Jump to content

Ilikuwa vipi? Hiphop zamani (reprise - part 1)

58 replies to this topic

#21 bongonian

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 60 posts
  • LocationArusha,Tanzania

Posted 22 August 2002 - 05:21 AM

niambie deezasta..kila siku naingia nasema nidondosha kamstari lakini muda unakuwa mchache...lakini mzee sosa naona kawakilisha enzi hizo vizuri sana kwani nikitaka kutengeneza documentary ya enzi hizo lazima nimtafute....

nakumbuka kipindi hicho bwana ..masela walivaa sana masweater siunajua mambo ya OPP ....

kunawale jamaa wa kurasini na mkumbuka mmoja jina lake lilikuwa Buva walitoaga video wako kwenye jumba moja bovu hivi...

mnakumbuka yule jamaa aliyeimba mi mamasai aliimba kibao kimoja cha reggae fulani kilikuwa kimetulia nacho......

kuna mtu amesema kuhusu 2 proud kujimegea ni nyimbo nyingi tu alijimegea kwenye albam zake sema siunajua enzi zile watu walikuwa hawaangali kwa sana .............

kuna mzee mmoja alitajwa sana kipindi cha nyuma lakini sijamsikia humu ndani saleh jbir (vanilla ice)

#22 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 22 August 2002 - 07:52 AM

Saleh Jabir wengi wanajifanya kum-dis lakini kwa wakati huo anafanya production kazi yake ilikuwa tight, na kingine lazima izingatiwe kwamba zama hizo rap ya Bongo ilikuwa haijafikia level ya ma-mcee kujitungia rhyme zao wenyewe wooote ilikuwa ukigeza nyimbo za watu mtoni unapata props za kutosha.....licha ya hiyo Saleh alionyesha uwezo tofauti wa kutunga maneno yake mwenyewe kwa kugeza style na beat za watu wengine hii haikuwa mbaya, cha kushangaza watu wengi walikuwa wanam-feel alipotoa album yake lakini baadae mam-cee walipoanza kuibuka na kutunga rhyme zao ndio chuki ikaibuka, kila kitu kina wakati wake.
Nway 1luv 2him whereva he'is (u made it,people do make it).
alcapaino escapirado
'the originol figure'

#23 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 22 August 2002 - 08:59 AM

Saleh J alikuwa anaishi Abu Dhabi lakini sasa yupo UK.
Sijui umesoma interview yake?

http://www.africanhi...wpage&pageid=34

#24 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 22 August 2002 - 12:38 PM

Yeah interview yake nimeisoma na ipo bomba sana, nadhani ni vizuri na wengine waisome kama bado ,wat if that head cum back again?
alcapaino escapirado
'zinc-amalgam in conc.Hcl'

#25 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 22 August 2002 - 12:45 PM

well in fact alikuwa na mpango wa kurudi kwenye fani!
nani asiwe na mpango huo, ukitazama bongo flava ilipo sasa utadhani hata bi.kidude awe na hamu ya kurap :P

#26 ODB

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 40 posts

Posted 23 August 2002 - 10:56 AM

Halafu hiyo interview kuna gazeti moja la udaku hapa bongo lilitoa habari za saleh jabir na picha hizi hizi zinazoonekana kwenye africanhiphop sasa sijui inaruhusiwa watu kukopi humu ila sikumbuki jina la gazeti manake niklikuwa na haraka siku hiyo nilipolicheck ila nilipoona tu nikajua wamefyonza

#27 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 23 August 2002 - 11:10 AM

Oya wazee mmesikia mwisho wa mwezi huu kuna party ya kuwakumbuka wasanii wa rap waliotutoka kama D_ROB na wengineo itakuwa tarehe 31 msikose

#28 Guest_Carren_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 02:58 PM

Hip hop ya zamani haikuwa bomba kama ya sasa, kwani wasanii wengi wa sasa wa muziki huu ambao wengi wamekuwa wakiuita muziki wa kizazi kipya kwa kweli wanajitahidi kuuboresha ili uweze kuoneka kuwa unakwenda na wakati, lakini tusitupe mbachao kwa msala upitao hata wale waanzilishi wa muziki huu hapa nchini wakina Salehe Jabri pamoja na Mr II nao walijitahidi kuiweka Hiphop nayo itambulike.

Lakini nawapa hongera wasanii wa sasa hapa nchini, ila pia ushauri mzuri kwao ni kwamba wasiige mambo mengi kutoka bara La Ulaya ya na Amerika kwani litawapotosha, wakumbuke wenzetu wa kule wameendelea, hata wakitembea uchi au kumpiga ngumi mtu hakuna anayejali.

lakini ni katika

Juma4 said:

Hii topic ya 'ILIKUWA VIPI' ilianzishwa mwezi wa 7 mwaka 2002, ilipata mesage nyingi lakini katika kuhama Forum kwa sehemu mpya ikafutwa, kwa bahati nzuri forum ya zamani ilinusurika, hivyo nime paste message zote hapa chini, na kisha mnaweza kuendelea mazungumzo.

unregistered

posted 09 July 2002 11:49
--------------------------------------------------------------------------------
Nafungua hii forum ili kukaribisha vile vichwa vyote ambavyo vinaijua hiphop ya bongo
toka zamani(including our finest mcees), maana siku hizi watoto wadogo weeeengi wameingia kwenye fani wakati hawajui hata beach-party zilikuwakuwa vipi wakati huo,maconcert wapi,vituko gani vya wakati huo,ma-dj waliotamba n.k.......lets use this forum to educate 'em fools & new comers......if u feel ur real then represen it!!!!!
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 09 July 2002 11:59
--------------------------------------------------------------------------------
Nakusoma vilivyo kabisa alcapaino,ni kweli kuna umuhimu wa kuanza kukumbushana historia ya hiphop ya bongo huko zamani wakati tupo primary, kiasi flani napata kumbukumbu tamu napoanza kukumbuka mambo ya long-time hasa sisi watoto tuliosoma boarding schools mbeya,dodoma ,morogoro n.k tulikuwa tunashindana kuchana nyimbo za marepa wa mtoni na samtaim tunatoroka shule kufata beach-party bongo,duh? ilikuwa ni balaa.Nipe muda nikumbuke zaidi narudi!!!
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 09 July 2002 15:04
--------------------------------------------------------------------------------
Katika matukio kabambe ya hiphop bongo ni kama lile la tamasha lililo fanyika empress cinema kutafuta mshindi wakwanza, wapilili na wa3. Haijatokea tena mkusanyiko wa vichwaa vya hiphop toka kipindi kile, kulikua na ma emcee mpaka wa mikoa ingawa wengine ndio walikua miyeyusho lakini wali rep hiphop ya kibongo.
Na beach party zilianza kuharibika zilipo anza ku tangazwa kwa sana mpaka wahuni wa msasani wakawa wanajaa kukaba watu ndio flava ikaanza kuisha, mpaka cloudz wakawa wanafanya beach parties kisiri siri ingawa zingine hazikua bomba sana. Nakumbuka long time tulilisonga mpaka o'bay na washkaji tukijua kuna mkwanja kumbe bila bila.
mnakumbuka marehem D'rob n.k walivyo chana "shifty" nyimbo ya onyx wakiwa katiuka lile garii kama lakubebea makontena tena alikuwepo na yule rasta nimemsahau jina aliimba "roho ya korosho".... au ile beach party ya mwisho mwisho ya yule dem ku chaniwa nguo na kubaki uchi? nazo kumbuka ni kama 4 hivi nilizo hudhulia na kuziona bomba. Au kipindi kile cha pool side hiphop kwa sana.....ebwanae ee ndio vile mida
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 09 July 2002 15:31
--------------------------------------------------------------------------------
lakini bwana hiphop ya bongo sasa hivi ni untouchable! wasanii wa longi labda ambao wana weza kutingisha radio za bongo ni kama 2 proud, Gwm, Hard blasterz imebadilika mno na huyo Jay sidhani kama alikuwepo mwanzoni wakati wa kina tuff jem, terry, ngida n.k, Kwanza Unit (sema wamesambaratika nadhani ndio kikundi kimesha kufa), N2P niggaz 2 public (one of my favourite groups nao wamepotea).
alafu mbona kuna watu wengi sana sasa hivi wana imba sawa? wanagezana au ndio style ya ki wilaya flani? sitaji majina nadhani mtakua meshasikia wenyewe.

Lakini bwana lazima nikubali hiphop ya bongo sasa hivi imejiskuma katika next level sio mchezo watu wanafanza mambo!!

--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 03:43
--------------------------------------------------------------------------------
Mzee Sosa nakubali kweli kumbukumbu unazo, hiyo ishu ya demu kuchaniwa nguo nakumbuka niliishuhudia mbele ya macho yangu,yule demu alikuwa malaya na watoto wa Msasani walipoanza kumzingira ndio soo likawa kubwa watu wakamchania nguo zote mpaka chupi na kuanza kumtia madole...(aliumia sana yule mwanamke mpaka kutoka damu)...bila uongozi wa Clouds na wadhamini ambao walikuwa ni Salama-Condoms kumsaidia yule dada kwa kumfunika nguo ingekuwa balaa(maybe kifo).
Cha kushangaza ni kwamba yale mambo yalikuwa hayafanyiki kifichoni ni palepale pembeni ya jengo la CoCo-Beach(Bongo watu wamedata...we acha)
---------------------------------------------
alcapaino..."the most illest M'faka"
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 10 July 2002 08:16
--------------------------------------------------------------------------------
Habari mbalimbali za hiphop ya bongo (bahati mbaya kidooogo kuna habari za ragga na reggae lakini msikonde yote kheri) mastaa wa zamani ambao wengine hawasikiki siku hizi, kwa faida ya watoto wa siku hizi kama mzee Alcapaino alivyo-request, hapo ndio utajua Caz-T au JayDee wametokea wapi, stuff like that, amani!
http://www.musikmuse...africa/dar.html
[ 10 July 2002: Message edited by: deezasta ]

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 10 July 2002 08:56
--------------------------------------------------------------------------------
Sosa umenikumbusha hiyo Concert hasa pale K.U walipo-perform nyimbo ya ONYX 'shiftee' juu ya gari na mdogo wake marehemu D-Rob anaitwa Ndoti naye alikuwa na verse fupi ndani yake waliosha balaa......nani anakumbuka D-Rob na Nigga-One walipofanya show nyimbo ya Brand Nubians inaitwa 'Punks jump up 2 get beat Down' pale Coco Beach........to be continued
*Mzee Deezasta bora umetupa hiyo Web nadhani nayo itasaidia kuwapa watu mwanga flani wa hiphop bongo....Big-up*
--------------------------------------------
#washkaji mlio mtoni na mamcee wa bongo toeni comments pia#
--------------------------------------------
alcapaino 'the long-time performer'
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 09:24
--------------------------------------------------------------------------------
si matani naona kumbukumbu zinazidi kuongezeka...naomba mzee J4(administrator) uondoe msg mojawapo ya 'alcapaino' kwenye forum naona kuna makosa yamefanyika mpaka zikatokea mbili zinazofanana.....mi nakumbuka wakati huo disco lilikuwa floor ya saba New-Africa na kuna kipindi Mabronzo wengi wa Bongo waliacha kuipenda hiphop ya mtoni wakaanza kuzimikia mayenu wakati huo nyimbo zilizotamba za mayenu ni kama 'Kidekude'..etc na kama huamini uliza Clouds(nadhani) jinsi walivyokuwa wana-make money pale Salender-Bridge ukumbi unaitwa 'Pink-Coconut' watu walikuwa wanaruka bolingo si mchezo...ila baada ya kipindi flani kupita mambo yakarudi kama kawaida hiphop ikaanza kuchukua mkondo wake.........I'll be back soon
#oyaaa wazee waambieni masela wenu mbalimbali wachangie kumbukumbu zao zinaweza zikasaidia hata Waandishi wa habari kwenye kutoa historia ya hiphop nchini#
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 15:02
--------------------------------------------------------------------------------
alcapaino ndio hiyo hiyo beach party niliomaanisha, lakini hiyo ya D Rob na Nigga One (R.I.P) sikumbuki...mida
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 11 July 2002 03:58
--------------------------------------------------------------------------------
Nakumbuka day-one wakati huo tunakaa Drive-In(msasani) tukapata info kamba kuna Beach-Party usiku saa nne hivi,homeboyz tukaanza kujifoji kimtonimtoni na kula 'ngondi' mpaka Coko(wakati huo mkoko adimu)...ile tunaikaribia Bahari tu mzee nasikia kitu hewani "Gimme something u cant understand,How I can just kill a man" by Cypress Hill,ngoma inakita balaa...vichwa vya hiphop lazima muikumbuke hii....wakati huo nyimbo zilizotamba BeachParty ni kama Slam, Shiftee, Off-N-On(Trends of Culture), Chief Rocka,They want EFX, Dre na Snoop nao ndio wamekoleza beef na Eazy-E,Ice Cube anatamba na 'Today woz a good day',Mc-Lyte na nyimbo yake 'Poor Georgie', Run-Dmc wanawika na 'Down withe King',Apache na single yake 'I need a Gangsta Bitch'... BlackMoon na 'How many mcees'...na wengineo weeeeengi including the single 'Punks jump up'....yaaani we acha tu long time ilikuwa balaa mazee
--------------------------------------------
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 11 July 2002 06:22
--------------------------------------------------------------------------------
Du sio matani na umesahao nice n smooth, fushnickenz (sikumbuki spelling yake), na cypress ilikua ina enda kitu kama hivi "there is somthing u cant understand, how i could just kill a man", house of pain (jump around), Da youngsterz lakini album yao ya pili wakawa mabishoo, Nas na illmaticz ndio album ambayo hakuna mpaka sasa inayosogelea unakumbuka nyimbo ya "one luv" "whoes world is this" "it aint hard to tell" "half time" n.k yani album ni clasic, Alafu apache was wack az hell! ni nyimbo moja tu kali tena hiyo gangtar bitch ambayo aliandikiwa lakini ukisikiliza album yake huwezi kuamini yani some weak ass shit, Grave Diggaz (lakini watu wengi hawakuwasikia kwa sana sijui kwanini?), Krs 1, souls of mischief, del da funky homosapian, funkdubiest, mad flava, milk bone, na ile nyimbo ya "back in the dayz when i was young im not a kid anymore but some dayz i wish i was a kid again"! ya ahmed (sikumbuki spellin), 2pac "keep yo head up" "holla if u here me", flava unit, queen latifa, ill al skratch, smiff n wesson, cnn capon n noreaga "blood money" "T.O.N.Y" nk nayo ni clasic sum ill thug album mpaka leo ninayo tape na illmatic, Positive K "ive got a man" n.k, leaders of the new school, De La Soul...n.k list ni ndefu mno...kipindi hicho hiphop sio ma bling bling wala nini kama Jay Z na Ja rule n.k alafu nas nae ka ingia murda ink yani miyeyusho tu atakua too comercial....lakini those days were the isht!
ukiangalia long time hata disco au beach parties kulikua na raha wakipiga hiphop vichwa vina weka kiduara na nini unakumbuka hiyo? siku hizi utakuta mabraza meni na madem tu wana tingisha mabega...nk. Au slam ndio ili kua mshike mshike yani raha tupu watu wanavyo wild out! waliokosa wamekosa mengi sana! bongo kuna ka spirit flani ka hiphop kamekufa kwa sababu ya ma chicken heads wamezidi kua wengi, au sivyo alcapaino?
mida masela!

--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

#29 Guest_Da-Brat_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 03:01 PM

sosa said:

Ndio ni kweli jamaa alikua na mtindo wa kulawiti watoto wadogo tena aliyefumaniwa nae ni kivlana, jamaa ana nyea debe tu sasa hivi.
Usinyambie hiyo nyimbo ya fresh G ni ile inayokwenda hivi:
FUNGUA CHAMPAIGNE,
NA HII NDIO KAMPENI,
USILETE SHINGIO FEN,

hiyo ndio hook ya nyimbo yake, sasa sijui ndio hiyo aliyokuimbia.

#30 Guest_Jack_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 03:03 PM

Ina maana mpaka mwaka huu huyu mtu hajaachiwa tu kwa kosa hilo? au yupo Uswahili? maana tuambianeni mapema tukimkuta sehemu tumkimbie maana huu mchezo wake kwa kweli si mzuri ni kama maneno ya Msanii AY katika wimbo wake wa Machoni ni kama watu moyoni hawana utu basi ndiyo huyu,...nijibuni jamani
()

Da-Brat said:

sosa said:

Ndio ni kweli jamaa alikua na mtindo wa kulawiti watoto wadogo tena aliyefumaniwa nae ni kivlana, jamaa ana nyea debe tu sasa hivi.
Usinyambie hiyo nyimbo ya fresh G ni ile inayokwenda hivi:
FUNGUA CHAMPAIGNE,
NA HII NDIO KAMPENI,
USILETE SHINGIO FEN,

hiyo ndio hook ya nyimbo yake, sasa sijui ndio hiyo aliyokuimbia.

#31 Guest_L'z_*

  • Guests

Posted 23 August 2002 - 03:08 PM

Oyaaaaaaaa mshikaji hiyo tumenyaka ila sisi kwa kweli hatujafurahia sehemu ambayo wameipeleka kufanyika, kumbukeni kuwa shughuli hii ni ya mwaka mara moja na watu watakuwa wengi sana na hako kaukumbi kenu kwa kweli ni kadogo sana, ni bora mngetupeleka katika ule ukumbi ambao kwanza ni Center ni pia ndio sisi wajanja wote wa hapa Bongo tumeuzoea, sio mtatupeleka kule inakuwa kama tamasha la Fiesta ambapo watoto wa Temeke ambao wamezoea kucheza mdundiko vitu kama vile hawajui baada ya kustarehe wanafikiria kutukaba tu sisi watu wenye fedha zetu
.
quote="nge"]Oya wazee mmesikia mwisho wa mwezi huu kuna party ya kuwakumbuka wasanii wa rap waliotutoka kama D_ROB na wengineo itakuwa tarehe 31 msikose[/quote]

#32 Guest_Bahati_*

  • Guests

Posted 06 September 2002 - 08:34 AM

Nilikuwa Bush one time, maswala ya net mswaki, ndo nimerudi. Hiii kitu simchezo....alca na sosa mmenikata sana kwa mamamemory ya longi.....
hiii ni shule tosha babake.
....Kw hapa Bongo sio siri mzee 2Proud alimaliza sana kwenye live concert moja ya mazingira mnazi mmoja, Itv walikuwa wana broadcast live..ilikuwa ni track yake moja hivi....."machinga anapopamabana na polisi, mdosi mechuna na glas ya juice....." huo ni moja ya mistari matata kwenye hiyo track na mambo fulani ya shauritanga.....
Mmenipa hasira sana....hadi muda umeisha, Nnakuja mazeee na mikumbukumbu....[/quote]

#33 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 06 September 2002 - 01:36 PM

imekua kipindi kidogo, poa lakini. Hii ni kwa Jack, jamaa bwana nadhani bado yupo jela lakini ni bora tu uwe makini manake watu kama hao wako wengi tu bongo.
Bongonian hao jamaa wa kurasini walikua wanajiita "N2P" kwa kirefu "NIGGAZ 2 PUBLIC" na nyimo ni "VIJANA KUA MAKINI".
poa mida masela!

#34 Barakah aka Shaheed

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 40 posts
  • LocationIllest On The Mic Since Malcolm Shabazz

Posted 06 December 2002 - 05:13 PM

alcapaino. said:

Am back again baada ya kupotea, nway nilipata misiba miwili ndani ya wiki moja, my young bro n then my Mom , (RIP). But still nakumbuka long taim wakati huo disco lipo Oysterbay ( La Dorce Vita) kipindi hicho kiingilio sijui buku mbili ila watu tulikuwa tunaruka ukuta kwa nyuma tunatokea kwenye bustani ya maua then tunaibukia chooni, umenikumbusha enzi za kuvaa black-boot na draft juu yake, sio siri ilikuwa mpeleke-mpeleke sana na masoja mitaa ya kati, huyo killa-B kwa sasa ni mtangazaji wa fm-redio na bado wana crew yao ipo kimara mwisho (maskani kimara) inaitwa Imeditation Kingdom(IK), yumo kwenye HBC album track inaitwa 'Time 4 action'. Last sunday(11thAug2002) nikiwa na home-boys tuna-sip some lika mitaa ya maskani nait ya saa tano na kuendelea kuna dj mmoja wa clouds alikuwa anatwanga mawe si mchezo mpaka wote tulipagawa baadhi ya track alizopiga ni 'push it' ya salt-N-Pepa, akapiga 'whats up Doc? na 'Laschmove', zote za Fuschnickens, akapiga 'Word-up' by Cameo na track nyingine kibao za longtaim mpaka pombe ikaisha jinsi tulivyokuwa tumeanza kucheza pale baa kama machizi.
Kuna concert moja kubwa ilifanyika Drive-In cinema(ubalozi wa marekani unapojengwa) nakumbuka master T alikuwa ana-introduce Cd ya Galinoma, wakati huohuo lemmy Ongara anawekaweka vifaa vyake vizuri ili aanze kutumbuiza, ikatokea 'beef' Lemmy akaanza kukoroma ili master-T aondoke kwenye stage sababu hakuwemo kwenye ratiba, sasa viumbe vilipojifanya havimsikilizi akaenda kuchomoa power-cable yake ambayo ndiyo ilikuwa inaleta umeme kwenye show nzima na show ikaishia hapo, watu wacha tuanze kumtukana lemmy na yeye akatukana sana akaishia na kagari kake, ilikuwa mida kama ya sasa nane usiku. Kwenye hiyo show GWM waling'ara sana na nyimbo zao 'cheza mbali na kasheshe' na 'haya twende haya twende', kwenye turn-table akiwepo Bonnie.
Wazushi walidai eti Lemmy hammaindi master-T sababu alikuwa hapigi nyimbo zake redioni(wakati huo radio One) anapiga za kina Galinoma.

damn Mgullu young bru[kelvin] and moms??pole sana ndugu yangu..mimi sikujuwa kabisa
Pole sana mshikaji anagalau nimechelewa kidogo..sorry bru

#35 Barakah aka Shaheed

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 40 posts
  • LocationIllest On The Mic Since Malcolm Shabazz

Posted 06 December 2002 - 05:15 PM

#36 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 31 May 2003 - 04:10 PM

Sup Barakah....its been a long tyme Mzee ila mambo mengi ya hapa na pale nadhani unaelewa. Thanks for 'Pole' hapo juu, haina noma au vipi! mambo ya kawaida yana-happen daily think u know.
Na-fail ku-holla na ninyi huko aint got ur e-mail add(s), gimme some!
Wape Hi washkaji! Big-Up!
alcapaino.Mg
'the Most Illest 1'

#37 Guest_mchizi wa maskani_*

  • Guests

Posted 10 June 2003 - 05:40 PM

Nimejaribu kupitia hii forum 'ilikuwa vipi hiphop zamani' nimegundua ni page nzuri saana kukumbushia mambo ya zamani though kuna mengine sikuya-experience wakati huo maana kuna nyakati flani nilikuwa nje ya Dar, nadhani hii ni sehemu nzuri kwa watu kukumbukia hasa ma-mcee wa siku hizi inabidi waangalie humu ndani wajue ni nini kilichokuwa kinaendelea nyakati hizo, kama inawezekana namwomba J4 aanzishe page special ya watu kutoa kumbukumbu za zamani kwenye miziki ya aina nyingi ya hapa bongo kwani hii itasaidia kuweka historia ya mambo ya kale kwa ajili ya kizazi kipya,ukisoma humu ndani utakuta kuna watu wanatoa comments kali sana inaelekea wametoka na hiphop zamani,nawapa Big-Up.
Mchizi

#38 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 10 June 2003 - 06:57 PM

Eeh si utani, hiphop imekuja long way. Pia katika section ya Africanhiphop Library chini ya Tanzania hiphop page pale kuna page moja kuhusu baadhi ya vikundi vya zamani ila haiko complete hata kidogo, ni maarifa niliyopata tu halafu mimi si Mbongo.
Una suggest ile sehem iwe ndani ya forums au?
Mi nnazo picha nyingi na tape scans za miaka 1994 hadi sasa kwa hiyo itabidi nipate muda wa kuziweka online... kwanza tutafanya hivyo na old school ya South Africa kwa kuwa hizo picha tunazo buku na kitu.

#39 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 02 July 2003 - 01:18 PM

Sema J4, hiyo ni idea nzuri sana ,nadhani ni vema hii forum ikawa na sehemu special kwa ajili ya watu kutoa memories zao za nyuma hiphop ilivyoanza na hii iwe ni kwa nchi zote zinazohusika na hii web-site africa nzima..... unaweza ukaweka hiyo page pale kwenye africanhiphop library na kwenye kila country pakawa na link ya forum so that kila anayetembelea kwenye hiphop page ya specific country anaweza ku-add comments zake kuhusu anachokikumbuka... hii itatunza kumbukumbu nzuri kwani kila atakayekuwa anasoma historia ya vikundi vya rap vilivyoanza( lets say vya Tanzania) atakuwa na uwezo pia wa kuona hiphop ilianzaje katika hiyo nchi...au Vipi!
Big-Up!

alcapaino.Mg
'the Most Illest 1'

#40 Guest_Radar Records_*

  • Guests

Posted 23 July 2003 - 04:23 AM

Jicho La Ra

Baada kimya kizito mshindo mkuu! Au baada ya kimya kikuu mshindo mzito!??
Majibu ya swali lako yatajibiwa na upeo wa maono yako. Kama inavyofahamika
Kwenye historia ya sanaa ya Hiphop, kundi la KWANZA UNIT ndio waasisi bila kupingwa. Kilio kikubwa kwenye nyoyo za wapenzi wa HIPHOP halisi kimekuwa sio tu kupoza wanachama watatu wa kundi hili bali pia kutokuwepo kwenye jukwaa kwa miaka kadhaa.

Baada ya kutafakari majukumu walioachiwa na Mizimu ya Sanaa hii, KWANZA UNIT ama KU- CREW kama inavyotambuliwa na wengi imeamua kumtuma moja ya manabii wake kuingia tena kwenye ulimwengu huu wa fani ili akaokoe jahazi linaloonekana kuenda mrama. Juhudi zimefanywa na wasanii mbali mbali na vyombo vya habari kwa kushirikiana na redio kadhaa zilizopo nyumbani kuendelezea sanaa pale walikoacha KWANZA.
Kwa mila na desturi ya fani hii KU wameonelea ni vyema kujivika tena majukumu, kusaidiana na wanajeshi wengine waliopo mstari wa mbele hadi leo kwenye harakati za ukombozi wa msanii.

Huu waraka ni kutaka kuwatangazia Rasmi kuhusu Ujio wa Yule mwanzilishi wa
Kwanza Unit na aliyeiweka TEMEKE kwenye ramani. Ra ama kama alivyokuwa akifahamika awali Rhymson anakuja na santurii mpya iitwayo
JICHO LA Ra. Radar records ambayo iko chini ya usimamizi na umiliki wa Samia X, moja ya waanzilishi wa kundi hili asilia. Samia amefanya juu chini kukamilisha ndoto yake ya kuhakikisha ile hiphop asilia inadumu. Akiwa na makazi yake huko Uingereza amefanikiwa kufungua studio ya kisasa, na baada ya wiki moja tu tokea amalizie ufungaji wa mitambo- alimwita Ra kuja kutekeleza majukumu.

Hivyo Ra akaingia kazini kwa muda wa wiki mbili, na hadi sasa wameshareodi nyimbo Zaidi ya 14 na kuna uwezekano wa kufanya nyingine hadi 30 halafu kuchagua chache kwa kufyatua santuri hii JICHO LA RA.
Wapenzi na mashabiki wa KWANZA huu ndo wakati wenu kukonga ile kiu ya muda mrefu. Tafadhali tunawaomba muwaarifu jamaa na ndugu wote wa tokea enzi zile na wale wanochipukia. Nyimbo ya utangulizi itatoka baada ya wiki mbili kuanzia sasa. Na santuri itatoka mwisho wa mwaka tarehe itatangazwa.

Kuunga mkono kwenu ndio mafanikio ya fani hii, kusema maneno pekee kunaweza kuondoa ile ladha iliyomo kwenye santuri hivyo mtakapo sikia
Ile nyimbo ya utangulizi basi tunaomba mawasiliano ili tusikie maoni na nasaha zenu, maana bila nyinyi basi hata hii sanaa yenyewe isingekuwepo. Kama tunavyotuma zile b-pepe nyingine mara kwa mara tufanye hivyo hivyo kwa waraka huu ili wabongo wote walio nyumbani na nje wapate habari. Ndugu zetu wa Kenya tunajua walivyotusaidia kutuvusha mpaka mara kwa mara, watu wa Uganda, Burundi na Rwanda kote tutafika- Fungueni milango ya upeo ili
Wote tuone kwa kupitia JICHO LA RA…
RADAR RECORDS

1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users