Jump to content


kiama kimefika kwa mamc wote wabovu


22 replies to this topic

#21 Knifebutcher

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 112 posts
  • LocationSouth Africa

Posted 13 May 2005 - 04:56 AM

Naona umepata backup ya ka-explo unadhani utasalimika ?
Kipofu kumwongoza kipofu ni kupotoka
Kwanza Chenji hilo jina noma eti sky walker
Wack emcee nakuapia, kamwe hutoponyoka
Unacheza na na gigbrain emcee lazima utanyooka
jaribu kuperuzi profile ya bucha ujue nilipotoka
unaropoka ropoka inaonekana hii dunia umeichoka
hujui nini maana ya hiphop unajifanya eti unafoka
unakuja tuu kama kaka poa na kuanza kushoboka
unanletea kishingo wakati nimeshikilia shoka
unakutana na mabomu baada ya viunzi kuviruka
nini unastuka, hii ndiyo taimu ya kuwehuka
nakufanya huishi bila ya uhakika na kukiona kifo chako kila dakika
hivi ni vita vya nyika ndani hiphop ya afrika
mkali wa wordplay, metaphorz kichwani nimejitwika
mistari yangu ya kitume popote ulipo inafika
sauti yangu inanguruma bila msaada wa spika
sikiza usia wa mzee Fid kuhusu kuchagua moja la kushika
sio unachanganya mambo utaleta patashika
tambaa na hardcore upate sifika na kuteka hisia za kila rika
au imba bongo flava kama shida yako ni albamu kuuzika
real emcii hapimwi kwa mara ngapi redioni husikika
bali ni uwezo wa mashairi na unabii uliotukuka
nina rymez zimefurika ndani ya mishipa mithili ya gharika
nikiziachia ni tsunami wala si elnino au masika
ninapochomoza africanhiphop vichwa feki vinahuzunika
machozi ya damu ndani ya mboni za maemcii yanatiririka
vina vyangu infection yake kamwe haiwezitibika
nilishamnyea kima mmoja aliyekuwa anafosi kuheshimika
nikiwepo ndani ya thread haonekani kutwa anaadimika


Bucha a.k.a Cypher Mathematician GigaBrain Emcee

#22 Jasiri

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 25 May 2005 - 05:10 PM

vina si tatizo nawala si ushairi
na hii ndo yako mbinu unahisi inakusitiri,
nimeng'amua hatauweke msisitizo kikafiri,
koleza wino hata herufi kubwa mbona shwari,
kukukabili ni yangu kazi nakiri niko tayari,

eti ukali wa line kama ndosi, kweli bro una mkosi,
ndosi nini ni kiswahili au kidosi?
hii kwenu intro lazimamfungue kesi
kuikabili hii kasi, nawapiga pasi ka' haisi
kituoni kimoja ka taksi' ni moto bati kwa hii nafsi
-----naendelea UPS inanialert umeme unatakatika soo!!

#23 AGNITO

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 36 posts
  • LocationUSA

Posted 28 July 2005 - 07:46 AM

I like what yall are doing here. Im from the USA. I need yall to chec out this new artist by the name of "NAIRA" http://www.sounclick.com/naira I want to try and get her over there for a concert
Proyfik Music Werks (ceo)





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users