Jump to content

Kora Awards 2002

5 replies to this topic

#1 Guest_Chuki XL_*

  • Guests

Posted 20 August 2002 - 01:09 PM

:evil:

Hilooo...
http://www.koraaward...asp?l=en&y=2002

hakuna hata mtanzania! Pia Wakenya walioingia sijui mabishoo gani tena.

#2 bongonian

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 60 posts
  • LocationArusha,Tanzania

Posted 20 August 2002 - 03:30 PM

kwa kweli inatiauchungu kuona hiyo kora kila mwaka hatujawihi kutoa mshiriki (nominee) hata mmoja ingawa sina uhakika na staili yao ya kuchagua hao washiriki sema niliwahi kusikia msanii anatakiwa apeleke kazi yake kitu ambacho kama ni kweli basi itakuwa ngumu kupata wshindi wa kweli si kwa africa mashariki tu bali nadhani kwa africa nzima.

pia hiyo kora kwa aina fulani inamapungufu mengi tu kwa upande wangu ..kwani kama ni ya africa inakuwaje hakuna nchi nyingine inayopewa nafasi ya kuyaanda zaidi ya sauzi africa au sauzi ndio africa yenyewe...

pili kwenye swala la watumbuizaji ..mimi kama ningetegemea wasanii wa africa wangepewa nafasi kubwa katika utumbuizaji kwenye ile siku yenyewe ya kutoa zawadi kwani ndio siku ambayo watu wengi wanaangalia zaidi ya ile siku moja kabla ya utoaji tunzo kama walivyofanyiwa akina JD....kwani siku ya tunzo zenyewe wanaoja kwenye utmbuizaji ni wasanii wengi kutoka africa kiasi kwamba hata hao wa kwetu wanafunikwa.

Nadhani Kora ingeangaliwa upya kwa ujumla ili kiwe kioo cha kutangaza muziki wa africa

#3 Guest_kisiwa_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 09:18 AM

mzzee bongonian kama unavyo jiita mwenyewe
umeongea point ila mwanangu muziki wa east africa tuna utangaza sana ndani ingekua vyema basi wana muziki wetu wangefanya ziara nje ya nchi
kutembelea kusin mwa africa,
watu kupeana ujiko basi majina makubwa
na kua na mademu basi wanamuziki wamemaliza
wangeunda hata umoja wao
wamebaki kutambiana mimi zaidi huyu kaiga nyimbo yangu basi !!!
mbona wanamuziki wa north africa wanakuja tushindwe sisi ni swali la kujiuliza
kuhusu uwenyeji SA inastahili kutokana na uchumi wake
sasa mzee unataka hilo tamasha lifanyike DODOMA au >?
tim!!!!
nduki!!!

#4 bongonian

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 60 posts
  • LocationArusha,Tanzania

Posted 28 August 2002 - 08:09 AM

oya kisiwa nimekuelewa pale unaposema wasanii wetu hawajitangazi sana nje ya bongo lakini pia kwa upande fulani sasa hivi nyimbo zao zinajitahidi kusikika hata nje ya bongo siunaelewa tekelinalokujia (technolojia) ...hilo swala la kujitangaza kimataifa nadhani lilishawahi kuzungumziwa kipindi cha nyuma na utaona kuna uzembe wa wasanii na pia vikwazo ambavyo vinakuwa ni vigumu kwa wasanii wenyewe kuvivuka.

turudi kwenye sehemu ya kora kufanyika.....nadhani waandaaji walipofikiria swala la kora walijua hali halisi ya africa kwani wao pia ni waafrika walio afrika ...hivyo sitegemei hicho ndio kigezo cha kuweka tamasha hili Sauzi kila mwaka....nia m\ni kutangaza na kuwatunza wasanii na kazi zao sio siasa ya ...kwani kama unafahamu vizuri hiyo sauzi inaweza kuwa kati ya nchi zilizoendelea sana afrika na pia ni moja ya nchi zilizo na umaskini wa kutupwa afrika...... kumbuka hizo awards zinafanyika ndani ya ukumbi sio barabarani hivyo hata hapo tanzania inaweza kuwa waandaaji kama kukiwa na fungu la maandalizi kutoka huko kora.

#5 Guest_kisiwa_*

  • Guests

Posted 28 August 2002 - 08:25 AM

mzee bongonian labda sikukuelewa au nilikua sijaelewa yaani nchi muandaaje wa hii kora kuna fungu la pesa analopata kutoka huko kora ili kuandaa hilo tamasha mzee?au nchi husika ina jitegemea
peace

#6 Guest__*

  • Guests

Posted 15 November 2002 - 11:35 AM

bongonian said:

kwa kweli inatiauchungu kuona hiyo kora kila mwaka hatujawihi kutoa mshiriki (nominee) hata mmoja ingawa sina uhakika na staili yao ya kuchagua hao washiriki sema niliwahi kusikia msanii anatakiwa apeleke kazi yake kitu ambacho kama ni kweli basi itakuwa ngumu kupata wshindi wa kweli si kwa africa mashariki tu bali nadhani kwa africa nzima.

pia hiyo kora kwa aina fulani inamapungufu mengi tu kwa upande wangu ..kwani kama ni ya africa inakuwaje hakuna nchi nyingine inayopewa nafasi ya kuyaanda zaidi ya sauzi africa au sauzi ndio africa yenyewe...

pili kwenye swala la watumbuizaji ..mimi kama ningetegemea wasanii wa africa wangepewa nafasi kubwa katika utumbuizaji kwenye ile siku yenyewe ya kutoa zawadi kwani ndio siku ambayo watu wengi wanaangalia zaidi ya ile siku moja kabla ya utoaji tunzo kama walivyofanyiwa akina JD....kwani siku ya tunzo zenyewe wanaoja kwenye utmbuizaji ni wasanii wengi kutoka africa kiasi kwamba hata hao wa kwetu wanafunikwa.

Nadhani Kora ingeangaliwa upya kwa ujumla ili kiwe kioo cha kutangaza muziki wa africa

1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users