Jump to content

Ilikuwa vipi? Hiphop zamani (reprise - part 1)

58 replies to this topic

#1 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 13 August 2002 - 02:23 PM

Hii topic ya 'ILIKUWA VIPI' ilianzishwa mwezi wa 7 mwaka 2002, ilipata mesage nyingi lakini katika kuhama Forum kwa sehemu mpya ikafutwa, kwa bahati nzuri forum ya zamani ilinusurika, hivyo nime paste message zote hapa chini, na kisha mnaweza kuendelea mazungumzo.

unregistered

posted 09 July 2002 11:49
--------------------------------------------------------------------------------
Nafungua hii forum ili kukaribisha vile vichwa vyote ambavyo vinaijua hiphop ya bongo
toka zamani(including our finest mcees), maana siku hizi watoto wadogo weeeengi wameingia kwenye fani wakati hawajui hata beach-party zilikuwakuwa vipi wakati huo,maconcert wapi,vituko gani vya wakati huo,ma-dj waliotamba n.k.......lets use this forum to educate 'em fools & new comers......if u feel ur real then represen it!!!!!
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 09 July 2002 11:59
--------------------------------------------------------------------------------
Nakusoma vilivyo kabisa alcapaino,ni kweli kuna umuhimu wa kuanza kukumbushana historia ya hiphop ya bongo huko zamani wakati tupo primary, kiasi flani napata kumbukumbu tamu napoanza kukumbuka mambo ya long-time hasa sisi watoto tuliosoma boarding schools mbeya,dodoma ,morogoro n.k tulikuwa tunashindana kuchana nyimbo za marepa wa mtoni na samtaim tunatoroka shule kufata beach-party bongo,duh? ilikuwa ni balaa.Nipe muda nikumbuke zaidi narudi!!!
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 09 July 2002 15:04
--------------------------------------------------------------------------------
Katika matukio kabambe ya hiphop bongo ni kama lile la tamasha lililo fanyika empress cinema kutafuta mshindi wakwanza, wapilili na wa3. Haijatokea tena mkusanyiko wa vichwaa vya hiphop toka kipindi kile, kulikua na ma emcee mpaka wa mikoa ingawa wengine ndio walikua miyeyusho lakini wali rep hiphop ya kibongo.
Na beach party zilianza kuharibika zilipo anza ku tangazwa kwa sana mpaka wahuni wa msasani wakawa wanajaa kukaba watu ndio flava ikaanza kuisha, mpaka cloudz wakawa wanafanya beach parties kisiri siri ingawa zingine hazikua bomba sana. Nakumbuka long time tulilisonga mpaka o'bay na washkaji tukijua kuna mkwanja kumbe bila bila.
mnakumbuka marehem D'rob n.k walivyo chana "shifty" nyimbo ya onyx wakiwa katiuka lile garii kama lakubebea makontena tena alikuwepo na yule rasta nimemsahau jina aliimba "roho ya korosho".... au ile beach party ya mwisho mwisho ya yule dem ku chaniwa nguo na kubaki uchi? nazo kumbuka ni kama 4 hivi nilizo hudhulia na kuziona bomba. Au kipindi kile cha pool side hiphop kwa sana.....ebwanae ee ndio vile mida
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 09 July 2002 15:31
--------------------------------------------------------------------------------
lakini bwana hiphop ya bongo sasa hivi ni untouchable! wasanii wa longi labda ambao wana weza kutingisha radio za bongo ni kama 2 proud, Gwm, Hard blasterz imebadilika mno na huyo Jay sidhani kama alikuwepo mwanzoni wakati wa kina tuff jem, terry, ngida n.k, Kwanza Unit (sema wamesambaratika nadhani ndio kikundi kimesha kufa), N2P niggaz 2 public (one of my favourite groups nao wamepotea).
alafu mbona kuna watu wengi sana sasa hivi wana imba sawa? wanagezana au ndio style ya ki wilaya flani? sitaji majina nadhani mtakua meshasikia wenyewe.

Lakini bwana lazima nikubali hiphop ya bongo sasa hivi imejiskuma katika next level sio mchezo watu wanafanza mambo!!

--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 03:43
--------------------------------------------------------------------------------
Mzee Sosa nakubali kweli kumbukumbu unazo, hiyo ishu ya demu kuchaniwa nguo nakumbuka niliishuhudia mbele ya macho yangu,yule demu alikuwa malaya na watoto wa Msasani walipoanza kumzingira ndio soo likawa kubwa watu wakamchania nguo zote mpaka chupi na kuanza kumtia madole...(aliumia sana yule mwanamke mpaka kutoka damu)...bila uongozi wa Clouds na wadhamini ambao walikuwa ni Salama-Condoms kumsaidia yule dada kwa kumfunika nguo ingekuwa balaa(maybe kifo).
Cha kushangaza ni kwamba yale mambo yalikuwa hayafanyiki kifichoni ni palepale pembeni ya jengo la CoCo-Beach(Bongo watu wamedata...we acha)
---------------------------------------------
alcapaino..."the most illest M'faka"
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 10 July 2002 08:16
--------------------------------------------------------------------------------
Habari mbalimbali za hiphop ya bongo (bahati mbaya kidooogo kuna habari za ragga na reggae lakini msikonde yote kheri) mastaa wa zamani ambao wengine hawasikiki siku hizi, kwa faida ya watoto wa siku hizi kama mzee Alcapaino alivyo-request, hapo ndio utajua Caz-T au JayDee wametokea wapi, stuff like that, amani!
http://www.musikmuse...africa/dar.html
[ 10 July 2002: Message edited by: deezasta ]

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 10 July 2002 08:56
--------------------------------------------------------------------------------
Sosa umenikumbusha hiyo Concert hasa pale K.U walipo-perform nyimbo ya ONYX 'shiftee' juu ya gari na mdogo wake marehemu D-Rob anaitwa Ndoti naye alikuwa na verse fupi ndani yake waliosha balaa......nani anakumbuka D-Rob na Nigga-One walipofanya show nyimbo ya Brand Nubians inaitwa 'Punks jump up 2 get beat Down' pale Coco Beach........to be continued
*Mzee Deezasta bora umetupa hiyo Web nadhani nayo itasaidia kuwapa watu mwanga flani wa hiphop bongo....Big-up*
--------------------------------------------
#washkaji mlio mtoni na mamcee wa bongo toeni comments pia#
--------------------------------------------
alcapaino 'the long-time performer'
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 09:24
--------------------------------------------------------------------------------
si matani naona kumbukumbu zinazidi kuongezeka...naomba mzee J4(administrator) uondoe msg mojawapo ya 'alcapaino' kwenye forum naona kuna makosa yamefanyika mpaka zikatokea mbili zinazofanana.....mi nakumbuka wakati huo disco lilikuwa floor ya saba New-Africa na kuna kipindi Mabronzo wengi wa Bongo waliacha kuipenda hiphop ya mtoni wakaanza kuzimikia mayenu wakati huo nyimbo zilizotamba za mayenu ni kama 'Kidekude'..etc na kama huamini uliza Clouds(nadhani) jinsi walivyokuwa wana-make money pale Salender-Bridge ukumbi unaitwa 'Pink-Coconut' watu walikuwa wanaruka bolingo si mchezo...ila baada ya kipindi flani kupita mambo yakarudi kama kawaida hiphop ikaanza kuchukua mkondo wake.........I'll be back soon
#oyaaa wazee waambieni masela wenu mbalimbali wachangie kumbukumbu zao zinaweza zikasaidia hata Waandishi wa habari kwenye kutoa historia ya hiphop nchini#
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 10 July 2002 15:02
--------------------------------------------------------------------------------
alcapaino ndio hiyo hiyo beach party niliomaanisha, lakini hiyo ya D Rob na Nigga One (R.I.P) sikumbuki...mida
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 11 July 2002 03:58
--------------------------------------------------------------------------------
Nakumbuka day-one wakati huo tunakaa Drive-In(msasani) tukapata info kamba kuna Beach-Party usiku saa nne hivi,homeboyz tukaanza kujifoji kimtonimtoni na kula 'ngondi' mpaka Coko(wakati huo mkoko adimu)...ile tunaikaribia Bahari tu mzee nasikia kitu hewani "Gimme something u cant understand,How I can just kill a man" by Cypress Hill,ngoma inakita balaa...vichwa vya hiphop lazima muikumbuke hii....wakati huo nyimbo zilizotamba BeachParty ni kama Slam, Shiftee, Off-N-On(Trends of Culture), Chief Rocka,They want EFX, Dre na Snoop nao ndio wamekoleza beef na Eazy-E,Ice Cube anatamba na 'Today woz a good day',Mc-Lyte na nyimbo yake 'Poor Georgie', Run-Dmc wanawika na 'Down withe King',Apache na single yake 'I need a Gangsta Bitch'... BlackMoon na 'How many mcees'...na wengineo weeeeengi including the single 'Punks jump up'....yaaani we acha tu long time ilikuwa balaa mazee
--------------------------------------------
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 11 July 2002 06:22
--------------------------------------------------------------------------------
Du sio matani na umesahao nice n smooth, fushnickenz (sikumbuki spelling yake), na cypress ilikua ina enda kitu kama hivi "there is somthing u cant understand, how i could just kill a man", house of pain (jump around), Da youngsterz lakini album yao ya pili wakawa mabishoo, Nas na illmaticz ndio album ambayo hakuna mpaka sasa inayosogelea unakumbuka nyimbo ya "one luv" "whoes world is this" "it aint hard to tell" "half time" n.k yani album ni clasic, Alafu apache was wack az hell! ni nyimbo moja tu kali tena hiyo gangtar bitch ambayo aliandikiwa lakini ukisikiliza album yake huwezi kuamini yani some weak ass shit, Grave Diggaz (lakini watu wengi hawakuwasikia kwa sana sijui kwanini?), Krs 1, souls of mischief, del da funky homosapian, funkdubiest, mad flava, milk bone, na ile nyimbo ya "back in the dayz when i was young im not a kid anymore but some dayz i wish i was a kid again"! ya ahmed (sikumbuki spellin), 2pac "keep yo head up" "holla if u here me", flava unit, queen latifa, ill al skratch, smiff n wesson, cnn capon n noreaga "blood money" "T.O.N.Y" nk nayo ni clasic sum ill thug album mpaka leo ninayo tape na illmatic, Positive K "ive got a man" n.k, leaders of the new school, De La Soul...n.k list ni ndefu mno...kipindi hicho hiphop sio ma bling bling wala nini kama Jay Z na Ja rule n.k alafu nas nae ka ingia murda ink yani miyeyusho tu atakua too comercial....lakini those days were the isht!
ukiangalia long time hata disco au beach parties kulikua na raha wakipiga hiphop vichwa vina weka kiduara na nini unakumbuka hiyo? siku hizi utakuta mabraza meni na madem tu wana tingisha mabega...nk. Au slam ndio ili kua mshike mshike yani raha tupu watu wanavyo wild out! waliokosa wamekosa mengi sana! bongo kuna ka spirit flani ka hiphop kamekufa kwa sababu ya ma chicken heads wamezidi kua wengi, au sivyo alcapaino?
mida masela!

--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

#2 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 13 August 2002 - 02:25 PM

Hii topic ya 'ILIKUWA VIPI' ilianzishwa mwezi wa 7 mwaka 2002, ilipata mesage nyingi lakini katika kuhama Forum kwa sehemu mpya ikafutwa, kwa bahati nzuri forum ya zamani ilinusurika, hivyo nime paste message zote hapa chini, na kisha mnaweza kuendelea mazungumzo.

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 11 July 2002 07:48
--------------------------------------------------------------------------------
Nimekubali kweli Sosa we ni kichwa cha hiphop maana kuna track nyingine nilikuwa nataka nizitaje naona umeshazitaja ...anyway kuongezea hapo unakumbuka track inaitwa 'Whats up Doc can we rock?'ni ya Fu-schnickens fet.Shak-fu,kuna mpini wa Dre ulihit kinoma 'Dre day' alikuwa anam-diss Eazy-E pamoja na Luke(wa 2live crew) kisha Eazy akajibu na track inaitwa 'Real mothafukin geez'....akaibuka pimbi mmoja naye anaitwa Tim Dog na track yake 'Fuck Compton' akapata umaarufu kishenzi ingawa alikuwa wack as hell...kuna demu alikuwa thug anaitwa Boss,kuna mchizi Dred Scott na track 'Back in the days',wakina BigDaddy Kane,Tone Lock sidhani kama hawa watoto wa leo wanawajua...hata ukiwaulizia Ed Lover & Doctor.Dre watakushangaa tu......Mc Eiht naye aliwika mno na style yake ya story telling refer track yake 'str8 up menace', kuna wakina pharcyde,digable planet...Organised Konfusion(baadae ikamtoa Pharaoh Monch as a Solo artist) na track yao inaitwa 'stress,kill,distroy'...Pete Rock&Cl Smooth...heltah skeltah, Heather B na wengineo weeeeeengi dah...natamani kurudi enzi hizo si matani
"hivi hawa watoto wa siku hizi wanajua hata Guru alitokea wapi..wanamjua Bushwik Bill(yule mtu mfupi) alikuwa na akina ScarFace na Willi-D."
Ni noma mzeeeeee........tukumbushane aiseeee.
Mbona wakina Ambax siwasikii au hawakuwepo wakati huo,anyway hata kama walikuwa mikoani bado kuna mambo huko napo yalikuwa yanatokea tuelezeni.
--------------------------------------------
alcapaino-'the most illest one'
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 11 July 2002 09:07
--------------------------------------------------------------------------------
Duu kweli alcapaino kichwa, na kumbuka yo MTV na ma host wake Dre na ed lover alafu waka toa na ki project chao lakini album haikua mbaya sana. tumemsahau red man, na bro wake Ksolo, EPMD, na digible palanets "im peace like that cool like that... ilikua tight, Hit squad, Unakumbuka nyimbo "the head banga" K solo- eric sermon- parish smith n.k, unakumbuka cool mo D, Big L, Shahim nae dogo alikua tight, Unakumbuka ile hit ya method man "M.E.T.H.O.D", M.O.P na "Ghetto warfare", ndio namkumbuka sana Boss the gangsta bitch alafu katika ile video ya onyx (slam) alikuwepo anatoka kwenye gari alikua ana shati la checkers rangi ya blue (remember that), slik rick, unakumbuka nyimbo ya bone thugz ya mwanzoni mwanzoni kabisa ilikua ina enda kama hivi "its the thugz n word iz born" wanakimbizwa na 5-0 mtaani kwenye video yake, smooth the hustler, Jaru da damager, groop home n.k .
Sana nakumbuka sana shak-fu na fushnikens "can we rock whats up dock" na Kwanza Unit wakaimba kibongo kidogo inafanana "haturap wacha utan-hatu rap...". Hiyo story ya Guru nadhani naikumbuka alitokea kitu kama Houston na huko ana sema walikuwa hawa mfeel akaenda new york akiwa hana nini wala nini zaidi ya gari na nguo..ndio aka kazana mpaka kupata rep newyork ndio ikajulikana kundi gangstar yeye na premier one the best hiphop producer out there. Bushwick bill alikua na kundi lake nimesahau jina lake waliimba "six feet deep" na unakumbuka ile nyimbo ya bushwick aliyo kua akimba sijui dem alivyo mtoa jicho na jinsi watu walivo kua wana mcheka ufupi wake n.k ile nyimbo ina gusa sana, siikumbuki jina lakini najua umenielewa kutokana na profile yako kama a true hiphop fan.
siku wapenda sana kriss kross, wala naughty by nature, na wrecks n effect na nyimbo yao hit "shake baby shake".
shak-fu alisha imba nyimbo na meth' na rza katika moja za album zake. Na unakumbuka "shook ones" "tempreature is rising" n.k mobb deeps first classic album.
Nakumbuka tulivyo kuwa na washkaji tuki sogelea box tukisikiliza mawe na kuyachambua kama tuko mahabara (spellin donno) lab, na watu wengi walijifunza kingereza bila kujitambua. Good ol' dayz ehheee... unamkumbuka chizi lilipo vuja wavez? ODB na "brooklyn Zoo"...ebwanae tuta kesha manake tumekua pett rock na CL smooth tuna "reminisce" ......mida cuz.
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 11 July 2002 09:16
--------------------------------------------------------------------------------
watu mbona hawa changii?? hapa ndio tunakumbushana history ya hiphop bila hiyo huijui hiphop inabidi ufanye utafiti na kutafuta recordz za longi na kizisoma.
Jamani hodiii kuna vichwa kweli humu au wote vichwa panzi???/
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 05:39
--------------------------------------------------------------------------------
Natoka Home nikasema ngoja nikamkumbushe Sosa na 'The HeadBanger-Hit Squad'...kufika naona tayari kitu hewani(Word is Bond)...ile nyimbo ya BushWick(from Ghetto Boyz) mpaka leo nikiikumbuka inanitouch mno.....Erick Sermon aliwaleta Illegal(Mal G & Jamal) madogo walikuwa Hard mno...Jeru mpaka leo namfeel pamoja na '1 ofthe dopest producerz' Primo ...nakumbuka kwa mara ya kwanza namuona Meth na nyimbo yake(M.E.T.H.O.D Man) wanafanya show MTV nikasema hawa jamaa wengi wametokea wapi kumbe ndio WU wenyewe baadae nikapata video ya ODB(Brooklyn zoo) na MethodMan(Release ya' delf) wakati huo tayari WU imeshatamba na 'Protect ya Neck', C.R.E.A.M and 'So simple',vipi Grave-Digaz, Shabaz the desciple na Sunz of Man, nadhani wengi hawawafahamu hawa watu tunaowaongelea, Cella Dwellas,Arrested Development(people everyday), tell me ilivyokuwa kali album ya Raekwon the Chef(Only built 4 Cuban links) na ya mzee Gza(Liquid swords)..unajua watu wengi wameanza kuwafahamu Wu-tang walipotoa 'WU-forever' ndio maana lugha tunayoongea hapa hawaielewi, niambie jinsi ulivyomfeel Keith Murray alipotoa single yake 'The most Beautiful' na album ya E-Double(Double or Nothing)...aisee ni balaa....TC-Quest na track yao 'Award Tour' wakati huo Queenz ikaanza ku-shine balaa maana alivyoibuka Nas,Royal flush,Capone hajaenda jela na The Infamous Mobb nao ndio ikawa Funga kazi, unakumbuka 'Danger' ya Blahzey Blahzey halafu kuna wakina 'Channel Live',hata mimi sikuwapenda Naughty wala Kriss-Kross anyway am sore for that(to their Fans).........
---------------------------------------------Nataka unikumbushe wakati huo tape za 'Yo MTV Raps' zilivyokuwa zinazunguka toka kijiwe mpaka kijiwe na single mpya ikitoka watu wanavyojazana Home kutaka kurekodi(wakati huo hakuna CD ni tape tu),usisahau pia sytle ya mashati ya draft ilipoingia...
---------------------------------------------
alcapaino-"the most illest One"
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 05:55
--------------------------------------------------------------------------------
Wazee mmenikosha sana bahati mbaya nimechelewa ku-join forum lakini hiyo haina tatizo tukumbushane mpaka forum ijae,kuna vikundi vingine mmevitaja hapo alcapaino na Sosa mpaka nikasema hawa jamaa wanatakiwa waingie kwenye museum ya hiphop bongo(am joking), zamani we acha tu unaweza ukakuta mtu ana tape ya video ya MTV anaringa nayo kinoma mpaka mumbembeleze ndio awape baada ya wiki mbili mkaiangalie tena na yeye anakuja mkimaliza anaondoka nayo,halafu ukipata single ya MC yoyote mtoni iwe mbaya au nzuri lazima umuhimu uwe nao maana ilikuwa shida sana kupata 'new-tracks' sio siri watu tulikuwa tunaenda Coco-Beach kila jumapili ili tusikie nyimbo mpya zikipigwa kwenye magari ya mabrazameni wa oysterbay, masaki, mikocheni maana hawa walikuwa wana ndugu wanawashushia toka mtoni,dah zamani ina raha yake,ntarudi tena na kumbukumbu nyingine
_____________________________________________
real-G the metaphorian
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 06:20
--------------------------------------------------------------------------------
Namuomba J4 naye achangie siyo anatuwekea web ya hiphop halafu hatuelezi anakumbuka nini huko 'bak ine deyz', na memberz wengine pia na nna wasiwasi mamcee wengi wa bongo wahakupitia huku maana forum ingewagusa na wangetoa maoni hii ni space ya kila mtu kuchangia siyo ya watu flani,labda hawatumii internet(siamini hivyo lakini),nyie wakina 2Proud,JayMo,Jay,JNature,GK,MwanaFalsafa,A.Y,Complex,SimpleX,KU family,Cas-T, Hard Blasters na wengineo wengi popote mlipo toeni ideaz mbona mnajitenga au ninyi ndio bora kuliko fans?
_____________________________________________
Real-G the metaphorian
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 08:23
--------------------------------------------------------------------------------
any way nilikuwa mdogo ila nakumbuka enzi hizo bro wangu alikuwa ananipigia makele sana kwa sauti ya redio kufunguliwa hadi mwisho nakumbuka wimbo wa fresh prince and dj jazz jef wa summertime,nakumbuka wimbo wa lord of underground Ticktack,nawakumbuka kina shabalou na bugalou sijui kama nimepatia speling bila kuwasahau kid n' play
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 12 July 2002 09:46
--------------------------------------------------------------------------------
Ebwanaee burudani sio matani....."summer time" ya dj jazz jeff na fresh prince ilikua tight kipindi hicho na sija penda nyimbo nyingine yoyote ya fresh prince zaidi ya hiyo yale ma "boom boom shake the room" miyeyusho.
Du yani alcapaino umenikumbusha kweli! "the most beautiful" yani nilimzimia sana keith na video yake nayo ilikua tight! nakumbuka ilinifanya nitafute yale ma timbz ya njano. Na PMD nae album yake nimesahau jina ila kulikua na tracks mikosi kama ile "hard core" sijui ndio jina sawa..aliyo washirikisha das efx kwenye hook. "only built for cuban links" nayo ni classic! "rainy dayz" "incarcerated scar faces" "wu Gambino" n.k, zote tight. Na Ghost face "when the smoke is clear" "all that i got is u" kwenye album yake ya kwanza ya iron man.
Nadhani hiyo tape ya mtv uliyo ona meth alivyo imba m.e.t.h.o.d ni ile gza kasuka na alikua kajifunika nusu kichwa na hood tena sweat shirt lilikua la blue kama sikosei na meth ana flana la njano na tena la jersy ya hocky na black jeans na brown timbs (remeber that....nakurudisha golden days).
AAaaa!!! GZA "liquid sword" Classic!!! unakumbuka ile nyimbo iliyo enda.."when the emcees came to give out the name..and to perform...some had to smoke cocaine to act insaine..." Damn yani ni mikosi hata album yake ya "beneath the surface" nayo ni tight lakini hai husiki kwenye mjadala huu manake ni ya 1999.
Sunz Of Man "walkin through the vally of death" "party with a teck" n.k na killarmy sema ujue mashairi yao yalikua yakujificha sana wana weza wakasema hili kumbe wana manisha vingine mtu anaweza akatukanwa na asijue mpaka baada ya wiki yani ndio style hiyo lakni nao bado tight mpaka leo na album yao mpya ya "fear, love, and war" lakini tena najichanganya tuko miaka ya nyuma.
Na kweli tape zamani watu walikua wanazithamini kuliko rafiki du yani hata kunyonya kanda kwa mtu tabu eti kanda yake ita chuja na haita toa stereo, yani niki kumbuka ni vichekesho. Na hata uki pata kanda ina bidi ujaze vikaratasi kwenye vitundu vya juu ya kanda manake walikua wanavi vunja ili kanda isifutwe hahaahaa!
na tape za yo mtv zilikua zina zunguruka kipindi hicho kuliko hata forward messeges za mtandao.
kipindi hicho disco "debe" gari "mkoko". Na madrafti yalipoingia yani alcapaino umenikumbusha watu walivaa ya kila aina.
Kipindi cha mawingu mawingu kweli unakumbuka ile "oya msela oya" nayo ili hit kwenye radio za bongo.
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 10:18
--------------------------------------------------------------------------------
Unapoongelea Shaba-duu na Bouga-lou unanidatisha kabisa maana nakumbuka wakati huo 1989/1990 nilikuwa mkali wa kucheza break-dance kwa watoto wenzangu balaa(nikiwa nna miaka 10) mitaa ya Drive-In(msasani). Sasa ilikuwa kama kuna sherehe mtaani lazima mi na Bratha wangu(Geoff-KG) tualikwe halafu tunashindanishwa kucheza breakdance(zilikuwaga ni show tamu mno I remember).
One day kwenye sherehe mojawapo hivi bratha aliingia kufanya show na nyimbo ya 'Yekeyeke' by Mori Kante (nadhani wote mnakumbuka ilivyo-hit hii song) akaosha kinoma na ukichukulia hiyo nyimbo ilikuwa inapendwa sana watu wote waka-bow down kwake mi nikaonekana mzushi...I cant forget that day aisee ni long time maana nili-loose wachumba wangu wote,...wakati huohuo flash-backs zinatamba Rap ilikuwa haijachukua mkondo wake si mchezo.
Na pia hiyo nyimbo ya Fresh Prince licha ya kwamba sim-feel lakini ni moja ya track nzuri alizowahi piga,kumbuka pia alikuwepo Monie Love na track 'Grandpa's party','its a shame' na baadae akafyatua 'Born to breed', Queen Latifah naye na track yake 'Fly Girl' nasikia alikuwa anampika vidongo Bobby Brown alimchomekea.
---------------------------------------------
alcapaino"the one who fake none"
---------------------------------------------

--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 12 July 2002 10:47
--------------------------------------------------------------------------------
its a shayyayammm.... du hiyo nyimbo mpaka nika i choka...unamkumbuka curious na nyimbo yake "im curious", unakumbuka mama sayed nock u out ya LL cool J.
Hivi kama mnakumbuka katika movie ya break dance part 1 walipo kua wana shinda kucheza kweny disco ule Dj aliekua kifua wazi na machain yame kross kifuani kama mikanda ya bunduki ya rambo...alikua ni ice T.
mida!
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

#3 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 13 August 2002 - 02:26 PM

Hii topic ya 'ILIKUWA VIPI' ilianzishwa mwezi wa 7 mwaka 2002, ilipata mesage nyingi lakini katika kuhama Forum kwa sehemu mpya ikafutwa, kwa bahati nzuri forum ya zamani ilinusurika, hivyo nime paste message zote hapa chini, na kisha mnaweza kuendelea mazungumzo.

unregistered

posted 12 July 2002 11:17
--------------------------------------------------------------------------------
Sosa tuombe turudi long time,mi nakumbuka tape za Radio zilikuwa zinafanyiwa ukarabati mpaka watu tukawa ma-local djs,kwanza ile tape inanyanyuliwa kile ki-head chake ili iwe juujuu ipige 'mchicha',halafu mtu akikuazima Chrome(type II) unai-copy tape yote kwenye Goldstar halafu unambadilishia utumbo ukimrudishia hawezi gundua labda naye awe mzushi,unanikata Sosa unapokumbuka mpaka dressings hata mi huwa nakumbuka maana kila nikiona 'shining-kali' nilikuwa nasema ntapata wapi ile wear!...hebu niambie wakati huo ukivaa nguo au Cap yenye chata ya 'Chicago White Sox','Los Angeles Raiders','San Fransisco 49ers','Starter','Parental Advisory' ama 'Chicago Bulls' (kabla wamachinga hawajaaribu chati yake) halafu ukaenda Coko-Beach jumapili jioni jamii ilikuwa inateseka kiasi gani?......kama haitoshi niambie watoto wa Boarding wanapokuwa wamerudi likizo halafu inakuwepo Beach-Party au Concert 'Pool side',si ilikuwa balaa!.....
Ile track ya GZA 'when the mcees came..' imechukua jina la album...intro yake kuna katoto ka kichina kanaongea na chorus kapiga RZA(rizah)......unamkumbuka Killah Priest?...tusiwasahau Outkast na track yao 'payers ball'....mtu aniambie haya maneno ya nyimbo gani 'Well here's another one/In the gutter one/Getting running up..Quiz hiyo naacha
---------------------------------------------"the most illest one"
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 12 July 2002 11:20
--------------------------------------------------------------------------------
correction kwenye hiyo nyimbo ya Outkast ni "player's ball"...some typing errors
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 12 July 2002 11:46
--------------------------------------------------------------------------------
"I'm a true,what!? I'm a true Fuschnikens I'm a true!"(FU)... "You can't play with my homegirl Yoyo! Yoyo"Cube na Yoyo. "Wheres the party? the party is over here, wheres the party? the party is over here" 2 Too Many.
"How cool can one blackman be"Kool Mo D. "Move the Crowd"Eric B&Rakim. Yule aliimba I have got the power na say oops-up ni nani vile? jina limenitoka kidogo, wakati huo disco lilikuwa bomba, siku hizi kama sina hela ya bia siendi disco lakini zamani unajichanganya tu. Unakumbuka boom shalaklak boom everybody?? ni House of Pain kama sikosei. Kulikuwa na mtoto mmoja rapa anaitwa Chi Ali sijui alienda wapi, nakumbuka hii message ya "age aint nuthing but a number" niliisikia kwa huyu mtoto zamani kabla ya Aaaliyah (RIP), watu siku hizi wakisikia wana-refer kwa Aaliyah (RIP) lakini sio, Chi Ali ndio aliitoa kwanza. Hivi washkaji mmewahi kuwasikia Master Gee na Wonder Mic? hawa ni wa long time kinoma, wakati rap inaanza kuingizwa kwenye break-dance. Mnakumbuka Pac (RIP but a u really dead?)na hii track "Brenda's got a baby" au "Soulja's Story" chorus yake ilikuwa namna hii "Tell me what to do a soulja, soulja!" Kulikuwa na track moja ya Leaders of the New School wakati huo Busta wala hana umaarufu wowote chorus ilikuwa "Here we go yo, here we go yo,......thats scenario" kitu kama hicho washikaji, mambo ya zamani. Eazy-E (RIP) nae nilikuwa namfeel kinoma, mnakumbuka alivyomjibu Dre ilikuwa 1993? baada ya Dre kutoa Chronic alipokuwa anamtambulisha Snoop Dogg, hii track ya Eazy-E (RIP) ilikuwa inaanza "19..mut.....in 9..3, and am back again...EAZY-E the hiphop buster!" au NWA na ile Fuck tha Police, zamani watu walikuwa wanatoa vitu sio kwa ajili ya pesa tu..... Kulikuwa na mademu wanaitwa BWP (Bitches With Problem) sijui wako wapi siku hizi.... Cypress Hill na track yao inaitwa "insane in the membrane".
Kumbe sisi wengine tunaochangia hii mada age iko juu kidogo, kwa sababu mzee Alcapaino mwaka 1990 mimi nilikuwa form three! poa thats how it is, tuzidi kukumbushana mambo ya zamani.....signing off!
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 12 July 2002 13:05
--------------------------------------------------------------------------------
Hiyo ni kweli deezasta long time ilikua sio mpaka ulewe chicha nene ili uweze kufurahia disco. alcapino hiyo isue yakubadilishiwa utumbo ilinitokea tena ilikua album ya ODB jamaa kanirudishia na utombo tofauti alafu mono ile kinoma, alafu anajifanya hajui kinacho.
Ive got the Power waliimba "snap" sijui ndio sawa au vipi mimi mwenyewe wamenitoka.
Albam ya NWA ni ile ambayo hutaki kusikiliza mbele ya wazee na hata kama unasikiliza sauti ni ya chini labda ue peke yako. Lakini ile ilikua some live gangsta music kipindi hicho Dre, yellow sijui yella.., ice cube, eazy E ni balaaa.
Master Gee na wonder mic? donno.
Alcapaino unakumbuka bongo watu walivyo anza kufuga ma afro? enzi za '70 zilirudi.
Da nakumbuka mambo ya Kofia nakumbuka nilikua nayo A's ya kijani nilikua naiona kama diamond vile.
Mnamkumbuka curious na nyimbo yake "im curios", "beat nuts" na "we get props", la the darkman wa wu, king just.
Alafu Poetic wa grave diggaz alifarika juzi kati.
Je mnakumbuka enzi za "MC HAMMER"?

--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 12 July 2002 13:11
--------------------------------------------------------------------------------
Alacapaino nadhani hiyo ilikua nyimbo ya lords of the underground.....labda.
Na ile nyimbo ya gruru na nice and smooth nimeisahau jina kuna sehamu guru ana in gia "ini mini minimo......N.k
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 13 July 2002 10:17
--------------------------------------------------------------------------------
Duh Sosa enzi za MC Hammer ilikuwa balaa, unakumbuka ile dancing yake? wanasema alikuwa ana loose kilo fulani kila baada ya ku-dance. Unakumbuka disco watu walivyokuwa wanageza ile dancing yake?
Kuna kitu kimoja kime-touch sana Sosa ulichoongelea kwamba tulikuwa tunaweka kaduara hivi machizi zamani wakati wa ku-dance, duh hapa nawakumbuka machizi wangu wa zamani, zamani ilikuwa raha mwanangu....
Umewahi kusikia group lililokuwa linaitwa Sugarhill Gang? hapa nauhakika kwamba watu wengi wanaoingia kwenye hii forum walikuwa bado watoto au wana mwaka mmoja au miwili (don't mind). Hii Gang ndio alikuwepo Master Gee na Wonder Mike, walikuwa track yao moja ilikuwa inaitwa "Rapper's Delight", nafikiri kama sikosei hata Redman amejaribu kuirudia hapo miaka tisini katikati kama sikosei. Mnawakumbuka Public Enemy? unakumbuka Flavor Flav alivyopenda kuvaa? na wenzake Chuck D na yule DJ wao Terminator X?
Haya mambo yote ya zamani ndio yamekuja kuleta hii hiphop yetu ya TZ leo..
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 13 July 2002 10:46
--------------------------------------------------------------------------------
Hiyo track ya Guru na Nice & Smooth ilikuwa inaitwa DWYCK, si ndio kulikuwa na kipande fulani anarap Greg Nice akisema uuh lala a wiwi kitu kama hicho....
amani
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

unregistered

posted 13 July 2002 12:02
--------------------------------------------------------------------------------
Ndio sasa nimukuelewa ujue majina siwajui nilikua nawajua kama group sugarhill gang...rappers delight nani asieijua kama yupo basi aitafute asikilize hit za old school..sio redman peke yake kuna watu wengi tu waliimba baadae...."to the hiphop the hippidy hip hop"..nk..najaribu kukumbukia kidogo.
Nakumbuka red man, eric sermon na keith mury katika album yao ya "elnino" ndio waliimba.
Ile dance ya Mc Hammer sio mchezo yani moves zilikua nyingi mno lakini common kwa sana ni ile kama unatembea hivi lakini huendi popote, sijui umenielewa siunakumbuka lakini.
Good ol' dayz, mida.
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

ambax
Long time member
Member # 61
posted 13 July 2002 13:06
--------------------------------------------------------------------------------
"back in dayz ...
i usedd to enjoy all tha wayz...
back in tha dayz andaaa i wish i could be a kid a again...!!"
ahh kumamake.....those dayz NWA.,ONYX,JERU THA DAMAJA,PUBLIC ENEMY....walinidatisha kinooma....nilikuwa na brother wangu ambaye alikuwa akinifundisha ku-rhyme ee bwana ee ilikuwa taabu tupu mamaneno mengine yalikuw awala hayana maana yoyote ilimradi flava iwepo na uonekane unjua kunata na beat....mademu wakubabaikie..!!

check dis out .....
"BAM SIGILIBAAM.WO IGOT IT WARM..WHEN I SLAM..
YEAH I GOT IT ...TIK TAK ....
DEMA I GONA REMA NAP TIP TAP...aand aa kumamake nishasahau..."

dah enzi zile pick up ya mzee ilikuwa inakoma ...maanake night kali masela kibao wamejazana..mara LANG'ATA kwenye mashindano ya kurap..mara beach party "coco"..halafu masella kibao wa TMK walikuwa wanaharibu ..."mnawakumbuka pakaweusi?"...enzi hizoo kumamame RAMSON anampa kitu bitoz master T LAIV KWENYE mic....

--------------------

http://www.africansoul.4t.com
ambaxgreat minds discuss ideas for solving problems,medium sized minds discuss about events,...and shallow minded discuss about people's negative aspects..!!!

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 60 | From: changanyikeni....dsm | Registered: Mar 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 13 July 2002 13:56
--------------------------------------------------------------------------------
ambax naona umeacha kuendelea na matibabu, manake zimesha kuruka tena.
Kweli bwana magari long time yalikua yana teseka sio pick up tu hata vi corola watu mpaka kwenye mabuti night kali siunajua usafiri wakurudia.

alafu hilo jina paka weusi nalikumbuka sema sio watoto wa mitaa ya drive-in kweli? au baadhi yao wametoka temeke?

--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 16 July 2002 07:16
--------------------------------------------------------------------------------
Ile Quiz niliyotoa...'Well,here's onother one/in the gutter one/getting running up/troublesome.....' ilikuwa ni verse ya kwanza ya 'fredro'(ONYX) ktk nyimbo ya 'Slam', anyway 2 proceed nilimfeel sana Mc-Hammer kwa mida ile alikuwa 'tait', tumkumbuke pia Vanilla-Ice though most of 'em Hard-niggaz hawakum-feel lakini aliamsha nyoyo za rap pia mpaka akamleta 'Saleh Jabir' kwenye jukwaa la rap.
Msimsahau AZ na Nas walivyokuja nadhani Sosa ameshaliongelea hili lakini ile track 'It aint hard 2 tell' ni balaa na nyingine zote kwenye ile album(shangaa Nas hakuuza sana Ilmatic lakini ni one of the best albums kwenye hiphop), kumbukeni kuna kikundi kiliitwa 'Technotronics' mwaka 1989 mwishoni walifyatua nyimbo yao 'Pumps up the jam' kitu kama hicho, mida ile ile ilipotoka 'Yekeyeke' na 'U cant touch this' by mc hammer...na ni mida hiyohiyo Salt-N-Pepa walitamba na 'Aaaaah...Push it', pia walikuwepo RedHeadKingPin walikuwa na nyimbo inaitwa 'Do the right Thing' ilikuwa si mchezooo,nawakumbuka NWA nilikuwa nna original-tape ya album yao 'EFIL4ZAGGIN' ni kinyume cha 'Niggaz4Life',King-Just namfeel mpaka leo alikuwemo kwenye album ya Ed-Lover& Doctor.Dre nyimbo inaitwa 'Who's the Man' pia walimshirikisha Natorious kwenye hiyo Cut, 'I am Curious' naikumbuka na ilikuwepo kwenye one of my MTV collections, mnakumbuka track inaitwa 'Brooklyn Blocks' aliimba BuckShot,Master-Ace & Special Ed pia track ya RedMan 'time 4 some action' ni tait balaa, walikuwepo B.U.M.S(Brothers under Madness) ila hawa walikuwa mabitoz kidogo...na pia Illegal(Malik & Jamal)nilishawataja hawa na track yao 'I get bizzie on the Mic'....nawakumbuka 'Flem-Lee'
na pia track ya Fu-schnickens it goes like 'LA-schmoove yo we don't got nuttin to prove',lazima uijue hii kama kweli ni hip-hopian maana wakati huo Das-Efx wanakata mbuga na 'Microphone Cheka' & 'They want Efx'....alikuja jamaa mmoja ana-appearance ya kizee-zee anaitwa Nine(9) sijui kaishia wapi huyu.....N-way naenda kula 2be continued
---------------------------------------------
'The Most Illest'
alcapaino

--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 16 July 2002 13:19
--------------------------------------------------------------------------------
rakim ndio rap master zamani
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

Barakah aka Shaheed
Long time member
Member # 14
posted 17 July 2002 00:42
--------------------------------------------------------------------------------
too many memories Mgullu...!
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: Mid-West....Wichita,Kansas[TZ in my blood] | Registered: Nov 2000 | IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 17 July 2002 01:34
--------------------------------------------------------------------------------
Unamanisha nini unaposema mgullu??
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 17 July 2002 10:58
--------------------------------------------------------------------------------
sema Barakah, mambo vipi mzee, hiphop zamani inanikumbusha that crew we'formed iliitwa 'Untouchables' kwa wakati huo ikimshirikisha abdallah(a.k.a Supu)..Baraka na mgullu(alcapaino)...anyway production kwa wakati huo haikuwa juu kama sasa lakini few years then,Baraka alifanya track(Battle field) with Abbas & Steve-B, kila mtu atakubali jinsi Undergroud-Souls walivyokonga nyoyo wakati huo labda kama hukuwepo nchini...sijui kwa nini hii crew haiku-proceed kuwasha moto kwenye hiphop- ground as a group...anyway hayo ni mambo ya hapa na pale,.....hiphop zamani inanikumbusha crew moja ya Mikocheni-B iliitwa No-Name(includes Funka-black,Ugali etc),hawa jamaa nao wali-kuwa tait mpaka leo nnazo some of their home-productionz.....
Sosa nna tape moja ya local-productionz ya zamani mno nai-feel sana wakati huo tuna-form 'Untouchables' sijui tulikuwa form two ukiisikiliza lazima uta-feel ingawa ipo old-school kiaina.....big-up wazee
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 17 July 2002 12:42
--------------------------------------------------------------------------------
Nakumbuka no name niliwaona waki perform empress, siku wasikia tena. Sijawahi kusikia kundi lako alcapaino, alafu kuna kipindi vikundi vilikua vingi sana mpaka mtu unakua huelewi yupi ndio yupi manake una weza kusikia nyimbo lakini usijue ni nani au wakina nani siunajua. Kama ile nyimbo ya "rhymson" (sijui spellin yake) iliyo itwa "you know the R" haiku sikika hata radioni kwa sana kwa hiyo kama hivyo ndio mana nyimbo zingine zina pita bila kuzijua. Na ile nyimbo ya underground souls niliisikia sema kusema ukweli verse ya pili siku ifeel, ile verse ambayo jamaa anasema 'my shit is boom boom" siunajua. lakini hook tight na kila kitu na beats nayo ilikua makini. mida
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

unregistered

posted 18 July 2002 04:39
--------------------------------------------------------------------------------
Those niggaz(UnderGround Souls) were tight kama puzee ya katoto kachanga....ile verse ya pili ilikuwa ya Steve-B(Radio-Clouds Dj), 1st verse alichana Abbas & the last verse woz my man Barakah, ile track niliisikia kwa mara ya kwanza nipo Arusha shule(Ilboru) nikasema Bongo inawaka moto soon,...those niggiz were representin' so'siri (big-up 2 'em all).....Sosa crew yangu haikuwahi kutoa nyimbo redioni lakini kuna some concerts tulikuwa tunafanya shows na kwa wakati huo Rap haikuwa inakubalika kama sasa so most of our works woz underground, tulifanya home-productions nyingi tu tukiwa na Producer wetu Tumaini(Tommy-G),One-Love Kid!,wakati huo ni mwendo wa instrumental za 'Kinanda' nadhani unakumbuka tulipotoka, ofcoz it woz str8 for fun not commercial.
I'll make u listen to those stuffs one day, Peace
--------------------------------------------
'the most illest one'
a tru' hip-hop head
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 18 July 2002 05:14
--------------------------------------------------------------------------------
hip-hop zamani inanikumbusha wakati huo walivyoibuka WWA-weusi wagumu asilia(one member tuliakaa nae Drive-In), hawa jamaa walijitahidi sana hasa kwa wakati huo na nnadhani ukimwondoa Saleh-Jabir,album ya kwanza(self-creativity) ya bongo-hiphop kuingia kwenye market ilikuwa yao,wakati huo watu wengi hawakuamini kama unaweza ukatoa album ya kiswahili na ukajulikana,it woz a long time,..anyway lakini walizikwa hela vibaya,wahindi waliwaingiza mjini na kwa watu wa mikoani kama Songea n.k watakwambia jinsi album ya hawa jamaa ilivyouzwa huko lakini wao walichelewa kujua hilo,kuna track zao zilitamba kama 'jua kali latuathiri wabongo','tunachum','mgumu wa shoka',n.k nilikuwa na copy yao nadhani itakuwepo kwenye Lab yangu,baadae walikuja jamaa wanaitwa DaYoungMob(kitu kama hicho) sijui walitokea Mwenge au wapi lakini nakumbuka nao waliwika sana nawapa Mic kwa kuitoa hiphop mbali,nani anakumbuka nyimbo moja hivi iliitwa 'kizaazaa' wakati huohuo Sos-B anatamba na 'kukuru-kakara zako'.....Hard-Blasterz waliwika na 'usiige mambo ya mjini','kua ukomae' n.k ,album yao ilikuwa tait mno walimshirikisha jamaa mmoja anaitwa Tough-Jam(naye alitokea Drive-in,Namanga), jamaa alikuwa anachana fastafasta hivi alikonga sana nyoyo za watu,wengi walim-nickname as (Bwana Masanja)....tusimsahau Fresh-G na Eazy-B(wote wa KU crew)
------------------------------------------------------------------------------------------
'the most illest one'
only built 4 hiphop headz
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

unregistered

posted 18 July 2002 06:47
--------------------------------------------------------------------------------
I waz really feeling Underground Souls,mara ya kwanza nilivyowasikia sikujua kama ni wabongo ila kuna maneno ya kiswahili kidogo mle ndani kama 'coco beach' na 'salamander corner' ndipo nikaamini,walikuwa wapo safi,mi mwenyewe namaindi mno hiphop nawakumbuka niggas 2 publick video yao inaitwa 'vijana kuwa makini' ilikuwa nzuri, pia GWM walipokuja na nyimbo zao 'haya twende haya twende' na 'kasheshe' niliwapenda mno na nilishaona concert zao mbili tofauti moja coco beach na moja ilikuwa kubwa ilifanyika Drive-in cinema(panapojengwa ubalozi mpya wa marekani) ilishirikisha mpaka bendi mbalimbali, ilikuwa bomba sana
tchaooooo

#4 Juma4

    African Hip Hop Admin

  • Administrators
  • 1,015 posts
  • LocationAmsterdam

Posted 13 August 2002 - 02:27 PM

Hii topic ya 'ILIKUWA VIPI' ilianzishwa mwezi wa 7 mwaka 2002, ilipata mesage nyingi lakini katika kuhama Forum kwa sehemu mpya ikafutwa, kwa bahati nzuri forum ya zamani ilinusurika, hivyo nime paste message zote hapa chini, na kisha mnaweza kuendelea mazungumzo.

Juma4
Administrator
Member # 2
posted 18 July 2002 07:16
--------------------------------------------------------------------------------
Soundtrack yake hii hapa: http://www.africanhiphop.com/core/modul ... d=7&page=1
ni mix ya saa nzima ambayo inapresent baadhi ya majina yalioyotajwa hapa juu.
Sasa ALPACINO umesema uko na tape moja ya zamani, hebu niambie kuna nyimbo gani hasa? Kwani natafuta zile za zamani hasa kama kwality si Goldstar sana kama unayo basi tufanye swap fulani nikutumie copy nyingine kwani ninazo kaset karibu zote zilizotoka ila kuna baadhi ya nyimbo zilizopigwa redioni ambazo sijaweza kupata kama SAA ZA KAZI ya kina HASHIM, BONNIE HARMONY, pia za Underground Souls, No Name, n.k. Niandikie kwenye e-mail j4-oldschool@africanhiphop.com

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 206 | From: Amsterdam | Registered: Nov 2000 | IP: Logged

Juma4
Administrator
Member # 2
posted 18 July 2002 07:18
--------------------------------------------------------------------------------
Pia katika tracklist ya page niliyokupa hapa juu kuna nyimbho moja ya Mr Ebbo!! Akiimba ragga stylee
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 206 | From: Amsterdam | Registered: Nov 2000 | IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 19 July 2002 06:55
--------------------------------------------------------------------------------
hamna noma J4,ntafanya hiyo kitu inabidi nirudi Lab kutazama hizo tapes its ma' hope kwamba zipo maana ni long time niliziacha kwenye makabati,...anyway who rememba' the song "sometimez i rhyme quik sometimez i rhyme slow'...ya zamani kinoma
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

Deezasta
Long time member
Member # 266
posted 21 July 2002 07:45
--------------------------------------------------------------------------------
Alcapaino, sio rap ya Nice & Smooth hiyo kama sijakosea? Ilikuwa 1992 hivi?
--------------------

Who feels it, knows it

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 32 | From: Arusha, Tanzania | Registered: Feb 2002 | IP: Logged

alcapaino.
Long time member
Member # 244
posted 22 July 2002 04:17
--------------------------------------------------------------------------------
that woz it,lakini kuna nyingine tena alipiga jamaa nimemsahau jina nilikuwa nayo kwenye Mtv collection zamani sana...N-one anayetaka kusikiliza hizo long-time tracks aende http://www.undergroundhiphop.com,...i just wanna make 'em heads remember wakati huo Mawingu-Band inarekodi video ya nyimbo zake(R&B) pale Cine-Club Mikocheni na Hard-Blasters walikuwa wanarekodi tracks(video) zao kama 'Usiige mambo ya mjini' n.k, nakumbuka wakati huo ilikuwa bomba sana.....pia ilivyorekodiwa 'Oya msela' kama utaangalia vizuri video yake kuna vichwa kibao vya hiphop mle ndani....na pia shooting ya KU-crew pale Tanesco basketball court(Drive-In) ni long taim kishenzi nakumbuka tulikuwa tunaona raha kinoma kuonekana kwenye shooting,u kno' way-back thangs,deezasta unakumbuka album ya hao jamaa Nice-N-Smooth inaitwa 'jewel of the nile' kuna track inaitwa 'old to the new' ilikuwa balaa hasa shooting yake, remember 'em ShowBiz & Ag walikuwa tait,powa.
--------------------

'definetly the most illest one'
100% correcto so pay respecto

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 20 | From: University-Dsm (bongo since day-1) | Registered: Jan 2002 | IP: Logged

unregistered

posted 01 August 2002 10:53
--------------------------------------------------------------------------------
naona watu mmelala hapa hata wale mliokuwa mnachangia sana naona kimya,kumbukumbu zimeisha nini? Msijali nilikuwa nawa-challenge tu lakini nahisi watu wengi hawakuwepo zama hizo zinazoongelewa, inasikitisha kidogo. Nimekumbuka oyaa msela ilivyokuwa inarekodiwa na kuna yule dada alivaa nguo ya kitenge walimweka kwenye chorus alisaidia naye,dah wakati huo kwanza unit wanatamba namkumbuka marehemu D-Rob akishapuliza kijiti-pombe anashuka verse balaa, Hard Blasters nawapa mic za kutosha walishawahi kuwa mabingwa wa rap(wakati huo J hayupo nao), hiyo concert ya Cine-club ya kurekodi video zao naikumbuka na nakumbuka Crazy one(wille) alikuwa amevaa soksi kichwani ila walikuwa wengi wengi sijui wengine wameishia wapi?
Katika kikundi nilichokuwa nakichukia ni hao wazee wazee nice&smooth sitaki hata kuwasikia walikuwa wanapiga kelele tu
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

unregistered

posted 01 August 2002 11:02
--------------------------------------------------------------------------------
mi jamani naomba tuongelee hasahasa hapa nyumbani jinsi ilivyokuwa lakini nilikuwa nashauri tukumbushie na flashbacks pia kwani wakati huo zilivuma sana na wengi tulizipenda hizo hata kabla ya Rap kuja kwa mfano blackbox madreamlover, been around the world etc. Oneni wenyewe nyimbo nyingi rap ya leo inafanya sampling kutoka huko.
tchaooo
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

pat
Recent member
Member # 170
posted 01 August 2002 13:31
--------------------------------------------------------------------------------
Nakumbuka combination ya HBC na DPTwakimshirikisha Dj born Luv
Iliitwa <1995>ninety five
--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 6 | From: Tanzania | Registered: Nov 2001 | IP: Logged

posted 05 August 2002 21:53
--------------------------------------------------------------------------------
Dahh eh bwana wehhhhhh,yaani hii history
ni soo kwa hao ambao walipitwa katika kipindi
hiki cha hip hop ndani ya Bongo!!!
Yaani masela mmeongelea kila kitu hapa,siyo
siri mimi sijafungua hii web kitambo kweli na
leo nimesema ngoja nifungue nione nini kinach
oendelea humu ndani.
Eh bwana nimesoma kila hoja mlizoelezea humu
ndani na watu wawili ndiyo wanakumbuka nini
kilichokuwa kinafanyika,au tunaweza kusema nd
iyo watu waliokuwa wanafuatilia hip hop na wa
naoijua,maanayake nimecheka mpaka basi hii le
o kwani kuna mambo mengine mshikaji wangu ya
likuwa soo!!!!Ahhhhhhh Ahhhhhhh h hhh,eh bwa
na nyie machalii wa sasahivi siuji kama mnawe
za kufaidi hip hop kama sisi wazee wa wakati
huo.
Eh bwana mi nakumbuka kipindi hiyo hapo unie
lezi kitu wala nini mzee nina mdundo wangu wa
jeshi au siyo bwana na jeans yangu kiaina kat
a K nina mdraft juu au nina T-shirt ya masela
wangu wa Cypress Hill(B-Real,Dj Smugg,Sen Dog
g)sina haja ya kuongea sana kwa nini nilikuwa
na wa-feel hawa watu lakini watu wazamani wen
yewe mnaelewa what's up?
Basi pindi hiyo hapo si mshikemshike na wajes
hi lakini masela tulikuwa tunakomaa hivyohivy
o,yaani ilikuwa uzushi wajeshi hadi ndani ya
club nini wanakuchojolesha,mwanao ndani unaka
aa kimachale dahhhh eh bwana lon' time masela
Pindi za "bottle party" hebu niambie mwanao
kweli kile kipindi kitarudi bongo?Hatahhhhhh!
Eh bwana watu wanavunja mic kama hawana akili
nzuri vile macopy,track zao wenyewe na kila
kitu.
Eh bwana hakuna tamasha litakalotokea kama la
Empress Cinema,maanayake watu walikuwa wanavu
nja ile kisawa,kuna dogo mmoja alikuja pale
juu alikuwa anajiita "Middle Finger" alikuwa
na mistari tight nafikiri kama sijakosea alik
uwa kama K-U Foundation kwani ndiyo aliokuwa
nao muda wote na alikuwa anatokea K/Nyama.
Sijui kama atakuwa yupo kwenye fani lakini ka
badilisha jina?Alafu tukio lingine ambalo lil
iniuzi ni pale mwana-raggamufin wetu Cyada Ma
n au Amanigga love-Chanta aha ahaha aah!alivy
o mtosa mshikaji wake alikuwa Mc au bado ni
Mc anaitwa Kevine jina lake la kisanii nimeli
sahau,dahhhhhhhhh ikuwa soo ile kinoma hebu
fikiria kwenye jukwaaa kila mtu anawatoleeni
macho alafu mzee unatoswa ile kinomanoma maan
ayake jamaa alikuwa anaifuata mic kabisa laki
ni Cyada alivyokuwa hana akili na siyo msanii
wa kweli alimtosa mshikaji badala ya kum-hook
up!!!Nakumbuka miaka ya karibuni alitoka na
kitu pamoja na akina J-Mo kinaitwa Hip-Hop Ra
gga kama sijakosea.
Mnawakumbuka akina Nigga Bass,mnawakumbuka ak
ina Killer B hao ni miongoni mwa the earliest
cats ndani ya fani(Bongo),kila B nasikia sasa
hivi yupo kwenye imani ya Rastafarian,one lov
son!kama unaingiaga kwenye hii web kujikumbus
ha na kujua jinsi gani fani hii inavyokuwa.
Eh bwana mi hapa nitarudi tena na mambo mengi
tu,na hii ni faida kwa wasanii wa sasahivi,ya
ani ni shule kwenu,
Amani kwenu wote majibaba wazamani
Ah hahah a ahaha ahahahahahaha aha a ha h!
--------------------------------------------------------------------------------
IP: Logged

sosa
Long time member
Member # 161
posted 06 August 2002 02:23
--------------------------------------------------------------------------------
Mjadala unaendelea, brainnocker nyambie kachaa wangu. Hiyo umenikumbusha Cyadaman alivyo mnyima mic mchaa....lakini huku kosea na alikuepo kwenye nyimbo ya hiphop ragga walikua wanajiita "wateule" sasa hivi nadhani wamebakia wawili tu.
Killa B ni rasta sikihizi na midread, lakini nadhani aliimba kwenye album ya hard blasters "kubwa kuliko".
Mida masela.
--------------------

"THE ILLEST CAT ON DA INTERNET"

--------------------------------------------------------------------------------
Posts: 143 | From: Tanzania, manzese kwa mfuga mbwa | Registered: Oct 2001 | IP: Logged

#5 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 15 August 2002 - 09:53 AM

Am back again baada ya kupotea, nway nilipata misiba miwili ndani ya wiki moja, my young bro n then my Mom , (RIP). But still nakumbuka long taim wakati huo disco lipo Oysterbay ( La Dorce Vita) kipindi hicho kiingilio sijui buku mbili ila watu tulikuwa tunaruka ukuta kwa nyuma tunatokea kwenye bustani ya maua then tunaibukia chooni, umenikumbusha enzi za kuvaa black-boot na draft juu yake, sio siri ilikuwa mpeleke-mpeleke sana na masoja mitaa ya kati, huyo killa-B kwa sasa ni mtangazaji wa fm-redio na bado wana crew yao ipo kimara mwisho (maskani kimara) inaitwa Imeditation Kingdom(IK), yumo kwenye HBC album track inaitwa 'Time 4 action'. Last sunday(11thAug2002) nikiwa na home-boys tuna-sip some lika mitaa ya maskani nait ya saa tano na kuendelea kuna dj mmoja wa clouds alikuwa anatwanga mawe si mchezo mpaka wote tulipagawa baadhi ya track alizopiga ni 'push it' ya salt-N-Pepa, akapiga 'whats up Doc? na 'Laschmove', zote za Fuschnickens, akapiga 'Word-up' by Cameo na track nyingine kibao za longtaim mpaka pombe ikaisha jinsi tulivyokuwa tumeanza kucheza pale baa kama machizi.
Kuna concert moja kubwa ilifanyika Drive-In cinema(ubalozi wa marekani unapojengwa) nakumbuka master T alikuwa ana-introduce Cd ya Galinoma, wakati huohuo lemmy Ongara anawekaweka vifaa vyake vizuri ili aanze kutumbuiza, ikatokea 'beef' Lemmy akaanza kukoroma ili master-T aondoke kwenye stage sababu hakuwemo kwenye ratiba, sasa viumbe vilipojifanya havimsikilizi akaenda kuchomoa power-cable yake ambayo ndiyo ilikuwa inaleta umeme kwenye show nzima na show ikaishia hapo, watu wacha tuanze kumtukana lemmy na yeye akatukana sana akaishia na kagari kake, ilikuwa mida kama ya sasa nane usiku. Kwenye hiyo show GWM waling'ara sana na nyimbo zao 'cheza mbali na kasheshe' na 'haya twende haya twende', kwenye turn-table akiwepo Bonnie.
Wazushi walidai eti Lemmy hammaindi master-T sababu alikuwa hapigi nyimbo zake redioni(wakati huo radio One) anapiga za kina Galinoma.

#6 Guest_nge_*

  • Guests

Posted 15 August 2002 - 10:41 AM

Nakumbuka bongo flava wakati huo KU walikuwa wanatamba naPUT YA HANDS IN AIR,nadhani mnamkumbuka SEBASTIAN Maganga wakati huo akiwa na kundi la Afro reign walitamba sana na wimbo wa JUVINILE na AFRO RAIN KWENYE JIJI LA BONGO yaani mnanikumbusha mbali sana wakati huo kulikuwa na combonation ya DiplomatznaHBC wimbo wa NINETEEN NINETY FIVE<1995>NADHANI SAIGON AU WILLIE TERRY AU BORN LUV NITAKUWA NAWAKUMBUSHA MBALI kwani born luv alipewa featuring ndani ya huo wimbo
Mnawakumbuka 4KREWZ FLEVA Enzi za kina Mr Paul amakweli watu wametoka mbali,akina Makay nasika makay sikuhizi ni presenter wa east african,akina mussa aka mos
Nakumbuka Mr paul alitamba sana na wimbo wa One you have na Party aliowashirikisha unique sistaz
Msiwasahau unique sistaz nao wametoka mbali walitamba na wimbo wa SUMMERPARTY kabla haujaja kufanyiwa remix na Master J

#7 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 15 August 2002 - 12:28 PM

alcapaino pole sana kwa misiba, ni mzito sana laknini inaonekana una stahimili hali.

Ila bwana kikundi cha GWM walivyo toa nyimbo ya "cheza mbali na kasheshe" wali shine sana, mpaka walivyo kua wakipanda kwenye maconcert watu lazima washangilie sana. Ebanae masela naona ma memory yamepotea ghafla, mida tena. :?

#8 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 15 August 2002 - 01:20 PM

Thanks mzee Sosa ndo' mambo ya Mwenyezi hayo hapana weza zuia, Ambax mbona kimya sana sijaona kumbukumbu yake ya maana humu ndani au alikuwa uspanyola zama hizo( akitengeneza singo yake-shangwe), namkumbuka Y-thang (KU crew) na track yake the modivator, thatshitwoztait. Kuna Beach-Party flani sitaisahau kwa mara ya kwanza nasikia nyimbo ya Snoop 'whats my name' na siku hiyohiyo wakapiga nyimbo ya Eazy-E 'Real Mothafukin Gees', kubabake ilikuwa ni balaa home-boys tulipagawa usiseme, halafu kuna mpuuzi flani akaibuka na style ya Snoop na nyimbo yake 'Froggy Doggy Style' ilisound the same na 'whats my name' ila maneno tofauti tu ,simkumbuki jina maana nilimsikia Beach-Party, kama mtu atakumbuka kwenye hiyo BeachParty watu walikuwa wanachana juu ya Canter(kenta), wakati huo ukitoa singo hata kama ni mbaya itapigwa tu redioni na jamii itakubali kwamba wewe ni emcee maana kipindi hicho studio zenyewe za kudonyoa kila mtu anakimbilia Don-Bosco.
Ntarudi tena ngoja nikumbuke zaidi,
Alcapaino-'the most illest one'
am :( like dat

#9 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 16 August 2002 - 07:54 AM

Year ngoja niwakumbushe kitu sijui lady jay dee yupo wapi?Wakati huo hajulikani alikuwa anapiga simu radio one kwenye Dj Show Halafu Dj Mike Mhagama wakati huo alikuwa anamwekea instumental ya Mc Lyte KEEP ON KEEPIN" ON na yeye anachana kupitia simu alikuwa anajitahidi siku nyingine akawekewa instrumental ya Fox Brown GET HOME TONIGHT akaimba verse kidogo akachemsha Baada ya hapo nilkuja kumsikia ameshirikishwa na jamaa mmoja sikumbuki vizuri jina ila nakumbuka jina ATTACK wakati huo lady jay dee anaimba rap sio siku hizi R&B

Halafu namkumbuka dogo mmoja alikuwa anaitwa Born Harmony alikuwa katika kundi la AFro Rain alikuwa Balaa huyu jamaa ndo aloimba na Hashim wimbo wa SAA ZA KAZI

Halafu mnakumbuka wimbo wa MAKONDA wa SOS B na Kundi lake la Black Armies wakati huo Hashim ndo yupo katika hilo kundi
Halafu ikajaga combination moja nzuri sana ya Mr 2 na SOS B wakati huo wote ndo wanatikisa bongo sikumbuki jina la wimbo ila albamu ilikuwa ya MR 2 NDANI YA BONGO

#10 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 16 August 2002 - 08:54 AM

Nilkikua nasikia tu kwamba sos b alikua kundi moja na hashim, lakini hata siku moja sijawahi kusikia nyimbo walio imba pamoja. Na kile kikundi cha hashim "bongo pschycological" kiliishia wapi? mbona sijasikia nyimbo yao hata moja au ni mimi tu ambae sijazisikia?
Hiyo ya Lady jay dee nakumbuka alikua ana imba kwenye simu, na watu wengine pia walikua wakifanya hivyo.
Hivi mnakumbuka ule wimbo wa "ukimwi" ilikua ina enda hivi kama sijakosea ".....niwakati wakujilinda sasa...ukimwi huo..." ilikua na video yake, nimesahau jina la kikundi. Jamaa walikua na ka mtindo poa kakuchana. Na nyimbo ya K-Single wa Kwanza Unit ilikua nzuri kiasi chake ili itwa "headz on the regular".
Lakini katika nyimbo hardcore za bongo ambazo ninazizimia kwa sana kutokana na mistari yake yani ile ya "noma kwako" siunajua, kama ile "jituuu jituu jitu gani" ya live with purpose na ile ya "kula konaaa" ya manzese crew sana sana pale jamaa verse ya pili anaingia ".....twefanya ubaya saa sita mchana mbuzi anakula jani" yani hiyo ni metaphore ya kibongo simchezo. Hata verse ya kwanza nayo tamu vile vile "...watu wakubwa wachangishana mapesa, lakini siyeee twasikitisha" jama ana ingiza ka sauti kakizenji.

#11 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 16 August 2002 - 09:23 AM

Ndio ule wimbo wa ukimwi ulikuwa unaitwa KITHAA THAA ambao umeimbwa na kundi lililokuwa linaitwa FUN WITH SENSE nakumbuka huyo jamaa unaesema alikuwa anaimba ki staili alikuwa anaitwa JOSE na nakumbuka baadhi ya maneno alikuwa anasema 'KINGA NI KUJILINDA KUNA MASHARTI USIWE MWASHERATI NA MENGINE YOTE UYAFUATE,UKIMWI KIMWI HUO SHAURI YAKO halafu kunasehemu nyingine anasema CHEZA NGOMA KUTWA LAKINI USICHEZEE KINYAMA UTAKUFA AU USIKILIZE MAAGIZO NA KAMA AKILI UNAZO,NAKWENDA NACHEZA NARINGA NA USIFANYE UJINGAUJINGA

NA KULE BUKOBA IMEBAKI MIGOMBA NDO BANDARI YA SALAMA HAKUNA USALAMA INGAWA SALAMA YATAMBULIKA KAMA ZANA BORA SANA
HATUNA BUDI,KWA JUHUDI SALAMA ZISAMBAZWE MPAKA HUKO SHULENI USIULIZE KWANINI HIVI NDIVO ILIVYO NA MAPENZE YANASHULE VYOVYOTE VILE NAJUA MNAWEZA WAJIKAJI TULIENI TUUWACHE UASHERATI,MUNGU TUMUOMBE TUCHINJE HATA NGOMBE KIJADI TUTAMBIKE

Naukumbuka sana huu wimbo mzee Sosa manake watu wengi walikuwa wanaupenda basi nikiwa school nikianza kuuimba sikilizia mademu wanavyonizunguka basi msela wako nakombea ujiko mzee nakumbuka mbali we acha tu!

#12 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 16 August 2002 - 11:19 AM

They got style, nakumbuka kidhaa-dhaa ilikuwa inachoma nyoyo hasa waliposema 'kule bukoba imebaki migomba', video yao walikuwa kama wapo kwenye ngazi majankii wawili wamevaa mashati ya draft, kitu kama hicho. Sos-B alivyohit na 'Makonda' ilikuwa bomba na niliipenda track sababu makonda mi mwenyewe ilikuwa ni beef daily. Mnakumbuka Mr.II na track yake 'siku yangu' alivyokuwa anajimegea na nyingine ilikuwa imetulia lyrically 'ni wapi tunapokwenda' kitu kama hicho nimesahau, nani anamkumbuka dogo mmoja anaitwa BuggsMalone alikuwa anajitahidi naye kwenye mistari mara nyingi alikuwa ana-hang na KU-crew.
alcapaino:oops:

#13 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 16 August 2002 - 03:28 PM

Buggzy ali tokea kwa mara ya kwanza na marehemu D'rob katika nyimbo yao "we keep it tight" na akaja baadae na nyimbo iliokua ina akili na hisia nyingi ndani yake kuhusiana na Africa ilikua inaitwa "kama hujui unapotoa" lakini verse alivunja yai.

Alafu kulikua na uzushi flani kwamba ile nyimbo ya "siku yangu" aliwa diss KU katika kipande baada ya mashindano ya empress ndio beef ilipoanzia. Kama pale aliposema "hii tisini na tano, hata mje watano..." na KU walikua watano. Na KU nao wakaja na track yao katika albam moja hivi jina nimeisahau lakini ilikua na nyimbo kama "nataka kunata" kuna nyimbo eazy B alikua katika kiitikio nayo walikua wana diss maemcee waliokua katika tamasha la empress kwasababu walikua wana sema KU walipendelewa ushindi wa kwanza. kiitikio kilikua kinaenda "suckers are flipin' are tripin', as if they realy got the pretensio, so chick the rhyme the instrumeno (tal)".
Ile ya makondo iliheat sana kutokana na watu kweli ni beef daily na makonda.
Unakumbuka ile nyimbo moja hivi "twayalani twaeleza" walikua wana paka madawa ya kulevya alafu ukitazama video yake karibu wote walikua bange kinoma yani vichekesho. Mtu analaani pombe huku kalewa, nikama hivyo yani siunajua big so'.

#14 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 17 August 2002 - 07:32 AM

Oyaa.. masela mnakumbuka hii sumsing:

http://www.undergroundhiphop.com/temp/r ... 928064.ram

#15 nge

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 42 posts
  • LocationK.I.M.A.R.A

Posted 17 August 2002 - 05:18 PM

Ndio mzee Sosa nawakumba sana wale waloimba Twalaani twaeleza madawa ya kulevya bila shaka walikuwa wanatokea temeke hivi halafu kulikuwa kama kuna dogo mmoja katika hilo kundi?Halafu wazushi wanadai eti kulikuwa na beef kati ya GWM na SOS B wakati huo na kwamba Kwenye wimbo wa KKZ kuna sehemu SOS anasema WANACHEZA CHEZA GRARIDE KAMA MP Halafu kuna wimbo GWM nao nasikia walimpaka kuwa ni SOS B wa mabitch Thats stand for B Halafu SOS akaja nae kupaka tena kwenye wimbo wa HADITHI NJOO But sina uhakika ni stori tu nilizisikia kwa mtu.
Kuhusu Buggs Malone ni member wa KU kwani wimbo wake upo ndani ya albamu ya MKwanzania.Halafu ikumbukwe kuwa KU walikuwa wengi sana sio watano tu KUna akina Y thang ambae anatangaza ITV anatumia jina la YUSUF LAMEK Kuna Kibacha a.k.a KBC au jina lingine K-single kama mnamkumbuka alikuwa mtangazaji wa Clouds Kuna Chief Rhymson Kuna Late D-Robert a.ka D-Rob na wengine wao majina yamenitoka labda nikiyakumbuka halafu watu wanadai katika wimbo wa MSAFIRI sehemu ambayo D-rob anachana ni kama alikuwa anakiona kifo chake pale anaposema

NILIKUWA MSEMA HADITHI SISEMI TENA
ROB-SI RAP TENA
MAOVU NI YAMEJAA HAKUNA MEMA
NIITE ZOMBA NATAKA KUPIGA BUNDA DUNIANI
KAMA MOTONI NAOTA NDOTO ZA PEPONI
NAMWONA SHETANI
ANIULIZA WE NI NANI
NA WATAKA NINI
PESA MAGARI NA MAJUMBA YA KIFAHARI
NJOO NIFUATE MIMI
NAKUWA MAKINI LAKINI NAONA GIZA
NASONGA MBELE NAPIGA MAYOWE
LITAKALO KUWA NA LIWE
NIPO MWENYEWE KATIKATI MBALI NYUMA MBALI
NAKUTANA NA MAMBO MENGI ILI MRADI TU HATARI
UNYAMA HAKUNA UTU NIGHT KALI
MIDA GHALI SHELI WAKATI HATUNA KITU
SAFARI NI NDEFU YOH
KAMA MAJESHI NA MITUTU
WAZUNGU NA MAKAPU
WAZIMA NA WAFU Ee MUNGU WALAZE WOTE AMINA
WALIOTUACHA KATIKA SAFARI TUTAONANA TENA
NAJUA IKO SIKU TUTAONANA TENA
KWANZA U.N.I.T KING KIKI VIPI MBONA HATUFIKI?

Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake si utani sehemu anayosema
'Nataka kupiga bunda duniani' Ndo inawafanya watu wengi wamuone kama alitabiri kifo chake kwenye verse hii
Kwa kifupi nilikuwa na mzimia kichizi huyu jamaa haswa ule wimbo aloshirikishwa na Lady jay dee wa MPENZI WANGU amechana vizuri kinoma

#16 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 17 August 2002 - 05:32 PM

Hiyo beef ya GWM na SOS B si kweli kwani D Cheif alikua ni mshkaji wangu wakaribu tokea JKT Sec. school na kulikua hakuna issue kama hiyo hata kidogo.
KU umewasahau waliotemwa Fresh G na Eazy B. Alafu sijui kulikua na KU foundation wakina Gadi Groov, Buggzy, Mdogo wake D rob na wengine.
Kulikua na jamaa moja siku mzimikia lakini nae alikua kwenye anga za hiphop ya bongo aliku anaitwa Mack Muga au "Muga Muga Wao". Jamaa hadi na video alitoa na nyimboi yake "maisha magumu" na "Mtanzania".
WWA nao walijitahidi kiasi chao.

#17 Guest_deezasta_*

  • Guests

Posted 18 August 2002 - 12:30 PM

Huyo Mack Muga nakumbuka aliwahi kutoa album kama sijakosea, huyo hata mimi sikuwa namzimia, alikuwa hana rhymes kabisa, na sidhani kama hata alikuwa anajua kwamba RAP ni Rhymes And Poetry ni kama mtu yoyote yule apewe mike halafu aanze kuropoka......

Bongonian vipi mwanangu mbona kimya? sijakuona hapa kwenye kumbukumbu..............

$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$

Who feelz it, knowz IT!

#18 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 20 August 2002 - 08:46 AM

'Sitaki rushwa, ukinipa naitupa', kitu kama hicho, hii track ilikuwa nzuri ila nakumbuka kwenye Beach party flani walipanda vichaa washakula bange zao juu ya 'long-track vehicle' wakaja na nyimbo inaitwa 'Nataka rushwa ukinipa naipokea', hawakuwa na rhyme kali lakini walishangiliwa sana kwa reply yao, michezo ya kujibizana naona imerudi tena kwenye uwanja wa rap kwa sasa, Nilisikia jamaa mmoja wa Niggaz2Publik aliswekwa ndani kwa kubaka katoto wakati huohuo kwenye nyimbo yao 'Vijana kwa Makini' walikanya tabia ya ubakaji....anyway hivyo ni vijistori 2 vya mtaani(vituko uswahilini) sina uhakika navyo sana.Fresh-G aling'ara sana na tongue-twisting zake na kama angeendelea vizuri angei-change rap ya bongo toka ule wakati wake sema madawa mengi wabongo bwana, nilikutana naye Rose-Garden 1day akawa anatupa mistari akadai album inakuja sasa sijui ni kweli au ni nguvu ya Monde,donno.

alcapaino escapirado
'always wear ashupapi aspinyo'

#19 sosa

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 168 posts
  • LocationTanzania, manzese kwa mfuga mbwa

Posted 20 August 2002 - 10:11 AM

Ndio ni kweli jamaa alikua na mtindo wa kulawiti watoto wadogo tena aliyefumaniwa nae ni kivlana, jamaa ana nyea debe tu sasa hivi.
Usinyambie hiyo nyimbo ya fresh G ni ile inayokwenda hivi:
FUNGUA CHAMPAIGNE,
NA HII NDIO KAMPENI,
USILETE SHINGIO FEN,

hiyo ndio hook ya nyimbo yake, sasa sijui ndio hiyo aliyokuimbia.

#20 alcapaino

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 76 posts
  • LocationRevolving around a Quantized nuclei

Posted 20 August 2002 - 10:30 AM

Nilikuwa 'bwii' kiaina na mcees walikuwa wengi wanatoa mistari hivyo sikumbuki rhyme yote lakini hilo neno 'champane' lina twist memory yangu kiaina yawezekana ndio hiyo, ila alikuwa ana-rhyme nyinginyingi za kutosha he can make a project but awe makini maana jamii sasa ivi imekuwa Bishi kama unaimba utumbo sana, huyo mtoto aliyebakwa nampa pole na jamaa wa N2P pia kwa kukaa sero, think he's gonna come correct kwenye rap-game atapo-be out
alcapaino escapirado
MuchyMuchy Karapinyo

2 user(s) are reading this topic

0 members, 2 guests, 0 anonymous users