Itakuaje

Itakuaje kuingia heaven bila kudedi/

inakuaje naota ndoto na sijalala/

ntashiba aje nasijala/

sonko ata kua aje safe/

na wengi wako hungry/

tutachekiaje vision 2030/

na viongozi ni walafi/

uta omba aje Sir God/

na hi pande ingine unaconsult mganga/

itakuaje mi ni brother/

sa yenye tu una need help/

tutaongea aje ju ya unity/

na wenyewe tunajiekea barriers/

umuhimu gani kuimba national anthem/

na huku tunajigawanya kwa tribal kingdoms/

utathink aje outside/

na ulisha ingizwa box/

mind zimefungwa ka dread locks/

uta fly aje na uwivu ya msaliti/

inakurudisha down kagravity/

nta fill aje blanks/

yet na uliza maswali hayana answer/
Sign In or Register to comment.
African Hip Hop Radio
Advertisement