bongo illest mc
Started by Guest_tino (-_-)_*, Jan 22 2003 10:31 AM
14 replies to this topic
#1 Guest_tino (-_-)_*
Posted 22 January 2003 - 10:31 AM
#2 Guest_bahati_*
Posted 24 January 2003 - 09:39 AM
inakuwa vipi kama jamaa ni illest halafu hautumsikii mitamboni? ni wazi tumjuao ndio tutendelea kumjua..je mtoto miaka ya themanini na nne atamjua jamaa?...nakubali nimkafiri katika sanaa, lakini ukimya mwingi....., upoo babaake..
whatever
whatever
#3 Guest_tino (-_-)_*
Posted 24 January 2003 - 10:08 AM
wabongo wana bana mwanao.........see you.......
:D
:D
#4
Posted 16 February 2003 - 07:11 PM
Hata mimi nakubaliana na hilo...so far sijasikia jamaa ambaye anachana ka Hash...lakini sio utani hata mimi sijasikia nyimbo zake tangu long time yaani ni miaka...ila kama alivyosema Tino nasikia kuna watu wanabana...sasa sijui sababu au ukweli katika hilo!Lakini sio utani nasubiri sana kazi ya jamaa!
#5 Guest_used to be ambax_*
Posted 04 April 2003 - 07:31 AM
am sorry j4 ...iam so in trouble with those posts in this battle page.naomba uondoe message zangu zote zenye lugha mbovu samahani sana AM STILL DIONG HIP IN A MAD WAY lakini hizo lyrics zime nikharibia mabo yangu.
aafikiri tutashirikiana vizuri kwa hilo.
thanks in advnce.
ambax
aafikiri tutashirikiana vizuri kwa hilo.
thanks in advnce.
ambax
#6
Posted 03 September 2003 - 06:54 PM
Bongo hapa hakuna Mcee Mkali...Ukali wa mcee ni mtu mwenyewe anavyoona.....ni kama mademu uzuri upo kwa mwenye macho litambueni hilo...na kama kweli wewe si mgeni wa fani hii nadhani unaelewa nachoongea hapa....mpaka marekani napo ni ngumu ku-rate kwamba flani ni mcee mkali kuliko wote hata kama ana infinity projects hewani.....hii siyo basketball au mpira wa miguu mnashindana ku-drible na kupiga danadana....hii ni sayansi ya silabi(maneno) so inategemea inamkuna vipi mtu(shabiki)........
alcapaino.Mg
'the Most Illeat 1'
alcapaino.Mg
'the Most Illeat 1'
#7 Guest_Tuffjam_*
Posted 04 September 2003 - 06:45 AM
Nakubaliana na Alcapaino. ni kweli mcee mkali ni kama "beauty is in the eye of the beholder". Rakim anaheshimika kama baba wa "tactical flow" zote yaani ikifika kwenye swala la skillz, delivery, wordplay sayansi yote kuhusiana na "ukali" katika rap, jina lake huibuka kwanza. Nas, Jayz, Canibus, Dre, Eminem hata 50 wote watakwambia baba ni Rakim.(rakim-central.com). Lakini jee tukilinganisha "bank account" au mashabiki wa Missy Elliot na Rakim, nafikiri jibu wazi hapa. Kuitwa mcee mkali ni heshima tu na siyo kwamba unazidi wote.
Knoka a.k.a Tuffjam
Knoka a.k.a Tuffjam
#8 Guest_HEKIMA_*
Posted 04 September 2003 - 12:28 PM
Ukali wa MC mainly unatokana na uwezo wake(kina chake cha fikra),na jinsi ya kuprezenti hizo fikra zake.Sio utani ni vigumu kusema MC mmoja ni mkali kuliko mwingine,lakini ni rahisi kutenganisha kati ya real MC na 'katuni'.Kuelewa kina cha MC lazima nawe mwenyewe uwe kina kiasi flani
na hiki ndicho kitu kikubwa ambacho watu hawana...
Mi nadhani kama nchi yetu ingekuwa ni 'English media' ma MC wangekuwa wabaya zaidi..bila ya kuwa na uwezo flani wa kuelewa 'lugha' ni vigumu kutanua upeo..unakuta ma-MC wengi ambao wanaweza lugha-wanakuwa kina kuliko wengine,simply kwa sababu wana-uwezo mkubwa zaidi wa ku-relate na mazingira...kama unaelewa traki za kiwanja ni advantage kubwa kwako but again, inategemea na mtu mwenyewe pia kama KICHWA!
PA1

#9
Posted 05 September 2003 - 02:14 PM
Hekima mimi natofautian na wewe kidogo kwa hilo swala la lugha...mimi kwa mtazamo wangu sidhani kama lugha ni factor ya kuwa kina labda useme kuwa watu wengi hawajui kiswahili vizuri ndio iwafanye wasiwe deep zaidi (tukichukua argument yako ya lugha kuwa factor) mimi nadhani mtu kuwa kina ni product ya kusoma sana na kuwa well informed pia lazima uwe smart period yaani ujue jinsi ya kucheza na maneno au kama wewe ulivyoiweka vizuri kabisa "(kina chake cha fikra),na jinsi ya kuprezenti hizo fikra zake." Kurelate na mazingira MC mkali no matter lugha gani anatumia anaweza kufanya hivyo...mimi nadhani ma mc wengi ambao wame master lugha ya kiingereza na kiswahili wako more educated na exposed tofauti na wenzao (hii ni reality kwa vitu vingi Bongo na wala sio HipHop peke yake!) na ndio maana wanaonekana kina zaidi ya baadhi ya wenzi wao hata hivyo nina uhakika kuna watu wako kina sana katika kiswahili bila ya hata kujua kiingereza...kuna uwezekano pia kuwa kwa sababu information nyingi bado iko katika lugha ya kiingereza ndio maana tunaona tatizo hili (mf. vitabu vingi, internet, n.k ingawa kuna exceptions!)
Ila nakubaliana na wewe wenye kuelewa kiingereza wana advantage zaidi kwani wanaweza kujifunza kutoka kwa ma MC wa nje (na katika case hii Marekani ambako ndio hiphop ilipolelewa) hata hivyo kichwa cha mtu kina play part kubwa kuliko lugha...Kuna washairi bongo wako kina balaa, au waimba ngonjera...tatizo ni kuwa hakuna anayewafuatilia na ndio maana unakuta hatugundui uzito wao. halafu vilevile sio kila mtu anaweza kuwa MC na ndio maana unaona kuna makatuni kibao...kila mtu kaona hapa kuna mshiko basi anataka kurap...real MC haanzi kurap ili apate pesa...pesa ni end product...MCing ni sanaa...na sanaa sio product kama colgate ili iuzwe madukani...ingawa inauzika lakini hiyo sio purpose ya sanaa...au msanii wa kweli!Hao makatuni wote ni entertainers tu lakini sio wasanii!

#10 Guest__*
Posted 05 September 2003 - 06:20 PM
oya bongo watu mamabo ya kujisifu kuwa na pamba wakati ni v-tshirt 2-3 vya rcawear hatutaki kusikia katika trax, na tafadhalini tamkeni majina ya hizo pamba yanavyotakikana, tunatiana aibu manchi ya watu...this is ZOOMTIME:::::UPANGA EASTSIDE, u heard???
#11 Guest_HE.KI.MA_*
Posted 06 September 2003 - 01:47 PM
Kama ukivyosema Mkuki,ni ufafanuzi! no-doubt umefafanua kina.Nadhani maoni yetu ni almost sawa but offcourse,vichwa lazima viwe na MIONO tofauti(kidogo) sababu tupo tofauti...
PA1
PA1
#12 Guest_Karata_*
Posted 12 September 2003 - 11:46 AM
Mi naoma ma emcee wakali "wapo/yupo", Hashim aka Osama! Track record ndogo yes lakini but inatosha kuonyesha prospects! Shadows of a dark destiny jamaa kaprove he can spit it hata kibongo n stil be deep. Saa za kazi na Tunasonga ndio kamaliza!!!!!!!!!!
#13 Guest_tino_*
Posted 12 September 2003 - 02:59 PM
Karata said:
Mi naoma ma emcee wakali "wapo/yupo", Hashim aka Osama! Track record ndogo yes lakini but inatosha kuonyesha prospects! Shadows of a dark destiny jamaa kaprove he can spit it hata kibongo n stil be deep. Saa za kazi na Tunasonga ndio kamaliza!!!!!!!!!!
yes yes,,i am glad you can see the real,sioni mwengine bongo kama dogo thats ma point of view,
#14
Posted 12 September 2003 - 03:23 PM
Nakupata HE.KI.MA shega tu...Mimi Dogo sio utani nakubali kuwa jamaa yuko fiti balaa na kina chake sio utani ni maji marefu...ila ndio hivyo ana track chache under his belt kit kinachofanya watu wawe wanamsahau lakini I am sure anajua anachokifanya. Nani mwingine mnadhani yuko kina pale Bongo? Mimi Prof Jay namkubali ingawa ana utofauti kidogo na ile kina original cha hip hop ni kama vile kusema Mos Def = Hashim na Tupac = Jay...Hashim ni better MC without a doubt ila Jay ana mass appeal hata kwa average people yaani sio lazima uwe critic ili kumfeel wakati Dogo lazima mtu uwe na knowledge fulani ya mizizi ya hiphop ili kumkubali ipasavyo...by the way jamaa wengine ambao ninawafeel ni Solo Thang (Huyu jamaa alivyotoka bado kidogo nidhani Hashim maana style zao zinafanana sana) Mack D, Halafu kuna jamaa wengine nakumbuka katika kundi la wateule nao walikuwa fiti sana (Hivi bado hili kundi lipo?) nakumbuka nilikuwa kwenye concert moja way back mambo club ambapo walishinda recording deal, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwasikia lakini nilikubali. Bongo sasa hivi tuna rappers wengi lakini ma mc bado ni wachache (Ninavyosema Rappers siwa dis ila nadhani kuna vitu fulani wana miss ingawa bado ninawa feel!) lakini inategemea na lengo la msanii mwenyewe na vilevile audience yake (wabongo wengi hawaielewi hiphop lakini wanajua sana rap mpya za akina Jay Z, Ja Rule na Nelly!) lakini kuna room for everyone ili mradi tu isiwe kama marekani ambapo wanasisitizia upande mmoja tu wa hiphop...commercial rap wakati rap is larger than that. Cha muhimu ni kuwa na choices!
#15 Guest_TZBOY_*
Posted 13 September 2003 - 04:16 PM
OYA MACHIZI MAMBO VIPI JAMA? AIGHT KABISA - NI HOUSTON TEXAS KWENYE WABONGO WENYE MA BENZ NA MA LEXUS, YAA. MIMI NI MCEE ALINGUAL NANIME SAPOTI HII FANI KWANZIA ENZI ZA SALE JABIR MAN SO I KNOW WHAT IM FUCKING WITH. ANYWAY HOMIES. I YAANI MIMI NATAKA NIFREESTYLE ONE TIME FOR AFRICAN HIP HOP DOT KUWA PONGEZA KWAKU SPREAD THE WORD THAT HIP IN AFRICA IS HERE TO STAY.
YOO MIMI NI TZ BOY,ALTHOUGH NAIISHI MTONI,NANINA DREAMS
ONEDAY NI TAKE HII HIP HOP GAME ANOTHER LEVEL
NGOJA UTAONA,UTANIONA SIKU MOJA NDANI YA TV NA FOKA FOKA
NATAPIKA UKWELI BILA KUSWET AU KUTETEMEKA KAMA TRACTOR
NATAKA KUSHUKURU AFRICAN HIP HOP KWA KU SAMBAMZA NENO LA HIP HOP
AND IT WONT STOP BABY, NJOENI TU CHAT
KONNECTENI NDANI YA HII WEBSITE,SIWATANIENI MTAONA JINSI ILIVYO BOMBA. CHAO

1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users