Sasa baada ya kutafakari nimerudi ili kutoa mchango wangu kwenye huu mjdala.
Napenda kuanzia na kurejea machache toka kwenye mjadala.
Natoa pongezi kwa huu mjadala kuanzishwa, hivyo Tulanongo endeleza moyo huo na tunapata mabadiliko. Kwa dada KHadija nakutakia kila la heri namiradi yenu huko, napenda tu kuonya tuangalie sana suala la UKIMWI kuna watu wanafanya hili janga kuwa ni mradi..Sasa labda tunaweza kuepuka kabisa kutumia jina hilo na kuweka msisitizo na suala la lishe bora na afya ya mwili na masuala ya kinga juu ya maradhi. Imeshafahamika sasa huko Ughaibuni kuwa Ukimwi hauui bali kinachoua ni lishe mbaya, na maradhi yanayoambatana na kukosa kinga nzuri ya maradhi.
Kuhusu Wewe dada hadija kushindwa kuongea kiswhili vizuri, nakushauri ukitumie hicho hicho kidogo ulicho nacho maana huko uliko Arusha uko na watu ambao utahitaji kuongea- Sasa kama wewe sio mwenyeji wa Bongofanya kila namna ujue, kama vile Wabongo wakija Ughaibuni wanavyojitahidi waongee kizungu.
Napenda kuunga mkono mawaidha ya Kwanzini kuhusu asili ya fani ya hiphop. Pia jambo la hawa wadhamini wanaoshikilia fani bila kuwa na upendo nayo. Ningependa kuhitilafiana kidogo kuhusu neno kuiga. Sababu ya kusema hivi ni kwa vile neno kuiga lingependeza wakitumia Warusi, wajerumani wajapani na watu wa makabila mengine yasiyo ya kiafrika wanaoifanya hii fani kwa nguvu- Sisi Wabongo na waafrika wengine ni rahisi kuelewana kifikra kutokana na sababu za kihistoria.
Kuhusu suala la lugha kama KBC alivyosema napenda kusema lugha hasa ndio msingi wenyewe wa utamaduni..heshima mlonayo kina KBC na KWANZA UNIT haitafifia, wala hatuna mashaka na uwezo wenu wa ung'eng'e- lakini mambo aliyoyafanya Ramsoni, Freshi Jii na Zomba ndio hasa kama vitabu vya kujisomea shuleni.. NANI ATADADIDISI NATA!?? HATURAP, MSAFIRI!??? Najua watu wanakua na ile hamu baada ya kujua mawili matatu kwenye lugha ya kigeni- inakuwa taabu tukianza kuisujudia-kama hiphop ni mfumo wa kuelezea hisia, sioni kama inaleta maana yoyote leo watu kule NY wajilazimishe kiswahili- wanaweza kujaribu mara moja moja kama wanaweza, lakini kuifanya ndo' lugha ya taifa ya hii dunia ya hiphop muda wake umeshapita. Niambie inspekta Harun aeleze hisia zake kwa lugha ya kigeni..Sugu aseme yote yale kwenye santuri 8 kwa lugha ya kambo!!!????
Nakumbuka Laurin Hill alipotua Nairobi watu walivyokuwa wakiongea nae aliwauliza swali kwa nini hamuimbi/rapu kwa kutumia lugha yenu!?? Swali liwauma watu wengi wenye hisia kwamba kujua kizungu ndo' kuelimika- sasa mambo yeshabadilika.. Kalamashaka wameleta mapinduzi kenya..Inasikitisha Kuanza Lunginga ndo' kunaanza kupotosha ladha ya kiswahili cha Bongo kwa kutaka kujitia zile za (wasapu wasapu kibao, kina dada nao hai nyingi!!!(USHAMBA TU).
Uingereza walifanikiwa sana kupeleka uharamia wao dunia nzima kwa kutumia lugha yao, sababu hadi leo tuna matatizo pale nyumbani ni kwa vile viongozi bado wamebanwa na minyororo ya kikoloni hawawezi kutoka..Sasa naipongeza jamii ya vijana leo kwa kufanya fani kwa kiswahili. Na kwa kuipa nguvu lugha yetu ndo' tunaweza kupandisha ngazi kwenye vilele vyahadhi ya kimataifa.
Wengine wote wamegusia mambo ya msingi sitaweza kunukuu kila kitu, nnachoweza kufanya ni kutoa sera zangu na tuone tutaanzaje kujenga kwa utekelezaji. Kitu cha awali nnachopenda kuwakilisha hapa ni kwamba inatubidi sisi tuwe na maazimio na kila mmoja wetu atoe mchango wake na hatua inayofuata ni kuanza utekelezaji.
Azimio la kwanza ni kuweka viwango vya uhalisi wa fani, jambo hili tunaweza kuwa na kamati ya watu wanaohakikisha hakuna msanii anayeweza kutoka hadi afikie kiwango kinachokubalika; viwango vitawekwa kulingana na makubaliano kama Loard Soame alivyogusia kuhusu elimu kwa hawa vijana.
Tunaweza kutumia uhuru huu wa mawasiliano kuandika b- pepe za kampeni kwa vichwa halisi wote wanounga mkono HARAKATI zetu na kutuma barua hiyo kwenye wizara ya utamaduni..Maombi yetu kwao yawe na misingi ya UTAMADUNI, hadhi ya Uzalendo na heshima kwa Taifa letu. Kama tunavyojua ndo' kwanza miaka hii wakenya wanaanza kuheshimia kazi zetu tokea zile enzi za kina Mbaraka Mwinshehe; waliyemwacha ateketee. Tunawalazimisha kuanza kupenda tena kiswahili wao hadi Uganda. Huu ni wakati ambao nadhani mzee Garvey, Nkrumah, na wahenga wengine walikuwa wakiutabiri kwa mika mingi. Afrika inaungana bila kuheshimia ile mipaka iliyowekwa na wakoloni, bila nguvu ya wanasiasa.
Nimesikia kuna jamaa wanajiita kamati ya UKOMBOZI wankutana kila mwisho wa wiki kwenye TARISHI, sasa nashauri kufuatilia hao jamaa- kama tutaweza kuunganisha nguvu nao- basi wale wanaoishikilia fani sasa hivi watakuwa mashakani. Maana kwenye vikao hivi ndo' tunaweza kuwaita hawa wasanii na kujenga nao. Tunaweza kuwaita hata baadhi ya watu wa vyombo vya habari ikibidi. Sasa kabla sijaendelea sana kama natoa mhadhara naomba mniambie mnayaonaje haya niliyoyawasilisha kwenu. Amani.
Manyotto Ndimbo
TUNAELEWA VIPI HIPHOP KAMA UTAMDUNI.
Started by Guest_Tulanongo_*, Jun 08 2004 09:45 AM
21 replies to this topic
#21
Posted 18 June 2004 - 06:16 PM
enyi vichwa kusanyikeni, fani iko mashakani
kila wazo laweza kuwa jambo halisi.
Manyotto Ndimbo
kila wazo laweza kuwa jambo halisi.
Manyotto Ndimbo
#22
Posted 10 July 2004 - 03:45 PM
yo I jump of in this mo$%#$$cker, with lots luv to all ho contribute their feelings and understanding, first thing first napenda kukupa heshima
yako K.B.C kama ndio that original one, if somebody else thats another
case. wewe ulikuwa kichwa napenda ku-confesse nilikuwa nakuamini
na nazani bila ya unafiki ulikuwa ni kioo kwa jamii iliyo kuwa inajua
really hip-hop. kuna vichwa vingine kama MR TU, SAIGON, nk, I remind
you one program ulifanya na masoud-masoud on Radio one, those day I was still in bongo ulikuwa na Mc mmoja simkumbuki alikuwa katoka nazani uk. man you were preach what hip-hop iz, nili kusikiliza nikaenda kwa saigon nika mwambia ume sikiliza radio one. akasema nimesikia nika mwambia this dude ana play hate, saigon akasema no he tells the trueth.
Ingawa kuna vitu uli ua kwa chuki binafsi sorry to be true( any way kila mtu ana chuki, woga, upendo na aibu).
nailikuwa nataka kuelezea maana halisi ya hip-hop. nazani tukitafuta defination ya hip-hop tuta chukua siku 365 bila kupata one defination. kwa kuwa imechanganyika na vitu vingi na kuna mambo mengi na watu wengi wanahusika katika utamaduni huo, kama unavyo jua america ni mkusanyiko wa mataifa mengi. lakini naona tukitaka kufika to lenge
sana hip-hop music badala ya culture kwa kuwa kuna tofauti sana ya black america na black african. man they lost thier loots, wame changanyika sana na kwa hiyo kiutamaduni sisi tupo tofauti.
kweli Bongo flavour imeua hip-hop sana kwa kuwa watu walio shika music bongo ni clouds tu. na ndio wanao ua hip-hop sijasikia RADIO ina kuwa na beef na MC.
kwa hiyo kitu cha kwanza ni kutafuta radio nyingine ya vijana ambayo itakuwa mpinzani wa Radio couds FM. tupo wengi
ulaya tuungane tuwekeze kwenye radio inawezekana kwa kuwa wengi wetu tume kuwa na tuna penda music. keep up your heads lads.
anny way naogopa koboa ingawa tayari nimesha boa.

1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users