Who's the best between Biggie&Pac
#1
Posted 23 June 2005 - 02:47 PM
#2
Posted 25 June 2005 - 07:23 PM
#3
Posted 27 June 2005 - 01:17 PM
#4
Posted 13 August 2005 - 12:10 PM
Rest In Peace Brothaz
#5
Posted 13 August 2005 - 12:28 PM
Ila pia kwa mtazamo wangu ni vema kwenye page hii hii tuka-compare mceez kama Nas-matic na Jigga na wengineo katika game, hata wa hapa bongo kama wana-deserve comparison.
Nikija kwenye point nilikuwa sim-feel Pac ( Sorry to his Fans), baadhi ya reason ni sababu ya kuji-show-off kwa sana, I needed music. Alikuwa ni mtu wa kutaka kuonekana ana vurugu sana ( inawezekana ni kweli alikuwa ni mtu wa vurugu maana simjui KIHIIIVYO! ama ni biashara tu). Inshort presentation yake kama yeye ndo 'EVERY Black Man' ilikuwa hainipi attraction KABISA.
Mambo ya kutukana polisi hadharani ili Media ikutangaze then upandishe Sales ktk mziki mi niliona ni stail za kizamani. Kama ni 'FUCK POLICE' walifanya EFIL-4-ZAGGIN (NWA) enzi hizo. Wangapi tulikua tunaskia Mceez wapo Jela na mpaka mjue kinacho ni mpaka The Source, BlackBeat etc ziwape habari kamili, lakini visa vikubwa ni crack selling ama gunnin' na wao wanachukulia ni maisha ya kila siku. Mfano ni C-N-N (Capone N Noreaga) walikutana jela na ndio kuja kuanzisha crew walipotoka kabla Capone hajarudi tena Jela, sidhani mtu kama huyu kesho ana haja ya kusimama mbele ya Mass atukane polisi ndo umuone Gangsta , historia yake inatosha kukueleza alivyo.
Anyway hiyo ni ktk maisha lakini ilikua ni sababu ya mimi kutokuwa na attraction ktk mziki wake pia na hivyo kutomzimia (this reason inacontribute sana kuwa biased kwenye comments).
Biggie alikua mtu wangu, labda sababu alikoibukia ndo nilikua napenda staili hizo, Biggie alikua cool na game yake ilikua tait, pia alitoka Ghetto.
But all in all, After death nimekuja kujua kitu kimoja kuhusu Pac, he was also an emcee, coz then i had time to listen to his art, especially lyrics.
So when it comes to WHO'S THE BEST? Hapo ni lazima kutenganisha kwamba tuna-compare kwenye kitu gani.
Lyrics? Life style? Sales? Gangster/Commercial music? etc.
Ila nachojua impact ya Biggie alivyokuja kwa mara ya kwanza ilitisha sana (ingawaje pia iliwekwa kibiashara).
Lemme listen to Heads (B Carefully to comment if you're East/West based)
alcapaino.MG
Rest In Peace Brothaz
#6
Posted 16 August 2005 - 01:14 PM
Pili kuhusu idea yako sio mbaya kama pia katika mada hii tutazungumzia other Mc's like Jay Z na Nas na wengineo na hata hapa bongo wanao deserve lakini lengo langu kubwa kwa hawa Mc's ni kwamba walileta mazungumzo sana katika jamii kabla na baada ya vifo vyao,so nilikuwa nataka different view na opinions za watu tofauti kuhusiana na hawa Mc's ndani na nje ya Tanzania wana wa jugde vipi au sio!!!! halafu kitu kingine mi nilikuwa napendelea tuwa judge hawa Mc's musical wise and nothin else sio sales,money etc.Kwa kifupi wameacha historia kubwa sana katika huu muziki wa Hip Hop ingawa hawakuanza zamani sana ukilinganisha na ma founder kama Kool Herc,Afrika Bambaataa&Zulu Natio,Grandmaster Flash,Grandwizard Theodore jus to mention few kwani ni wengi sana ingawa hawa watu hawakufahamika sana kwa watu labda ni kwa sababu enzi hizo Hip Hop was in its Real Essence hakuna cha beef wala nini ilikuwa rhymes tu ili kupata respect mtaani.
Kuna kitabu kimoja kilitungwa na rapper wa zamani kidogo ila sio sana Kool Moe Dee kwa bahati mbaya nimekisahau jina kilikuwa kinaongelea Mc's lakini ilipofika kwa 2PAC mzee Kool Moe Dee akasema to him 2PAC wa jus a musician and not ana Mc kitu ambacho kilikuwa moyoni mwangui so when i saw that nikasema duh!!! two minds work together hii ili ni convince kwa sana mazee!!! na kwenye real Hip Hop siwezi nikamsimamisha kama 2PAC ni Mc i don't know why lakini maybe i don't feel him kabisa,sema kitu kimoja pac bwana anapendwana watu hata machinga ukiwauliza we unampenda nani kati ya 2PAC&Biggie atakwambia 2PAC maybe kwa sababu ya maugomvi yake na nini halafu and his big mouth kwa sana,lakini they don't judge about music.
Mwaka 94 Biggie came wit his debut album "Ready To Die" album mzee ilikuwa classic,humo ndani kuyna production za watu kama Dj Premier,Easy Mo Bee,Chunky Thompson,Diamond etc album ian jumla ya nyimbo kama 17 hivi,kuna nyimbo kama "everyday struggle" ambayo inamgusa mtu yoyote amabaye bado ana fight na life ni nyimbo inayotua matuamini sana kwa evry hustler in this world,kuna verse kama"i don't wanna live no more sometimes i heard death knockin' on front door" nyingine ambayo ilimuongezea Biggie umaarufu ni "Juicy" nafikiri hakuna nyimbo yake kali kama hii ambayo ilikuwa ikielezea ukweli kuhusu maisha yake,kuna verse kama "birthday was the worst days" then kuna verse nyingine kama "we use to eat sardines for dinner" halafu mwanzo anasikika akisema "he was hustlin' to feed his daughter" kwenye original version sikuipenda sana nyimbo ile sema lyrics wise ilikuwa noma tupu,sasa huyu mtu anayeitwa Dj Premier akaifanyia remix mzee mkono wa huyu jamaa ni noma kwani ana golden touches mi namuita the beat scientists,for more info me na mfeel sana Dj Premier a.k.a Chris Martin hili ndo jina lake halisi,jamaa smart in his brain kapiga buku Praire View University in Texas na alichukua Computer Science kwa hiyo ule utundu si mchezo ndugu yangu,ee bwana next time tutaendelea na uchambuzi wa track zake kwani nina exams wazee ngoja nikapige paper next time 1ne luv!!!!!
#7
Posted 16 August 2005 - 05:00 PM
Mazee kuna kitu 'Machine Gun Funk' huwa inadisturb stimuli zote za brain hasa jinsi anavyoanza ' So u wanna be Hardcore'. Inshort Biggie was balaa na ana staili flani kama analing'ata neno la mwisho wa mstari kisha la kwanza la mstari unaofata linapanda, kitu flani adimu sana (nadhani uzito wa ndimi yake unamsaidia kuleta lafudhi flani maridadi).
Kaka umemgusia Premier aisee yule jamaa ni kichwa cha HipHop hakuna tena mwanangu, huwa nam-feel sana huyu jamaa + Pete Rock. Ukiongelea HipHop productions unawagusia hawa watu. Nikikumbuka hata album ya Nas - Illmatic mipini ambapo Primo kaweka mkono mtu mzima inatisha.
Biggie alikuwa Hard kweli, presentation yake ilikuwa fo real. Unajua nini, wen the game imefikia miaka ya hapa juzi nikawa nam-feel sana the Canibus, becoz of his battle-lyrical stamina na kwenye trak '2nd round knock-out' kuna phrase anasema....
:arrow:
'...Cause the greatest rapper of all time died on March 9th
God bless his soul rest in peace Kid
It's because of him now at least I know What Beef is...'
Hiyo mistari hapo juu anamzungumzia Biggie kama 'the Greatest Rapper of all time'
Mceez wengi tu wanakubali mkito wa Biggie Smallz....
Ebana Man nipo Cafe wanafunga si unajua tena mwana.
alcapaino.MG
'the MuchiMuchi'
Rest In Peace Brothaz
#8
Posted 18 August 2005 - 10:22 AM
jogoo a.k.a kokoliko
#9
Posted 22 August 2005 - 04:51 PM
Ok turudi basi kwenye uchambuzi wa track za Biggie ingawa naona hapo juu kuna watu mshaziongelea lakini lemme contribute mine au sio!!!!! kuna pini moja inaitwa "The What" iliyomshirikisha John Blaze a.k.a The GhostRider namuongelea mtu mzima Method Man hii track imetulia balaa ilikuwa produced by Easy Mo Bee,hii track inaonyesha jinsi watu walivyobobea kwenye sanaa wanavyo switch verses kuna line "Fuck the world don't ask me for shit"halafu kuna line inasema "Verse two comin' with EO brew i got connected son!!! dah nimesahau kidogo jinsi alivyoendelea hapo mbele,halafu kulikuwa na track nyingine inaitwa "Warning" track hii anzungumzia washikaji zake ambao wanataka kumuharibia na wanajua wazi kwamba yeye kahangaika kiasi gani utasikia anasema "damn why do you wanna stick from my paper".Ukiachana na hiyo track kuna intro ya Ready To Die nayo ni intrio yenye science sana kama umeiskiliza mwanzo inaanza mwanamke mjamzito anajifungua makelele ya watu kama P.Diddy nafikiri hii ilikuwa home sio hospitali wala nini kwa sababu on the background kuna pini kama 4 hivi zinatandikwa kama Top Billin',nyimbo moja ya Snoop nimeisahau inaitwaje,halafu inafatia track ya pili "Thing Done Changed" kwamba mambo yamebadilika,huo ndo mwaka ambao Snoop akatoka na album yake ya kwanza kabisa,then before Biggie na mchizi wake hawajavamia SuperMarket na kufanya uharamia then wanadakwa na kusweka ndani,humo polisi anamuuliza Biggie maswali ya ajabu kama you will always come over here then Biggie anamwambia i got big plans basi pale pale track la Things Done Changed linaachiwa,ee bwana next time wazee naona net wanafunga tutaendelea kama kawa.............RIP in Pece Complex&Vivian!!!!!!!!!!!
#10
Posted 26 August 2005 - 04:39 PM
Second nikirudi kwenye mada inayosema nani mkali kati ya big na pac
from my self nasema bigie ni zaidi kutokana na lyrics zake naweza sema zina hisia na zimetulia.Pac alikuwa mzuri ila haoni ndani kwa bigie kwa upande wa lyrics.Unajua kuna link fulani ambayo unaweza ukatofautisha wasanii ndio lyrics but ni vipi ile lyrics yako ina uzito au imeingia indeep kiasi gani sio mashairi mepesi.Pac yeye amebase sana kwenye tittle za nyimbo zinamvuto lakini ukisikiliza nyimbo haivutii kama inavyovutia tittle ya nyimbo,Naweza nikatoa mfano wa msanii juma nature kuna wimbo kama SALIO LA VERSE wimbo ni mzuri ila nathani title hii angepewa solo thang au profesor jay au Zaharan sijui ingekuwaje.Hata hapa bongo leo hii tukimpambanisha nature na msanii yeyote ni wazi nature atashinda kutokana na kupendwa na watu kama ilivyo kwa pac ila kwa upande wa lyrics Bigie antisha
I learned a lot in this world
Got a profession that keeps me stressin
Facin criticism,
And you still keep me happy and healthy
Nyuma naona mbali
bora mbele kuelekea.
#11
Posted 30 August 2005 - 02:55 PM
Ebana ni kweli mtu mzima kifo cha ' Complex - X ' kimetokea kimazabe sana, last time I woz watching Channel Ten kuna jamaa alikuwa anafanya nae studio moja alikuwa anaongea huku analia kwa uchungu akasema kwamba Complex kalogwa. Not only haamini kwamba kafa lakini pia kile kifo ni cha kulogwa, according to Him anadai game ina mambo ya kichawi sana. Hapa nanukuu tu. All in all Complex woz cool, anayekwenda kwa Vina na mistari yake ina tungo tata mara zote, ladha kamili. R.I.P Brotha.
Kaka turudi kwa mtu mzima Biggie, Miko umenikumbusha hiyo track ya Aaron Hall na Redman 'Curiosity', pini lilikuwa tamu sana lile mwana, acha tu babake. Unajua Biggie wengi wanaweza wakawa wamemjua juzi...msikilize vema kwenye track 'Dolly My Baby - rmx' ya Super-Cat wapo na 'Puffy' hiyo ni zamani mtu mzima, hapo anaanza verse kwa slogun yake ya siku zote
'I luv it wen u call me Big Poppa'
The show stoppa, the rhyme droppa...'
...hiyo yote cha mtoto kuna track inaitwa 'Who's the Man' ipo kwenye album ya Dr.Dre & Ed Lover (Back Up Off Me), humo yupo pia King Just na Todd One, Biggie anamalizia verse four ebana kaumiza balaa...mwishoni nakumbuka anadai....
...I'm the killa, No 1 Gets Illa
Who's the man? I see him every morning in the mirror.
UH!!!
alcapaino.MG
Rest In Peace Brothaz
#12
Posted 31 August 2005 - 01:30 PM
Ee bwana kweli Alcapaino umeanza kusikiliza long time Hip Hop,hizi video mi nimeziona kama ya Super Cat na Who's The Man,ila Who's The Man ilikuwa soundtrack ili consinst Ma Mc kibao tena hii ilikuwa kabla hata Biggie hajaipua Ready To Die baba ake ilikuwa tight sana ile track mzee
Kuna kitu kimoja nimegundua kwenye hii forum kwamba watu wengi wanastukia what is Hip Hop all about,sorry for the Pac fans kwani its not kwamba nam diss NO!! kwani kuna track za Pac nazi feel kinoma kama "My Block","I Get Around", then kuna nyimbo moja hivi ipo kwenye "All Eyes On Me" sijui inaitwaje vile........yupo Redman,Method Man,Kurupt,Nigga Daz...........zipo track zake baadhi nazi feel sana especially alivyokuwa East Coast he was doin' some grimy real Hip Hop,kuna mchizi mmoja hapa katoa mfano wa Nature kushindanishwa na Mc mwingine ni obviously Nature ata win sio kwamba ni mkali sema jamaa ana kismati cha kupendwa nafikiri the same as Pac jamaa anapendwa sana hata chinga ambaye hana deal na mziki ukimuuliza atakwambia ana mfeel Pac,but anyway ni choice ya mtu tu!!!
Nikirudi kwenye uchambuzi wa Biggie small is The illest nillishia kwenye "Things Done Changed" sasa mambo yamebadilika kivipi mtu mzima,kwamba kipindi kile anazaliwa kwenye background kulikuwa na pini za long time zinatandikwa na zilikuwa zinatamba that time,then anafanya robbery na kuwekwa ndani kuserve his sentence kwa muda na anapotoka anakuta Snoopy ndo ka hold game yaani.............sasa hapo ndo inakuja maana halisi ya "Things Done Changed" kwamba mambo yamebadilika leo Snoopy ndo ana hold game baba ake,sijui alikuwa na nia gani kufanya Intro kama hiyo then kufuatia track ya "Things Done Changed"
:arrow: Next time wakuu au sio!!!!!!
1ne!!!!!!!!!!!!!
#13
Posted 31 August 2005 - 04:25 PM
Miko inaelekea hii trak ilikugusa sana....'Things Done Changed'....Nakumbuka kwenye Intro wakati katoto kanazaliwa kuna mipini ilikuwa inapigwa ya zamani track ya Curtis inaitwa 'Super fly' pia track ya Sugerhill Gang's 'Rappers delight - the boogie to the Boogedy Beat'....Baadae jamaa wanaanza kufanya robbery.
Kuna the Source flani front page lilikuwa na picha ya Biggie kakaa kwenye kiti cha utukufu huku kashika fimbo ina gold-or-platinum coating, na phrase imem-quote Biggie ikisema 'I used to Love Her' ndani jamaa walifanya mahojiano mengi na Biggie lakini hiyo issue ilitoka wakati tayari kuna Beef kati ya Biggie na Pac, Biggie akawa anasema kwamba ana-feel mtu atapoweza kusema kwamba 'My Best Artist is Biggie', lakini anashangaa Magazine kama the Source inapoweza kumuelezea yeye kama Mcee bora wa HipHop wakati haoni hata verse yake moja imo kwenye 'HipHop Quotable' ya gazeti hilo.
Nadhani hiyo ishu ni wakati kaja na album ya Life After Death.
Ebana narudi baadae! Network inaleta matata hapa.
:arrow: alcapaino.MG
Rest In Peace Brothaz
#14
Posted 01 September 2005 - 12:03 PM
Mzee una dig down sana mtu mzima zile nyimbo zilikzokuwa zinatandikwqa background nilikuwa nazisahau sana ila nilikuwa na original Cd walikuwa wameandika majina ya wale watu wazima,anh! ila kuna mapimbi flani waliniumiza baba ake sasa hivi ni copy tu mwana, mule ndani majina lazima yawepo kwa sababu ya Royalthies......si unajua tena wenetu Music ni biashara kubwa sana sio sisi tunachukua beat ya mtu then kunakuwa hamna malipo wala ku show anykind of luv kwa mwenye nayo.... we need to learn brothas about the Business of music au sio!!!!!
Halafu kwenye XXL Magazine ya October 2005 yupo Suge"Marion"Knight(sio lengo langu kumzungizia huyu bwana lakini fatilia),mwandishi wa XXL alikuwa anafanya naye interview kuhusu kuanzishwa kwa Deathrow mpaka kufa kwake na kutaka raise up tena teh khusu Eminem,mara kifo cha Biggie ila hii interview inachekesha sana kwani baadaye mwandishi kama alinyang'nywa tape recorder mzee enh(tuyaache haya)....... na mambo mengine kibao yamezungumziwa yaani,sasa kuna sehemu mwenyewe Suge"Marion"Knight a.k.a The Most Feared Man In Hip Hop anakwambia "Can’t never say Biggie wasn’t tight on the mic. He was always rappin’ about some grimy hood-type shit, type of stuff we about".(hizi words ni za kwake mwenyewe Suge sio mimi) ngoja niachie hapo ila ilikuwa zinga la interview ina mambo kibao lakini!!! lengo nilikuwa nataka kuonyesha hata Suge mwenyewe na beef zao zote lakini alikuwa ana mfeel Biggie you know!!!!
Ee bwana Alcapaino hiyo magazine ya TheSource unayo? kama unayo mwana itabidi niipate nafikiri ndo ilikuwa cover ya Biggie ya kwanza kwenye TheSource ingawa kweli mpaka leo hii nafikiri sidhani kama kuna Hip Hop Quotable ambayo Biggie yupo mi ninayo moja lakini Biggie hayupo wapo ma Mc wengine tu kama Jeru The Damaja,Pete Rock,Craig Mack,Redman,Raekwon etc ni ka kitabu kadogo dogo tu labda page kama 35 hivi kama sikuosei.
Next time nitaizungumzia hii track ya "Unbelieavable" au sio wazee!!!!!
Super Nintendo Sega Genesis!!!!!!!! I Used To Be Dead Broke i Couldn't Even Figure This" We Used To Eat Sardines For Dinner"
#15
Posted 06 September 2005 - 01:05 PM
Pamoja!!!!
#16
Posted 08 September 2005 - 04:11 PM
Mimi mwenyewe na binafsi nasema PAC ni mkali kuliko BIG, kwanza kabisa tukijaribu kudi nyuma kabisa tunaona kwamba PAC alikuwa mzoefu kwa kiwango kikubwa katika kuandika mashairi yenye akili na kuvutia jinsia zote pamoja na umri bila kupingwa,kwa mfano ukisikiliza nyimbo kama Dear Mama nafikiri hapo utaona kabisa ni jinsi gani huyu jamaa alivyokuwa na upendo wa ajabu ingawa alikuwa GANGSTER au ukisikiliza nyimbo kama KEEP YA HEAD UP nafikiri mzee Miko na washikaji wengine mtakubaliana nami kabisa kwamba huyu jamaa alikuwa anatisha kabisa kimashairi,lakini kwa mtu kama Big sidhani kama alikuwa na mashairi yaliyokuwa mazito kama Pac, bali kilichokuwa kinambeba sana BIG ni sauti yake basi lakini kimashairi alikuwa hana mashairi yenye ujumbe mzito kupita ya PAC. Mzee MIKO na mweheshimiwa ALCAPAINO wote twatambua hii fani nia na madhumuni yake yalikuwa ni kumpa nguvu mtu mweusi ili apate kusikika na hasiwe ni mtu wa kubaki nyuma au kuonewa na ngozi nyeupe,kwahiyo basi,kazi nyingine ni kuelemisha na kukosoa mambo mabaya yaliyokuwa yanaendelea katika jamii na sio kuonyesha majigambo ya mavazi,magari wala dhahabu unazomiliki kama tunavyoona sasa, ndio maana tunaona watu wazima kwenye fani kama JERU THE DAMAJA mashairi yao yamelenga sana kwenye maisha halisi zaidi na si midosho kama tuonavyo hiphop ya leo. Mr. MIKO hiphop ni mashairi zaidi yaani ujumbe kama mzee PAC alivyokuwa imara. Kuna site moja alikuwa anaojiwa MC REN,aliulizwa hivi kutokana hiphop ya sasa inavyokwenda PAC angefufuka ingekuwaje? yeye alichosema ni kwamba kwanza G-UNIT angewapeleka kuzimu maana wanafanya utumbo husioeleweka, na hata MC EIGHT alikazalika amesema hii si hiphop inayoimbwa karne hii sijui tuiiteje maana wazungu wamefanikiwa kuiuwa gangster rap na kuleta hii michezo watoto wanayocheza sasaivi na wasichana,ambayo ata yeye mwenyewe MC EIGHT alikataa kabisa kufanya hiyoo biashara ya kutengeza nyimbo za kupati CLUB NA WANAWAKE na akasema ni bora hasifanye kabisa music afanye kitu kingine kabisa maana hayo si maisha anayoishi yeye compton kwenye kitongoji chao. Point yangu hapa ni kwamba hiphop inaitaji mashairi mazuri yenye mafunzo nakueleza zaidi hisia zako za ndani ambazo zinaigusa sana jamii kwa kiasi kikubwa kitu ambacho PAC alifanikiwa zaidi kuliko BIG. Wazee ndio maana mimi SEBBY nasema PAC ni zaidi kuliko BIG.
Shukrani wazee.
Quertzal a.k.a lyrical blower
#17
Posted 14 September 2005 - 08:44 PM
Kumcompare Tupac na Biggie, kwa kweli hakuna comparison! Tupac was a way much deeper than biggie would ever been! Mi nina uhakika kama tungepata chance ya kumu-uliza Biggie mweyewe angekubali hilo!!!-no doubt! the only reason why Biggie never hit Pac back its coz he nu the truth...!
sito-ongea mengi sema ningeomba kwa wenye uwezo wa kupata hii DVD-'The resurection' waangalie kwa makini halaf wa re-view mawazo yao juu ya hii ishu! plz mazee muitafute hii DVD- PAC hakua ni MC tu, yule msenge alikua ni Genius! mi namcompare na watu kama Mohamed Ally(kama ushasikiliza akiwa anaongea),sio utani ka mohamed Ally angekua MC angekuwa my favourite-NO FUKIN DOUBT! alikua na skills mdomoni ka mikononi.Sito-ongea mengi mazee, jus look for dat DVD!
1luv
#18
Posted 18 September 2005 - 08:38 AM
#19
Posted 20 September 2005 - 11:20 AM
Kitu kingine ambacho nilikuwa siki feel kuhusu PAC ni the type of Producers he use to work wit em,are not basically who dig Hip Hop to the fullest nafikiri naeleweka hapa,huwezi kum compare mtu kama Dj Premier na Dj Quick nafikiri ni vitu viwili tofauti potelea mbali wanakotokea sehemu tofauti but at the end of day its all Hip Hop cuz its Universal,the only producer ambaye yupo tight na alifanya kazi na PAC ni Easy Mo Bee tu wengine wote ni jus average producers,labda kitu kingine ni PAC kwenda ku deal na West Coast wakati yeye alikuwa haishi maisha ya West Coast kwani wale ni watu wa starehe balaaa! how can they spit somethin' serious?????? ingawa najua PAC alienda West Side kwa matatizo maana ake The Most Feared Man In Hip Hop...........Marion"Suge" Knight aliwekas bail ya 1.4$ million ili aweze kuomtoa jela hope mnafahamu hiyo!!!!
Another issue nyimbo nyingi za PAC zilikuwa radio playable joints huwezi linganisha kabisa na uzito wa beat ambazo Biggie alikuwa nazo,ingawa West Coast wana vi beat vyao ambavyo vimejaa vinanda kwa sana halafu nyepesi...............ndo style yao lakini siwezi sema sana hata hivyo,ingawa kuna ma artists wa West Coast lakini mbona they rock hard utafikiri hawatokei West kama CALI AGENTS(Planet Asia&Rasco),PHARCYDE,DILATED PEPOLE,MADLIB,QUASIMOTO BLAKCALICIOUS etc,hawa jamaa wana different style kabisa which is very good for me!!!!
Kwa leo ngoja niishie hapa !!!!! nawasubiri watu wazima mtoe opinion zenu au sio!! kuhusu "Who's The Best Between Biggie&Pac
Pamoja!!!!!!!!!
#20
Posted 21 September 2005 - 02:20 PM
1. Pac alisoma kiasi fulani, i min seriously sio kupitia-pitia tu shule kama other dropouts(no dis-respect!).Alisoma kwenye shule ya good standard(udogoni) uki-compare na wengi weusi ambao walisoma shule ambazo kwa wakati ule hazikua chochote kutokana hali halisi(ubaguzi!).Kwenye moja ya interview yake anasema, shule aliyokua anasoma na mazingira aliyokua anaishi yalikua tottaly opposite,anasema alikua akienda nyumbani anashindwa kuongea na rafiki zake kuhusu William shakespear na vitabu vingi ambavyo vilimvutia yeye shuleni-simply sababu hawakuweza kumuelewa! angalia huyu msenge alivyokua deep kabla hata hajaanza mambo ya hiphop.
2. Anasema 'all his roots to the struggle are deep' Mama yake alikua panther au vip? anasema mamake kamfundisha vitu 3 maishani search for knowledge,Respect na cha tatu sikumbuki sasa mnaona kwamba huyu mtu kina kilianzia nyumbani!
3. 2pac ameishi miji mingi tofauti katika masiha yake kuliko MC yeyote ambae mi nishawi msikia, ona jinsi huyu alivyokua exposed to mazingira tofauti..kama we unaelewa unajua wot that mins! anasema kitu ambacho wato weusi wana-share katika sehemu hizo zote ni 'umasikini'
4. 2pac hakua MC tu wamistari, msenge alikua ni revolutionary!(a modern panther) kwenye hiyo DVD kuna clip moja wameonyesha alikua anatoa speech kwenye 'Malcom X conference' kitu kama hicho, anasema inakuaje sasa hivi yeye anataka kufuta footsteps za panthers watu wanamuambia eti a-chill? anasema panthers wote wakati ule walifungwa hivyo ule upeo haukua passed down to the next generation anamshukuru mamake kwa sababu alikua anaspaend time na yeye na dadake kuwaelezea wots up unlike wale frontliners ambao wote wali-end up in jail-knowledge lost!
5. Tupac kaanza hiphop kwenye 'poems' sio freestyle za mitaani kama Biggie!baaade ndio akaanza kuzifanya nyimbo, ila anasema ule muda wote ambao alikua anaandika poems alikua ana-Rap! anasema alianza hiphop the day he wrote his first poem at junior high!-noma!
6.Tafuteni pia kitabu chake cha mashairi ukiacha lyrics ' a rose that grew from a concreate' ukichambua utagundua ni anajiongelea mwenyewe!
NB: Biggie anayajua haya yote kwa sababu alikua nae close wakati fulani ndio maana ninasema tukimuuliza biggie mwenyewe ka angekuepo kuhusu hii topic nadhani dah.....................
nway, RIP Copmlex,Pac, Biggie etc....
1luv
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users













