Jump to content


KITAMBULISHO


1 reply to this topic

#1 J-Dogg

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 229 posts

Posted 30 January 2006 - 01:01 AM

Jicho langu la tatu limeshaona mambo mengi/
darubini la ubongo wangu unatazama mambo mengi/
dunia la leo imechoka,hatujui tunaelekea wapi jamani/
hatujafungwa pingu wala kengele lakini bado tupo utumwani!/
kama ulidhani tupo huru,ulikosea ndugu/
wanasiasa wanasema vijana wamedata/
wanadhani si wote ni walevi na wahuni--wanapenda sana kutupaka!/
--wazee wetu,msiiponde bongo flava, si muziki wa kihuni ni hali halisi ya maisha/
na tena inatusaidia sana si vijana kwa kutupa ajira/
ni muziki wetu kwa ajili yetu/
wasanii ni kama walimu wenye dili/
tunazidi kusonga mbele,hatuangalii nyuma wala chini/
tuongeze bidii jamani,tusiache kukamua/
nawakilisha masela wote,wanaokaa uswahilini na hata wale wa kishua/
nawasihi msikonde,muwe shupavu na kuzingatia utu/
J-Dogg, nipo jikoni napakua ngoma za kufa mtu/
kuna wanaonifagilia na wengi wasionifagilia/
lakini mimi siwamaindi wapinzani/
kila siku napanda chati/
Mwenyenzi Mungu hunibariki na kwa kila pumzi nampa shukrani/
jiulize siku ya hukumu utakwenda wapi??/
utaelekea mbingu au utabusu shavu la shetani??/
siku zinapita na mabadiliko siyaoni/
tumepagawa na pepo la starehe na inaelekea hatoki/
lakini tusikate tamaa,siku zote tembea na kifua mbele/
ongea na matendo,funga mdomo na wacha kelele.......au sio!!!
Knowledge isn't everything...how you use it is.

#2 vinama'na

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 159 posts
  • LocationNyanDa Za JuU KuSini -Green CitY

Posted 05 April 2006 - 08:44 AM

usipojua unakoelekea,
wezi jua ulipotokea,na wapi unaelekea,
so take care,we kimelea,cha bacteria,
fristyli inakufua,bado hujajua,
wataka nyanyua hisia,
za watu tulo na nia,
sema hujui jinsi ya kuingia,
so kimbia,elekea
elewkea kwenye kujua,tambua,
wakati unaotembea,
ZAO LA MTAA
T.M.K akademy-non shobo squad





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users