Jump to content


FIESTA UWANJA WA TAIFA?


30 replies to this topic

#21 mkuki

    African Hip Hop Regular

  • Members
  • 132 posts
  • LocationDar es Salaam,Tanzania

Posted 21 September 2002 - 05:06 PM

Kweli kabisa Soul; sometime watu wanafanya vitu ku prove kitu!Mimi lakini nadhani hao watayarishaji wangeweka ulinzi wa kutosha regardless!Hata kama ingekuwa oysterbay,masaki na kadhalika bado ingetokea fujo kama ulinzi usingekuwa wa kutosha...watu wakishakunywa wanasahau ustaarabu na hata huko masaki kuna vibaka vilevile!
Anyway next time labda jamaa watarekebisha!

#22 Guest_DIBRO&WALKER_*

  • Guests

Posted 23 September 2002 - 12:49 PM

clouds mpango wenu haufai wala nini hiyo fiesta yenu mliyo andaa kwanza nataka kuwambia ilikuwa haina dhumuni lolote kwa sababu zifuatazo(1)MUDA MLIOUWEKA HAUFAI NANI ATAKAYECHEZA DISCO SAA 4 ASUBUHI
(2)MKIWA MNAJUA TEMEKE USWAHILINI KUNA VIBAKA MLIKUWA MNA NIA GANI NA SISI WAPENDA STAREHE
(3)MTAWALIPA NINI WALIO PATA MADHARA KUTOKANA NA TAMASHA LENU
MWISHO MKAE MKIJUA KUWA NINYI NIWASHENZI KUANZIA MKURUGENZI MPAKA VIBARAKA WA HAPO OFISINI KWENU....
M.....................................@@@@######$%^&*???? :lol: :oops: :roll: :idea: :shock:

#23 Guest_scorpa_*

  • Guests

Posted 23 September 2002 - 06:33 PM

cha kushangaza nikwamba pamoja na clouds kufanya matamasha yao ya hatari ya kufa watu wananchi na wenyewe hawakomi tu kwenda huko hata mimi jamani ni muhudhuriaji mkubwa ila huko uwanja wa taifa wataenda wenyewe... :wink:

#24 Guest_mr blow_*

  • Guests

Posted 24 September 2002 - 07:35 AM

:lol:

#25 soulrebel

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 6 posts

Posted 27 September 2002 - 11:23 AM

ZILE SIO “FUJO”

Hip-hop ya bongo tusipoangalia itaanguka na kusahaulika tena muda mfupi tu ujao. Ntarudi tena baadae kufafanua kwanini nimeanza na hiyo sentensi, kwani ntakachoandika nafikiri kilitakiwa kiwe na thread’ yake tofauti ila kutokana na baadhi ya watu kuwa na upeo zinazotofautiana kwenye hii mada, nimeonelea nichanganyie kwenye hii mada ya “fiesta” kwani yote yaliyotokea humo yana mtiririko unao fatana ama kurandana. Kwa mtazamo wa kisosholojia kama nilivyoeleza hapo juu hapa watu tunaishia kulaumu wasio husika saana(blaming the victim) na kuwaacha wale wanaoleta sifa mbaya kwa waswazi (kwani wao sio wa kulaumiwa sana,) kwa namna nyingine ni kama kuwaona wapalestina ni wabaya kumbe wote tunajua sivyo. Mkuki nimekupata uliposema kwamba uwekwe ulinzi wa kutosha lakini tatizo halitatatulika kirahisi hivyo bila kurudi kwenye misingi ya hiphop bongo “bongo flava” (BF) na kuinezi, ambayo haina tofauti yoyote kubwa na ile misingi ya Hiphop ya Marekani, au reggae na hip hop carribean islands, ya kwamba umaarufu wa bongo flava sasahivi ni kwa kiasi gani inaweza “kuwakilisha hali zetu halisi” na ukweli wa mambo ya Tanzania kwa ujumla. Hapa tunagundua kwamba BF culture, hususan mashairi (ukiachilia upande wa mavazi na kadhalika) imepanda chati hususan kwenye kueneza na kufichua ukweli wa mambo halisia ya mtanzania wa kawaida, Mtanzania wa kawaida nikiwa na maana ya wale walio wengi ambao ndio wanaosota hasa: walala hoi (nikiwa na maana halisi ya neno hili), watanzania wale ambao kipato chao ni chini ya robo dola kwa siku! Maana ya umaskini kamsikilizeni ras lion, amejaribu kufafanua. Hali halisi za mnyonywaji wa Tanzania ambaye mtakubaliana nami ya kwamba kwenye upande wa siasa inachukua picha mbaya hapa kwetu (kwani umaskini sio kiuchumi tu, siasa sinachangia sana) Siasa za ovyoovyo na sera za kipumbavu na michezo ya kuigiza ya wabunge kule Dodoma na baadhi ya vyama (kama alivyoainisha mzee mwenyewe profesa Jay) na kukumbatia sera za kibepari ambazo sinawanufaisha wakubwa kutokana na ten pasenti ya kamisheni, ndizo hasa zinazozidi kumkandamiza mwananchi wa kawaida, kuongeza tofauti ya kimaisha kati ya Temeke na Obay au Masaki. Hata pamoja na sekta zingine za maisha ambazo hazitumiwi vizuri kwa nia ya kumsaidia mwanchi ajinue kiuchumi.
Kwa mfano kule U.S uvunjwaji wa makusudi wa nyumba za watu wa rangi kwa ajili ya kupitisha barabara miaka ya mwnzo ya 70 kule jiji la New York iliongeza matatizo sana kwa hawa watu kiasi cha kushamiri u ‘hustler’, kutumia madawa, na kufanya party nyingi ili kuondoa mawazo ya siasa za kibepari ambazo zilikuwa haziwajali watu wa rangi ambao sio weup.Humohumo vijiweni hiphop kwa kifupi ilianza kushamiri kwani watu walikua wamechoswha na maisha ya kuonewa na sauti kutokusikika, wakifanya fujo polisi (tafsiri yangu ya polisi ni watu waliowekwa kulinda wale walichonacho wasiguswe na wasionacho) wanaingilia kati, sasa rap ikawa satili ya kufikisha hasira zao huko juu, ila wajanja (na hapa kwetu ndicho kinachotokea) waka u-commercialize kwa faida zao, na baadhi ya mamcee wakoneshwa kama njia ya kuondokea kwenye hali mbaya ya kimaisha. Kwa hapa Tanzania BF ni sauti za vijana zinazotoka kuwaendea wazee (wapo asilimia 8tu nchi nzima!) wanoatuambia sisi ni taifa la kesho, wakati wao wanaendelea kufanya madudu huko juu na kula kuku kwa jasho la kodi zetu, lakini vijana tuna rise na kusema ‘sisi wa taifa la leo’ kwani BF ndio sasa inashamiri kutokana na uwezo wake wa kufikisha sauti za wanyonge na maskini, kitu ambacho kwenye siasa kinaonekana cha wazee kama kina makani, mrema, lipumba na kina mkapa. Jamani BF ndio silaha tuliyopewa tusipoangalia vizuri itatekwa kama inavyoelekea sasa hivi.
BF mimi nionavyo tofauti na miaka kama mitano iliyopita, sasa inashamiri kutokana na watu kuimba mashairi yaliyoenda shule! Sasa yameenda shule kivipi? Mengi ni yale yanayowakilisha jinsi mtu au mwimbaje anvyo tumia angle yake yaki sanii kuyaelezea yale yanyo isibu jamii (na kwa hakika kwa hapa kwetu mengi hayapaswi kufanyika) ni umaskini unaozidi kupanuka, hii ianjionesha hata kwenye mashairi ya BF ya kimapenzi pia (achilia mbali yale yaliyodairect kama yakina jay) kwa mfano jinsi Inpekta (maskini) anavyohangaika kumpata mtotto wa geti (kitajiri) hebu angalia yale mashairi yanavyotoa reflection ya reality! Mtu msikilizaji wa kawaida anaweza kufurahia mziki tu juujuu kutokana na beats na flow hivi lakini picha inayotolewa na ule mwimbo nizaidi ya beats pekee, na tena kikubwa, ni hali halisi iliypo dar na Tz kwa ujumla, hali ambayo japo ipo lakini si haki kuwepo, Inspekta anaelezea hali ya utofauti uliopo kati ya maskini (yeye), na matajiri, (kilichobaki unakijua) wa lakini kutokana na mfumo wa maisha ambao unapendelea wachache, ndio maana upo, sasa wana BF wansaidia kufikisha ujumbe kisanii, wansema hapana kwa mfumo mzima wa utandawzi unao gandamiza wachache na kufaidisha wengi. Miaka ya nyerere mtu usingeweza kuimba hivi.

Sasa turudi kwenye Somo na kwa nini nimeandika “upuuzi” (kwa wengine siyo)wote huo hapo juu? BF sasa hivi imeingiliwa, na ninatahdharisha (ili nsijeeleweka vibaya hapo baadae), na watu wenye uchu wa hela (watanzania), wengi wameelezea hapo juu, na ya kwamba kutokana na mfumo wa maisha kubadilika yaani, mziki sasa hivi uko “commodified” (commodification of BF), umekuwa bidhaa ya kununua kwenye soko kwahiyo lazima yule anaye upromote umlipe faida, tena kubwa, kuna hatari ya wanamziki wengine kwa namna fulani kukata tamaa, tena wapo ninaowafahaumu walioshuka, na hakuna tofauti na kilichotokea marekani. BF kwa namna fulani inageuka kuwa “commercial music” siyo vibaya ila kwa level yetu ya ubepari na utandawizi tulioingia (no! Tunaoingizwa kwa nguvu) wana BF wa kawaida wanasahau msingi ile inayoinyanyua BF yenyewe. Jinsi BF inavyowakilisha mashairi yaliyoenda shule yanayoelezea hali halisi (naupa mic zote mwimbo wa suma G “vituko uswahilini, hapa ni mfano tu) ya watanzania walio wengi. Tuwe tunafanya safari za kwenda vijijini huko, tunajidanganya na hapa dar, hebu nedeni kwa fano kwa hadzabe, sumbawabga huko au kasulu ndanindani, muweze kuielewa Tanzania mnayoishi ikoje,na watu wankimbilia mjini tu, tena kama mwanangu mwenyewe Bambo alivyo wakilisha! “Dar kuna maendeleo fasto fastoo” (mic kibao!) ndio maana tunakimbilia huku.

FIESTA: misingi, hali halisi (saa zingine ni “very relative” huu msemo) ya watu wa Tanzania inayoimbwa na mashairi ya BF (arguably ndiyo yanayoipandisha chati BF), yaani wale walala hoi ambao ndio “victim” wa mfumo huu wa utandawizi tuliopo, wale vijana na watoto wa wanyonywaji ambao siku ile ya fiesta walikuwa pale nje (ndiyo sikatai wengi wa temeke ndio maskini kuliko kino, na wanafujo bob Marley “a hungry man is always an angry man”- yaani mwenye njaa kila wakati ana hasira-kweli, hasa ukichukulia njaa aliyonayo ni watu au mtu mwingine amesababisha) waliokaa nje wale sio kwamba walikuwa hawataki kuingia,la hasha! Tena walikuwa wengi zadi ya walioingia, walikuwa hawana hela jamani (hela zao nafikiri wachahche mnaokaa vizuri mumezikumbatia huko obay,masaki na kino), hawa ni wale watu mnaopata ujiko, mnaowawakilisha, mnaowaimbia mashairi yaliyoenda shule, ni wale akina matonya walionyimwa haki ya kwenda shule eti hawana karo ya elfu mbili kuanza primary inabidi wauze ubuyu au mahindi usiku mzima apate mia 200 ya kunywa chai bila sukari kesho yake, sio waliobarikiwa kama wewe unayetmbelea gari, wamekuja hapa town kama Bambo na RD walivyoainisha, wanshindwa kwenda kuona laivu kile kinachowagusa kwenye nyoyo zao, kile wanchosikia kutoka kwenye redio zao za betri zilizopondwa ili zisiishe chaji, nyimbo ambazo finally kumbe kuna sauti za kuwawakilisha huko juu, wana BF ambao wamekuwa maarufu kupitia migongo yao (hata kama nao walikuwa huku uswazi lakini nao wanachotwa na vijisenti na umaarufu na kusahau walikotoka) ni VICTIMS wa mfumo wa utandawizi unaoshamiri bongo. Sasa kinchotokea ni kwamba mapromota kama vile clouds (ambao nao ni promoters wa BF wazuri tu) ila nao wanataka kula, lakini bila adabu! Wao pamoja na wanamuziki (pamoja na BFs) wengine wameshaonja asali ( ubepari) na kusahau walipotoka, wamekuwa “commodity” bidhaa ya kununuliwa dukani ila wale wenye hela tu, sasa jamani wengi wa wabongo bado tu maskini...... (tuna abject poverty) wengine watahama mitaa yao kwwneda kukaa mitaa ya maproducer wao, masaki huko, na blahblah kwingine, yaani kama mamcee wa mamtoni mwanangu: kwa wao kama mfumo wao unavyojieleza “the American Dream” na sisi vilevile tumemezwa humu kama Inspekta na Karama walivyoeleza kianina kwenye “nje ndani” je, na bado wataweza kuwakilisha? lakini inakuwaga shida kidogo (hii nayo inahitaji thread yake). Lakini kuna music nyingine huwa zina stick na falsafa zao za muziki, ndio maana mimi reggae fulani fulani zinakuja first, BF namba mbili kutokana na kile wanchokifanya, achilia mbali miziki ya kina shaggy (kwanaza haimbi reggae yule, bali pop!) kuna watu kama kina Sizzla, Anthony B, Capleton (kwanza Capleton na judgement yard yake, au Sizzla wao kwao jamaica, kingston, wanatunza kila mtu hood yake nzima! hela wanayopata kutokana na wanchoimba, wanawalisha watu, huduma zote muhimu wanawapatia, Capleton ndio namba moja sasa hivi Jamaica, ni mwanamuziki wa reggae mwenye namba ones nyingi zaidi kwenye charts ukiacha Bobu M! respekt, sikilizeni nyimbo zao muone) hawa falsafa zao ni kinyume kabisa na ubepari kuanzia wancahoimba mpaka na wanvyoishi, hata shoo zao wanachaji chini ile mbaya, Eminem au spears kiingilio chake si chini ya $100, kuna kipindimpaka $1000 kwenye black market na watu wananunua!lakini kutokana na kwamba watu kama kina Capleton au Sizzla, au Jah Mason hawako kwenye kuuzwa kama pipi huwa hawachaji sana, watu hulipa mpaka $7 per kichwa, tena kwa Europe unaingia, ili tu wale ambao wanawawkilisha wapate kuingia na kuwaona na shoo zao yaani zinakuwa bomba kishenzi, hawako kwa ajili ya mafaida makubwa kama wengine ili tu wapenzi wengi wale wanoimba juu ya shida zao wapate kuingia (burn babylon! burn! Bombo klaart!). Sasa pointi yangu ninayotaka kuchangia hapa kwetu mapromota wanatak faida, na kwenye forum watu wanawa tupia lawama “wafanya fujo” tu, na wale wenye nacho wengine wanasema hawaendi kwenye shoo hizo lakini sijasikia (labda kuna thread sijaisoma) mtu aki suggest ni vipi hawa watu wataonaje fiesta?? Hawa mnaoimba juu yao wanao shindia ugali kwa mbilimbi? Watu wasukuma mikokoteni ya uchafu ya nyumba za wakubwa (Zay B anaowakandia) , hawa sio watu jamani? Ombaomba wataingiaje kwenye shoo kama hizi nao wajirushe kinominomi? (bila ombaomba Bambo angeimba nini?) hakuna mpumbavu yeyote anayejali! (nobody gives a f-----n damn shit!) kwasababu gani? tupo kwenye mfumo unaojali maslahi binafsi tu! Na tunaathirika nao kimawazo pi, inakuwaje mwanmziki anaimba alafuanaambiwa ni kutokana na juhudi zake binafsi, angeimba nini suma kama kusingekuwako umasikini uswahilini? Waimbaji ningewashauri warudishe angalao kidogo kwa wanachi, uimbaji usiwe ngazi binafsi ya kuondokea kwenye umasikini bali hata kuhudumia wale tuimbao juu yao. (Kwa wale wanopenda kusoma (nasisitiza) wakasome kitabu kizuri sana ccha Murray Forman kinachoitwa “THE HOOD COMES FIRST: Race, Space, and Place in Rap and Hip-hop” cha mwaka huu 2002, ukitaka nitakupatia ukatoe kopi, kinarandana kidoogo na hii topiki)
Kwani kuna ubaya gani kiingilio kingekuwa buku au mia tano ile steji ikasogezwa mwisho kabisa kule ikanyanyuliwa zaidi, (si mnacheki wenyewe mapromota wa miss TZ walivyofanya, hapa namaanisha kupamba steji na ukumbi sio kiingilio) ili jamani kila mtu ajirushe-mwenye kipato kidogo, kikubwa, maskini tajiri, ombaomba, mkulima mfanyakazi, msukuma mkokoteni, mvuvi, muuza karanga, chipsi, mitumba, mwanfunzi wa primary, sec,vyuo nk, nakadhalika: na hakika hela ingerudi, uwanja wa taifa ungejaa wote ule kubabake, hata wafanya fujo wangeingia na kusahau fujo zao, polisi ulinzi uimarishwe ndani (bila kusahau nje) concert za senegali wenyewe mnazijua, tujifunze huko. BF inakuwa kwa ajili ya watu fulani fulani tu wenye uwezo, yaani kama hunacho uchukue taimu siyo???????! Ubinadamu gani huu?? Tena kuna jamaa wale walioimba “wazo la leo” wamezungumzia hili lakini wanonekana wanataka hela tu(labda kweli). Ukitaka kujua huu mfumo unavyoteka watu kupenda vihela mbuzi, na kufaidisha wenye navyo kuna yule mpumbavu mmoja wa certain promtion sijui!. Yule mshenzi aliyeandaa tamasha la kuwasha mshumaa kuenzi wanamuziki waliofarki zamani kama kina Dandu, Salum Abdallah,Mbaraka Mwinshehe, nigga one, DRob (to all,much Respekt!) hawa jamani ni marehemu, alafu watu wanataka kula juu ya migongo yao tena kiingilio eti buku tatu, kiwanja chenyewe Mambo club obay!! Jamani!, Huko obei nani anaeweza kufika daladala zenyewe mwisho saa kumi na moja, wanotakiwa kukaa huko lazima muwe na magari, (yaleyale wa tabaka fulani) Sidhani kama hata iyo hela ingewafikia wajane au wattoto wa familia zao, cha kusikitisha zaidi ni pale ambapo hata wasanii wenyewe wa BF eti walitakiwa kulipa kiingilio! Kwa ajili ya wasanii wenzao! Tena kwa ajili ya kuwaenzi tu marehemu? Tunaelekea wapi jamani kama siyo kuiua BF huku? (mizki ya bendi kama tot au m&m inawakilisha kinamna inataka kusurpass BF!?), tamasha kama hili la kuwasha mshumaa kwanza lilitakiwa liwe bure, lifanyike kama pale jangwani hivi au uwanja wa taifa, watu waelezwe maana yake na nia ya tamasha, na polisi wote wawepo bila hata kulipwa, kwani kazi yao si kulinda raia jamani? Mimi maoni yangu ni kwamba kunakamtindo ama kameibuka au kanataka kusurface” kwa nguvu kwa kuona kwamba au kuufanya muziki uwe wa watu fulani, na masikini nchini hawatakiwi kwenye starehe hizi, hakuna juhudi madhubuti za makusudi kabisa zianzowekwa kuwakilisha kikwelikweli wale watu ambao muziki huu BF umepata mafanikio makubwa kutokana na hali zao za kimaisha kwa ujumla, na hii yote ni matatizo na ubwanyeneye wa mfumo mzima wa utandawizi ambao unajali faida za wachache tu. Mimi ninachoomba kwa ma mcee wa bongo wasitekwe nakujisahau kule walikotoka, mkipata ma kasri yenu mtaanza kuimba “Uswahilini ndiko nilikotoka, hapa nilipo kimaisha nimeokoka!” au kama Dr DRE “..ve been there done that”, kwahiyo wale mlio waacha siyo watu wenu tena? Mimi nahisi kuna kipindi wananchi walala hoi watasema basi (kwa mtazamo wa kisosholojia zile “fujo” za fiesta ni muonekano mmojawapo): kama kanda zikipanda bei, viingilo kama kwenda kumuona kanda bongo man alipokuja mwanzo, wakati huo huo umasikini unazidi kukithiri nchini (purchasing power inapungua) faida hiyo ndogo wanyoitaka itatoka wapi? Sikuhizi hata kupigiwa muziki redioni mpaka msanii atoe hela tena, hizi njaa gani jamani??????????????????!!!!! Itafutwe njia mbadala ya kuweka shoo ambazo wale wanoimbwa (ambao hapa kwetu wengi ni masikini) waweze kuingia, fiesta iwe nzuri, tuache ubinafsi japo kidogo. Tusibweteke na kale kamsemo ka “sasa hivi BF inalipa! Inamlipa nani? Faida gani? Inamsaidiaje yule mwannchi wa hali ya chini kabisa? Tunawakilisha kwenye M.I.C na kwenye real life je? Swali kubwa la kujiuliza zadi ni je, tunawaburudishaje masikini (kwa bei ambayo ni reasonable) na BF zaidi ya kusikilizwa redioni tu? Sasa kinachotokea ni hicho ambacho kwa mtazamo wa kawaida kinaonekana ni fujo,lakini ni fujo ambazo chanzo chake ni “more complex” ya tunavyodhani, ni resistance ya utandawizi inayokuja kwa picha ya “fujo”.




Ma mcee wa bongo endelezeni moto!

#26 soulrebel

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 6 posts

Posted 27 September 2002 - 11:29 AM

MASELA HIZO NAMBA ZILIZOINGIAINGIA HAPO JUU NI MAKOSA YANGU KIDOGO, NILI TYPE PEMBENI NA KUPASTE NAFIKIRI NI AINA FULANI YA VIRUSII!!! UNAJUA TENA SPIDI ZETU ZA SISIMIZI INABIDI UANDIKIE PEMBENI, MSIZITILIE MAANANI KABISA! SAMAHANI TENA, KAMA J4 UNAWEZA KUZIONDOA TAFADHALI.

MO' FAYA'!

#27 Guest_mr blow_*

  • Guests

Posted 27 September 2002 - 06:10 PM

hi script himechukua one hour kusoma.......... :lol: lakini msikaji umekopi wapi uwo uchafu mzee kwasababu hizo number hazi leti mahana yoyote hile.....aluuuuuuuuuuuuuuuuu

#28 ODB

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 40 posts

Posted 28 September 2002 - 11:46 AM

Aksante SOULREBEL kwa kuwaabalisha hawa jamaa manake hawa jamaa wanataka kutukandamiza tu,ndo maana nilikuwa nakula sahani moja na clouds ambao ndo waandaaji wakuu wa matamasha mengi ya BF
Ni kweli kabisa walalahoi wamesahaulika katika kupewa burudani na matokeo yake hawa jamaa wamebase kwenye financial
Tukumbuke kuwa miaka ya nyuma miaka ya 95,96 nyakati za siku kuu labda ya uhuru na nyinginezo za kiserikali kulikuwa kunafanyika matamasha ya wazi pale Mnazi mmoja na viwanja vya jangwani na wasanii wengi walikuwa wanakuwepo mfano nakumbuka upande wa BF wakati huo kulikuwa na MR 2 ,fun with sense ingawa wakati huo muziki wa dance ndo ulikuwa unashika chat lakini bururdani iliyokuwa inatolewa watu waliifurahia lakini leo hii hakuna matamsha kama hayo tena.
Hivi kwanini Clouds wasiamue wafanye onyesho moja la mwaka labda viwanja vya jangwani?na kiingilio kiwe bure.Hivi watapata hasara gani?kama watapata hasara mbona zamani watu walikuwa wanafanya matamasha ya bure iweje sasa?Mi nadhani wanatakiwa waandae utaratibu na wasanii nadhani hakuna msanii atakae kataaa kupanda jukwaani kuwasuuza washabiki wake eti kisa hawajalipa.
Mi nadhani wasanii nao waagalie ni wapi walikotoka enzi hizo kupanda jukwaani walitakiwa walipe hela na sasa wanapanda jukwaani wanalipwa hela kwa hiyo wasinate saaana
Vile vile umefika wakati wasanii wa BF kuwa na chama chao ili pindi clouds wanapowaitaji au promoa yoyote anapoitaji wasanii anawasiliana na chama chao

#29 Guest_mr blow_*

  • Guests

Posted 02 October 2002 - 04:26 PM

sasa hii topic aina mwisho au......kwasababu fiesta imekwisha lakini ninashanga bado mijito hiko nayo sababa...................mtu anzishe topic . :wink:

#30 ODB

    Advanced Member

  • Members
  • PipPipPip
  • 40 posts

Posted 05 October 2002 - 02:02 PM

we fala naona unawashwa sana unatafuta beef na watu sio?we huku ujalazimishwa kuingia kama mada haikuhusu piga bunda kwanza mi sioni unachochangia huku.Kama vipi tuma topic kama unaona mada haina mwisho watu hatutaki usenge humu.Kama nimekukera basi ajali kazini!

#31 Guest_mr blow_*

  • Guests

Posted 06 October 2002 - 11:55 AM

tangu mwanzo wewe ni kuma tu... :oops:





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users