka ondoa, ulelekeo wako dili kwa sheikh yahya nshasoma,
ntakuinua tu mwana kuanguka kwako ni lazima,
iwe leo au kesho mi nipo nshapima,
ntakuinua tu ila sema siwezi badili utabiri ilhali ndo mwendo wako kitasfiri,
hata mpofu anaijua chungu ya hiyo shubiri na ndo chako kituo katika hii safari
wakafiri ka mie ni shwari ka azaliwapo mtoto wa kiume kutahiri,
gari kwenda mbali faida kwa wakaa karibu na huko mbali wote watapanda au siyo mshairi
mwenye mashaka yasisiyo sitiri? hebu piga chini ndo hapa ni mwisho na si lelemama hilo ni dokezo sabiri,
na mwisho wa yako safari

#63 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 14 August 2007 - 12:52 PM

nageuka mafioso kigadhabu kukufunza adabu rapa yoso
uzito huna jione puto huu ni moto mkubwa kwako we mtoto
nakuachia ndoto za mchecheto huu mkito ni bila instrumento
taharuki umekivaa kisiki hiki mwenyewe unaparamia mkuki???
bwamdogo nakushambulia kidogo tu usione kama kundi la nyuki
hamaki umeamsha hasira lukuki tahadhari usijetoka nduki
n'lishasheheni fataki kitambo hii michano hii mitambo huwezibaki
itfaki zangu kiitikadi endelea kutaradadi huwezi kwepa radi zisizoidadi.....
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#64 bahati

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 9 posts

Posted 28 August 2007 - 03:36 PM

Nipo tena ka askari zamu yangu ndo hii kaka,
maswali hakuna mida mibaya lindoni umejimix na kunyuka, ndani na kusweka
uwe mwema raia,jambazi au kibaka, majibu yote kukipambazuka,
eti mi ndo last dyte!!ushaumia mwana cheki hapa au pale mi sipo mbona unamaka
mtoto wa momba ndo wanaume dunia haa huu ndo ulimwengu shujaa,
ka nilikupa bia si kwamba we rafiki, ni mzuka wa kijamaa muamala ukiwa umejaa,
tena tele mambo yote monde lete tule..last dyte hivi kweli bado upo,
au ni kivuli ndo kipo, kimekalia kopo, henu piga makofi ka shwari..
usinune mpwa mi wako mwanamistari.
oh ni j4 nikadhani ijumaa nikakupe japo safari...
mamaland au 2000 grocery? unako sign lako daftari
njoo na njaa starter ipo leo ni mtori ciao

#65 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 05 September 2007 - 02:05 PM

najiona mwenye bahati kukutafuna kilaini kama biskuti
sifati zako hoja tungi bwabwaja zama kwenye hizi futi
ona kizungumkuti,naona kwa mbali unaonyesha ishara ya saluti
umejitusu pabaya ila nakuchana nusunusu kwa mikono situmii ndusu
kwenye hii topic nakuweka mahabusu ujio wangu usiungoje ka wa yesu
mad wakujisifu hili bifu naliona hafifu ila mi kumbuka ndio kiongozi wako mwadilifu
halafu ntakuongozaga makilakitu mzee kama viumbe dhaifu
sichezi rafu_tazama juu_chini sarafu inasimama sasa unazama....kima tena wima..
endelea kupima.
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#66 mizani

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • Locationmombasa,kenya

Posted 19 September 2007 - 10:55 AM

huwezi kuzima moto kwakuweka mkono motoni
ama mnadhani mkionyesha vifua mtamshtua ndovu vitani
ka kumlaumu aliyejenga ukipiga ngumi ukutani
usione unatambaa ukadhani unaweza kupaa angani
haya ndio mazishi ya whack mczs
nimechoka kuwatazama hiphop mkiitia nuksi
mwajipendekeza ka mapogo mnadhani mtapata soko
kujipiga vifua mnadai respect wanoko
kumbukeni sio kila cha mvunguni hupatikana hata ukiinama
mwishowe mtakata viuno maana angazetu hatuwezi zama
AMEEN.
:evil:

#67 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 19 November 2007 - 01:53 PM

mjasili asili akili mali
mzawa mkazi mjuzi
kiongoz mkombozi mwangamizi
mtimizi c mtenguzi
mnazi umepata mkwezi
mtatuzi kati ya kizazi
kisichofata maelekezi
wapuuzi hamna mabawa
mnataka fika juu bila ngazi
angaza twende sawa
umeona nini safi au masizi!
kazi makuzi mkufunzi chizi
mimi.... ndimi.... sivumi.....
mizani ya unyoya huwezi p ma tembo
rym zako lyn kama mafuta kimbo
mi ndo yakaribu fimbo
nyoka baki chimbo
hii crim jisurubu c unapenda urembo
sema THANXX! :twisted:
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#68 mizani

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • Locationmombasa,kenya

Posted 22 November 2007 - 09:53 AM

teke za kuku hazitikisi msuli wa nyati
ila jibu dogo humfanya kuku abusu mauti
kwakukwea mnazi haimaanishi utaitafuna nazi
cheky unavyoporomoka si heri ungetumia kitanzi
sikizia mshindo wa kimya ghafla ka mwizi
nakuibia uhuru oo0h haikukuokoa hirizi
wanaojua maana ya mziki wanafarijika na imani zangu
nao wafuasi wa dini ya chuki wanatamani wangekuwa mungu
vina vya kubahatisha yaani vina viso maana
ka kumulika kurunzi ujue yalofichwa moyoni na haitawezekana

#69 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 27 November 2007 - 09:26 AM

naporomoka kutoka chini :D
mtaani HIPHOP dini
baini wa pembeni
ili umjue wa mbali :roll:
usirukie bahari
c kila ufukwe beach
maisha kabali
kitaa ndo yangu pich
zingua upate kibari
cha kulibusu kaburi :shock:
damuni nimejaa zaburi
mmoja mstali kwako ajali :cry:
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#70 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 27 November 2007 - 09:39 AM

naporomoka kutoka chini :D
mtaani HIPHOP dini
baini wa pembeni
ili umjue wa mbali :roll:
usirukie bahari
c kila ufukwe beach
maisha kabali
kitaa ndo yangu pich
zingua upate kibari
cha kulibusu kaburi :shock:
damuni nimejaa mithali
mmoja mstali kwako ajali :cry:
ni kama zito kabwe
mafisadi kiwewe!
vile nakata zako ngebe
kusanya vyako jibebe
R.I.P mizani kama dube :twisted:
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#71 mizani

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • Locationmombasa,kenya

Posted 06 December 2007 - 11:10 AM

unaporoka kutoka chini yaani huwezi kuhimili joto la ndani
unapumzi nusunusu shingo nimeikaba kwapani
yaani usikimbilie ugali ka bado maziwa ndo yapitayo shingoni
mizani sizikiki ila nabadili wanaodhani watanifukia mimi
sa kaa chini ukue kimawazo misitari imee ndevu
la sivyo usinisumbue na misitari yako rojo ka dafu.pumbavu :evil:

#72 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 13 December 2007 - 09:04 AM

acha mayowe na kiwewe
we c wa kwanza kupatwa na yangu mawe
hizi flo zinakufanya fake unengue
jiengue pungua endelea nikutengue
kiuno unacholingia!umeingia kilinge
kisicho! kenge huwezi kuwa mamba
ambaa na hii kamba kajinyonge
we kamasi nikupenge zengwe
huna hoja ka kingunge!
niite dokta chifu matunge
sindano ya sumu sogeza tako nikudunge :lol:
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#73 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 20 December 2007 - 10:42 AM

sihubiri.....usidhani ni misa massege zangu ni zaidi ya kanisa
nshasambaza kasa hii sumu nawachecki mnavyonasa
nna skills kihiphop kwa kipofu hizi levo ana acha kupapasa
angalia kabla hujaumia nakuachia magumashi
ni sawa na mvuta fegi anavyobwenga huoni moshi
usijiulize mara mbili, mara ya tatu nakugonga bila kiatu
wanaita pekupeku,tafakari huu ni mtama nawatega ka kuku
mistari ni ya kigaidi kamwe sishushi mdadi nararua ka radi
nshatoa displini usinione nimechill we ni budi kutia akilini
nasepa kuliko upepo afu napatika night nione popo....
Yeah.........
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#74 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 18 April 2008 - 09:55 AM

naishi kibishi kiuhalisi si rahisi
risasi ya kasi, yabisi ka uzalendo
konde la mwendo mdundo,uskonde
kibonde! kibonge kidoleni_bange!
pima uelewa zima pepewa hewa..
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#75 Emigee

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 178 posts

Posted 24 April 2008 - 12:22 PM

Moyo umekua mwepesi, sababu ya vitu vingi tumevitupilia mbali. Wakati wowote ule unapohitaji vitu fulani, bidii ni kitu cha lazima. Kenya ni inchi ya watu wengi wenye kabila mbali mbali. Na wenye mali na hali mbali mbali. Mimi hoja kuu nikukua mkali mithili ya pili pili. Ukipita mahala flani unawawacha watu waki lia nikama wakati vitungu vinatayarishwa. Sitaki kuonekana nikama nimepoteza wanaosoma mawazo haya lakini kuaelimisha kwa kiwango flani. Ndiyo badaye nisikiye flani wa flani alibarikiwa kwa kusoma yale maandishi niliyoandika. Lugha ni mgumu mno lakini ni bora kushida kutosoma am kuandika mawazo niliyonayo. Nataka niwemarufu kwenye msafara, jina liweze kungara msafada, litambulike kati ya majina marufu duniani. Wakati Professor Jay, Juma Nature na Solo Thang wanapoitwa, jina langu liweze kutajwa wakati huo. Mimi si mwana bongo lakini ni kujaribu tu kutunza tamaduni hilo njema. Kusema ninaweza kusema mpaka keshona hayo yote yawe yenye vina na maana lakini lile nililopenda haliwezi kwenda. Walinena kuwa siwezi andika swahili lakini nipo na hata sijashtuka akamwe. Nitalichambua lugha ubaki umeshangaa. Ah! Umezubaa, nabado niko nimchanganyiko ya vitu vingi duniani. Mtu wa kabila langu haweze kuandika lugha jinsi hii, hapana. Ni mapendeleo niliyonayo moyoni. Hebu tazama jamani, fani blia mimi itakua nikama utani, basi hamna mahali niendapo, niko mahala humu, ndani ya fani yani nimedunga hema, nime tia nanga na niko tayari na njora kujilinda, kujikinga kwa wale wanaofikiri mimi ni wa makamo na sifai mahali humu. Watu wa makao wafanya fani yangara, na Professor Jay aliwasimulia. Jamani kuweni makini ni bora kusikia kushinda kutosikia na kupotea, hamja sikia elimu ni nguvu basi tia fora, tia manani kwa kila utendacho, kwa vile maisha tunayoishi si yetu sisi bali ni kwa wakati huo huo kisha itatoweka. Mahala upo na ulifikia mshukuru Mola. Jamani ni uandishi wa lugha

#76 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 12 May 2008 - 10:03 AM

mswazi swahili asili kuongea kibali
mali ya wana kando ya bahari
kama zali wamekijua na wale wa mbali
fahari kujua kiswahili...zake moja mbili
kama vitendawili na mithali
hiki kizuri hakijiuzi
hiki mzuka kamili kwenye yangu makazi
HOI!!kiswahili .....one
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#77 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 13 May 2008 - 02:56 PM

fedhuli fadhili sisi ufisi ufisadi
taradadi hali lijali misosi mabosi
wepesi tupu boksi jua ungua utosi pumua
itikadi wasiwasi midadi radi kemkem
chemchem rasilimali watukufu watukufuru
bendera uhuru juu wafu halafu msururu
lowea lewea wakfu milele ubia tanzania
tukufu mbele maana kitanzi cha wenye masuti
ganzi wananchi mauti taifa maafa vijisenti
balaa n"gatuka geuka shujaa tukuka stuka
we..bun"gaa mkwanja watambaa vibatiki shangaa
funzo komaa hayawani na kichaa: mafuta ya taa na mkaa
kiberiti cha gesi zika tetesi mashahidi halisi na kesi..........PA1

DYTISM......
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#78 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 14 May 2008 - 09:50 AM

mzawa uzalendo damuni
viongozi na vitendo vya kihuni
kipimo cha ubwege wetu umasikini
nchini chini uswahilini elim duni
jembe la mkono vijijini....
slaa kaisoma ramani moto bungeni
mwamko wa kizawa vichwani
chamani malumbano alindwe nani
kwa nini na ana nini hadi lini tutakua na makufuli mdomoni
ugoni anakamatwa mzini na binti-madini
kunyongwa ndo suluhisho la mwisho
uamisho ama kujiuzuru ni kichekesho
kesho mwingine hatoogopa kufuja posho
wakati wa uamsho ni vitendo sio vitisho
........social concious........................... :shock:
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad

#79 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 29 August 2008 - 03:05 PM

MIILI TULIYONAYO LEO NDIO KESHO MAFUVU
KWA MVUTA FEGI NI LAZIMA LITOKEE JIVU BAADA YA MOSHI
WALIOTNGULIA DAIMA HUACHA MAKOVU
KWA JAMII NA HII NI ASILIA HUTAKIWI KULIA
NI BORA KUWAOMBEA KWA MOLA SABABU KILA MTU LAZIMA ATAREJEA.....

PA1_
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:

#80 LAST DYTE

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 242 posts
  • LocationSluMz oF HeLL

Posted 30 August 2008 - 08:33 AM

dish!dish!dish!natoa mlio wa ngumi kama kwenye movie za kihindi/
gangstarr bado naroll ado ado naruka vigingi nawapiga bao bila kuingia kingi/
kimsingi mfuko wangu wa kulia na kushoto ushasheheni masimbi/
nna shillingi kinachofuata we pimbi kaa mbali bado nna vina vingi/
nimevaa kihuni ila bwamdogo nina busara kama madingi/
bongo fleva naipiga kama mitungi mirungi mibangi/
nacheza kwenye maji kubabake siloani usipime hiki kipaji/
narudi kuendeleza mauaji niogope babu sababu hii kwangu dibaji/.......

pa1
I'm a weapon that fires/
Lyrical projectiles with no mercy/
I'm cold blooded like reptiles/
Touch a pregnant bitch and make her give birth to a dead child/___IMMORTAL TECHNIQUE:





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users