Jump to content


Waimbaji acheni kutangazia biashara watu katika hip hop !


10 replies to this topic

#1 Guest_Golden Lecoq Club Arusha._*

  • Guests

Posted 28 October 2002 - 02:58 PM

Oyaa washikaji sio kupata hii chansi ndio mnaongea mmabo ya kinoma.Kuna baadhi ya wanamuziki wa hipo hop nashindwa kuwaelewa sijui walivyosikia kutunga tarck za kibongo basi ndio wanatunga ilimradi imeitwa hip hop basi ndio imekuwa nongwa.
Washikaji lazima mnatunga track za maana sio mnatunga nyimbo za ajabu?lazima mnatunga nyimbo ambazo zinaendena na ukweli kwa mafano mambo ya mademu?wewe kama unamfukuzia demu fulani basi mfukuzie sio unatungia nyimbo inamzungumzia mtu?Kwa mfano Dj Jd atakusaidia nini huyo au ndio mnatangazia biashara jina lake kusudi awapigie nyimbo zenu redioni?Koma we afadhali uachie ngazi atutaki wapiga debe katika hip hop.
Wewe umeshawahi kuona Bundi akirika na njiwa?Toa nyimbo isifiwe sio mnaleta mambo ya kibishoo bongo?tunataka nyimbo zilizoenda shule hata huko katika chart ya hip hop wakisikia wanasema yes" wabongo wako fiti sio mnatangazia biashara kazi za watu! kama umempenda Jd basi siumfuate na sio unatangazia redioni.Tunataka wana hip hop wenye busara na sio mabishoo wakibongo?
Mtabakia kunawa tu! nyie wapiga debe kula halii?
Wana tennis
Galden Lecoq club
Arusha :P

#2 Guest_Mtoto wa kocha Arusha._*

  • Guests

Posted 28 October 2002 - 03:11 PM

Oyaa waeleze hao mabishoo wakome kabisa! tunataka tarck za maana sio mnaleta matangazo ya biashara katika hip hop! We umeshawahi kusikia hip hop za Mamtoni zinamsifia Dj we koma sia afadhali umsifia baba yako anayekupa kunya?
Nyie ndio mnaoleta mambo ya kupigiana debe katika hip hop sio vyama vingi hivi subiri kipindi cha vyama vingi ukampigie huyo Dj Jd agombee na kina Mkapa na sio mambo ya hip hop koma tunataka washikaji wenye busara.
Washikaji wa hip hop kama mmekosa nyimbo za kutunga afadhali mkochome mahindi semeni tuwachangie kama hizo pesa za kunulia jiko la mkaa sio mnatunga nyimbo za ajabu?
Washikaji tunataka track zinazoongelea mambo ya maana sio mnatunga nyimbo za ajabu.

Mtoto wa kocha.
Arusha. : : :idea:

#3 soulrebel

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 6 posts

Posted 31 October 2002 - 09:58 AM

Inaonyesha jinsi gani sisi kwa sisi watanzania tusivo peana "heshima", kama una hoja, toa kwa mpangilio alafu iwe na mbadala(alternative). Hapo mmekandia na kutukana tu kwamba watu waimbe vitu vilivyoenda shule, ni vipi? Kwa mitazamo ya wengi hata yenu (kwa kuwasaidia tu) nyimbo zinazohusu tofauti kati ya watu (kimaisha) siasa, uchumi, elimu na mambo yote ambayo kwa ujumla yanakera jamii kutokana na jinsi yanavyofanywa kipumbavu na wachache na kuumiza wengi wa hali ya chini.)

Lakini kitu utamaduni (culture) ya mamhali fulani, watu wengi hupenda kutafsiri kama"maisha kwa ujumla ya watu fulani mahala fulani na muda dulani" yaani kila kitu kuanzia uchumi, siasa, kijamii, nk. Kama bongofalava inatakiwa kuimbwa kwa kuelimisha jamii pekee, ni kwa namna gani? Na mapenzi nayo si vitu ambavyo vipo kwenye jamii pia? je viimbwe kivipi? toeni ushauri ili waimbaji wajue la kufanya

Ma mcee wabongo endelezeni moto!

#4 mkuki

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 132 posts
  • LocationDar es Salaam,Tanzania

Posted 01 November 2002 - 06:23 AM

Ni kweli soul naona watu wameshika bango kukandia tu wakati hawataki basi kutoa mwelekeo wanaoona wao unafaa...huu ndio ugonjwa wetu watanzania/waafrika tumekaa kupiga kelele "ooh hiki hakifanywi sawa" "hiki si sahihi" na kadhalika, wakati hata siku moja huoni mtu akatoa wazo jamani hivi tunakosea tufanye hivi...hiyo ndio njia ya kuelemisha na kuweka mwelekeo ambao wewe unaona ni sahihi sio kashfa tu kama watoto wadogo. Mimi sioni ubaya wa mtu kumtaja JD kama itamsaidia yeye rekodi zake kupigwa kwenye madisko au redioni...kumbuka kila kitu kinaenda kwa ku network...unampa props mtu na yeye anakupa props una m hout out mshkaji na yeye anakufanyia hivyo hivyo...ni swala la exposure tu...u scratch my back, I scratch yours!
Halafu kuhusu hizo hiphop za mamtoni mbona kila siku wanawapa shouts ma dj wao au washkaji zao?Halfu nani kasema kwamba kila kitu tufuatishe hiyo hiphop ya "mamtoni?"
Ebwana Soul vipi mwana mbona ulikuwa umepotea hivyo? Si unajua tena nyie ndio wachache mliopo wa kujadiliana maswala ya maana sasa mmeondoka unaona hapa kila siku matusi kama wendawazimu tu unakuta mtu hata la kuchangia unakuwa huna...nilikuwa nakupa shouts tu au siyo...nakumbuka uliniuliza e mail yangu wakati fulani...nsharekebisha unaweza kuicheki...poa basi au siyo...ibuka ibuka kama hivyo ili bodi iwe alive kidogo...masela wengine pia akina sosa na wengineo...mida

#5 Guest_911 Disco Club_*

  • Guests

Posted 04 November 2002 - 04:42 PM

Umeingia mnyeweoo umetoka mnyeweoooo!huu mkuki ulinitupia umenigusa kinoma!!oyaa babu yangu mimi sio kuwa namind au vipi ni poa kama tunabadilishana mawazo pyee tu!
Niaaaambieeeeeeeee huu ujumbe nimenyaka na pia minyee we sinanoma ila Mshikajiiii unasema kuwa nilikuwaomba email sii mimi umejichanya mnyieewe!
Mimi babu yangu sijacheza ndani ya bongo kama miaka minne inakatika hivi niko natafuta maisha hukooo kwa bwana Chirac!!!Kwa hiyo nilitoa kijiwazo tu!nisikie vipi wachizi watamind hiyo maada?
Wachizi mimi sio utani nawasifu sana kutokana na kupata hii chansi sio tukabadilishana mawazo kama unavyojua ukishakuwa nje ya bongo sio kuwa ndio mwisho wa kukutana lasivyoooo!haha!!
Babu mimi nimekuelewa chart yako sawa kama ulivyotalk hapo up!! ila ingekuwa fresh wachizi wanagusia maswala mengine yanayohusu maisha ya wabongo sawa unajua pia kama washikaji mtatea masilai yetu itakuwa fresh au vipi?
Nadhani unajua sana viongozi huwa wanajiweka wenyewe katika maslahi yao na pia hapo bongo lazima washikaji ujipigie kifua ndio mambo yako yawe freshi?Na pia washikaji nawasifu sana kutokana na vipaji vyao vya kuweza kuongea point ila lazima katika hizo point wanazotoa lazima ziwe na mwelekeo ndani yake.
Hip hop ya bongo hivi sasa inapanda kwa kasi sana kiasi mnashtusha ulimwengu sawa na mimi ninauwakika iko siku wabongo mtachukua chart katika hip hop.
Mshikaji unajua hivi karibuni tu!huku Mamtoni sawa nilikuwa napata Track kutoka kwa wachizi huko bongo sawa hii Track washikaji walimind kinoma sawa ingwa unajua tena lugha ya kibongo magoli na pia washikaji hilikuwa haipandi ila wakaipa point sawa wakaomba niwape kopy basi nikawataflia wachizi wanasoso vipi?wao wenyewe wakasema bongo hip hop magoli basi mashikaji nikachukua maajiko kishezi na tarck zetu nikaona oyaa poa tutazidi kusikika ingawa najitaidi kuzipiga hizi tarck huku kwa Mzee Chirac ila zitazidi kusambaa tu!
Pia nawapa washikaji usia tu!msichoke kusoso!!!!iko siku tutafika tuuu!ndio Mzee;;;Watanzania mnakubali ndiyo mzee;;;;;;;


911 Disco Club
sony_boy J.J
Kwa Mzee Chirac.

#6 Guest_Kwa wavuja jasho Ferri_*

  • Guests

Posted 04 November 2002 - 04:56 PM

mwanampotofuuu weee!!malaya wa maisha wambieeeeeeeeeei Sony _boy sosaa wanangu sosaaamwangu chart yako hiyo kimya kilitawala lete urodaaaaaaaaaSony boy.Hipohop zisambaze mwanagu mwakilishi wetuuuuuu hata mzee Chirac mpatiiii tu! asilkilizeee vijana wanasemanii!!!
huku vijimanenoo tu! ndio vinatufanye tuadimike kyelooo tu!Feriiii tunacheza na samaki tu! ferrriiii babu yangu!!!!iko siku tutazuka tuuuu!!!
Msalimieee Ziggylah huko Sweeden. :twisted: :twisted: :twisted: :twisted:

#7 Guest_bibi Aga.kigamboni._*

  • Guests

Posted 04 November 2002 - 05:03 PM

Sony _boy J.J vipi kichaaa! chart yako eeee!karibu kichaa sema yote tupo urooda vipi mweziiiiiiiiumeandama huooooooo hip hop hizo sonyboy vijana wanakupa ndio Mzee je unaswali sonyboy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

#8 soulrebel

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 6 posts

Posted 12 November 2002 - 09:06 AM

Mkuki unajua tena mambo ya kuhangaika mzee, hasa hasa kama uchumi haukuungi mkono mfukoni, huwa napitia pitia tu kiaina. Washkaji naomba msimaindi hii salamu kwenye forum.


Mamcee wa bongo Endelezeni moto!

#9 Guest_Bishololo_*

  • Guests

Posted 17 December 2002 - 05:21 PM

Oyaa walala hoi na walusha vumbi kijiweni na hasa wale walioko majuu
salamaaaaaaa
najuwa kuna wanaotesa na wanaoteseka lakini poa tu hamna noma wala nini kawaida.Bongo naipenda kinoma.Kuna washikaji ambao wakiluka majuu basi inakuwa tabu watu hawakohoi mtaani kwa mbwembwe na michakaliko yao ya kidizaini sampuli.sawa bingwa ulikuwa majuu je kuna maendeleo uliyoyafanya? au unabaki kusema tu mimi nilikuwa kwa baba sadali time fulani au mamtoni au babiloni sawa hayo hayatusaidii sisi wakati tunaona unalukaluka na kubangaiza hata ya ngama baada ya kudondoka tena hapa bongo yetu ya mzee rukhsa na kujichanganya na masela.Nawausia wale wote waliobahatika kuluka mamtoni au place yoyote ile wawe makini na watusaidie sisi ambao hatukubahatika kuluka iwe ni kimasomo wameruka au kwa kutafuta uchache
oyaaaaaaaaaaaa
bishololo.

#10 Guest_TX_*

  • Guests

Posted 27 December 2002 - 09:56 AM

Oyaa poa tumesikia ishu yako!Sisi sio kuwa tunaikanda bongo no!no!no!!!!!!Unajua tena mambo fualani ndio yanatufanya tuwe huku ila bongo siotani mali kinoma na pia bado tunakumandi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ila unajua tena mambo fulanifulani ndio yanatufanya tuondoke hapo kwa Mzee Kipara.dili sasa hakuna bongo watu wamebakia kufuatiliana kiana aina tu!wabongo tunashindwa kujadili ishu muhimu tunabakia kukandiana tu!Sio lazima wote mje Mamtoni unafikiria wote mkija huko Mamtoni Mkapa atabakia na nani?au hao wanafki ambao wanafuatilia mambo ya watu watabakia na nani?Wewe ukiona mambo ya bongo unayamindi basi endelea kukumbatia upumbavu wako?
Washikaji wacha sisi tuchachike na mambo yetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Tx
France.

#11 Guest_Nyenyere_*

  • Guests

Posted 07 September 2003 - 08:30 PM

E bwana wazee mbona mnashindwa kuelewana, Kitu ambacho mi naona bongo hiphopers wanakosea ni ile kuridhika mapema afu na ile kujiona baab kubwa wakati njaa tupu. inabidi wakaze matako hasa ili wafike mbali bahati nzuri kuna watu watatu watatu prof jay, afande na Solo wanakemea sana wale fake Mcs.
utakuta mtu album nzima ni kujifagiliaaaaaaaa we mpaka inaboa au kufagiliana wao kwa wao, watu watakuwa hawasikilizi uzushi wao.





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users