New forum: KiSwahili Battles - na Msitukane tena huku

Nimefungua forum mpya kwa ajili ya wenzetu wanaopenda kushindana kwa kutunga rhymes: KiSwahili Battles - tazama main page mtaikuta.

Nimefanya hivi hasa kwa sababu kuna mashindano fulani yanayoendelea yaliyo na matusi kibao... kuna wengine ambao wanatembelea hii site wakiona tu wataamini kwamba sisi wapenzi wa hiphop hatuna ustaarabu.

Fikiria wazee wako wakiingia huku na kusoma kuhusu shoga kufirwa na nini, watasemaje.

Hayo si maoni yangu ila nadhani ni vizuri kama tunabainisha sanaa na maisha, hivi matusi yanaweza kutumika lakini hasa kwa mahali pa ku battle. Pia mtu mmoja kumjibu mwingine kwa lugha yenye matukano haifai hapa, lipeleke Battles!

Comments

 • 1 Comment sorted by
 • Vote Up0Vote Down
  edited August 2002
  Mambo namna gani J4?

  Duh hapo mshkaji umefanya jambo la maana sana

  Maana huko mzee ndio tutakuwa tunaoneshana

  Kwamba nani ni nani katika mambo ya vina

  Na ndipo washikaji wote nitawaonesha uchawi wangu kwa kina

  Mpaka watabaki macho pima

  Duh SmokeyOBL ametusimamisha wima

  Kwa rhymez zake kali

  Kweli Smokey jemedari!

  Thanks sana kwa kufungua kiswahili battles.........
Sign In or Register to comment.
African Hip Hop Radio
Advertisement