nipe dakika
#1
Posted 20 June 2008 - 08:08 AM
nikipiga goti,noti nazihitaji ila, kunifanya mtumwa zinajua sitaki,
lyf ka wimbo wa jitihada, kiitikio ni kuwajibika kesho isikose ladha,
nataka kubonyeza keyboard ukweli utawale screen daily buda,
inakuwa ngumu ka kumrembesha punda kwa poda, kisa
manunguniko ya tumbo yananikumbusha nipo likoni sio runda.
moyo mfuasi wa wema mwili unashawishiwa na adui wa simba wa yuda
makaisari wa hizi siku hawataki nibaki na chakumtolea aliyeniumba
hizi fikra teule ka mchizi wangu wa angazetu
je mtafika mle, muijue ladha ya msosi wetu
hii style ipo huru sihitaji kalamu kueleza ukweli mtupu
hiphop ni nuru ila mafunzo ya mola, kwa wapumbavu minajifanye bubu
nashukuru nishaona ndoto yudas kamba shingoni,si alisahau kutubu
kipato chasiku hakitoshi hata malipo ya sapata
ikifika saa nitapata na hata isipofika, commercial haitanipata
nimeiomba dakika nikiandikacho kisipofika
sio ruhusa kusononeka ila ruhusa kuyatafakari na kuwajibika.
upendo wa dhati kwa kila kichwa cha hiphop.amani ya mungu iwe nanyi
#2
Posted 21 June 2008 - 09:49 AM
wanapiga nduru wanabana nakuumiza nyap zao makoko
si kontroliwi na soko ,najua hii lugha ngumu kwa mapoko
tru kwa kalcha, kwa nguvu za mighty ,wanashangaa kwangu milima haiko
yakuiacha saa haiko, majira ya mola usitupe jicho kwa seiko
naspit nikicheka napata faida, hasara wanaobweka nakutojijua waliko
ka kahspah a.n.g.a ndio zetu design ya nako
sijali kuwashika hamtakikani kwa fani ka kinachotolewa na tako
imani ya mola sindano kumuokoa ngamia
usifikiri utapona hiki kibano hata ukijifungia, tumboni mwa ngamia
mnaangamia mkiona ka adui wa noah, merikebu inajivunia dunia
tym ina run sumu kwa d wack emcee emu- sihi, tamaa yako isikumalize nanii.
#3
Posted 01 July 2008 - 08:35 AM
maisha ya wengi hata baada ya mapigano kutoka mbio
ukweli uliosahaulika,flani kizimbani,flani mchangani(kenya)
makovu aina tofauti,nawaza hali ya mzimbabwe
nika nyavu imepasuka ambayo demokrasia isingeruhusu waibe
story ya wizi regency ni 1.85,2.9 ama hata 7.5 zote be
hichi kilio cha dakika kwa hakika kitavuna hata bongo za masikio kadhaa?
hisia zinateketeza chaka mkulima usilisahau jembe jombaa
tutafika umoja ni nguvu,ila manunguniko zii hayana acha jibu ata ladha
tuungane tuutwae ushindi.
#4
Posted 01 July 2008 - 01:31 PM
elevate yaself mo in swahili.
u gonna b a crazy kenyan swahili hip hop cat in the future.
peace
#5
Posted 05 July 2008 - 08:14 AM
niandikacho hakikosi shabaha na sijafika kiganjo
nipo true kwa imani zangu sihitaji chanjo
wapo speed na nyavu zao kuja kuivua bahari
kucha za paka mwambani upata ukali ambao ni ufahari
ila hautasikia mwamba ulisukumiwa mbali
dakika ina zaa saa ka juhudi zinavyonifaa
nitanganganiaije gari halitanificha roho ikitaka kupaa
kwa sanaa shufaa hakuna juakali kwa sana
mnaduwaa na kufukuzwa bila kwaheri kinyama
#6
Posted 30 July 2008 - 11:22 AM
siku ka hizi za giza
siku kaa hivi ukiigiza
watu mbio ka uvumi skioni mwa mnafiki
mbiu inawaitia anasa babake mzazi wa dhiki
ndio samahani ka nishakukanyaga
chuki ka kuku ukiifuga inataga
sipendi ikipumua tabasamu ikiaga
lyf fupi adui ndio rafiki asiyefaa mauti
namuombea wakati ka thiongo kesho ashuhudie umati
kujijua ndio bahati iliyopuuzwa na wengi
nafsi kwakuistawisha sio benki
#7
Posted 31 July 2008 - 11:44 AM
kunavile ni wachache sana wanauwezo wa kuandika mawazo kwa swahili.
keep on bro!!! nice swahili
http://emigeeish.blogspot.com
#8
Posted 08 August 2008 - 08:28 AM
kwanza pumzika, wenye pupa pumzi zilikatika tukawazika
vikwazo kuvivuka ushindi usio tuzo kudhihirika
uafrika wa dhati mwenyeji wa bara linalonajisiwa kila wakati
dawa za kulevya nika zimeajiri machizi kisa ukosefu wa kazi
vibeti na simu zinavoponyoka utadhani zina bifu na mikono
maisha yanayotukabili sister haoni mbaya kuuza mwili
utamaduni umepigwa kombora wengi wanaukumbatia ugomarrah
hawakufanikiwa ndo maana wanachokora pipa waliofanikiwa wanachokora kuiba
wanaopenda afrika tunaamini juhudi zitalipa
#9
Posted 13 August 2008 - 11:01 AM
hatuna viongozi ila walafi wasioaibika
yaliyotutuma vitani hatujayafuta upendo ulioanguka haujainuka
kisha karua hana nia ka ya martha kuona uchumi lazaro ukifufuka
ye ndio wakumridhi kibaki bila kujali cha kubaki
siezi kumuunga tena mungatana
ashanionyesha ukabila na cheo ndio bora tena bora sana
asset ka port ifilisishwe kisa ukabila
hasa ka sivai koti ndo chanzo kuninyima ajira
cv iongee sio hivi tuwahonge
waliokwenda kumsaka huenda ndio waliomficha fazul
pazuri,tazama zaidi ya uwezo wa macho
huenda jibu unalo kabla swali halijaziba jicho.
kisha machizi ka emigee,couz, krym na yoyote anayefeel kazi yangu upendo sana.(onelove)
one love
#10
Posted 13 August 2008 - 02:58 PM
maneno yanageuka kuwa makali ya upanga gizani /
na kuwaacha wanasiasa na wafuasi wao vichwa wazi /
akili zikiachana na ubongo / fikra nazirukisha viunzi /
bila shaka nawapatia mtazamo mpya wa maisha /
na hata nikifa leo nafsi yangu itabakia kuhakikisha /
kila mara kuwakujia ndotoni hata kabla hamjalala /
na mashairi yanayoibua mengi maswala /
kama kutembea katikati mwa adui kifua wazi bila silaha /
ndivyo ninanvyo jiamini na yangu akili iliyogeuka nyeusi /
kwa fikra zenye undani zaidi ya shimo lisilo na kimo /
kurasa tutazidi kuzijaza mafunzo yanayozidi mistari /
jus' to make u' think outside that box u' call a head/
* I don't only think ahead, but ma' thoughts surpass those of a single head * |Couzifer|
#11
Posted 14 August 2008 - 09:31 AM
kulimega tunda lake la kati(uchumi) ndo kilichowafanya wamfate
afrika anachechemea hakuna haja ya mayor
ka kipofu aliyelemaa miguu na kupoozwa na anaowategemea
watoto wake wampendao wamenyimwa kujitegemea
sera hazioni zinatutuma vitani ka sieraleoni
hata lini mtajua ukweli yaani nyinyi
siasa ndo kamba iliyotiwa kwa afrika shingoni
uhuru ni wakuongea uhuru si wa kufuraia
212 wabunge wanakufuru uraia wanamsulubu raia
nika wameshindwa kumzibia mzimbabwe
faida ya kura si uongozi bali kulijaza debe
kenya ili zima taa yakumumulika shujaa
kenyatta na kimathi kwasasa jiulize nani angetupa shufaa
we ndio hero hivo tukomboe palipo baki budaaa.....
sawasawa
#12
Posted 30 August 2008 - 07:59 AM
kunufaisha wenyekuupenda ukweli vile ulivyo kwa uhakika
alhamdulilahi wapo ndugu wenye mitazamo kama hii nayoiandika
waliochoshwa na uongo toka siasa na upumbavu unaojiita kapuka
sioni haja ya kuruka ka bidii yangu kwanza haijatambulika
radio inayofaa kuni teachi inaniambia eti nishike matiti
fuck afadhali nicheki watoto wakicheza ukutiukuti
vijana jobless mabuda wakistaafu wanarudishwa wazidi kuokota noti
ngeta imekua desturi mitaa ka likoni
machozi yanabeta na kuuchoma moyo baada ya kuchoka kuchafua surani
ni mengi tu nawasioona ajabu pia niwengi tu
#13
Posted 22 September 2008 - 07:49 AM
hai navyopumua nawatwanga na kuzika wa juu ardhini
sio madini yasiofaidi thamani yake ya ndani
kwa tv sipo sikioni wenye booth hawaelewi umuhimu wa ulimi
mavuno hutoka mchangani hivyo nifwate nini hewani
redio zinaniogopa si underground inahusiana na mchanga uchafu yani
kuishi kandege wanilenge na nisijue kukoje kutokako madini sio mimi
mizani yamaisha inipate na pupa za senti
kwenye kupumbaza utu ni keti na sisitiza huko unipati
mwili na akili zenye uzani na mapenzi ya kweli
ningekua bendera upepo ungenifuata mimi nakiri
kwenye hizi haba za chemichemi za haki
kujaza kibaba nisihofu mamwera street
ungerground najivunia thamani
#14
Posted 24 September 2008 - 10:37 AM
nikose redioni na tv, ingawa sura hauijui ka rangi ya oxygen
'niandikacho tamani ka jua kwa watokao mamtoni
hakichubui hii ni tu, ka ukweli unaudhamini moyoni
ila moto kwa walionishuku gaidi kisa sera za thamani
kunipakazia mungiki maana kamau niliitwa utotoni
njeri ouma mi ni nzioka mwamdawiro
ikubali pete maana navyokufia hakupimiki na kilo
usiniambie story za kabila eti wajomba wataleta hila
ulisema mi kwako zaidi ya jua mwanga usioweza kukaa bila
tulipopendana emilio ,tinga,musyoka na ata mghanga hawakuwepo
tulichopendania kisiuliwe na sababu za kipepo.yess zishindwe
je upotayari kuolewa nami we sema ndio yaani..
#15
Posted 24 October 2008 - 10:42 AM
hii movement haina nywele ila akili zimefurika
naps ikinipotezea hekma goti kwa jah naamini nitafika
misitu iliyofungika nashukuru busara zitaifyeka
hamna hamna napata wakinikanyagia miguu yao itachomeka
jua ni mwanga najua pia nimezungukwa na wanga
madamu kwa vidole vyao ka firstborn wa adamu
utamu niki free hata bila kipaza bado watanihukumu
naomba msamaha ka cygon bia ilinidhulimu
njiani traffic hawachukui hongo hii lyf kichwa gurudumu
siku njema niliiona seco kongowea wakimshutumu
yote tisa monalisa mavolture walimfunza wallet
kaka ni ndugu mc mzinga hauna asali ila mishale ya nyuki
hukumu za umati hakuiba aliuliwa
system dirty aliua hakukusudia
#16
Posted 29 October 2008 - 11:19 AM
watu humu kwenye fani wameweza kupoteza lile la maana kuzungumuzia./
tumebadili mpago wa kuelimisha jamii/ shida yametukumba sisi bila kufikiriwa/
jamii ime kosa maana kwa maisha ya binadamu/
mtu hataki kukuona ukiwa unpiga hatua ya mbele/
yeye huyo hata kua hapo mbele kuku zibia mpenyo./
Wafanya kazi kamili bila malipo, huku ukiuliza nikama haukwepo/
mabinti wameonelea kazi maalum bila shida ni umalaya/
kujipata kuuza na pia kuna wanunuzi/
pombe imekua kama suluhu,/
kwa hakika viwanda vya pombe ime zidii kupunguza bei ya kinywaji/
nikama wao kazi ni kuuza hawa jail masilahi ya wanadamu/
twaishi kama wanyama, kwani tuta kula kwenye mataka, na kuishi kama wanyama wa mjini/
sentensi zangu kwa hakika zitawatata/
lakini ukiwa makini sana utanipata/ haya ni malamishi ya binadamu kawaida/
binadamu anaye elewa yale yaliomo/
mimi sina kipimo, uandishi nitautenda mpaka niupate mwelekeo/
kama hamna mwelekeo basi neno nitanena, kwa vile mimi ni kioo cha jamii!
http://emigeeish.blogspot.com
#17
Posted 31 October 2008 - 10:15 AM
hawatoki wanacheka hawachoki kuteka
shida zangu zulia wanakalia wakiveveka
watainuaje msalaba ambao utawatundika
waki ni mwaki wanakariri hawautaki
asilimia kuu haijui asli na nia ya hawa wakuu
nahisi uchungu na aibu kumuona mama aliyepanua miguu
kwa tv njaa ikimpa ujasiri mbele za kamera kuitoa siri
bungeni mikopo yakununua gari mitaani ukope ule ama upeane mwili
huku wao wanajilipa nyingi mpaka macho wanayanunulia pazia
pa kuanzia wamepatia miba elimu bure watoto wanaachishwa namimba
fuck politics labda itazaa shufaa
#18
Posted 10 November 2008 - 04:40 PM
ka rangi ya bahari chota uone kwa mbali jicho lilisleki
labda mabreki na sio dere wa tuktuk
hakutoka akilamba poda hazikwi nayo ajabu haiachiki
mpe dakika sio useme mizani yake haipimiki
poa ka onyx moyo hauna doa ingawa mwili hautamaniki
unavyoiona sivyo labda ndivyo ki jay ka kinyonga habashiriki
ye hasingizii mwiko kukosa sembe ni mfuko haumshiki
hukumuona akigawa ila yuko mbio hashikiki
uongo ukiutoa mmoja mmoja ka mshikaki kwa kijiti
asalamu nidhamu roho giza ka likifunikwa kaburi
mashughuli hazimlipi usidhani mwani anaufanyia ufahari
kweli sivyo, midomo,sura za bunge sio mwili na matendo ya hawa fahari
kwa sheria hakimu wallet mkosa na mkoswa hivo hatutawajua kamili
jivishe kiatu chake kabla mawe na matofali
uhuru ni mwana wa jomo nchini bado ni swali.
#19
Posted 11 November 2008 - 01:18 PM
mizani said:
hawatoki wanacheka hawachoki kuteka
shida zangu zulia wanakalia wakiveveka
watainuaje msalaba ambao utawatundika
waki ni mwaki wanakariri hawautaki
asilimia kuu haijui asli na nia ya hawa wakuu
nahisi uchungu na aibu kumuona mama aliyepanua miguu
kwa tv njaa ikimpa ujasiri mbele za kamera kuitoa siri
bungeni mikopo yakununua gari mitaani ukope ule ama upeane mwili
huku wao wanajilipa nyingi mpaka macho wanayanunulia pazia
pa kuanzia wamepatia miba elimu bure watoto wanaachishwa namimba
f*ck politics labda itazaa shufaa
nice words you do have away with swahili and keep the blaze up, usizime moto wacha moto upashe!!!
http://emigeeish.blogspot.com
#20
Posted 11 November 2008 - 01:21 PM
mizani said:
jivishe kiatu chake kabla mawe na matofali
uhuru ni mwana wa jomo nchini bado ni swali.
nice!!!!!
http://emigeeish.blogspot.com
1 user(s) are reading this topic
0 members, 1 guests, 0 anonymous users












