Jump to content


TUNAELEWA VIPI HIPHOP KAMA UTAMDUNI.


21 replies to this topic

#1 Guest_Tulanongo_*

  • Guests

Posted 08 June 2004 - 09:45 AM

Eh bwana Vichwa halisi wote ningependa kuona tunajumuika kujadili mada hii, maana naamini kwamba italeta mchango mkubwa kwenye kuwafanya watu kuelewa nini na ni yapi mambo ya asili ambayo lazima kujifunza kwanza katika Tamaduni hii ya HIPHOP, kama Umcee [RAPPING], DJ [CUTTING AND SCRATTCHING ETC], Graffit ART, Break DANCE, na Hii kitu sasa inayopewa kipaumbele sana yaani UFAHAMU [KNOWLEDGE] na mambo mengine kama GRIOT na kadhalika.

Binafsi na amini kwamba, kwa kuyazungumza haya tunaweza kuihimarisha Tamaduni hii ya Hiphop na Vile vitu vyake vya asili yaani ELEMENTS nilizozitaja hapo juu.

Hii pia itasaidia kufanya Muziki wa Rap kudumu kama wengi mnavyo onekena mna kiu ya muziki huu ambao ni mmoja ya Tamaduni za Hiphop Kurudi kwenye ile hadhi yake ya zamani na UDUMU, pia kwa kupita mjadala huu na amini tutaweza pia kumjua nani MC na nani HIPHOP. Nini Hiphop na nini RAP. Nani Hiphop na nani si HIPHOP.

Naamini pia yale majukumu ya DJ yatajadiliwa na vitu kadhaa wa kadhaa ili tuu, kuhakikisha kwamba TAMADUNI INAELEWEKA na watu kujua ama kuelewa ni yapi yanahitajika ili tamaduni hii iheshimike na ifuate mikondo yake,.

Pia ningependa kufahamisha wale watu msivamie mada hii kama hauona uweleo mzuri, HIPHOP siyo uvutaji Bangi wala vitende vyovyote viovu, ningependa kuona wale HIP HOP halisi na wenye ile mioyo ya kweli [YENYE DHAMIRA YA KUFANYA UJENZI] Watu tujaribu kuzunga mada zenye ukweli na nia ya kutoa njia yenye kufanya HIPHOP izidi kuheshimika na mapokeo yake yazidi kuwa makubwa,. Kero zizungumzwe na zilenge kutoa ufahamu, haswa kwa hawa wenzetu waliyo vamiia na wenye kuonesha kutokuwa na woleo wa kina ndani ya Tamaduni yetu hii ya HIPHOP ha USWAZI.,

Ismail.

#2 Guest_mkongwe_*

  • Guests

Posted 08 June 2004 - 07:21 PM

yo! tulanongo, ki binafsi nafikiri maada hii ni maada ambayo inatakiwa kupewa kipa umbele cha hali ya juu. Kwani hivi sasa, sanaa pendwa na takatifu imejawa na uovu wa hali juu sana, utakuta mtu anajiita mc wakati hafahamu hata maana ya jina hili mc lina maana gani. Nafikiri kuna haja kubwa ya kuelimisha jamii na kuachana na mambo ya kufikiri hip hop ni kuvaa mavazi mapana, na madini shingoni la hasha.



Harambeeee lets pul it together

#3 Guest_khadija_*

  • Guests

Posted 09 June 2004 - 04:43 AM

peace brothers/sisters
my swahili is really bad, but i just wanted to big up what you were writing about. Hip hop is a lifestyle and a philosophy that should be respected. It has nothing to do with what is shown on commercial TV and I like best what you said about Hip Hop being about building , ujenzi.
I m working on a project right now which will be started in Arusha in October of this year, where we invite hip hop crews to ORGANIZE themselves to be real builders in their communities. We ll be providing trainings and workshops on various forms community organizing and asking the hip hop crews to take these skills to their communities to address vital issues such as HIV/AIDS, lack of education, poverty, homelessness, etc. Its about time African youth RISE UP and use our skills, and talents in a REAL WAY. If youre interested in finding out more information about this project, drop me an email at dida015@hotmail.com
Peace
Khadija

#4 Guest_Bahati_*

  • Guests

Posted 09 June 2004 - 06:00 AM

Sawa sawa mzee Tulanongo, Mkongwe na Khadija..Mimi kwa mtizamo wangu naona ingekuwa ni vyema tufahamu utamaduni ni nini kwa kina kabla ya watu kueleze uelewo wao katika hilo.
Nasema hivi ili kama mtu atakuwa anaenda kinyume na dhana halisi ya hili neno utamaduni basi iwe ni rahisi kumbaini. Kuna baadhi ya watu wakiona forum wanataka tu kuchangia hata kama ufahamu wao ni finyu.
Sio kwamba najisemea tu, maada hii ni nzito na pana mno ambayo inahitaji elimu zote mbili, ya shule na mtaa. Kama alivyosema Tulanongo tuwe makini na sio blah blah tu tukaishia kupoteza muelekeo.
Kusema utamaduni ni jinsi vile bibaadamu anaishi, inatosha sana, lakini bila ufafanuzi wa kina inaleta utata vivyo hivyo kwa hip hop kama utamaduni.

Bahati

#5 Guest_Tulanongo.._*

  • Guests

Posted 09 June 2004 - 02:57 PM

All HIP HOP Holla !! yeah big up 2u Khadija.. and what you said about hiphop it's all true, my pray is for your success and God bless your PROJECT , I truly I appreacite all what u said about HIPHOP, Lifestyle let me add somethi' here : with it's on language, stlye of dressin' music and mind set,. Ooh PROJECT?? that is SUPERB Babe! and that's part of KNOWLEDGE I was talkin about.

Please don't worry about writting in English Because I am sure someother Hiphop they will Understand you as well as all other Visitors. I only decided to use kiswahili because of winnin' majority understandin' and participant. We just need all ma homies to GET SOMETHING EASLY.

Bahati na Mkongwe Amini Mazee.. Nimependa sana jinsi mlivyoanza kutoa michango yenu na amini tupo watu wenye nia ya kuendelea na huu mdahalo kwa dhamira ile ya UJENZI Siyoo tuu kuvamia mada. Ili tujenge ningependa kuona watu tunafanya na mauchambuzi fulani kidogo katika mazungumzo yetu, yaani kama pale mkongwe uliposema MCEE basi unakuwa unashusha na maufahamu yako juu ya nini Umcee.

Amani.

#6 Guest_KBC_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 03:26 AM

SAlaaM SALaam VICHWA HIPHOP!!

First and Fore Most..Alots of thanx to that ladt KHADIJA..for your Efforts
of spreading AWERENESS to our Tanzanians Young Ones..
AIDS is REAL...but most people would avoid the RESPONSIBILITY of
PREVENTING the lost of more Lives...cos its not a FUN JOB TO DO...
so we rather be Accountant,Businessmen,..or Whatever!!
SO Thank yu KHADIJA and everybody else who is on da FOREFRONT of this Battle..
NOW BACK to HIPHOP CULTURE..
wazee naona mmechoshwa na UONGO wa vyombo vya HABARI..
Mara nyingi watu huniuliza maswali kuhusu My opinion on HIPHOP ..
Especially in BONGO..Majibu ambayo niliwapa ni kwamba BONGO FLAVA
imeiUA HIPHOP in BONGO!!...hawakunielewa...
Wengi HUFIkiri...Mimi Nina CHUKI na wale walio CHUMA kutokana na
BONGO FLAVA...which is not True!!
WATOTO SIKU HIZI HAWAJUI HIPHOP...
WANAFIKIRI BONGO FLAVA NI HIPHOP...NOOOOO!!
Bongo Flava is just a NEW type of URBAN BONGO music..
It just USES ONE of da HIPHOP Elements....To ROC da MIC in SWAHILI
NOW THAT DOESN'T NESSESARILY MAKES IT HIPHOP...

BUT WHO IS GONNA TEACH THESE KIDs DA TRUTH???
RADIO?....PROMOTERS??...wahindi??...
HEBU NIAMBIENI....RADIO ARE FIGHTING AGAINST REAL HIPHOP!!

#7 Guest_mkongwe_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 12:27 PM

Yo! KBC i am with u 10000000%, I remember those good old days, when Tanzania Hip hop was good. Unfortunately we lost some of the tightest mcs in the Game i.e Adil "Niger one" and Zomba rest in peace hommies, with Bonie love spinning them vinyls at New africa hotel ghorofa ya saba. But still we got cat like ur self KIBACHA if i am correct can still push the Tanzania hip hop wheels to the recognisition. Nafikiri jambo la kufanya kwa sasa, ili tuiokoe fani na tujiendeleze kisanaa ni kupata watu waliokuwepo mwanzo kipindi kile hip hop ya bongo ilivyokuwa na kufanya WORKSHOP NYINGI tu na tujitume wenyewe instead of sitting down and watch tamaduni inakufa. Fuck the media (ma' bad) but I have to express my hunger. I think we should have a lot of real hip hop shows in around Tanzania, lakini tusifikirie sana mambo ya pesa kwa sasa. Kwani penye nia njia upatikana.

Amani na upendo

#8 Guest_Bahati_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 12:37 PM

Nakubaliana na KBC kuwa kwa fleva sio local hip hop bali ni mkusanyiko wa aina mbali mbali za muziki ambazo hapo awali hatukuwa nazo,na wengine wanaita ni muziki wa kizazi kipya,nakubaliana nao
Kama ntakuwa sikosei, ujio wa muziki wa hip hop hapa nchini(local hip hop) ulikuja kwa mshindo mkuu mara baada ya kuanzishwa kwa FM stations.Kabla ya hapo ulikuwa ni kwenye matamasha. Katika hali ya kuupokea na kuibariki local hip hop kama sanaa yetu, neno bongo fleva likatumika. Ikumbukwe kwamba siku hizo bongo fleva ilikuwa mostly ni hip hop maana miziki mingine imekuja kuwa maarafu baadae. Reggae ilikuwepo lakini katu haikuitwa bongo fleva.
Ujio wa miziki hii mingine ullingia ukiwa umegubikwa na wingu nene la jina bongo fleva kiasi kwamba nayo ikajikuta inaitwa bongo fleva!! Watu wa media, radiO na magazeti hawakuwa makini kuweka mambo sawa, kipi ni kipi. Lakini hali iko wazi kwamba now bongo fleva ni kitu kingine kabisa..na si local hip hop tena....
Upotoshwaji mkuu niliouona mimi ni lile shindano la mfalme wa Rhymes!!! najua rhyme ni part ya hip hop, how comes RnB singers wanashiriki?Dancehall????
Mi nadhani ilifaa iitwe mfalme wa bongo fleva!!! n way, nikirudi kwa KBC, wale watu wa radio na magazeti ndio pekee wanaweza toa elimu ya hip hop kwa vijana wapya..vinginevyo wataendelea na hii hali wakijua kuwa wako sahihi wakati sio..wachache wapo wanajitahidi, wengi wanapotoka wakishauriwa na local producers, watangazaji nk, anything thats real hip hop radio hazipigi kabisa..nahao ndo wanaweza kuwafikia watu wengi kwa maramoja...inatisha!!
Ni watu wacheche mno walioko kwenye media wanaujua ukweli juu ya hip hop kama culture achilia mbali some elements ambazo wao wanziintertain!! kama afro hits wanapata 3hrs air play, kwanini kusiwe na program kama hiyo kwaajili ya real hip hop na si bongo fleva!!!! watu wenye upeo wapewe nafsi wajadili, wafanye mfamo wa nini kinatakiwa...
....nashangaa sana mcee ana-freestyle wimbo wa kwenye albam!!!! is this a real fee style??? where are metaphors??? vina vina....hip hop si vina tu kuna mengi>>>kOreKt If Im wRoNg!!!!


Bahati

#9 Guest_Sikunne-Saanne_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 06:44 PM

Nashukuru sana kwa hii Mada tukufu iliyoanzishwa na Bwana Tulanongo na kuchangiwa vizuri na wengine. Nafikiri hili suala ni zito na linaitaji kuwekewa kipaumbele na njia kubwa itakayowezesha mafanikio ni kuunda kikosi cha kuokoa sanaa (KCKS) na kuanzisha midahalo mbalimbali ndani ya huu mtandao pamoja na kupanga mikakati ya kushambulia vyombo mbalimbali vya habari na kuwasilisha mada zetu.

Kwa kifupi kwasababu sitaki kuandika mengi sana humu, ni kwamba hakuna Hiphop bongo.Hiphop ipo lakini imefichwa sana na hawa hawa majangili wachache ambao wanajaribu kuua sanaa wakijifanya wao ndio wanaojenga. Hawa hawa wachache wanaovimbisha matumbo huku vichwa halisi wakipiga miayo ndio ambao tunatakiwa tuwapige vita. Natoa changamoto na kuwasihi vichwa wote ambao wako tayari kwa mapinduzi ya kweli ya hii sanaa kuanza kupanga mikakati ya kuungana na kuanza rasmi kazi hii kubwa ya kung'oa huu uozo mkubwa uliotia wingu la uvundo ndani ya sanaa hii yetu muhimu yahiphop. Uozo huu unajulikana kama 'Bongo Flava'. Hii ndio sumu yenyewe. Ukisikiliza kazi za wakongwe na waanzilishi wa sanaa hii 'KWANZA UNIT' hilo neno halijawahi kutumika hata siku moja! Nani alisema Hiphop ni bongo flava? nani alianzisha hili neno?
Tangu lini kuwe na mfalme wa rhymes wakati hakuna hata mshindani anayeelewa 'rhyme-structure? Nani aliandika vipengele vya kuchagua mshindi na je aliyeandika au walioandika wana uzoefu gani na HIPHOP? sitaki kusikia majina ya majaji kwasababu niliyasoma, nachouliza ni NANI kaandika vipengele? kama ndio hao hao majaji basi kweli hii sanaa iko kwenye hali ya hatari!
Naomba nimalize hapo lakini tunaitaji watu wengi wenye mapenzi na hii sanaa kuingia humu na kutoa changamoto la kweli. Nguvu ni Umoja! (nimeanza na Nguvu kwasababu inaitajika nguvu kwenye umoja tutakaoujenga). Asante kwa kusoma mawazo yangu.

#10 Guest_gr8kwanzini_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 11:07 PM

swali zuri sana. nakubaliana na bahati, kusema kwanza tungeangalia kwa kina maana ya "utamaduni." halafu swali langu ni, je tukisema hip hop tuna maana gani au tunaijua maana na asili yake?

ninavyoona kila siku ni kwamba wengi wetu tunafuata mkumbo tu bila kujua tunafanya nini, ili mradi kitu au jambo fulani ndiyo mtindo uliowiva kwa wakati tunaouzungumzia. kwa mfano, ni kweli kwamba wanaozoza au kusema (rappers) kwa kutumia fani ya hip hop kama chombo (media) wana ujumbe au usongo ambao wanataka kuuweka uwanjani kwa lugha ya kiswahili, lakini ukweli bado uko pale pale kwamba ni fani au style ya muziki ambayo tumeiga. nataka kusema tungeitumia hip hop lakini pia tuongeze ufundi mwingine ili iwe 'yetu'. yaani isiwe tu tunatumia midundo ya kimarekani (funk na mipigo mingine mizito ya "kinywamwezi" au phat beats) lakini tuchanganye kidogo na mipigo ya "kinyumbani." kwa mfano, juzi juzi niliusikia muziki fulani wa ki-hip hop au bongo flava new york lakini mtunzi ni mkali wa toka unguja, ambaye alitia madoido ya mahadhi ya taarabu kichati, kiasi kwamba muziki ulinifurahisha na kunivutia zaidi. hii ni pembe mojawapo tunayoweza kuiangalia huku tukijiuliza hili swali la kuhusu hip hop kama utamaduni. yaani pia tuangalie jinsi ya kupanua muelekeo wa hii fani ili isiwe tu inaburudisha lakini pia inatufunza na tunafunza wengine kitu fulani, huku tkiognezea mitindi au ala zetu. kama wanavyofanya ndakaru (au dakar), senegal ambako ma-rapper wake wanatumia lugha yao ya kiwolof na kimandingo na vyombo kama vile ngoma za tama, wakati waki-rap au kutumbuiza kwa style ya dance hall (jamaica) au banghra (uk-mchanganyiko wa ngoma za kihindi na reggae na dance-hall style).

wasanii wengi wa hip hop marekani, akiwemo common, talib kweli na the roots, wanalalamika kwamba hip hop imepoteza nguvu zake za zamani, enzi zile ulipokuwa muziki wa kichini chini (underground). kila msanii wa hip hop anadai kuwa anawasilisha na kusema ukweli kama ulivyo bila kuficha (representin'/keepin' it real). ukweli ni kwamba hip hop ni biashara nzuri sana hivi sasa - marekani inaingiza dola bilioni 10 kwa mwaka. (swali ni je, nani anayepata pesa hizo?) hivyo ni rahisi kuona jinsi gani kila mtu anataka apate ulaji na kipande cha hii keki ya hip hop, hata kama hana la maana la kusema. ndiyo sababu kadiri muziki unavyokuwa na matusi na kuzungumzia matumizi ya silaha, kuua na uchimvi ndiyo unavyouzika zaidi.

jijuwe we nani.

#11 Guest_gr8kwanzini_*

  • Guests

Posted 10 June 2004 - 11:13 PM

swali zuri sana. nakubaliana na bahati, kusema kwanza tungeangalia kwa kina maana ya "utamaduni." halafu swali langu ni, je tukisema hip hop tuna maana gani au tunaijua maana na asili yake?

ninavyoona kila siku ni kwamba wengi wetu tunafuata mkumbo tu bila kujua tunafanya nini, ili mradi kitu au jambo fulani ndiyo mtindo uliowiva kwa wakati tunaouzungumzia. kwa mfano, ni kweli kwamba wanaozoza au kusema (rappers) kwa kutumia fani ya hip hop kama chombo (media) wana ujumbe au usongo ambao wanataka kuuweka uwanjani kwa lugha ya kiswahili, lakini ukweli bado uko pale pale kwamba ni fani au style ya muziki ambayo tumeiga. nataka kusema tungeitumia hip hop lakini pia tuongeze ufundi mwingine ili iwe 'yetu'. yaani isiwe tu tunatumia midundo ya kimarekani (funk na mipigo mingine mizito ya "kinywamwezi" au phat beats) lakini tuchanganye kidogo na mipigo ya "kinyumbani." kwa mfano, juzi juzi niliusikia muziki fulani wa ki-hip hop au bongo flava new york lakini mtunzi ni mkali wa toka unguja, ambaye alitia madoido ya mahadhi ya taarabu kichati, kiasi kwamba muziki ulinifurahisha na kunivutia zaidi. hii ni pembe mojawapo tunayoweza kuiangalia huku tukijiuliza hili swali la kuhusu hip hop kama utamaduni. yaani pia tuangalie jinsi ya kupanua muelekeo wa hii fani ili isiwe tu inaburudisha lakini pia inatufunza na tunafunza wengine kitu fulani, huku tukiongezea mitindo au ala zetu. kama wanavyofanya ndakaru (au dakar), senegal ambako ma-rapper wake wanatumia lugha yao ya kiwolof na kimandingo na vyombo kama vile ngoma za tama, wakati waki-rap au kutumbuiza kwa style ya dance hall (jamaica) au banghra (uk-mchanganyiko wa ngoma za kihindi na reggae na dance-hall style).

wasanii wengi wa hip hop marekani, akiwemo common, talib kweli na the roots, wanalalamika kwamba hip hop imepoteza nguvu zake za zamani, enzi zile ulipokuwa muziki wa kichini chini (underground). kila msanii wa hip hop anadai kuwa anawasilisha na kusema ukweli kama ulivyo bila kuficha (representin'/keepin' it real). ukweli ni kwamba hip hop ni biashara nzuri sana hivi sasa - marekani inaingiza dola bilioni 10 kwa mwaka. (swali ni je, nani anayepata pesa hizo?) hivyo ni rahisi kuona jinsi gani kila mtu anataka apate ulaji na kipande cha hii keki ya hip hop, hata kama hana la maana la kusema. ndiyo sababu kadiri muziki unavyokuwa na matusi na kuzungumzia matumizi ya silaha, kuua na uchimvi ndiyo unavyouzika zaidi.

jijuwe we nani.

#12 Guest_KBC_*

  • Guests

Posted 11 June 2004 - 08:00 AM

Sasa Wazee...naona mna machungu mengi,
lakini itabidi mchague Ajenda gani mnataka ICHAMBULIWE..
Maanake ubora wa utamaduni wa Hiphop ni kitu kimoja
Na Biashara ya HIPHOP ni JAMBO lingine Tofauti...TUSICHANGANYE..

Kuhusu uchanganyaji wa muziki wa REAL HIPHOP na Vionjo vya Nyumbani
TUMBA,ZEZE,TAARAB..DANSI,MNANDA..n.k. SIO TATIZO..
As long as they Do it THE RIGHT WAY..mfano mzuri MSAFIRI -Kwanza Unit
Produced By RHYMSON...DR.DRE did it...TIMBALAND did it..
VIONJO vya Muziki havibadilishi...MANDHARI YA HIPHOP..
IF DA HIPHOP ESSENCE REIMAINS THE SAME...
i've heard a song by PETE ROCK...yenye vionjo vya KENGELE ZA NG'OMBE...na midundo ya ngoma za KiafriKa..Lakini da Emcee still
KeepS It HIHOP...TONY TOUCH and DA BEATNUTs always uses alot
of SPANISH samples...But still Keeps it HIPHOP...
NA LUGHA SIO TATIZO KABISA...

SASA IMEKUWAJE WANASHINDWA TO KEEP IT HIPHOP IN BONGO??
i 'll tell yu WHY...
VIONJO vipo Kiibao
MAPRODUCER...Wapo lakini Wengi ni Wavizu..halafu Hawajui HIPHOP
hata wale Wanaoijua...They Love Money more than
HIPHOP...
MAPROMOTA....they dont care about musik...if mo people go see taarab
They'll put their money in Taarab..(no Disrespek)
EMCEEz...........Very Few left,..Too many LAAPPAzz Nowadays

MEDIA.............has already been poisoned...so they PASS the Poison
its like hiphop left the RADIOs and TVs as soon as KBC
and RHYMSON left Clouds and ITV ...
DEEJAYs..........BonnyLUV plays at BLUE PALMs Once a week
NOT HIPHOP....he plays OLDIES..

MAYBE WE NEED TO DO A REASEARCH ON HOW MANY PEOPLE WUD
VOTE FOR REAL BONGO HIPHOP...English+KiswaCentriK...AGAIN

AND HAVE A POLL ON EVERY BONGO WEBSITE...AND THEN WE KNOW WHAT WE WORKING WITH....
OR MAYBE GIVE THEM A CHALLENGE...HIPHOP VS BONGOFLAVA..

..AU WAZEE MNASEMAJE....
RA uKO WAAPI???.....GET OUT OF THAT STUDIIOO...

I HOOOLLA!!
KBC..

#13 Guest_Sembe_*

  • Guests

Posted 11 June 2004 - 11:15 AM

test

#14 tulanongo

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 11 June 2004 - 05:21 PM

Hayoo ndiyo mambo.. Kwanza kabisaa nashukuru kuona vile vichwa Halisi vya hiphop kujitokeza katika mswaada huu, nimefurahi kuona Hiphop kama KBC kushirikiana nasi katika ile dhamira ya UJENZI, Pongeze sana kwa hilo na tunahitaji watu zaidi, hususani Wakongwe kama nyinyi katika tamaduni hii ya hiphop.

Pia ningependa kuwashukuru ndugu zangu wote mliongia na kutoa maoni yenu, nawaita ndugu maana naamini wote nyie ni Hiphop. Sikunne Saanne na GR8Kwanzini shukurani zangu ziwafikie, hili jina la siku nne saa nne nimejaribu kulitafakari kwa haraka naona napata Jibu la Mkongwe fulani wa sanaa hii [Hizi ni zile Metaphor alizozitaja Mgeni Bahati tena hii ni ya hali ya juu] sasa sijui kama ndiye yule nayemfahamu mimi ama lah, kama ni wewe na amini unanifahamu, basi nifahamishi tuu km ni wewe, naona mzee ungali bado unaendeleza Ubunifu ambao kwa mimi niliyewahi kukutana nawe mara chache falagha ningependa jamii iige au ijufunze katika yale uliojaaliwa na Muumba. Laiti kama ndiye basi mada imepata watu wake.

Haya jamaa, ningependa tuu niwakumbushe pia, kuwa MUZIKI wa RAP ni sehemu tuu ya Tamaduni hii ya Hiphop, naona wengi mmelalia kwenye Muziki ambako ndiye kwenye KERO nyingi kulingana na zile sehemu nyingine, hilo silikatai na nadhani hili ni pana zaidi na nakubalina nanyi kabisaa kwamba sehemu kubwa iliyoathirika na yenye kuhitaji kuhimarika ni hapa kwenye muziki ambapo ndiyo kama MEDIA yetu kama alivyosema GR8Kwanzini, ila ningependa kuwakumbusha tuziguse na zile anga nyingine pia.

KBC naona umemuita Ra, Jina nadhani ndilo RHYMSON analitumia, pia nitafurahi kumuona akijumuika hapa, huku Bongo tumebahatika kusikia baadhi ya nyimbo zake zilizomo ndani ya Santuri yake ya JICHO LAKE, binafsi nampa pongezi sanaa, na hapa naweza kusema kweli MEDIA zinapaswa kupewa lawama, ufanisi alioonesha katika TENZI zake Binafsi ulinigusa sana, na hii inanifanya nizidi kuamini ni bado sana kwa wasanii wapya kuichukua ile heshima ya KWANZA UNIT. Ndani ya zile nyimbo mbili za utambulisho kuna balaa kubwa ambalo nakiri kusema wasanii wa sasa waanapaswa kujifunza mengi kutoka mule, hususani katika kuandaa TENZI ama LYRICS zao. Mshafti kwako Mjeshi Rhymson.

Niliudhunika kusoma Habari zako humu african hiphop bila kusikia zile nyimbo zako, sasa sijui kama zilifika katika Media zetu za hapa Uswazi, hususani kwenye redio.

Katika kutoa kero zangu, mimi naona kwamba Tamaduni yetu hii ya HIPHOP kwa uvivu na ukosefu wa ufahamu ndani ya Media Hususani Radio na Magazeti, wengi wanashabikia zaidi kuandikia na kuzungumza pasi na uelewo juu ya wanachokifanya. Inanikera pia kuona watu wanachanganya BONGO FLEVA na HIPHOP. Nadhani sasa wakati umefika wa kurekebisha jamii. Najua wapo watu kutoka media tofauti tofauti wataanza kufuatilia habari hii, pia ningependa kuwaomba watokapo kusoma habari hii basi wabadili muelekeo wao wa uandishi na utangazaji, na wanapowafanyia mahojiano hao wasanii wawe wadadisi zaidi, ili waweze kutofautisha yupi ni hiphop na yupi ni mbongo fleva na pia waijenge jamii juu ya swala hili na wasitishe upotoshaji.

GR8Kwanzini nakukubalia kama alivyokukubalia KBC kazi hiyo inawezekani iwapo tuu MC hatobadili na madhari ya HIPHOP. Hii ni kazi kubwa ambayo wataarishaji wanapaswa kuifanyia kazi na mambo yakabadilika.

SOKO na MALIPO kwa Rapper yeyote ni swala la kuliweekea Msingi, Ila soko hili linapotafutwa katika misingi ya Kiuvivu na kuipotosha jamii na kuandaa jamii ya Mafuska nahakika baada muda kutakuwa na madhara makubwa mno. Watu wanaimba mambo hata yasiyo fanana na maisha yao, hii inaudhunisha sana, watu wanaimba Mapenzi bila mipaka na Media zinazo tegemewa kueleimisha jamii zinazidunda tuu kwenye masafaa!! Jamani hii tunajenga ama tuna bomoa?.

Mimi nadhani media sasa zinahitaji kubadilika na Ma Dj wao kutimiza wajibu, simulizi za kujenga Hiphop na Jamii zinahitajika kwenye hizi redio [GRIOT] ili muziki upate nafasi ya kujenga jamii. Tunahitaji watu kama akina Kaka Masoud Masoud/ Kunakazi iliwahi kufanywa na KBC pamoja na RHYMSON siwezi kuisahamu, watu kama hawa wanahitajika warudi kufanyakazi na ma mc wabadilike wajijue wao ni nani, MC aliye kamili ni lazima atajihisi yeye kama MJUMBE aliyepaswa kujenga jamii yake. Na si vingine, atuburudishe na kisha atuelimisha.

Uchungu na uzuni niliyo nao siwezi kuumaliza kwa leo hii. Wale wote walio na dhamira ya UJENZI nia ya kuleta UKOMBOZI basi naomba tujumuike uwanjani hapa.

Kila lakheri wakuu!!.

#15 Sikunne-Saanne

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 1 posts

Posted 11 June 2004 - 09:45 PM

Sasa naona hii Mada iliyoanzishwa na bidii kubwa ya bwana Tulanongo inapamba moto sawia.Hii inadhihirisha wazi kwamba wakereketwa wa hii sanaa bado wako hai na tayari kwa mapambano.Hii inanipa furaha kubwa sana moyoni sio utani.Hapa naandika hii wakati Mhandisi wangu wa mitambo ya sauti studio anaandaa mambo tayari kwa recording session ya nguvu usiku wote.Mawazo yenu wanahiphop yatakuwa nami niingiapo kwenye chumba cha vocals na nafikiri siku itafika kazi itakuja kusikika hata kama wenye redio wakifanya njama za kubana.

Nafikiri cha msingi ni kuendeleza tu juhudi. Ni kweli kwamba rap ni kipengele tu kimojawapo na ni sawa kabisa kwamba inafaa tuangaze macho kwa vipengele vyote vilivyopo ndani ya sanaa hii. Dada anayepanga Warsha ya sanaa Arusha nakutakia mafanikio mema sana nafikiri mchango wako ni bora zaidi ya hawa wanaopata majina na ujiko bila kuwa na mapenzi yoyote kwa sanaa hii. Moyo wangu unafurahi sana kusikia kazi za wasanii kama Ra ambao hawafanyi hii kutafuta hela au ujiko bali kwa mapenzi tu ya sanaa. KBC nafurahi kukuona humu ndani maana wewe ndio mkongwe hasaa kwenye hii sanaa.

Bwana Tulanongo kama umeweza kuchambua hili jina na kujua ni nani basi hakuna shaka kwamba upeo wako wa uchambuzi na ufumbuaji mafumbo uko juu sana.Naomba nikupe pongezi kubwa ingawa sina uhakika kama umdhaniaye ndiye. Amani na upendo kwa wote.

#16 Lord Soames

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 12 June 2004 - 09:23 PM

Amani iwe nanyi wapenzi wote wa Hip Hop popote mlipo.

Kwanza ningependa kutoa maoni yangu wa Webmaster/ Designer wa hii website. Ukiandika text yoyote kwenye hii page kisha uka-press Esc kwa bahati mbaya inakuwa umefuta kila kitu. Imenitokea hapa baada ya kuandika maoni yangu kwa zaidi ya 45 minutes, kufumba na kufumbua vyote niliyoyaandika yameyeyuka. Tafadhali rekebisha scripts kwa manufaa ya wengine.

Salam kwa Chief Ismail aliyenidondoshea barua pepe na kunijulisha kuhusu huu mjadala. Nikiwa kama mwana hip hop ni wajibu kuchangia maoni yangu, na hivyo basi yanakuja kama ifuatavyo.

Naona kabla ya yote ni muhimu kukubali kuwa hip hop inakua na kubadilika the world over. Ukiangalia since 1970’s Grand Master Flash, Sugar Hill na wengine walikuwa na style tofauti kabisa kulinganisha na NWA miaka ya 1980’s. MC Hammer and Puffy (Diddy) came along in the 1990’s na kuendeleza mabadiliko hayo, 2000’s kuna kina Nelly, Eve na wengine, history will tell. Kwa mwendo huu naona tukubaliane kuwa kila kitu kinabadilika kufuatana na muda, as much as I DISLIKE bongo flavour, naona nikubali tu kuwa hayo nayo ni mwendelezo wa hayo mabadiliko kama nilivyoeleza.

Hoja nyingine ni kuwa Hip Hop ni UTAMADUNI, na kama ilivyo tamaduni yoyote huwa inakuzwa au kuendelezwa na watu wenye sauti na nafasi (influence) katika jamii husika. Katika jamii ya Hip Hop watu hawa wenye sauti na nafasi ni mapromota (wasiojua/wala kujali nini maana ya Hip Hop), radio Station owners (wanaopenda hela zaidi ya Hip Hop) na radio Dj’s wanaotaka umaarufu kwa ku-support music bila kujali kama ni Hip Hop au Bongo Flavour etc. Hawa ndio watu wanaoshikilia kioo cha Hip Hop katika jamii, bila ya haya makundi kubadilika safari itakuwa ngumu sana.

Solution: Wasanii wa Hip Hop lazima waelimishwe kuhusu hizo Elements 5, wajue kuwa hip hop ni zaidi ya ku-rap na kuvaa jeans kubwa, ni zaidi ya kuvuta bangi, ni zaidi ya kutoa wimbo redioni. Hip Hip ni mimi na wewe kila utakapokuwa kama una jeans over size, unaenda college, una elimisha wadogo zetu kuhusu madhara ya bangi na Aids, unanunua LEGAL copy ya REAL hip hop album, unahudhuria tamasha la REAL hip hop, unatoa maoni yenye nia ya kujenga hip hop, kwenye jumuia za wana hip hop n.k Hiyo ndio Hip Hop. Kama Rhymson na D’Rob (RIP) walivyosema “Sis Wasafiri Bado Tupo Njiani, Sijui lini Tutafika”

Kila la kheri

Lord Soames.

#17 tulanongo

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 13 June 2004 - 12:44 PM

yeah yeah nimerudi tena..

Lord Soames nimependezwa kuona umetoa maoni yako, mabadiliko yapo katika kila Tamduni, sikatai yatatoke tuu kwa sababu Hiphop inaishi. Lakini Bongo Fleva ni zao jingine tuu la muziki ambalo si Hiphop, Ningependa pia tuzungumzie yaani yale mambo yetu ya Breakdancing, DJing, Beat-boxing, MCing, Graffit Art, Knowledge,Trade na Fashion. Lakini katu tusikubali mabadiliko haya yaondoe mandhari ya Hiphop na kwa mtazamo wangu tuu Bongo Fleva si Hiphop kabisaa, Hiki ni kitu kingine ambacho kimetoke sehemu nyingi duniani. Kwangu naona Bongo Fleva ni kama zao, na kuna kipindi Mkongwe KRS One aliwahi kusema kwamba kufaninisha hiphop na zao ni sawa na Utumwa.. hapa alikuwa akihojiwa na Mhandishi mmoja wa habari anayejulikana kama Nathan RABIN.

Mfano: Tazama pale Pouerto Rico, kwa wasanii wapya kama akina Don Chezan, yeye ameunganisha vionjo tofauti ukiwemo Rap na lakini hapakazii kama anafanya RAP.. na wapo wasanii kama Tego Calderon kutoka kule kule Puerto Rico yeye amechangana salsa na bambo katika Rap zake lakini mazingira ya Hiphop yapo pale pale na kumfanikisha kuuza nakala laki moja ndani ya nchi yake. Pia unaweza kutazama wasanii kama Kwanza Unit walivyofanya katika msafiri nk kama alivyosema KBC na pia tazama kama X-PLASTAZ wanavyo mudu kutengeneza ma mix fulani na kubakisha mazingira ya ki Hiphop kitu amvbacho kimewasaidia kufanya mauzo mpaka nje ya nchi. Kwahiyo naona ni bora kutazama ni mabadiliko gani ya kayakubali na kukataa.

Maoini yangu kwa ma hiphop wote wa Bongo wawe mstari wa mbele kupinga Muziki wa Hiphop kuitwa Bongo Fleva hii ni moja ya vitu vinavyo changia kusahaulika kwa Hiphop ya Tanzania [BONGO].

Watu wa MEDIA wao ndiyo kigezo, laiti kama kweli hiphop wote tunataka mabadiliko basi hakuna budi kubadilika na kufanya mapinduzi kwenye nyanja zote kuanzia pale ulipo., Km wewe ni Hiphop na upo kwenye media jiulize unachangia nini kwenye hiphop.. na kama wewe ni mfanyabiashara jiulize unachangia nini kila mmoja ajiulize kutoka kwa yeye alipo, Hiphop si muziki tuu jamanii jiulize kwanini unapenda Hiphop na una ielewa vipi hiphop.,

Wasanii wa Rap nyinyi sasa ndiyo kama MEDIA hususani kipindi hiki.. na yeyote aliye Hiphop ni lazima ajiulize je mimi naishi kama Hiphop yaani kuanzia kutoa tafsiri na kila kitu : hapa namaanisha kwamba je jikague unaishi vipi na unatoa picha gani kwa watu juu ya tamaduni hii ya Hiphop? Uhuni wako au Busara zako ndizo zina athiri jamii.

Wewe MCee unajua nini juu ya Ume cee au maswala ya ujiko tuu na kujitafutia pesa kwa kuipakazia Hiphop.. Jamani tunapenda wote tuwe Hiphop lakini kama wewe na sisi ma hiphop tunahitaji kuelimishwa na kuburudishwa na muziki wetu lakini siyo kuona leo watoto wetu na wadogo zetu kupotoshwa.. Mtazameni Mzee wetu KK alifanya nini siku ile pale DIMOND JUBilee katika kuchangia mfuko wa chuoo cha kiislamu.. aliimbisha watu I CAN.. Ile ile ya Nas Escoba, yote tuu kwa sababu ya Ujumbe ulikatika nyimbo ile na ndiyo maana kaijua mpaka kuiimba,.

Tunahitaji mabadiliko jamaa la sivyo huko tuendako tutakuja kuona jinsi hii Hiphop itakayo tuadhibu kwa kuto ipa heshima na adhi yake.

Kila lakheri wakuu... na pia wale wenye maoni na kushindwa wanapenda kuzungumza nami faragha basi.. mnaweza kunshushia barua pepe hapa: tulanongo@hotmail.com nakaribisha wale tuu wenye dhamira ya UJENZI.

Tulanongo..

#18 gr8kwanzini

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 14 June 2004 - 11:42 PM

kbc, umesema kwa uzito sana, yet again.
nadhani tungeanzia kwenye kufafanua chanzo na maana ya hip hop. na kufananisha au kuonyesha kinachotofautisha hip hop na bongo flava. nionavyo mimi ni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana watu wengi, wakiwemo wasanii wanaojiita wana hip hop pale bongo, hawaelewi maana ya mc au anachokifanya kwenye 'context' ya hip hop. inavyoonekana wengi wamo wamo tu kwa ajili ya pesa, kuliko usanii na kundeleza ubunifu wao. yaani hawana la kusema bali wanalopoka lolote lile mradi wana midundo mikali inayovutia (catchy beats and phrases).

pia tusisahau wadhamini au wafadhili, kama ni mwenye studio au kibopa mwenye magoto (nadhani wadosi wadosi wengi wamo kwenye mkumbo huu). wao wanachojali ni kwamba muziki utauzika (au jina lao litatajwa kwenye wimbo au kuweko kwenye cd au cassatte, kama wanavyofanya nchi nyingine). hawajali sana kiwango cha muziki au ufundi wa kutunga. wasanii wengi wapya hawana ile busara ya kusema au kujua kuwa; "if you have nothing to say better to stay quiet than open your mouth to remove all doubt." kwa maneno mengine, kama huna la kusema afadhali ukae kimya kuliko ukifungua mdomo na kubolonga

nina maana ya kusema watu watumie busara ya kuzaliwa na kuelewa kuwa maji yameshawazidi kina. lakini kutokana na mafanikio wanayopata watunzi, hata wasio kipaji, wengi wanaamini kuwa na wao wanaweza kusimama ulingoni na makabambe wengine - kama kina ra (gwiji wa kwanza unit) na wengineo waliokomaa.

kbc na tulanongo naona mnaelewa sana nini kinachoendelea katika hii fani. ombi langu ni kwamba shikeni mwenge juu sana ili wengine pia waone kwa upeo. au vipi? rhymson niko naye sana kwa hiyo nazijua kazi zake na jinsi alivyogangamaa kimsimamo. kweli, ra, ungeingia hapa utoe mawili au matatu ya busara. nadhani ili kuendeleza zaidi hii fani ni lazima kuwa na upeo na kina cha fikra, kitu ambacho kwanza unit walionyesha kuwa nacho. walikuwa ni visionary au walioona mbali na kufungua milango ambayo wengi hivi sasa wanaingia na kutoka bila kujua jasho lililotiririka hadi kufikia hatua hii.

kisha nadhani hivi sasa muziki huu umefikia hatua ambayo litakuwa kosa kutengenisha usanii na biashara (business aspect) ya hip hop. nadhani ili msanii afanikiwe kutokana na jasho lake na ubabe wake wa utunzi, ni lazima uelewe jinsi gani ya kumiliki matunda ya ubunifu wako. nadhani hii itapunguza nafasi ya washashi wanaojifanya ma-promoter na wenye nia ya kusaida wasanii kumbe wanadokoa dokoa kwa faida yao bila ya kujali wasanii na njaa zao (starving artists) kuweka mirija. hata kama wengine watafaidika kutokana na usanii wako lakini isiwe kiasi kwamba msanii anakufa na njaa wakati wasiojua chochote, ila kuwa na visenti tu, ndiyo wanazidi kuvimba kwa uchu wao.

mwendo bado mrefu.
funga macho uone kwa kina

#19 Lord Soames

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 2 posts

Posted 15 June 2004 - 01:52 PM

OK,

Let’s Rewind.

Hip Hop: 5 Elements, what are they and what do they involve?

Back in '98 KBC and Chief Rhymson had a tutorial on radio 1, back then with Dj Mike Mhagama. They went through these 5 Elements which helped to shed some light into many hip hop heads at that time.

I think it will be a good idea if we could turn this debate into another tutorial of similar kind. Many Hip Hop heads of the moment don't know what these Elements involve and so we can't blame them for calling Hip Hop, Bongo Flavour!!

Knowledge is the key, let’s just put some names of the books, websites, magazines, videos tapes etc that one can go and do their own reading.

Hip Hop 4 ever.

#20 Manyotto Ndimbo

    African Hip Hop Newbie

  • Members
  • 3 posts
  • LocationYombo

Posted 16 June 2004 - 04:51 AM

Hongera kwa mijadala hii.Nna machache nataka kuchangia vichwa, sasa ntarudi tena kutoa nasaha zangu kuhusu huu UJENZI. Napenda tu kusema inabidi kuweka mikakati ya vitendo ili kufanya mabadiliko yoyote..Ubao huu ama hali ya teknolojia sasa inaruhusu kuanza HARAKATI za nguvu bila watu kuwepo kwenye chumba kimoja. Nikirudi ntaweka sera zangu wazi..Binafsi mimi hupenda vitendo kuambatana na maneno, asanteni wote.
Manyotto Ndimbo
enyi vichwa kusanyikeni, fani iko mashakani
kila wazo laweza kuwa jambo halisi.

Manyotto Ndimbo





1 user(s) are reading this topic

0 members, 1 guests, 0 anonymous users