Jump to content


kiama kimefika kwa mamc wote wabovu


22 replies to this topic

#1 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 07 April 2005 - 05:45 PM

kiama kimefika kwa mamc wote wabovu.
wasiojuwa kurap kazi kufanya upumbavu,
wakati umeshafika wakuvunjana mbavu
kwani gemu hii inahitaji ukakamavu,
lasivyo takupa ngumi kwenye shavu.
mc kichwa ngumu,mc bila ndumu,kama jada nakupa rhymes nifanye mada,chukua mtoto wa mama rymes hizi utoe track
miaka mitano ndani game na track tano redioni,bado hujatoka.
mshikaji acha wenye vipaji wakupe flava kama unataka,
nahitaji beat kali,nahitaji mdundo mzito nimwage zege mi kizito.
kisima cha mashairi kama unahitaji mc rijali mimi nipo
nikupe lyrics harafu utoke,kwenye jua kali uokoke.............

#2 Knifebutcher

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 112 posts
  • LocationSouth Africa

Posted 08 April 2005 - 02:32 PM

unaryme au ndio unatuonyesha uchovu
mithili ya mesia naleta wokovu
kama ni elimu ya cypher hapa ndio kitovu
sina simile nakutenda uovu
ndani ya medulla nakuachia makovu
kila punchline unamwaga povu

#3 quertzal

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 49 posts
  • Locationkimara maskani

Posted 11 April 2005 - 11:45 AM

kweli knifebutcher huyu mtoto amedamka kabla hakujakucha,hajui wazee tumetulia uku tumeficha makucha,
sasa kakwama, wazee ngoma ziizosimama, tutamvusha wima wima,hata kama bado hajapima, tena nimemsoma kumbe kwao Musomaaa,
anyway kijana husione noma,tupo ma informa, misaada kibao hata watu wa kukoroma,najua unapenda rhymes za kweli,zilizo simama kiakili na zenye kutunza maadili,tupilia mbali fikra zisizo ona mbali,zenye kufuraia utamu wa asali na kudharau nyuki wenye asira kali,mwana hili jabali yaitaji nguvu ya akili na sio ukubwa wa mwili,vichwa vimetulia midosho hapa daima wanaliaaa.......


keep it up, gud try man...

Lyrical blower!!
"Guys don pretend keep it real so dat kids can learn n grow from us"

Quertzal a.k.a lyrical blower

#4 Knifebutcher

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 112 posts
  • LocationSouth Africa

Posted 12 April 2005 - 09:21 AM

mjanja wa kijijini brazameni skywalker//
nilidhani nabatto kijogoo kumbe nambatto mbushi//
kaomba batto halafu kapotea kizushi//
dogo umehofia nitakufanya matusi//
muulize kenge mwenzio mkurdi mweusi//
kachomoka kwenye cypher hivi sasa kawa msusi//
huu ni uzani mzito katafute maecii wepesi//
utanipa mada kesi, bora ukastop kuja resi//
batto ikisha lazima iitwe ambulensi iliyojaa manesi//
Hii ni chimpanzee mazee usithubutu kuifesi //
nikichomoza shusha chako kibesi//
nakudundisha kwenye cypher kama kitenesi//
nakujaza hofu na wasiwasi//
unachutama kila dakika kuhofia zangu risasi //
natoa big up kwa kikosi, waheshimiwa nyie mikosi //
hizi rymes funga kazi full msosi,ajifanye mtu bosi //
kama hajapigwa nyundo ya utosi //

#5 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 17 April 2005 - 01:56 PM

si rahisi shujaa kunyamaza,lazima niendelee kuchakaza/
haijalishi uko bondeni au kimara/
au we ni knifebucha ama quertzal/
kipaji hakijichi popote nyie mabraza/

#6 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 17 April 2005 - 06:01 PM

yooooooo yoooooooooooooooo yoooooooooooo/
kijana umedandia treni kwa mbele/
Nilifikiri bado hujasikia kengele/
kumbe bado unapiga kelele/
Kwenye kundi la vifaru unapiga misele/
kutoka huku unakokuita bush/
nafunika huko mliko nitoe kabisa ubishi/
Musoma ndo maskani maisha safi kama kwa Bush/
sitishiki huko mliko kidume rijali kutoka kush/
dalili ya moto kijana ni panafuka moshi/
huniwezi kwa rhymes hata kwa kash/
Huu ndo mtambo wa kurekebisha nyodo za mabronzo/
Nyundo hii isikutishe kwani bado ni mwanzo/
Uliza ndugu zako jinsi ninavyozua mzozo/
Kila kona ya Bongo sky nimekuwa gumzo/
si kwa michongo ya kitoto,michongo ya kirume/
Kikosi chako hakisikiki mbele ya vifua vya wanaume/
moyoni najua unakubali katika rhymes mi ndo mfalme/
Bishoo utasema nini mbele ya msela uso wa meeee/
Lazima mwaka huu mstarini nikuondoe/
Niharibu heshima yako na kwenye gemu uboe/
Kifupi mshikaji huwezi,Labda tafuta mtetezi/
Nisije ghafilika nikuvunje zako tezi/
kutoma msm mpaka mbezi kwenye kipaza mi na blaze/
dharau sitaki kifupi mi simind ushe****
jaribu kuwa na heshima kama ni mtungi mi mc kenzie/

CHORUS;
Knife bucha na mwezako quertzal/
niko ready kuwachakaza/ 2


Verse ya pili ndo kiama,kwa nyinyi watoto mama/
Nasubiri mkorome ili nije nifanye unyama/

ANY WAY MNAJITAHIDI KEEP IT UP

#7 quertzal

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 49 posts
  • Locationkimara maskani

Posted 18 April 2005 - 02:36 PM

Ni Quertzal kwenye miamba nasonga// nyonyo zote na gonga// chakaza miti visiki na wote wanao nizonga//
vinabo nishawadhiti na wenye viji maneno kuchonga//
angalia status mjomba ndio uridhie kima cha hongo// quertzal kazoea konyagi mnataka kumnywesha gongo??// eboo uncle hii hiphop husijezania bolingo//naumiza kichwa kidosi boss mzee na make bingo//
sasa nimejenga mashua wafuasi navua//jeshi limetulia kombora mithili ya mvua//hakuna noma// nakuja wekeza musoma//jenga shule nyingi za underground skywalker na wenzie wapate soma//hiyo ni haki yenu ya msingi sipendi mbaki nyuma//na hold mic tano kila kona quertzal navuma//unataka wika mjini//wakati unahold v tatu jeshini//unacheza na ma field marshal nini//weee vumilia vumbi vijijini//kama ni uchizi quertzal nshakata fyuzi//ukita makuzi test zali mi a.k.a tarik Aziz//nina AK 47 hapa wabush lazima mbanane//sita kukawiza hata kama number yako ya cmu imeishia 48//unajiita skywalker// au ungo uliorithishwa na babu yako unakufanya kufoka//hapa watu tumechoka//tutakutafuna hata kama una ugonjwa wa sotoka//quertzal,knifebutcher juzi wametoka milembe//kijana tutakunyamazisha na hizo kelele za debe//;;;;;;

Mind blower//
Quertzal.
"Guys don pretend keep it real so dat kids can learn n grow from us"

Quertzal a.k.a lyrical blower

#8 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 18 April 2005 - 06:15 PM

mwanzo niliwaza kuwa mwaweza kuwa wendawazimu/
Kumbe kweli juzi tu mmetoka milembe/
sidhani kama tayari mmeshapona uchizi/
anyway nashangaa kuona game limevamiwa/
hâta na watu waliochanganyikiwa nao kipaza washike/
ndo maana unawaza kujenga shule/
Ili machizi wenzako wakuunge mkono/
Usijali kamanda mi nipo nikubadili/
najua unapenda kuwa mzima kiakili/
kisha kama unavyopenda ushuke mashairi/
Natamani nije dar ili bure nikufundishe kurhyme/
nakisha niende bondeni nimpe shule knifebucha/

#9 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 18 April 2005 - 06:31 PM

Heshima kama hakuna yabidi kuitwaa hata kwa nguvu/
Sioni hatari kupigwa mkwara na mc mlemavu/
Mc mwili mkavu ulingoni na mc shupavu/
Heavy weght kama tyson niko ready kukuvunja mbavu.....

I WILL BE BACK TOMMORROW MEEEEN MY SHOW IS ON THE WAY TO START BANGÎNG...........

#10 quertzal

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 49 posts
  • Locationkimara maskani

Posted 20 April 2005 - 01:23 PM

Watu wa mjini ndio wa kwanza kuliona jua//
nafikiri hili wewe bwana mdogo wa bush bado tambua//
na ni sisi tunawakilisha na kufanya nyinyi ki-mc mpate kukua//
sasa unatukana wakunga je hiyo mimba utajifungua??//
hichi kichwa kimejaa thawabu na hekima za ki-mababu//
uki-battle babu hapa aibuuu na maisha yako ki-mc yatakuwa ya taaaabu//
naona unajaribu traatiibu kukwea merikebu iliyojaa waarabu//
mikono yako laini utaishia chezea tuu zangu sharubu//nitakupa hifadhi na moja ya vazi lako binti skywalker itakuwa ijabu//
natumia nguzo na itikadi zenye misimamo//si fanyi tuu vijimambo watu kama nyinyi mpate msemo//natoa ujuzi ikibidi niletee demo//
nabadilika kutokana na mingi yangu ya maisha mifumo//najua huwezi kujifunza bila kuchafuka njoo hapa nitakuogesha kwa omo//mimi ni sebby a.ka. quertzal mind blower//mbona huna hema si ulikuja moto hapa umepoaa//nimekata yako kauli nimekuacha unakoa//
quertzal n knifebutcher ndio wazee saluti mpaka kwa machangu doa//

kama kawa//
Mind blower//
Quertzal//
"Guys don pretend keep it real so dat kids can learn n grow from us"

Quertzal a.k.a lyrical blower

#11 Mchapakazi

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 213 posts
  • LocationDeventer, Holland

Posted 21 April 2005 - 08:34 AM

Yule katoka shamba huyo katoka mjini/
Am from nowhere niko na zana zote majini/
hip hop sio dini/ nakupa tahadhali hilo weka akilini/
panapo Bucha na Quertzal uwezi nikosa mimi/*
sky game changa laini kama ndimi/
usiulize kwa nini/ wala usiseme maini/
ni mistari tu ndio nimekubaini/*
u need more lecturer kama modules sitini/
labda kidogo waweza kuwa makini/ ila usifungue pini/
kuwafunza wanafani wadogo kama wewe is ma daily routine/*
don ask nilianza lini/ ila naflow toka nikiwa ufini/
dogo uko chini/ lakini seems unapenda sana mpini/
haya vua bikini/niscore goal ishirini/*
she is million dollar baby & am million man rhymes kama ujabaini/
uliza wa mjini maqueen/ wanaopenda kuzini/
karibu uwajani sema nao kunywa nao ila usiunguze ini/
ukaanza ishi kwa wasiwasi kama muhaini/*
I screw few b**** wanaolipa kama k-leann/
color,height,figure ndio vitu navyothamini/
uliza kote hata mshikaji wangu Amini/
haya wapi watoka? musoma shamba au mjini?/*


Da LeAf MoVeMEnt

Ma thesis proposal is ready am back yoh!!!

I'll give this Punk 60 modules za hip hop atatembea kwa mguu toka musoma mpaka Dar kuomba msamaha kwa machizi wangu.
HIYO NI INTRO, Module one coming soon!!!

They keep us talking, but if we stop talking about them then they should worry!
Bitches are like tornadoes scream when they come,and take everything when they leave

#12 quertzal

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 49 posts
  • Locationkimara maskani

Posted 21 April 2005 - 10:20 AM

Bwana mdogo hii tsunami//unataka kuburuzwa chogo hii kambi ya army//
naona unatema fyongo huyu ni quertzal 120 hata kona za mto wami//
rudisha kikosi nyuma pindi pale upepo wangu unapo vuma//
huwa sina huruma/nachakaza kizazi chenu maendeleo narudisha nyuma//
unacheza na nyati wakati hauna shati//ni sawa kupiga kelele jukwani bila kipaza sauti//ukija mjini njoo smart lakini husi chomekee suti//jipulizie perfum husije unanuka hudi//umepita mtaa wa magaidi/utachokozwa ikibidi hata kwa maksudi//wewe ni kinyama cha mwitu halali ya mafisadi/
kama unapenda beef qurtzal hapa sheriff//kama unataka utiifu hiki kichwa cha chief//si pendi vita na wenye game dhaifu//uwa nazoa point bila kufika uwanja wa beef// nina jeshi zaidi ya siafu sijali wewe ni mwana ccm au cuf//inavutia mc wa musoma mtandao unapokuunganisha na sisi watu wa dunia//bado kitu kimoja rhymes zako hazija simama hilo staacha kukuambia//anyway keep hooked na mazoezi mengi yatakuinua//hii ndioo dunia quertzal 4life AMINIAAAAAAAAA!!!!!

Mind blower!!
Quertzal!!

Knifebutcher yupo kiwanja mara moja hata kwenye ndoto atakuzukia don worry keep cloz to ur short.
"Guys don pretend keep it real so dat kids can learn n grow from us"

Quertzal a.k.a lyrical blower

#13 Mchapakazi

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 213 posts
  • LocationDeventer, Holland

Posted 21 April 2005 - 12:52 PM

Natupa mashuti sharti upate/
kwa hizi lines lazima nikupate/
nikupe ladha ufikiri mkate/ mi nakula mate/ babake/ *
anga hizi walikimbia wengi nawe waja najua utake usitake/
kama mwanamke na siku zake/
ukichoka kuishi musoma njoo viwanja tukupakate/
nikuvalishe shanga ucheze ngoma ya kwenu na kiuno ukate/*
am more experienced in tha game muulize Pate/
kama unaweza ingia kati tulisakate/
ila nikipiga denda usining'ate/ denda mpaka tudate/*
muite ngate,sate,latte kama wanaweza utake/
niwape vina vya kweli watakate/
kwa ulevi wa mashairi kama mbwa wabwake/
huko mashortie wakiscream mambo mwake/*
you ain't ma type though nimechukia naanza....../


DA leaf movement
Bitches are like tornadoes scream when they come,and take everything when they leave

#14 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 22 April 2005 - 04:04 AM

Amini usiamini Sky nageuka 50cent wa bongo/
Walikuwa wawili na sasa mwingine kaja ana usongo/
Bila shaka uko tayari mtembea angani umpe mgongo/
Posa yako binti mchapakazi ipo,kama hujui nakupa mchongo/
Dada zako qurtezal na Busha wako tayari kupokea Bingo/
Anyway sura yako ndo matata utadhani unakunywa gongo/
Watoto wa jirani hawana amani kila ukipita mtaani unaacha skendo/
Battle langu mi na wewe haliishi tu african hippop.com/
Nataka nikushow kwenye game kwamba mi ni storm/
Mi ni jemedari nalipuka rhymes mithili ya bomu/
Uwepo wangu tishio hasa nikija Dar es salaam/
Mfuniko huko mliko pindi nitakaposhika kalamu/
Mchapakazi hapa husimami kimsingi nakuona mchumba/
We ndo mlaiiiiini huogopi kuongea pumba/
Unasema rhymes zangu changa au unataka uvishwe shanga/
Nakuona tu kifaranga apigae kelele mbele ya kipanga/
Au ndo nyie hata muziki muutafutie waganga/
Mchapakazi hautatoka ni bora ungeuza karanga/
Mamc wenye vipaji wabaki wazigawane faranga/
Jaribu last time ukarekodi Mropokaji/
Harafu track yako ichezwe bongo chipukizi/
Tatizo wabongo hamtaki kumsikiliza afande/
Wakati enzi za shule mliogopa umande/
Unataka uimbe muziki wakati dailly unakula kande/
Msanii pasua kichwa unataka na we upewe pande/
Toka ufukuzwe kwa P funk bado tu unachonga/
Kaimbe tu kwaya au bolingo na bendi ya mchinga/
Battle ya hip pop huiwezi labda mipasho ndo utatamba/
Utanambia nini Mchapakazi mshamba ndani ya jiji la makamba.

Tafadhari j4 nishikilie haraka kabla sijamvunja vunja huyu mrugaruga.

#15 Mchapakazi

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 213 posts
  • LocationDeventer, Holland

Posted 23 April 2005 - 09:55 AM

Sisemi nani bingwa, nani mkali wataamua wanaojua vina/
acha ubwege kila mstari unataja majina/
split vina/tafakari kwa kina/
alafu utabaini mashairi mimi nina/*
Fuck Jay D, I fuck gal name Tinna/
Najua utachonga maana umekulia uswailina/
alafu wajifanya mswailina/*
Big up Kapilima/na Yanga imara kama Mlima/
endeleza mapambano achana na wasenge wa takrima/
84 I was in da crib with Pac kule Peru Lima/
umerukia matawi ya hiphop ujui hata shina/
when I do ma steady flow hakuna kupima/
hakuna kulima/ na mimi kinyongo sina/*
I'II wash u clearly, upige magoti ground badala ya sky kama mchina/
ili jeshi kama Kikosi na Pina/ au sauti na auntie Ndina/
Asswhole if u wanna rili batlle lete watu wakutoa winner?/*


Cheza kwenye misingi ya uandishi wa mashairi ya hiphop sio unataja mchapakazi mchapakazi inabore I need to see skills, Punchlines za maana na in a cordial way, hip hop kazi usikurupuke Son. RIP
Bitches are like tornadoes scream when they come,and take everything when they leave

#16 Mchapakazi

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 213 posts
  • LocationDeventer, Holland

Posted 25 April 2005 - 05:43 AM

Nilijua tu utakimbilia mbali kama Lindi/
coz hauna hoja ya msingi/
kama beef za plastic au udongo za Nyandindi na Msindi/
hiyo ndio fact son nakupa kipindi/*
nakupa mashairi unasikia baridi kuliko ile ya Mufindi/
I leave ya tiredless hadi demu wako anasema udindi/*
that means mimi mshindi/pindi/
unapoenda kutafuta wasaidizi kwa wingi/
I don give damn hata uje na masilingi/*
nakuona mlevi fake tena wa kindi/
Am doing ma thang in a steady way/
sucker like u, I swear u can't play/
anyway/*
nakutreat kama kapombe wa dadey/
kwangu wewe ni kama manutd na game ya away/
nitakupa mashuti toka january mpaka may/
to make sure kimashairi uendelei/*
mtoto mzuri unashindana na machangu wa Osterbay/
najua huna pay/ najua huna AK/
mimi ni moto kuliko wale vijana wa pompey/
I got experience za both Bronx & Brooklyn a.k.a BK/*


I don't give a fuck what you sold, that shit is trash
Bang this, cause I gurantee that you bought it
Heavy airplay all day wit no chorus
Bitches are like tornadoes scream when they come,and take everything when they leave

#17 Knifebutcher

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 112 posts
  • LocationSouth Africa

Posted 29 April 2005 - 04:56 AM

mtengenezeeni huyu kenge jeneza
bucha mazee ndio nimekuja kummaliza
Mob ya maemcii ndio imeshaingia
tunakuminya hadi J4 anakuhurumia
Kama unanin'ginia bora ukajiachia
nakupa huu ushauri ili usije kunichukia
Nitakufanya kitu mbaya ushindwe kusimulia
kupanda ulingoni na bucha haiwezekani
hiyo ni sawa na matumla kuomba pambano na tyson
umeanzisha bifu bila kufuata itifaki
Waambie nduguzo batto ikisha waje kukusanya yako mabaki
hapa si mawe kinachorushwa ni fataki
uemcii sio kumwaga mistari utitiri
inahitaji upeo mpana wa mashairi
na vina vilivyoenda shule mpaka vikaghairi
kama unadhani mafanikio ni bingo na kunawiri
sasa nakueleza huo ni upofu wa tafsiri
hii fani inakwenda kijangiri
unaleta shombo kamwe hatuwezi kukusitiri
ndani ya cypher wewe ni batili
sina utani na makatuni nawachinja kikatili
unanchezea ,nina mori kama mangati
vina vyangu ni sime nitakugawa katikati
naivusha hii fani jangwani sinai
wewe kuwa msanii sikatai
ila kujiita emcii ndio nasema haifai
choko sio siri unaleta kinai
akili imedumaa kama papai
huwezi nifesi hata uje na wenzio lundo
nakufanya unuke uvundo
nakutwanga na punchlinez mithili ya nyundo
unamwaga haja kubwa ukisikia vyangu vishindo
kila unapolalamika ndio naongeza kipondo
unafleti kama kifaranga chenye mdondo
usifananishe hii game na msondo
bora utimue usijekufa bila mtindo

#18 XPLO

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 77 posts
  • LocationDEEP IN UR MEDULA OBLANGATA

Posted 04 May 2005 - 08:15 PM

ok, nani mkweli ili muongo tumpe kibano/
si batto machalii, nataka mc mwenye msimamo/
vina kwa vina sitaki ushoga au malumbano/
we butcha acha ukorofi na huo upuuzi acha kupost/
mi ndio ticha line zangu kali kama ndosi/
ki vina we ni mdosi hebu chukua poz/
njoo kwa malenga upatiwe kamili doz/
hakuna gozgoz, anza kunoa kimlomo mentali nichane hiyo ngoz/
yap ndo hivyo bwana kamanda larejea au vipi
msiogope

out!!

#19 skywalker

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 35 posts
  • LocationFrom the hood

Posted 05 May 2005 - 11:10 AM

Sikiliza kwa makini shujaa nashusha mpini/
Niko so fierce yanibidi kubwaga dini/
Kwa hawa mafirauni wanaodiss na mimi/
Niko fresh makini kwa batto heavy nanyinyi/
No retreat no surrender vita vyasonga mjini/
Ok tusonge kwafujo nite kali kama 50 na shyne/
Nataka yangu nishani nipeni yangu midani/
Napiga kabali kama jet nafanya unyama tena gizani/
Wachovu kama ninnyi Sky mnieleze nini/
Naziba gubi midomo,hamuwezi fanya migomo/
Viwete wa game nanyi mwataka promo/
Si rahisi kwa pumba zenu wacha mpewe somo/
Mi ndo ticha kwa mchapa na nife bucha/

You mother fu** I aint scared cause you are both so simpo,Lemmme tell you some......... this is everlasting battle, so fu*** up-

#20 quertzal

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 49 posts
  • Locationkimara maskani

Posted 10 May 2005 - 01:05 PM

Vipi kijana sky mbona sana midomo unachonga//
huna mpya naona kwa wanaume sasa wajigonga//
ni quertzal kidume wewe hapa ni shoga//
husije kwa woga na meno kuchonga hapa utafanywa boga//
hivi ni wewe kijiba fyuzi mtoto wa juzi juzi//
uliyepata tuu ni simulizi za wakufunzi wa hili kulunzi//
twende kazi kama unajua ku-kwea mnazi//
hili ni nyundo la kijambazi kaa wazi nikupe kazi//
husipende siasa wakati hauna darasa//
sawa kupenda anasa na kelele wakati huna kinasa//
huna thamani na karata yako garasa//
wee we wee weee kaa kimya tena fyata mkia//
tunapopita amkia huna sifa utakula vilivyo bakia//
unajaribu tunisha msuli kwa ugali kiporo na dagaa mbili//
unakuja umevaa msuli na kutunisha zako mbavu mbili//
kijana mdogo mvua mawingu yake dalili//
hapa tutakupembua tukubakizie punje mbili//
karibu dsm tufunze japo kiswahili//
utapate sema nasi tukusajili//
"Guys don pretend keep it real so dat kids can learn n grow from us"

Quertzal a.k.a lyrical blower





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users