Jump to content


check me out


8 replies to this topic

#1 kichwa

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 5 posts
  • Locationsouth africa

Posted 19 August 2002 - 09:20 AM

yoh yoh
peke yangu ndani ya ulingo
nani asogee maji ya shingo
kasome kwanza hisabati kisha njoo upime mzingo
wa eneo la upeo wa huu mviringo
naweka watu roho juu ka milioni kumi za bingo
okumu bin agoro anduru mweusi kama mpingo
kelele nyingi lakini sina hata singo


hoya machizi napiga hodi ndani ya bongo hiphop scene naombeni ushirikiano wenu

#2 Guest_kisiwa_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 09:27 AM

we pumbavuuu kabisaa sasa umeimba nini kuna ujumbe gani hapo
kama huna kipaji cha kuimba mzeee usikurupuke tuu sawa mzeee
ushauri wangu ni kwamba achana na hii fani kabisa ,,,,, :twisted:
nduki!!!

#3 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 23 August 2002 - 12:06 PM

Wazee mnanipagawisha manake na hasira ya kuchana

mbona tupo wengi utasemaje peke yako
hadi sasa tuko watatu hatuoni dada zako
waje kwenye forum waache kuliwa uroda
vichwa vipo humu,vya panzi vinakula boda
wakati huna kazi,iweje uwe na voda
vipochi havina mali,vipodozi mpaka poda
ukiwakuta kiwanja,wanakuzuga na soda
eti sinywi pombe nimekatazwa na dokta
kumbe ni gia yao,ukilewa wanakuteka
madada zetu,kwa nini mnavibweka
mnatuungisha matela,halafu mnatucheka
nasikia mnaogopa mimba,mkiipata tu mnaifyeka
mnapenda ngono,kuzaa hamtaki
mkaenda beijing,eti kudai haki
kwenye forum tuwaone,kama mnataka haki
nge naondoka,mkiniitaji nitabaki

#4 kichwa

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 5 posts
  • Locationsouth africa

Posted 08 October 2002 - 08:14 AM

naipiga moto mic nataka iwake
nna machungu na gadhabu kum***KE
natembeza mkon'gotofake mc's matumbo joto
tungo zao zimedorora
zangu zinatia fora
zaongezeka ubora na thamani kama dollar
nashukuru mola
ni lafudhi zevye ladha vitu heavy kama safari laga uridhi kwa walevi
kipaji hiki adimu ka' sadaka ya dhulmati
changanya falsafa fasihi na hisabati
naimla nadharia istilahi zenye nishati
lafudhi zenye ladha utamu wa sharbati
mihadarati, maneno yanalevya umati naifadhi misamiati
hiki kichwa kama kabati
napanda chati mwenye akili hakosi bahati

tieni mguu na hapo nyooo

#5 Guest_rshijaus@yahoo.com_*

  • Guests

Posted 08 October 2002 - 11:44 AM

kisiwa said:

we pumbavuuu kabisaa sasa umeimba nini kuna ujumbe gani hapo
kama huna kipaji cha kuimba mzeee usikurupuke tuu sawa mzeee
ushauri wangu ni kwamba achana na hii fani kabisa ,,,,, :twisted:
nduki!!!

Hi Mr Okumu Andoro.

Mzee mavitu yako nimeyaona ni makali unatisha mzee.

Ingawa kuna baadhi ya watu wanajifanya wanakurudisha nyuma lakini mi nayakubali hakuna noma mzee.

Wewe endelea tu achana nao hao washikaji wanakuroga tu wachawi hao.

keep it up! Mzee

#6 Guest_rshijaus@yahoo.com_*

  • Guests

Posted 08 October 2002 - 11:44 AM

kisiwa said:

we pumbavuuu kabisaa sasa umeimba nini kuna ujumbe gani hapo
kama huna kipaji cha kuimba mzeee usikurupuke tuu sawa mzeee
ushauri wangu ni kwamba achana na hii fani kabisa ,,,,, :twisted:
nduki!!!

Hi Mr Okumu Andoro.

Mzee mavitu yako nimeyaona ni makali unatisha mzee.

Ingawa kuna baadhi ya watu wanajifanya wanakurudisha nyuma lakini mi nayakubali hakuna noma mzee.

Wewe endelea tu achana nao hao washikaji wanakuroga tu wachawi hao.

keep it up! Mzee

#7 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 10 October 2002 - 01:06 PM

hivi nyie watu mbona mekimbia shule mapema? sasa hayo mashairi yenu ya taarabu simgeyapeleka kwenye swahili battle? hapa ni majadiliano tu mbona mnatuaibisha wabongo.

#8 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 11 October 2002 - 08:04 AM

Unajua nini Sosa? Hii topic ilipostiuwa wakati swahili battle ilikuwa haijaanzishwa.Ngoja niwape watoto mistari huru kidogo.


Naona mnajikongoja lakini hamtofika
sana sana mnajichoresha kama si kuaibika
mnajiita vichwa na tungo zenu sio za uhakika
mwingine ni kisiwa,upo tayari kwa kuzama
kwa nge ni kama zenji,hamruhusiwi kuinama
ni kilemba cha mobutu sio kilemba cha osama
ndo maana nalilia wapo wapi dada zetu
mnaowarubuni na kuwapiga pekupeku
kisha unadiriki na kujiita dume la mbegu
mademu hawana kazi lakini wapo bize
ndomaana hatakwenye forum wanaogopa kupiga mbizi
wengine mnawabaka wakati mnajua ni machizi
mnawatia nyuma wanawake bila hajizi
ndo maana wana sagana wanaogopa wanaume
hawataki kuolewa kisa mnaoana wanaume
mbona wanyama hawakosei kulengana
iwenye binadamu mume mnapinduana
wengine mnasifa za mimba kuzikana
mnafikiri ni nini?hii yote ni laana
na mtajibu tu ukifika siku ya kiama

#9 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 11 October 2002 - 12:28 PM

:lol: nge wape mapande hao mabinti





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users