cLICK hAPA...'uONE bEEF yA aLCAPAINO'
#1
Posted 28 April 2003 - 10:09 AM
#2
Posted 28 April 2003 - 10:24 AM
maskani yangu Kimara, ila hapa ndio Hom
tazama zangu lyrics, ingawa leo hujanikuta kwenye form
sina papara, bado nipo underground kama earth-worm
Je, upo tayari kupokea hii 'Vocal Bomb'?
ina weight 700Mb exactly kama CD-Rom
itakufata popote, Arusha, Mtwara hata kama upo Dom
wengi wenu mamcee, ila shairi zenu uniform!
.....aaaaH hii freestlye inatosha kwa leo....
alcapaino..'the Most Illest One'
#3 Guest_mr blow_*
Posted 30 April 2003 - 04:46 PM
#4 Guest_bahati aka Mad_*
Posted 01 May 2003 - 10:16 AM
au majingambo pembeni yake?
tuko gado kama tanzanite thamani yake,
naona kimya, nahisi umerudi kwenye yekeyeke,
kama unabisha tia timu uhenyeke,
ni balaaa sio sekeseke,
lazima uliwe zako kete teke,
ni mshikimshike, lazima nikuteke.
.............aminia
#5 Guest_HISABATI_*
Posted 01 May 2003 - 11:17 AM
ni vita vya key board ya computer nafasi hatuna kwa kalamu na wino/
mwanajeshi achagui msitu yeyote aje na iwe jino kwa jino/
kwa silabi ama nomino/kwa maelezo zaidi mulize hekima na tino/
inatosha kwa leo nakwenda kwenye mawindo/
#6 Guest_mr blow_*
Posted 01 May 2003 - 02:15 PM
ni kama mtoto mchanga//
kufanya asichokijua//
bahata rhymes zako ni kama bahati na sibu//
kali kuliko jack-pot//(lol)
uwezi kumiliki pen kama una mkono//
mawazo yangu yananiambia demu kakutungia//
hahahahahahahahahha......//
hisabati ulizani nimekusahau//
"kwanza" rhymes zako haziendi na jina//
je itakuaje ukiitwa mc shorrri//
kama we ni mwanajeshi//
mbona umeua moja//
labda we ni self guard//
pale nbc................
hahahahahahahahhahah
#7
Posted 02 May 2003 - 09:27 AM
cheki rhyme zangu, kila kona zinavyovuma
Mamceez wanadata, wanaelekeza kwangu shutuma
Lyrics zangu matata,ingekuwa uchoraji mi ni John Kaduma
nimebaki mwenyewe mtu kati
mistari ipo makini inastahili ya-juu Hati
na pia freestyle zangu sizitungi kwa bahati
sijui ingekuwa vipi kama mngeilipia Vat?
Wasanii wenye chuki bado wananiwekea gundu
wanalonga mtaani 'eti wananitoa manundu'
kuna siku mpaka walitaka kunichanja na Mundu
wanashindwa kutambua 'alcapaino ni msanii mtundu!'
...........................2B Continued
alcapaino.Mg
probably 'the Most Illest Rhymist' in Bongo
#8
Posted 02 May 2003 - 09:55 AM
Jinsi ulivyo mwoga, nashindwa kupata picha
Beef haijakamilika, mistari mipya kila kukicha
nataka nikupe somo, sababu mimi ni Ticha
nawatafuta wale wote, waliofanikiwa kukutisha
wakafanya uogope, kwenye hii Web kuwakilisha
kitendo unachofanya kila mtu kinamsikitisha
inaniuma sana, kwa kweli siwezi 'ficha
Nakutahadhali Mr.Blow, usiulize alipo Sosa
nimepata mpya tetesi, watu wameshamtolea posa
tokea awe Mwana-mwali, Masela ametutosa
Mshkaji wetu haonekani, kuchumbiwa imekuwa kosa?
.........................2B Continued
alcapaino.Mg
a.k.a 'A.K.A'
#9 Guest_mr blow_*
Posted 02 May 2003 - 04:42 PM
alcapaino muda wakufa sasa//
nazani huwelewi jinsi ya kuva vest//
sasa ni mimi tu kukumaliza//
mstari yangu sii tu "ill"//
bali pia ni weapon za kemikali//
wewe huta sema huko fiti//
kwangu mimi nikama mwana funzi//
ndio kwanza hunaanza shule//
sema mwengi lakini chunga husije kusogea//
kwasababu hutakuwa hunaongea sana//
kadli nitakavyo kuchapa nondo//
hata huelekei kama ni mc wa leo//
nazani rhymes zako kila kona//
zina pingwa..............................
hahahahahaha
dont make sense you sayin the illest bongo rymist
its more like none existing lines
#10 Guest_Bunduki_*
Posted 03 May 2003 - 05:56 AM
#11 Guest_mr blow_*
Posted 03 May 2003 - 04:26 PM
#12 Guest_(-_-)_*
Posted 03 May 2003 - 05:02 PM
NAONA MC WENGI NA MAJINA YA SIO YAKUBATIZWA//
KILA MOJA HANA JARIBU KUWA MC "SHUJA"//
LAKINI WENGI WAO NI KAMA "WAKIMBIZI"//
UKICHEKI MWENDO WALIO VAMIA NI KAMA "NYUGU"//
MIMI SIO REPORTA BALI NINA WAKILISHA "HIP HOP"//
PIA SIONEI MOJA BALI NINA FUNIKA BOARD ZIMA//
KAMA WE NI MC PUNGUZA MANENO NA ONESHA UWEZO//
KWA JINA TINO NINA MAANA KATI YENU NA MIMI//
WE UTASEMA UKO FITI LAKINI MIMI BADO NA KUJA KAMA "UMEME"//
NITATEKA WENGI NA KUKUSANYA KAMA LUNDO LA "TAKATAKA"//
NA KISHA KUTUPA KWENYE BIN LA UNET//
NIKIBAKIZA UBONGO ILL KUSOMA WEAKNESS YAKO............
(HISABATI YOU GOTTA LOVE ME ON THIS ONE NIGG) TINOMATIC :arrow:
#13 Guest__*
Posted 05 May 2003 - 07:56 AM
Huyu Bunduki ni jamaa, au ndo wale wala kozi,
hakuna mapenzi labda uje na nyeti zako(bunduki) ziko wazi,
Bunduki bila risasi, ni shwari utaishia kutoa ushuzi,
ni mwendo mdundo hatutaki makuzi,
niko kamili gado natoa berenge wapembuzi,
uyakinifu wao finyu kama rhyme za mpiga miluzi,
sikuachi alcapaino japo utaniletea ubaguzi,
Hakuna somo la leo hisabati mi nsha hitimu,
utantaka napo kupa hiki kitim tim,
nagonga gonga zote mpaka zile za kwantam,
sio masihara naujua wake utamu,
ustaarabu wangu wa maneno unakupa hukumu mgullu,
usiangalie saa bado wakati wa mimi kushika sululu,
kubali wazi utade wa hi mistari ni zaidi ya lulu,
ukikataa kweli wee Mmbulu,Na utatumia yako migulu/
kunikimbia maana tuko kwenye msululu
#14 Guest_Mad_*
Posted 05 May 2003 - 07:57 AM
Huyu Bunduki ni jamaa, au ndo wale wala kozi,
hakuna mapenzi labda uje na nyeti zako(bunduki) ziko wazi,
Bunduki bila risasi, ni shwari utaishia kutoa ushuzi,
ni mwendo mdundo hatutaki makuzi,
niko kamili gado natoa berenge wapembuzi,
uyakinifu wao finyu kama rhyme za mpiga miluzi,
sikuachi alcapaino japo utaniletea ubaguzi,
Hakuna somo la leo hisabati mi nsha hitimu,
utantaka napo kupa hiki kitim tim,
nagonga gonga zote mpaka zile za kwantam,
sio masihara naujua wake utamu,
ustaarabu wangu wa maneno unakupa hukumu mgullu,
usiangalie saa bado wakati wa mimi kushika sululu,
kubali wazi utade wa hi mistari ni zaidi ya lulu,
ukikataa kweli wee Mmbulu,Na utatumia yako migulu/
kunikimbia maana tuko kwenye msululu
........bado nafuka moshi.......
#15 Guest_Mad_*
Posted 05 May 2003 - 08:18 AM
Karibu sana lakini mwisho wake utablow,najua,
Rhyme zako no doubt zinaugua nyongea,
Nimezicheki kikafiri kwakuwa mi ni mwana sanaa,
Sijasomea na wala sisomei hii kazi,
Usije ishia kusema ooh! mad ni ova saizi,
uwezo wangu haufikiwi hata uje na nyambizi,
majini sikimbii na nna hasira nawe kama mkizi,
nakuja kimya kimya niko nyuma yako wee ni mwizi,
nigizani hunioni nimepakaa uso mzima masizi,
siko bize kwa hiyo huu moto huzimiki saa hizi,
umejifanya mjuzi ,mi nakujua wee bado la Aziz,
kunikataa huwezi, na ntakukuja kwenu mwisho wa mwezi,
ntatoa posa kwa wazazi, nikakufaidi kwa wanyamwezi,
sina hofu na wewe najua 'utakizi' matumizi
.....haha haaa!!.....inapendeza
#16 Guest_HISABATI a.k.a AL'GEBRAH_*
Posted 05 May 2003 - 08:30 AM
banza stone ama chuki/binafsi za ally choki/
risasi zako sishituki/visasi vyako kiutawala siianguki/
machimbo niliko sifichuki/fata mzinga uwaone nyuki/
wewe risasi inahitaji shule sana..kuelewa mashairi nauuhandishi...
sina muda sana hapa cafee see ya! but we battle for good! anyway
((LEAVE UR KNIVES AT HOME AND BRING UR SKILLZ TO THE BATTLE))
#17
Posted 05 May 2003 - 03:45 PM
kisha nachukua nafasi, wazushi niwatoe kamasi
tazama navyoangamiza, kwa hasira na hii kasi
mnataka beef na mimi, mkononi mmeshika patasi!!??
kaeni mbali Bros', msije mkanipa kesi
hamwezi vita na mimi, mtabaki mnapiga resi
mistari yangu ina-resemble kabisa na sumu ya gesi
bado nawashangaa mnapo-mess na hizi versi
watoto wadogo mnajifanya mna ki-besi?
kwangu ninyi wachumba tu, vueni kwanza hizo 'jassy'
hii ni Rap jamani, hatupo kwenye kozi ya u-nesi
inahitaji akili nyingi kama mchezo wa chesi
...................................2B Continued!
alcapaino.Mg
'the Most Illest Mothafaka'
aithee kumbe Hisabati ni Adilli, nimejua leo. 'Much Props Brotha'.
#18 Guest_HISABATI_*
Posted 06 May 2003 - 06:31 AM
mistari yangu haiwezi kufika tamati/
sio mpaka ufike top ten ndio upande chati/eeh bwana alkapino naona umei tawala hii african hip hop kwaani battle yako si ya kisenge/
#19
Posted 09 May 2003 - 03:37 PM
basi wacha niendelee kuupeperusha Mwenge
alcapaino na Adili, waliobaki wote Kenge
wanasota kutunga rhymes, freestyle tumezikatia denge
wakitukuta maskani, wanasema ni la wahuni genge
au imekuwa kosa sisi Masela kuvuta bange
msifananishe mtindo wa Rap na miziki ya Wenge
au Maskani Kimara na Arusha pale Kijenge
Cafe inafungwa but........2B Continued
AlcaPAINO.mG
'the Most Illest Metaphorian'
#20 Guest_Mad_*
Posted 10 May 2003 - 10:57 AM
basi lazima ulihisi ni ya kisenge,
haumesi na mR blow, au jamaa wa singe(bunduki);
ila ni wakafiri wenye michomo mikali kama nnge,
kama ni movie basi hii treila subirini kitatange,
naona mnakuja mande kama wakimbiza mwenge,
na hapa ndo siondoki na ndo kwaanza nasimika zengwe;
ni kazezee babaa, uliza babu kazenzele,
hata wewe alka utajifanya humjui akinyele?,
mpaka mtakapo kuja, ngoja nikapige misele,
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












