Jump to content


Albamu za zamani za HipHop Bongo!


2 replies to this topic

#1 mkuki

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 132 posts
  • LocationDar es Salaam,Tanzania

Posted 17 August 2002 - 11:17 PM

Ebwana nilikuwa naulizia uwezekano wa kupata albamu za zamani za hiphop Bongo hususani Albamu ya Kwanza Unit ile yenye "Msafiri" nadhani hii ni albamu pekee waliyotoa vilevile albamu za deplowmatz na za Mr II enzi hizo anaitwa II proud, vilevile ya Sos B pamoja na wengineo!
Nakumbuka zamani sana J4 ulikuwa unauza online CD ya KU Crew nilikuwa nauliza kama kuna uwezekano wa mimi kuinunua au labda kama unaweza kunielekeza wapi ninaweza kuipata nitashukuru sana!
Mwenye old skool joints zozote za bongo naomba tuongee uwezekano wa ku swap mimi nina new skool nyingi zaidi na oldies chache...amani!

#2 Guest_mtambo wa kushushua_*

  • Guests

Posted 23 May 2003 - 11:04 AM

we kama huna track za zamani unasikiliza nini sasa kwenye bongo fleva....lazima utakuwa ni mshamba tu unatafuta nini kwenye hii web?
pumbu we!

#3 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 23 May 2003 - 12:55 PM

vipi mzee wa mtambo sio lazima kutukana wadogo. pengine mtu alikuwa na umri ndogo wakati KU walipotoa albam zao kwa hiyo kakosa.

Ninazo kaset nyingi za zamani na kweli zamani tulikuwa tukiuza Kwanzanians ila siku hizi hatuuzi tena kwa sababu ilikuwa kazi mno.

lakini wewe si upo DSM? basi inabidi Kwanzanians bado inapatikana, hasa Ukuru street pale Kariakoo halafu tena ukipinda kulia pale roundabout mwisho wa kariakoo area, kuna duka moja Wholesale ya cassettes MAMU stores au wadosi wengine walikuwa wanauza cd yenyewe ya Kwanzanians!

au kama uko town pale askari monument anayeuza caset kwa jina la TALL (jamhuri) atakueleza maanake alikuwa nayo cd.
kanda nyingine labda DISABLED KIOSKS karibu na uhamiaji kuna jamaa mmoja irie anauza kanda na kama hana umwulize akutolee copy labda.





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users